SOURCE KUU ZA CHANGAMOTO ZA UCHUMI NA AJIRA / HATA NYINGINEZO

 

Kila changamoto inayokukabili ina source yake. Na sources kwenye ulimwengu wa roho zimegawanyika mara nne.

  1. Human causes.

  2. Man-made causes.

  3. Demonic / spiritual causes.

  4. God’s response causes.

Kujua cause ya changamoto yako ni muhimu sana, kwa sababu itakusaidia kuto-tibu mguu wakati jipu lipo kichwani. Kama cause ni spiritual, hata ujitume vipi bila bila.

Kama cause ni human causes, hata uombewe na Papa Leo wa 14th, hakuna kitu kitabadilika, kwa sababu spirits zinashangaa kuhusika na jambo lako kivipi sasa. Ya nini kuzisingizia?

Kuna watu wamefungwa na viburi, uvivu, pride. Hata ukeme pepo asubuhi mpaka kesho asubuhi, hakutakuwa na jipya. Mtu ha-apply kazi kabisa. Uvivu tu ana-uendeleza. Atapata vipi kazi ambazo haja-apply?

Kuna watu wana pride na kuona watu takataka. Hata afungue biashara gani lazima ataradiate wrong vibes, wateja wote wakimbie. Hata kama biashara iliwekwa wakfu na mtumishi mtakatifu kiasi gani au maarufu vipi.

  1. HUMAN PROBLEMS / CHALLENGES.

Hizi ni changamoto ambazo zinachangiwa kwa kiasi kikubwa na ubinadamu wetu.

Mfano njaa. Hata uwe na upako vipi, njaa ikikukamata vizuri utaanguka madhabahuni kama mzigo. Fatigue pia. Uchovu. Mwili ukichoka, dawa ni kupumzika tu. Njaa ikiuma dawa ni kufakamia misosi.

Kuna watu wanajaribu kufunga siku 40, kufikia siku ya 14 wanaishia drip mkononi hospitali. Mwili una goma.

Huwezi kuikemea njaa. Hata Yesu, wanafunzi wake walimwambia Rabi njaa inauma. Sabato au sio Sabato, njaa inauma vibaya. Yesu akawaruhusu wavunje masuke ya ngano wapooze njaa. Humwoni Yesu akiikemea njaa. Daudi na wenzake nao kuna siku walivamiwa vibaya wakala sadaka za hekaluni. Mnafanya mashahala na njaa nyinyi?

Muonekano wako. Mungu kakuumba flat screen. Tko kubwa wewe huna. Hakuna maombi ya kuongeza tko. Solution sio kufanya ibada t*ko liongezeke, bali Mungu akupe mwanaume anayependa vimbao.

  1. MAN-MADE CAUSES / PROBLEMS.

Hizi ni changamoto zinazotengenezwa na maamuzi ya binadamu mwenyewe.

Uvivu ni kipengele kikubwa cha man-made causes. Watu wengi hawafanyi mambo kwa sababu ya umalaya, bali kwa njaa na uvivu.

Uvivu wa kazi unakutanya ulale na maboss, mwisho wanakupa maradhi tu.

Pride ni man-made cause. Tabia ya kujiona na kujisikia inapishana na destiny helpers.

1 Peter 5:5-6.

God resists the proud but gives grace to the humble. Therefore humble yourselves under the mighty hand of God.

Man-made problems zinamalizwa kwa improved man decisions. Maombi kwenye haya ni kutwanga maji kwenye kinu.

  1. DEMONIC / SPIRITUAL CAUSES.

Hizi ni changamoto ambazo mtu hana control nazo. Roho chafu ndizo zinacontrol.

Kuna oppression, bondage na addiction.

Oppression ni kunyanyasika bila sababu. Bondage ni kufungwa na minyororo. Addiction ni kushindwa kuacha jambo.

Pornography ni portal ya kupitisha maroho. Haitoki kwa will power.

Suluhisho ni Ministry of Deliverance.

Luke 13:10–17.

Yesu alimuona mwanamke aliyekuwa amefungwa na roho kwa miaka 18. Hakushughulika na dalili, alishughulika na roho nyuma ya tatizo.

  1. CHANGAMOTO ZINAZOTOKANA NA ADHABU YA MUNGU.

Kuna changamoto ambazo ni matokeo ya dhambi.

Kula zaka za Mungu huleta kukosa ajira. UPAKO hauwezi kumpinga Mungu.

Toba ya kweli ndiyo tiba.

Zaburi 51:17.

Dhabihu za Mungu ni roho iliyovunjika. Moyo uliovunjika na kupondeka, Mungu hatauudharau.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Scroll to Top