Prosperity

 

Biblia  inatoa miongozo, kanuni na mafundisho  kuhusu ustawi au mafanikio (prosperity) katika nyanja mbalimbali kwenye maisha.Tujifunze kwa pamoja kuhusu mafundisho haya:

Msingi Mkuu Mmoja wa Prosperity

Kumbukumbu la Torati 8: 18

Bali utamkumbuka BWANA Mungu wako, maana ndiye akupaye nguvu za kupata utajiri, ili alifanye agano lake alilowapa baba zako, kama hivi leo.

Kuna utajiri wa aina nyingi lakini tutazingatia utajiri wa pesa na uchumi.Mpendwa huwezi kutajirika kwa kulia kwa uchungu usiku kwenye Maombi yako. Aidha huwezi kupata kazi kwa kulia au kusikitika kwa uchungu. Lia kwa kiasi unachoweza lakini kanuni za kiuchumi za ulimwengu wa roho hazitikiswi na hilo na kadri unavyo lia ndio kwa kiwango hicho hicho hakuna chochote kitakachofanyika, huo mzunguko wa tupu ( cycle of nothing) haiishi.

Mpendwa Uchumi ni hali halisi hivyo inakubidi ujitahidi kuwa halisi kuhusu malengo yako au kuweza kuyafikia malengo yako, Jitahidi kuzikimbia hisia na mawazo ya kufikiria. Hata katika Biblia neno linasema Mungu atakupa nguvu za kupata utajiri, Neno kuu ni NGUVU ikiwa ina maana Utajiri hapa haukuwa katika ngazi ya matokeo, hivyo katika hizi nguvu kuna matendo inabidi uyafanye ilizifanye mwendo.

Mpendwa Pesa zote ziwe za madafu, ziwe Dolla , Euro, Faranga, Lira, Real, Rand au etc zote zipo hapa duniani, Mbinguni au katika ulimwengu wa kiroho hakuna kitu kama hiko,Hivyo unachokitafuta tayari kipo duniani ni kufanya mchakato kija upande wako ikiwa na maana changamoto hapa ni mzunguko ukufikie wewe.

Kwanini Pesa hazikufikii? Huenda sababu umeshaiambia akili yako kwenye gereza kwamba pesa kufika kwako ni ngumu.Akili yako inakwambia umelaaniwa, una mikosi, huna bahati au umefungwa na umaskini. Huenda akili yako inawaza kufeli muda wote, na kama nilivyo waambia katika mafundisho ya Gereza chochote kinachokaa kwenye akili yako kwa muda mrefu kitathibitika. Hata kazini wewe ni bora kwa boss wako mara 10, Unafanya wewe kazi zote, Boss anasimamia na unapata mshahara mnono ila marupurupu mpaka jasho likutoke. Boss anahakikisha unajua kuwa jina lako haliwezi kuwa Boss ilihali yupo, na hata akiondoka shetani anamtumia kuhakikisha kuwa huwezi kuwa boss pia. Devil is a master of fresh relim.

Henda umewaza sana, umeomba, umetoa sadaka zako, umekuwa mtiifu hujatumia shirki, unajipa moyo kila siku kuwa ipo siku Mungu atakupa kitabu cha kumbukumbu juu ya mwenendo wako kazini au kwenye biashara na atakufidi lakini hii imekuwa njia ndefu sana ambayo unawez kuja kupata cheo chako hata katika miaka ya uzee. Mpendwa ukielewa Kanuni za Prosperity kwenye spiritula relim utaweza kuongoza matokeo yako mwenyewe kwa msaada wa Mungu.Utapata matokeo haraka na utakula ujana wako kikamilifu katika wingi wa raha na mafanikio.

Kanuni za Prosperity

  1. Akili safi na makini muda wote juu ya malengo yako ya kiuchumi.Mpendwa Lengo lako ni nini? Je ni kutafuta kazi? Weka lengo lako halisi! jiwekee muda wa mwisho (deadline), Mfano mwezi huu lazima nipate kazi, kwa kuwa na uhakika na imani na Mungu unayemtumikia, hakuna KAMA wala LAKINI. Hakuna vijisababu kama ” Ooh Serikali haiajiri au kozi niliyosomea haina soko. Mungu yupo enzini kukamilisha ulipo pwaya hivyo weka lengo na weka tarehe ya mwisho. Kama ni Biashara weka lengo kila mwezi unataka ufikie mauzo kiasi gani na kuwa na uhalisia ukizingatia kama dukani hapo una mzigo unaoweza kukuzalishia faida ya kiasi hicho unachotegemea, kama uko kazini weka lengo kuwa mwaka huu lazima uwe Mkurugezi au Team Leader.

