SAFARI YA MATOKEO KUWA HALISI (SUNDAY WORD)

Wengi tumekuwa brainwashed kwamba una muomba Mungu kitu, then you forget about it afu siku ya siku Mungu ana ku surprise! Taraa! Hiki hapa.

And reality is always stranger than fiction. Maana kinyume na expectations zako unaona miaka imepita 10 Mungu haji gus. Unakata tamaa na kupanic. Issue sio Mungu, issue ni approach zenu.

Mungu anaweza kujibu na akaachilia matokeo kabisa ulimwengu wa roho ila huku mwilini bila bila! We receive in spirit but we have physically! Hizi ni dimension 2 tofauti kabisa na haziingiliani. Ukipwaya mmoja umeishaaa.

You receive in spirit na after receiving unaweza kuona maono kabisa kwamba upo kazini, unaolewa, upo kwenye biashara yako. Lakini reality yako vice versa is always true.

We have things physically. We have jobs, kids, husbands, businesses, houses, cars. Mambo yapo live na yapo lele. Kama unacho unacho kinaonekana kwa macho na kinagusika, na kama huna huna. Hakuna mambo ya mimi mdogo kimwili ila kiroho mkubwa. Hizo dunia 2 tofauti.

Watu wengi issue sio Mungu kuwapa au wao ku-receive from God, issue ni kuzishinda nafsi zao mpaka mambo yawe halisi.

Either mtu ana yabananga kwenye receiving game au having game. Hizi angle 2 ndo korofi hasa hasa ambapo usipokuwa makini hata mlokole legit kabisa unatoka kapaaa. Sio kwamba maandiko huyajui. Vitabu umevimalizaaa. Ubabaifu mdogo tu unakugharimu.

Kuomba sio issue sana. It’s a 2 minutes job kama ukiwa mtaalamu wa maandiko. Ku-reference andiko is hardly 2 minutes. Kama kuamini ushaamini zamani hizooo. Imani imejaa na kumwagika. Kumpokea Yesu usha mpokea zamani hizooo. So kuomba kitu mbele za Mungu it will take you hardly 2 minutes.

Kupokea hicho kitu sasa ndo balaaaa lilipo. It can take even forever. Wewe tu na ubabaifu wako. Unavyotaka na mbingu zinataka hivyo hivyo.

Sio kwamba kitu hakiwezi kuachiliwa rather wewe unashindwa mwenyewe kukipokea. Una nawa na inakula kwako. Ukiona wenzio tunavupokea kwa wingi, tunakuhakikishia hamna upendeleo wowote. Mbingu zimenyoooka. Sisi tunanyoosha na kukomaaa zinavyotaka mbingu na sisi tunataka hivyo hivyo mpaka tupate.

KEYS TO RECEIVING RESULTS FROM GOD

Majibu kuchelewa ni sehemu ya maisha. Na kwanini yamechelewa sio issue sana maana hata ukijua kwanini na majibu bado huna si kizungumkuti kile kile tu. Issue ni kukaza na kushupaza fuvu hii situation ya majibu kuchelewa isi kukengeushe ukapishana na Mungu wako. Ni kubakia kwenye uwepo wa Mungu hata kama majibu hunaaa. Asikwambie mtu sio rahisi.

  1. Ku-maintain moyo uliovunjika na kupondeka throughout ukingoja majibu yako.

Hapa inatakiwa kwanza uwe na hofu ya Mungu, as in una muogopa Mungu kweli kweli. Bila hivyo hutoboi. Ni rahisi sana kujikuta umeyatupa maneno na kumkufuru Mungu asubuhi na mapema, au unasusa na kutamka kabisa kwamba hicho kitu hutaki tena, na ulimwengu wa roho wanapublish kufuru zako against you. Kutimiza hii condition unatakiwa uwe mkomavu kweli kweli wa imani.

It is hard accepting you are a victim. Na muda wote akili itakujia uchezeshe karata kujitoa kwenye victimisation, ikibidi ucheze hata jokari.

Mimi nawahudumia watu humu. Dakika 2 wapo magotini. Dakika 2 wana mkufuru Mungu na kuniona tapeli sijui nilicho watapeli nini. Dakika 3 mama mwanangu nimerudi tuendelee. All! Nachoka mimi mjukuu wa mzee Mwandambo.

