Sadaka ni nini?
Sadaka ni matoleo ya kumkaribia Mungu kwa njia mabalimbali ikiwemo toba, maombi, shukrani, mazungumzo etc. Lengo hasa la mtoaji kutoa sadaka ni mtoaji kumkaribia Mungu na kupata attention yake.
Je Sadaka ni lazima iwe Pesa?
Hapana! Sadaka inaweza kuwa ni kitu kama mazao au mifugo. Mfano katika Biblia tunaona Kaini na Abeli wakitoa sadaka za vitu na katika agano la kale aina kubwa ya sadaka iliyotoewa ni sadaka ya vitu kama mazao, mifugo nk.Musa alaitoa mwanakondoo wa pasaka kama sadaka. Aidha tunaona pia katika agano jipya watu wakitoa madini kama fedha, shaba na dhahabu kama sadaka,Mitume walijitoa katika utumishi kama sadaka, Mungu alimtoa mwanaye wa pekee kama sadaka ya ukombozi wa mwisho,Pia Abrahamu alitaka kumtoa mwanaye Isaka kama sadaka. Wapendwa katika Torati ya Musa sadaka za watu, watoto zilibatilishwa na Mungu alisema hazimpendezi.
Fahamu makosa makubwa muda wa kutoa SADAKA
Mpendwa kwanza ningependa tufahamu kuwa Mungu hana shida ya Sadaka kamwe.Maandiko yanasema utajiri na heshima yote ni mali yake, sasa anaanzaje kuwa na shida ya sadaka kutoka kwako? na hapa ndipo watu tunapokosea sana. Mtumishi anaweza kutumikia vibaya na shetani kuendekeza njaa lakini Mungu kama Mungu anawalipa vizuri watenda kazi wake. Hivyo nipende kukusihi mpendwa kufuta kabisa dhana ya kuwa Mungu au huduma yake inahitaji msaada wako au kusaidiwa. Hapana!.
Mpendwa wewe ndiyo unahitaji msaada wa Mungu, na unatoa sadaka yako ili mbingu zikusaidie na hapa ndipo sadaka zinapoteketea. Ukishaona Mungu au huduma yake inahitaji msaada wako basi umeshafeli yaani Mungu wa mahali hapo umeshamdondosha na anawezaje kukutendea maajabu? WEWE NDIYO UNAHITAJI MSAADA WA MUNGU. OMBA SANA UPATE MSAADA.
Je Sadaka inapewa huduma au Mtumishi?
Hii pia ni changamoto nyingine.Mpendwa ukitoa sadaka kwa kwa kumpa mtumishi au kuisaidia huduma utapata matokeo yak kadri ya upako wa mtumishi au huduma.Mpendwa sadaka yako mtolee Mungu wwak wa Israeli! Adona!.Hana changamoto moja kwa moja maombi yako yatafika mbinguni na kujibiwa.Mtumishi ni mpokeaji tu kwa niaba.Ukimtolea Mungu mkabidhi Mungu na fuatilia kwa Mungu.Sio unaanza kuchunguza imetumika vipi.?. Mpendwa ukimkabidhi Mungu imani yako Mambo yako yatanyooka na tukumbuke unachokideclare wakati wa kutoa ni muhimu sana. Mpendwa yabidi kuwa na imani kiasi cha kusema mimi sadaka naweka kwenye bahasha au natumbukiza kwenye sanduku namalizana na Mungu, wala neno lake kuitamkia sadaka sio issue kwangu na nitapata matokeo yangu.
Fahamu sadaka zilizompendeza Mungu
- Sadaka ya Abeli (Mwanzo 4: 2- 5)
- Sadaka ya Ibrahim (Mwanzo 12)
- Sadaka ya Nuhu(Mwanzo 8: 20 )
- Sadaka ya Musa(Kutoka 12)
- Sadaka ya Kristo(Injili zote nne(4)).
Mpendwa hizi sadaka maarufu tu, ila zipo nyingi sana kwenye maandiko na kuna watu wengi waliotoa sadaka zika mpendeza Mungu kama Isaka, Yakobo, Ayubu, Samweli, Daudi, Solomoni, Mitume , n.k..etc. Mpendwa pitia Biblia na Usome.
Je nitakuwa na uhakika ganiu kama sadaka yangu itajibiwa?
