Suala la Mume au Mke wa Kiroho ( Spiritual Husbands or Wives) linafahamika sana katika ulimwengu wa kiroho na suala hili limekuwa likiwatesa watu wengu katika maisha ya kila siku na limeambatana na dalili nyingi kama ndoto zisizo katika hali ya kawaida. Mpendwa Biblia imetoa suluhu la changamoto hii ,tufatilie kwa pamoja;
Fahamu Dalili mbalimbali za Mume au Mke wa Kiroho ( Spiritual Husbands or Wives)
- Kuota Unafunga Ndoa na mtu usiye mjua.
- Kuota umeolewa na una familia
- Kuota unafanya mapenzi (una-sex) na mwanaume au mwanamke usiyemjua.
- Kuwashwa kidole cha pete hasa ukiomba.
- Kuhisi umevaa pete au unapete kidoleni.
Fahamu chanzo au milango ya roho hizi
- Mila na desturi mbovu, matambiko ya kuozesha watoto kwa mizimu (Hii ni mbaya sana kwani ufanyika wakati mtu ni mtoto na hajitambui).
- Uzinzi!, hii hutokea mara nyingi katika tendo la ndoa unakuta mwenzio tiyari anachangamoto hii hivyo inahamia kwako, Mfano hai katika maisha ya kawaida unaweza kukuta mwanamke ana jini mahaba la kike na hili ni dhahili huwa mara nyingi amelitoa kwa mwanaume.
- Picha na Video za Uchi ( Pornography na X-Videos) au Masterbation mambo haya hukuweka wewe katika hali hatarishi (vurnerable) kutumika na roho hizi.
- Kwenda kwa waganga na kufanya maagano nao na kutumia vitu vyao.Vile vitu vinakuacha katika hali hatarishi ya kutumika na roho hizi.
Mpendwa hata ukifanya maombi ya aina gani kama hautazifunga roho hizi ni kazi bure lazima zitarudi tena na kuharibu maisha yako na hii ni dhahili kwani Maranyingi wengi mnaombewa lakini haipiti muda mrefu roho hizi zinakurudia tena , Suluhu ni kuzifunga kwa kufunga milango inayoruhusu roho hizi kuingia kwenye mwili wako na kuanza kukutumia na mpendwa yapo maombi ya aina nyingi sana ya kupambana na roho hizi.Mpendwa ukiwa mtu wa ibada sana unayesali inavyotakiwa unazimaliza nguvu roho hizi automaticaly!! na katika njia hii zinaweza kufifia na kuisha kabisa, Kabla ya kulaa unajizungushia damu ya Yesu, Zaburi , Moto wa Roho Mtakatifu haziwezi kukugusa tena.
Mpendwa tufahamu mlango wa roho hizi ukishafunguliwa unakuwa wazi kwao muda wote na wanaanza kupita wanavyotaka na njia rahisi ya kuzuia ni kufunga mlango kwa haraka. Watu wengi wanafanya makosa ya kufanya maombi mazito lakini wanasahau kufunga mango hivyo unakuta anaomba lakini usiku hali inajirudi katika hali yake ya mwanzo ,kinachohitajika ni kufunga mlango kwanzandipo maombi yafanyike.
Kutoka 123 : 8 – 13 Habari Njema.
8 Watakula hiyo nyama usiku huo, wakiwa wameichoma moto, watakula pamoja na mikate isiyotiwa chachu na mboga za majani.
9 Msiile nyama hiyo mvunguni, wala msiiache isalie asubuhi. Yeyote atakayoisalia mpaka asubuhi, ni lazima aiteketishe.
10 Mle hiyo nyama hivi: Mjiandae kwa safari, mkiwa mmepasuka nguo zenu na viatu vyenu miguuni mwenu, na fimbo mikononi mwenu. Mle haraka sana, kwa maana hiyo ni Pasaka kwa ajili ya Bwana.
11 “Kwa hiyo, itakuwa hivi: Ile hiyo Pasaka ya Bwana, nitapita katikati ya nchi ya Misri usiku huo, nami nitapiga wazaliwa wa kwanza wa Misri, wa wanadamu na wa wanyama, nami nitawatenda hukumu dhidi ya miungu yote ya Misri. Mimi ndiye Bwana.
12 Damu itakuwa ishara kwenu katika nyumba zile mtakazokuwa humo; nitakapoyaona hayo majilio, nitapita juu yenu, wala tauni isiwapate ninyi.
13 “Damu ile itakuwa kwenu kuwa ishara juu ya nyumba zile mtakazokuwa humo. Nawaona hayo majilio, nitakapoyaona damu, nitapita juu yenu, wala hapatakuwako ndani yenu tauni itakayowapata ninyi, nitakapoyapiga nchi ya Misri.”
Kutoka 12 : 22 – 23
22.Mtachukua majani ya husopo na kuyachovya katika damu ndani ya birika na kupaka kwenye vizingiti na miimo yote miwili ya milango ya nyumba zenu.Mtu yeyote asitoke nje ya nyumba hiyo hadi asubuhi.23. Maana mimi Mwenyezi-Mungu nitapita kuwauwa wamisri. Lakini nitakapo-iona damu iliyopakwa kwenye vizingiti na miimo ya nyumba zenu nitazipita na wala sitamruhusu mwangamizi kuingia katika nyumba zenu.
Mpendwa kufunga mlango wa roho hizo kupita utatumia andiko hili la Kutoka sura ya 12 na ukisoma lote itakuwa vizuri zaidi, Utatumia damu ya mwanakondoo kwenye andiko hili kufunga lango wanalopitia katika ulimwengu wa roho,hivyo wakija watakuta damu ya mwanakondoo na kuvuna upanga tu.Mpendwa omba kupitia andiko hili maranyingi mpaka uone mambo yako yako shwari na uendelee kusali kabla ya kulala na kuacha lango wazi hakika mambo yako yatakuwa mazuri.
Amina,Mungu akubariki Mtumishi nimeanza leo haya maombi pamoja na kufunga
Amen,Mtumishi.