Mpendwa Mungu kagawa bahari ya shamu na watu wakapata kupita itakuwa wewe kupata kazi au kuuza dukani kwako, Hapana mpatie Mungu sifa. Ukifanya hilo uwe na uhakika 100% kukata mawazo yote hasi, jitahidi hata mara moja kuwa na mawazo chanya kuhusu kazi yako , promotion na biashara, ukiona ile hali ya uhasi inakupigia hodi kumbuka watu wakidhuhudia bila wewe itakuwa jambo la aibu kwako bora ujikaze na upambane, Jitahidi uwe na roho shupavu sana kwani hata wenye hela hawataki wewe upate hivyo ni lazima na wewe uwe makini na upambane, hakikisha hauachi hisia zikuongoze bali uhalisia tu na kumbuka una mtumikia Mungu muweza wa yote.

Day 1 : Prosperity

2 Wathesalonike 3 : 10

Kwa kuwa hata wakati ule tulikuwapo kwenu tuliwaangazia neno hili, kwamba ikiwa mtu hataki kufanya kazi basi asile chakula.

Baba yetu uliye mbinguni, watu wako  wako tayari kufanya kazi, sawa sawa na andiko lako lakini Bado kazi hazipatikani na zilizo patikana hazina masilahi, Baba kazi zisipo patikana watu wako watakula nini? Mungu fungua mlango wa kazi, biashara na mafanikio.

Zaburi 90: 17

Na fadhili zako BWANA Mungu wetu, ziwe juu yetu, Na kazi ya mikono yetu na uifanye thabiti, Naam kazi ya mikono yetu uifanikishe.

Waebrania 1:9

“Wewe wapenda uadilifu na kuchukia uovu. Ndiyo maana Mungu, Mungu wako amekuwekea wakfu na kukumiminia furaha kubwa kuliko wenzako”

Hebrews 1:9

You have loved righteosness and hated wickedness, therefore God has annointed you with the oil of gladness beyond your companions

Kwa kuwa umeutambua wema na uovu, umekombolewa na Yesu kristo uwe unajua au hujui, ni kuwa kuwa ORDAINED mbele za Mungu kupata zaidi ya wenzio ambao hawajaokoka. Sasa tumia hili agano kumkumbusha Mungu juu ya habari ya Kazi au Biashara yako.

Mpendwa simama na Zaburi ya 90: 17 umsihi Mungu kazi ya mikono yako aifanye thabiti na aithibitishe, msihi wakati ni sasa.Mungu wetu ni mkubwa sana atakutendea. Achana na nini kilijiri huko nyuma! Zingatia hoja hii iliyooko katika maandiko haya ambayo inahimiza kumsihi Mungu akupe hiyo nafasi , huenda huko nyuma hukuwa na hoja ya msingi lakini lakini hivi sasa hoja unayo kilichobaki ni kuinua imani pekee, simama na mstari huu wa Zaburi.

Mpendwa kesho tunahamia upande wa uhalisia (vitendo) kwani hivisasa upande wa kiroho tumemealiza. Yesu Kristo aliwaagiza mitume 12, ilikuwa ni siku moja na kwa wakati mmoja, lakini wanne (4) tu kati yao ndio wanasikia na kuitenda kazi waliyo agizwa na kuacha alama kubwa katika ukristo. Hivyo upako pekeyake hautosh kuweka alama kwenye maisha ya kazi.

Day 2: Prosperity

Leo tumemsihi Mungu afanye annointing juu yetu na atu ordain mbele ya wengine kwenye habari ya uchumi  na kazi.Sasa wengi huwa baada ya annointing (upako) huwa tunapumzika na kuiacha annointing (upako) uweze kutenda kazi kwa niaba yetu peke yake na hii ndio sababu wengi tunaanguka kanisani, tunashukiwa na Roho Mtakatifu na kunena hadi kwa lugha katika habari ya kazi na uchumi lakini baada ya hapo kunakuwa kimya.

Mpendwa annointing ( upako) huwa inakujaza nguvu na kukuongezea uwezo wakufanya yale ambayo kwa nguvu ya kawaida usingeweza hivyo inatupasa kuitumia nafasi hiyo vizuri sana, kwani wakati ni huu. Kama ulikuwa unaomba kazi kumi (10) kwa siku sasa jaribu kuomba kazi thelathini kwa siku utashangaa huchoki kabisa, Mpaka utasema naacha sio kwa sababu nimechoka ila nimeridhika. Hata ubora wa kazi unazoziomba pandisha juu kwani umeshapewa gate-pass na usipoamua kupita getini ni wewe tu.Mpendwa annointing (upako) hauto-ondoa ugumu wa hali bali utajaza nguvu kuu.