Habari njema kuna agano kabisa Mungu ameliachilia juu ya kujibu sadaka zinazompendeza. Na pia kuna maandiko mengi Mungu amejicommit further hivyo ni uhakika na kweli kabisa kuwa ukifanya sehemu yako lazima Mungu afanye yake pia.
Complicated Fact
Mungu amejicomit mno kwenye suala la sadaka lakini cha kushangaza hakuna sehemu amejicomit juu ya kufunga na kuomba. hakuna sehemu amejicomit kuwa mkifunga na kuomba lazima atafanya A,B,C! kama Password ya ucumi sio kufunga na kuomba.Hakuna mtu aliyetajirika kwa kufunga na kuomba. Hivyo mpendwa wale wa nafunga sana, na kesha sana natumaini mmepata majibu hizo so funguo au pasword za lango hilo mnaloangaika kulifungua. Achilia Sadaka Dada.
Agano au Convenant ni nini?
Ni deal au makubaliano yanayojibainisha kwa kina sana kuhusu vitu abavyo pande zote mbili zimeridhia na kukubaliana. Mpendwa kama una agano maana yake ni upande mmoja utawajibika endapo tu upande mwingine utatimiza makubaliano yaani ikiwa na maana Upande A usipotimiza makubaliano automatically upande B hautowajibika na agano, na ili Upande B uweze kuwajibika lazima upande A awajibike.
Maandiko ya agano la Mungu juu ya Sadaka inayoleta matokeo
Mwanzo 8 : 21 – 22
“21. Bwana akaipata harufu ya ile harufu ya upendelevu, Bwana akasema moyoni mwake, Sitawalaani tena nchi kwa ajili ya mwanadamu, maana shingo za mwanadamu zinaovu tangu utoto wake; wala sitakapoua tena kila kilicho hai, kama nilivyofanya. 22. Mchana na usiku havitakoma, kutoa mavuno wala kuvuna, baridi na joto, hari na baridi, wakati wa hari hautakatika mpaka wakati wa kuvuna.”
Yeremia 33: 20 – 21
“20. Bwana asema hivi, Kama ninyi mtaweza kuyavunja maagano yangu ya mchana na usiku, hata mchana na usiku visikome, 21. ndipo na agano langu na mtumishi wangu Daudi litakapovunjika, hata asiwe na mwanaume aitwaye mfalme katika kiti chake, na kwa ajili ya Walawi makuhani wangu wasiositawi kwa kuhudumu mbele zangu.”
Kumbukumbu la Torati 28 : 11
“Bwana atakufanya uwe na neema nyingi katika hazina zako, katika matunda ya tumbo lako, katika wazao wa wanyama wako, na katika mavuno ya ardhi yako, katika nchi ambayo Bwana aliwaapia baba zako kwamba atakupa.”
Mithali 11: 25
Nafsi ya mtu mkarimu itastawishwa, anyweshaye atanyweshwa mwenyewe.
Mwanzo 22: 16 BHN
Akamwambia,”Mwenyezi Mungu asema hivi: Nimeapa kwa nafsi yangukwamba kwa kuwa amefanya hivi, wala hukuninyima mwanao wa pekee hakika nitakubariki na wazawa wako nitawazidisha kama nyota za mbinguni na kama mchanga ufukweni mwa bahari, Wazawa wao wataimiliki miji ya adui zako.
Wafilipi 4 : 18 – 20
“18. Nimekwishapokea malipo yangu yote ya ziada. Sasa ninavyo vitu tele kwa sababu Epafrodita amekwisha niletea zawadi zenu. Hakika zawadi hizi ni matoleo yenye harufu nzuri ya manukato inayokubaliwa na kumpendeza Mungu.19. Na Mungu atawapeni ninyi kila kitu mnachohitaji kwa kadri ya Utajiri wake mtukufu katika Kristo Yesu.
Malaki 3: 10
Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema BWANA wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni na kuwamwagieni baraka hata isiwepo nafasi ya kutosha au laah.
Maandiko haya chimbuko lake ni Mwanzo 8 : 20 ambapo Muhu anamtolea Mungu sadaka na Mungu anaweka AGANO. Kwenye AGANO anazungumzia kanuni ( peinciple) ya kupanda mbedu na kuvuna. Na anakuja kusisitiza kwenye Yeremia kuwa agano lako hatolivunja.
Je sadaka yako unapanda mbegu kwa Mungu? na kama hupandi kwa Mungu unategemea kuvuna kwa msingi gani labda?.na kama Muda wa kupanda mbegu unazugazuga hupandi, utavunaje? Ndio maana unaomba sana lakini Mingu zikiangalia hazioni ulichokipanda.