Dakika 2 mama upweke umenichosha, lazima Mungu anifungue, nivuke, niwe na mwenzangu, lazima niende kazini mama. Dakika 3 mama mambo ya uhusiano sitaki tena. Sitaki sitaki sitaki. Wala usinisemeshe hilo eneo. Tufocus kwenye kazi kunakoenda. Sawa mwanangu. Kuvuka kwa pakacha nafu ya mchukuzi. Mwezi mrefu sana. Mama mahusiano mama.

Psalm 51:17

My sacrifice, O God, is a broken spirit; a broken and contrite heart you, God, will not despise.

Wengi mnatoa dhabihu hata million 510 shida zenu ila moyo uliovunjika na kupondeka kumtolea Mungu sio kweli kwenu.

Una shida na unahitaji Mungu akusaidie ila bado jeuri na kiburi vile vile, na unashangaa mbona majibu yako yanachelewa.

Ukionyesha moyo uliovunjika na kupondeka mbele za Mungu kwa consistency utamshawishi Mungu kukupa majibu yako mapema zaidi.

Shengesho zote shetani anazofanya lengo ni moja tu, ukufuru kwa Mungu na ujiharibie. Kwishaaa habari yako.

Lakini ukikazaaaa, akupindue anavyokupindua. Lazima usome maandiko na lazima usiku usali. In short swala ni 3 kwa siku. Mungu atakujibu mapemaaa sana.

Wengi deliverance mnaanza vizuri. Mtalipa zaka hata miezi 6. Ila tu uanze. Utaanza week 3, ya nne kitatokea ka kitu very very minor. Ndo mwisho wa deliverance na kusoma neno na ibada na kila kitu.

Moyo uliovunjika na kupondeka hamna hata kwa mbali.

Matthew 5:3

Blessed are the poor in spirit, for theirs is the kingdom of heaven.

Heri maskini wa roho kwa maana ufalme wa Mungu ni wao. Je wewe ni maskini wa roho mbele za Mungu?

Unaweza kuwa maskini wa hela ila tajiri wa roho. Maskini jeuri. Shida unazo na ibada hufanyi vile vile. Shida unazo sadaka hutoii. Wala maandiko husomi. Huo utajiri wa roho shoga angu.

Huwezi kuwa maskini wa roho hujasoma Injili zote 4. Sisi maskini wa roho agano jipya tumefutaaa. Tutafanyaje sasa na ufalme wa mbinguni tunautaka bila Mungu hatutoboi.

Vitabu vinaboaaa, vinanichosha, ila bila umaskini wa roho itakula kwetuuu. Unavyosikia maskini wa roho usijue juu juu. Kapuku wa roh ooo. As long as Mungu ndo anataka tutajikaza kufanya ili mambo yetu yaende. Maskini wa roho ndo sisi sasa.

Unajijua kabisa bila Mungu maisha hunana kenge wewe. Huna nyimbo wewe kabisa. Mungu aki mute imeishaaa. Lazima uwe omba omba mbinguni.

Psalm 34:18

The Lord is close to the brokenhearted and saves those who are crushed in spirit.

Siku ukivunja vunja moyo wako na kwenda mbele za Mungu akupe msaada itakuwa tofauti. Akiona umesagika moyo na umemeza kiburi na jeuri atakukaribia.

  1. Praying the prayer of mercy and help.

Psalm 107:6

Then they cried unto the Lord in their trouble, and he delivered them out of their distresses.

Usikae kimya kama mambo hayapo vizuri. Usivumilie. Lia, piga kelele, galagala mbele za Mungu. Muite Mungu 24/7.

Marko 10:46–52

Yesu, Mwana wa Daudi, nihurumie.

Usikae kimya mbele ya mlima wako. Muite Mungu mpaka sauti ikauke.

  1. Panda mbegu ya kuomba msaada.

Galatians 6:7

Do not be deceived: God cannot be mocked. A man reaps what he sows.

Kila mtu ni mkulima na atavuna alichopanda.

1 Corinthians 3:6–8

I planted, Apollos watered; but God gave the increase.

God cannot be mocked. Unachopanda ndicho utakachovuna.

John 8:32

Tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru.

Isaiah 43:18–19

Msiyanganganie mambo yaliyopita, wala msifikirie vitu vya zamani. Tazameni, mimi ninafanya kitu kipya.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Scroll to Top