Utakuwa na ujasiri wa juu sana kuvuka vitu vilivyokufanya mateka maisha yako yote, Ile hofu ya mahojiano ya kazi ( Interview) na Annointing ( upako) hautafanya interview kuwa rahisi bali ule uelewa wako wa maswali utakuwa juu, kumbukumbu yako na utajihisi kuwa juu ya kila kitu hadi utaanza kuwaza huko nyuma ulikuwa unafeli wako.

Malaki 3 : 16 – 17

Ndipo wale waliomcha bwana waliposemezana wao kwa wao, Naye BWANA akasikiliza, akasikia na kitabu cha ukumbusho kikaandikwa mbele zake, kwa ajili ya hao waliomcha BWANA na kulitafakari jina lake. Malaki 3 : 17; Nao watakuwa wangu, asema BWANA wa majeshi katika siku ile niifaayo, naam watakuwa hazina yangu hasa nami nitawaachilia kama vile mtu amwachiliavyo mwanaye pekee amtumikiaye.

Kuna kitabu cha kumbuumbu ( Book of remembrance) ukisoma katika andiko hili kwenye English Bible utalifurahia zaidi. Ila jambo kuu la msingi ni kujua kuwa kuna kitabu cha kumbukumbu ambacho Mungu hukiitisha na kuwapatia haki waliocheleweshewa.Mpendwa sasa simama na andiko hili msihi Mungu kuhusu habari ya Kazi ulizoomba. Kuwa na msimamo wako mkuu na taja aina ya hizo kazi, Taja tarehe ulizoomba na nafasi ulizoomba. Msihi Mungu afungue kitabu cha kumbukumbu upatiwe haki yako sasa hivi kwani umepakwa mafuta.

Kama upo kazini upako (annointing) ikupe nguvu ya kufanya zaidi ili upandishwa ngazi au cheo. Kama huwezi kuongea kwenye kikao anza kuongea kwa rasha na kujiamini  na kama zamani walikuwa wana kushusha sasahivi wakupigie makofi. Mpendwa ili upako (annointing) yako ifanye kazi lazima uamini na uitumie. Lazima uamini na uitumie laasivyo itakufa kifo halisi na pia utambue kuwa unavyozidi kuw na imani ndivyo inavyozidi kukua na kujithibitisha ndani yako.

Yesu ali-annoint mitume 12, Na tutambue kuwa Yesu  ni Mwana wa Mungu na Mitume ni highest level of ordaination ilio-wahi kufanyika katka historia ya dunia. Maana mitume walikuwa ordained by ht son of God himself na ilifanyika kwa wote katika siku moja, wakati mmoja na Mungu yule yule.

Lakini baada ya Yesu kupaa mbinguni, anasikika mitume wanne (4) tu. Vipi kuhusu wale wengine saba (7) maana Judas Eskariot alifariki.Nini kilfanyika juu ya annointing yao? Kwanini hawasikiki  tena?, Kwanini hwajaacha alama yoyote kwenye injili na wanaosikika ni Petro, Yakobo, Yohana na Mathayo na wengine wanatajwa kidogo sana. Hivyo wapendwa katika hili tunaona kuwa suala sio aina ya annointing (upako) ila ni jinsi gani wewe nautumia upako wako.Leo Mungu ame wa-annoint  ( amewapaka mafuta) wote kwa andiko moja, tumia hio annointing (upako) kumfanya Mungu ajivunie kuhusu wewe katika maisha yako.

Mitume baada ya Yesu kuwa-annoint (kuwapaka mafuta), Watu walio wa-annoint (wapaka mafuta) wao kama wao walifanya vizuri sana mfano mkubwa tunauona kwa Paulo na Sila, walifanya vizuri sana kwani pamoja na annointing ( upako) walifungwa jela, walipigwa mawe, walipata kila aina ya kadhia lakini hawakuitilia shaka annointing yao, hawakurudi nyuma au kusubiri kwanza.

Hivyo Mpendwa sitegemei kwa siku hizi mbili (2) amabazo hujapata kazi utaanza kurudi nyuma , kusubiri kwanza na kujiuliza hivi Binti Mlokole sini street pastor tu Yule ?????, sasa naamini vipi annointing yake?, Mpendwa wewe umemuomba Mungu aliyejuu mbinguni na hata mara moja usithubutu kurudi nyuma kwenye gereza lako la kukosa kazi.

Mpendwa Mitume na Manabii pia walipitia magumu lakini hawakujiendekeza na kurudi nyuma no matter what!! na kiufupi Mitume wengi waliuawa kwa kueneza injili  unayosali sasahivi , hivyo unavyokuwa unacheka cheka na shetani hawakuelewi kabisa.

Nabii Isaya inasadikika aliuawa na Mfalme Manase. Nabii Yeremia pia aliuawa.Yohana Mbatizaji alikatwa kichwa, Elia alinusurika kuuawa na Jezebel.