Mpendwa unaweza ukaona msimu wa mahusiano yako haupo kabisa sababu haujapandwa au ulikaushwa na makosa ya Bibi na katika hili jambo la msingi ni kupanda mbegu na Mungu ya mahusiano bora.(Hapa uwe umekamilisha Toba, deliverance na Maombi ya mtu sahihi.)So ukipanda hakika inakuwa mbegu bora. Na Mungu ni mwaminifu utavuna msimu sahihi. Hata ukijipumzisha ni sawa kwani kuna agano la kupanda na kuvuna, Wewe umepanda tayari kinaxhobakia ni mavuno.
Uchumi , kazi ,Promotion hiyo misimu kama haipo kwenye maisha yako inatakiwa ipandwe katika agano hili.Na baada ya hapo unamwagilia maombi na kungoja kuvuna.Hujapanda halafu unangoja kuvuna kivipi? kuwa serious na maisha yako.
Ukame wa uzazi
Panda mbegu na ufalme wa mbingu ya msimu mpya wa uzao ulio bora. Mbegu bora inaleta mavuno bora. Kama kuna kitu hakipo maishani mwako maana yake ni kuwa hakijapandwa sasa utavuna vipi ilihali hakijapandwa. Mpendwa AGANO lipo ila wewe tu ndio unayumbayumba.
1 wakorintho 15: 43
“Unapandwa katika aibu, unafufuliwa katika utukufu, unapandwa katika udhaifu unafufuliwa katika nguvu.
Hvyo ni kweli unaweza panda mbegu ya kuuwa msimu wako wa machungu, Msimu wa kutokuokolewa, Msimu wa kutokupata kazi, Msimu wa kuwa Tasa, Msimu wa Divorce. Na kuomba Mungu akuletee msimu mpya utakapo vuna.
Zaburi 126: 5 – 6
Wanaopanda kwa machozi, watavuna kwa shangwe, wanokwenda kupanda mbegu wakilia, watarudi kwa furaha wakichukua mavuno.
Watu wengi tunamchukulia Mungu katika urahisi hii ni hata kwangu kwani nilikuwa na tabia hii pia. Nilikuwa nikiwaza kuwa Mungu ni muelewa na mwenye amani sana lakini Pator ndiyo anacomplicate na kutwist mambo. Sio kwamba sitoi sadaka wala sina nia mpaka siku niliyokuja kutuliza kichwa kwenye haya maandiko.
1 Wafalme 17 : 10 -12
Basi, Elia akaondoka, akaenda Sarefathi na alipofika kwenye lango la mji alimkuta mwanamke mmoja mjane anaokota kuni. Elia akamwita mwanamke uyo na kumwambia “Niletee maji ninywe”. 11. Yule mwanamke alipokuwa anaondoka, Elia akamwita tena na kumwambia,”Niletee kipande cha mkate pia”. 12. Huyo mwanamke akamwambia,”Nakuapia kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mungu wako aliyehai sian mkate hata kidogo. Nilichonacho ni konzi ya unga katika chungu na mafuta kidogo katika chupa.Nimefika hapa kuokota kuni, kisha niende nyumbani kupika chakula hiko, mwanangu na mimi tule kisha tufe”.
Mpendwa mwanamke huyu alikuwa na hali mbaya sana na katika historia ya mtu aliyekuwa hana cha kuto akabisa mwanamke huyu alivunja rekodi. kwanza ni mjane,pili ni mwanamke asiye na kitu na aliye na uchungu kuhusu mwanaye, mpaka anajiapiza. Je Biblia inasema aliambiwa sawa njaa ikiisha utatoa tu??, Sasa kama mjane huyu akuwa exempted au kuondolewa katika agano hili wewe unaanzaje kujiondoa? Mpendwa makinika. Angalia Elia anachomjibu baada ya kujiapiza.
