Toba ni zawadi ya kiroho inayotuwezesha kuunganisha nafsi zetu na Mungu wetu mwenye upendo. Ni njia ya kutuongoza katika kurekebisha mwelekeo wetu, kuachana na dhambi, na kuelekea nuru ya msamaha na neema ya Mungu. Tufatilie mafunzo mbalimbali yaliyotolewa katika Biblia kuhusu Toba.
Day 1 : Toba
Isaya 59 : 2
Dhambi zenu ndizo zzinazowatengs na Mungu wenu, dhambi zenu zinamfanya ajifiche mbali nanyi asiweze hata kuwasikia.
Maombi ni kupitia Zaburi ya 51.
Prayer Point
Baba naomba msamaha,nimekosa mimi, nimekosa sana mbele yako na hii dunia.Sitarudia udhalimu, nirehemu katika ghadhabu yako kumbuka rehema. Nirudishie uso wako na fadhili zako.
Day 2 : Toba
Luka 13: 3
Nawaambieni hakika sivyo; lakini nanyi hali kadhalika, msipotubu mtaangamia kama wao.
Luke 13 : 2
No, I tell you; but nless you repent, you wil all likewise perish.
Maombi ni kupitia Zaburi ya 6
Prayer Point
Natubu bwana, nimekosa mimi nimekosa sana mbele yako ni hii dunia.Nirehemu ee Mungu. Usiniache niangamie kama wao.katikati ya ghadhabu yako kumbuka rehema. Nirehemu mja wako.
Day 3 : Toba
2 Mambo ya Nyakati 7 : 14
Ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu; watajinyenyekeza na kuomba, na kunitafuta, na kuziacha njia zao mbaya; basi nitasikia toka mbinguni na kiwasamehe dhambi zao na kuponya nchi yao.
Maombi ni kupitia Zaburi ya 32.
Prayer Point
Baba najinyenyekeza mbele zako nikiomba toba na rehema.
Day 4 : Toba
Mnaposimama kusali, msameheni kila mtu aliyewakosea chochote, ili baba aliyembinguni awasamehe nyinyi makosa yenu.
Maombi ni kupitia Zaburi ya 38.
Prayer Point
Tafakari watu wote uliowabeba rohoni na kushindwa kuwasamehe lakini wasamehe wote na kuwaachilia rasmi.Hata kama walikukosea kiasi gani.Mpendwa usiposamehe unazuia rehema yako na Breakthrough.
Day 5 : Toba
Yeremia 3 : 22
Rudini, enyi watoto waasi, mimi nitaponya maasi yenu. Tazama, tumekuja kwako; kwa maana wewe u BWANA, Mungu wetu.
Maombi kupitia Zaburi ya 37
Prayer Point
Bwana tuponye na maasi yetu, tumekukimbilia wewe tusiaibke milele
Day 6 : Toba
Hosea 5 : 15
Nitakwenda zangu niparudia mahali pangu, hata watakapo ungama makosa yao na kuutafuta uso wangu; katika taabu yao watanitafuta kwa bidii.
Hosea 5 : 15
I will return again to My Place untill they acknowledge their offense.They will seek my face;in their affliction they will earnestky seek Me.
Maombi ni kupita Zaburi ya 102
Prayer Point
Baba nakubali uovu wangu nihurumie na kunionesha uso wako.
Day 7 : Toba
Yoeli 2 : 25 – 27
Nitawarudishia miaka ile iliyoliwa na nzige, kila kitu kilicholiwa na tunutu, papare na matumatu., hilo jeshi kubwa nililo waletea! mtapata chakula kingi na kutosheka; mtalisifu jina la mwenyezi Mungu, Mungu wenu aliye watendea mambo ya ajabu.Watu wangu kamwe hawata dharauliwa tena. Mtatambua kwamba mimi nimo miongomi mwenu, enyi Waisraeli; kwamba mimi Mwenyezi Mungu, ndimi Mungu wenu wala hakuna mwingine. Watu wangu kamwe hawatadharauliwa tena.
Prayer Point
Baba nimetubu toka moyoni. Pokea Toba yangu, unirehemu na kunifanyia urejesho kamili sawasawa na neno lako ulilolinena kupitia Nabii Yoel kupitia Yoel 2 : 25 – 27