Petro mtume alisurubiwa Roma   huko na Warumi kichwa chini miguu juu. Yakobo alikuwa wa kwanza kuuawa na mfalme Herode kwa upanga.(Matendo 12).Yohana aliteseka sana na mwisho kuuawa huko Efeso. Andrea na Philipo waliuawa vitu hivi vip na ni ukweli kabisa.Paulo alichinjwa huko Roma karibia mda mmoja na Petro. Mpendwa focus sio masikitiko na uchungu wa kilichowakuta.Focus ni how serious were these people kwenye kazi waliyokuwa annointed nayo.

Death was always a posibility kwenye kazi ya utume.Mana mwana wa Mungu tu walimsurubu kweupe. Hivyo walijua hatari iliyokuwepo ila annointing iliwatia nguvu ya ajabu kutembea katikati ya moto na kuutazama mmoto uso kwa uso. Annointing iliwabadilidha kabisa wakawa wapya.

Hivyo wewe baada ya leo usitazame zamani yako, usijali umefeli mara ngapi,umekaa nyumbani muda gani, umekuwa bure ofisini mara ngapi, None of all matters any more. Na usiruhusu ikudefine.

Mpendwa kuanzia leo umekuwa annointed by God himself kufanya kazi aliyokukusudia.Na ukaifanye kwa ukubwa sana mpaka wamuone Mungu kupitia wewe na Ukipata changamoto usirudi kwenye before annointing, anzia hapohapo kwenye annointing , na Mungu akuongezee Nguvu. Now you are endorsed by the heavens, yo will be reporting to the heavens.

Hata kama upo kwenye interview unaona maombi hayaeleweki call the heavens.Usipaniki na kurudi nyuma kwa kujiona kuwa huna lolote, mpendwa umevuka ngazi hiyo.Ziite mbingu zikutetee.

Ukikaa waza ni kazi gani unataka ufanye na utaifanya vipi. Mpendwa ita hiyo kazi,iamuru ije mapema! Put the annointing into practice. Mwanzo utakuwa unatetemeka, Baadaye utazoea, Omba kwa kusema kwa mamlaka niliyopewa na Mungu Baba Mwenyezi nakuamuru HR wa TBL uniite interview this week kama Mungu aishivyo. Una declare siku ya 1,2,3 hadi ya 4 , unapigiwa simu na kuambiwa sisi ni TBL Tunakuomba uweze kufika kwenye interview.

Mpendwa acha kulia na kudeka bali shinda una command ( amuru) mambo yafanyike, tengeneza mambo kwenye ulimwengu wa kiroho. Na mambo yataanza kujithibitisha na kutokea kwa ukubwa sana, mpendwa mambo makubwa yanahitaji imani kubwa sana.

Day 3: Prosperity

Heaven Introduction

Luka 9 : 35

Sauti inatoka kwenye lile wingu ikasema “Huyu ni Mwanangu mpendwa, niliyemchagua, Msikieni yeye”

Unaweza pia kutumia Marko 9:7, Mathayo 17: 5, Mathayo 3: 17.

Msihi Mungu akufanyie  introduction kwenye harakati zako. Yeye ndio akaitambulishe annointing yako. Ukiwa serious na ukafanya maandalizi yako ipasavyo and if you live to the expectation God will introduce you.

Jesus was the son of God! Yeye kam yeye alikuwa very powerfull! Yet still God introduced him as his son.Twice actually!! Mara ya kwanza ilikuwa  wakati anabatizwa na mara ya pili ilikuwa wakati alipokuwa anatransfigure (akigeuza sura) akiwa na Musa na Elia.

Mathayo 17 : 5 – 6

5 Petro alipokuwa bado akizungumza ghafla wingu linalong’aa likatanda juu yao na sauti ikatoka kwenye wingu hilo ikasema ” Huyu ni mwanangu mpendwa, ambaye nimependezwa naye: msikilizeni yeye”.6 Wanafunzi waliposikia haya walianguka chini kifudi fudi wakajawa na hofu.Ukitaka kufaidi anza na Mathayo 17 : 1 – 9! utafaidi mkasa mzima. Hio mara ya pili Mungu anamtambulisha Yesu  kuwa ni mwanawe mpendwa hivyo asikilizwe.

Hivyo Mungu anaweza akakutambulisha popote pale uunapohitaji na endapo akikutambulisha uweze kusikilizwa ni LAZIMA utasikilizwa, na ukiona watu hawakusikii wala hawakusomi basi tambua kuwa unahitaji kutambulishw vyema. Mpendwa simama na mistari hio miwili msihi babab yako wa mbinguni akufanyie utambulisho yeye mwenyewe. Iwe kwenye interview, Business deals, ukweni hata popote pale deal na baba yako wa mbinguni.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Scroll to Top
× IT Help Desk