Elia akamwambia, ” Usiogope.Nenda ukafanye kama ulivyosema. Lakini nitengenezee mimi kwanza na kuniletea andazi dogo, kisha jitengenezee wewe na wanao chakula. Wapendwa ninavyowaambia Mungu yuko serious na agano hili naomba mzingatie. Jaribu kufikiri wewe ndiye yule mama! Sawa Elia ndio mmekutana, kwanza yule mama hakuwa mu-israeli useme anajua mambo ya Mungu na Musa, alikuwa Msidoni.Huenda kasikia kwa mbali Mungu wa Israeli ni hatari. Kweli ndiyo ajicommit kwa huyu mgeni anyesema ni nabii wake jumla tu hivyo na kujiapiza mbele ya Mbingu na Dunia na anaambiwa na Nabii wa Mungu kwanza atie suna alafu kitakachobakia ndiyo utakula wewe na wanao,Ungeweza???
Tunaona yule mama aliweza kutii na ule unga na mafuta havikuweza kuisha mpaka njaa ikaisha. Ila kanuni ni ileile, Mwanamke alianza ndiyo Mbingu zikafata.
Tuendelee kwa Ibeahimu Mtoto mmoja na wapekee, alafu Mungu anataka huyo huyo ikiwa ni wakati wake wa uzeeni. Je unadhani alikuwa hamuwazi Sara Mkewe? Unadhani changamoto hiyo ingekuwaje? Na ujiulize kati ya wewe na Ibrahimu nani hana zaidi ya mwenzie?.
Ukija kwa Elia na Manabii wa Baali.Baada ya kuona Baali yupo kimya na muda unaendelea kwenda mbele wakaanza kujikata visu wampatie sadaka ya damu zao.Na wale mpendwa ni wapagani lakini wanajiongeza kwani asiyepata kitu hapati kitu.Iko hivyo Simple and Clear.
1 Wafalme 18 : 28
Manabii hao wakapiga kelele zaidi, wakaji katakata kwa visu na simi, kufuatana na desturi yao, hata wakabubujika damu.
Basi mlihisi nimetunga ukweli hauwezi kuwa mchungu hivyo.ukweli ndiyo huo hata ukimbilie upande wa pili hali ndiyo hiyo.Tena kwa mganga ndio gharama utayotoa ni kubwa zaidi. Nafuu upande mbegu kwa Mungu wetu wa uhakika, Yehova Shaloom! Adona! Yupo ambaye yupo.
2 Wafalme 3: 26 – 27
“26. Bali mfalme wa Moabu alipoona ya kuwa kushindwa kwake kulikuwa kubwa mno, akachukua pamoja naye watu sabini atikilie upande wa pili wa mfalme wa Edomu. 27. Ndipo akatoa mwanawe wa kwanza, aliyekuwa atawalaye badala yake, akamtolea sadaka kwa kuteketezwa juu ya ukuta. Kukawa na ghadhabu kubwa juu ya Israeli; basi wakatoka kwake, wakarudi nchi yao.”
Huyu alikuwa mfalme wa Moabu, alikuwa ameshapigwa vitani. Akakumbuka sadaka ina nguvu ya kutikisa Miungu ya Kimoabu imsaidie abakie kwenye utawala wake hivyo akamchinja mtoto wake na kumtundika kwenye ukuta wa jiji . Tunaona waisraeli wanaghairi kumtoa madarakani siku hiyo na kurudi kwao. Hivyo miungu yake ilipokea sadaka yake na hii itufahamishe kuwa ukiwa unajipeleka kwa mganga suala la sadaka liko palepale,ila aina tu ndiyo tofauti na kama huna haupati chochote. Hakuna cha bure ni kufanya sehemu yako naye afanye sehemu yake.
2 Mambo ya Nyakati 33:6
6 Pia aliwatoa wanawe kama sadaka ya kuteketeza katika bonde la mwana wa Hinomu. aliiga ramli, alibashiri na kutumia hirizi, hata alishirikiana na waaguzi wa mizimu na wachawi,Alitenda maovumengi mbele ya Mwenyezi-Mungu, akamkasirisha.Wapendwa huyu ndiye alikuwa kiboko ya wachawi,Mfalme Manaseh wa Yuda. Katika uchawi sadaka ni kama kawaida tena ni kubwa.Wembe ni ule ule Panda uvune,Jiongeze tukusaidie.
Yohana 3: 16 – 17
Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe wa pekee, ili kila mtu amwaminiye asipokee,bali awe na uzima wa milele. Maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili akauhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika wewe.
Wapendwa Mungu mwenyewe katoa Sadaka kubwa abisa kwa jinsi alivyoupenda ulimwengu. Sasa kama Mungu mwenyewe Yeshovanisi! Adona!, Alfa na Omega katoa sadaka wewe ni nani usitoe? Makinika.