Prayers to be found by your Husband ( Maombi ya Kupatwa na Mumeo)

Mpendwa programu hii inahusu mfungo wa siku tatu (3) ,wenye kulenga katika kuachiliwa kwa ndoa kwa wale ambao hawajaolewa,Maritual Breakthrough, kuondoa Marital Delay na kuondoa vikwazo na changamoto katika ndoa, usikose mfungo huu ni muhimu sana.

“Noah alianza kujenga Safina kabla hata tone la Mvua halijaanza wala wingu halijakuwepo, fanya ibada wakati mambo yako shawari.”

Maombi ya Ufunguzi wa Program

Baba tunakushukuru na kukukaribisha katika katika Programu hii.Tunakushukuru kwa uwepo wako, uongozi na matokeo, tunakushukuru kwa upako wako,marital breakthrough na ndoa zitakazo achiliwa mbinguni kutokana na programu hii na kuthibitika duniani.Tunakushukuru kwa kuwaunganisha wanao na wenza wao na tunakushukuru kwa kuwa Marital Delay halitakuwa fungu lao tena.

Baba tunasali na kuomba huku tukiwa tumefunikwa na damu ya Yesu na uwepo wa Roho Mtakatifu.Tumejifunga Mkanda wa ukweli mbinguni, tumejivika Mkanda wa haki, ngao ya wokovu iko mikononi kwa jina la Yesu.Tumejivika viatu vya amani ya Bwana wetu Yesu Kristo, tukishika upanga wa neno la Mungu upenyao kokote in the might name of Jesus (Kwa jina kuu la Yesu).

Mathayo 21:22

” Na mkiwa na imani, chochote mtakachoomba kwa sala, mtapata”

Sala

Baba ninaomba neema ya kuamini kwamba Ndoa yangu itakuja kuthibitika duniani.Ninaomba neema ya kuamini kwamba umeshanitendea na imeshafanyika hivyo ni suala la muda tu.Baba ninaomba imani ya kupokea maombi ya kuolewa na mtu sahihi kwako na aliye pendo lako.

Chochote kinachonizua kupokea kile ulichokiandaa katika suala la ndoa nakiondoa kwa nguvu ya upanga wako wa kiroho kwa jina la Yesu.Baba nina decree na kudeclare chochote kinachozuia ndoa yangu na kunizuia kukutana na mwenza wangu kuondolewa kwa upanga wako wa kiroho katika jina la Yesu.

1.Grace to be found by your husband/Neema ya Kupatwa na Mume wako

Baba napokea imani ya kupatikana na mume wangu mtarajiwa kwa jina la Yesu.Roho yoyote ya kusita sita, wasiwasi na kukata tamaa itoke kwa nguvu iliyopo kwenye damu ya Yesu.Mashaka yoyote yale juu ya ndoa yangu yatoke sasa kwa damu ya Yesu.

Mashaka yoyote yatokanayo na maneno ya wazazi, unabii wa uongo, ndugu na mazingira yangu yatoke sasa kwa jina la yesu, Baba ninakataa kwa nguvu iliyopo ndani ya damu ya Yesu Kristo.

2.Grace to be found by man who will love you all 4 Pillars/ Neema ya kupatikana na mtu atakayekupenda katika hatua zote nne.

Baba ninaomba mwanaume ambaye atanipenda kama mke wake amaye nitavutiwa naye physically,emotionally (hisia),spiritually (kiroho) na sexually(Kimapenzi). katika jina la Yesu.Babab naweka ombi hili chini ya kiti chako cha enzi katika jina la Yesu.(Be specific  unataka nini). Baba ninaomba mwanaume amabaye nitampenda katika nguzo nne.Baba nakushukuru kwa kuwa imefanyika tayari.

3.Guide oh how to position yourself and game plan/ Muongozo wa namna ya kujipanga na kuweka mpango.

Baba niongoze jinsi  gani ya kujipanga na unipe hatua ambazo nikikutana naye mamabo yatakuwa mazuri.Lord I ask for guidance and details.Roho wako mtakatifu aongoze hatua zangu ili unabii usiniponyoke katiak jina la Yesu.Lord I ask for Strategy and Game Plan.Mungu niongoze nifanye yale Mtumwa wa Abrahamu aliyokuwa akiyatafuta kwa Rebeka.Babab nainuka kinyume na mambo yangu machafu yanayonikwamisha kwa jina la Yesu.Naenda kinyume na tabia yangu ya kiburi,dharau na majivuno, Nang’oa kwa jina la Yesu hazitanihukumu tena.Roho mtakatifu nioneshe njia mabayo mbingu inataka nipite kukutana na kupata kibali mbele ya Mume Mtarajiwa.Niongoze niwe wapi na nisiwe wapi,niongee nini na nisiongee nini.Baba naomba mwongozo jinsi ya kupatikana kwa mume mtarajiwa katika jina la Yesu.

3.Kumtenganisha na yeyote anaye kaimu nafasi yako kama mpenzi wake kwa sasa.

Baba ninaomba mwongozo wa jinsi gani utanikutanisha na mume wangu na nitapako kutana naye nijue kuwa ni yeye.Baba ninaomba kila mwanamke aliyeshikilia nafasi yangu kwa sasa kama mwenza wake asiye halali namg’oa kwa nguvu iliyopo katika damu ya Yesu na imefanyika kwa jina la Yesu.Roho yoyote ya Varshti iliyoshika nafasi yangu na kutuzuia tusikutane itoke kwa jina la Yesu.Baba nipeleke kwa mume wangu sasa na atambue kuwamimi ndiyo Esta wake na sio Varshti kwa jina la Yesu.

4.Muite Kiroho Popote alipo

Bbaba namuita mume wangu kokote alipo kwa nguvu iliyopo kwenye damu ya Yesu. Naomba chukue hatua za kuja kunitafuta kwa nguvu iliyopo katika damu ya Yesu.By the Power in the blood of Jesus I call my husband spirit forth.Icall him forth in the name of Jesus (Naita roho ya mume wangu katika jina la Yesu).Thank you Lord because it is done in the mighty name of Jesus (Asante Baba kwa kuwa imefanyika katika jina la Yesu).

Day 1 : Prayers to Be Found By Your Husband.

1.Roho zozote zilizoko ndani yako zinazozuia ndoa yako zitoke kwa nguvu ya damu ya Yesu.

Roho zozote chafu zilizo ndani yako zinazozuia ndoa yako zitoke kwa jina la Yesu ,Zitoke Sasa in the mighty name of Jesus.Roho za uzinzi, masterbation ( Punyeto), pornography ( Picha na Video za Utupu) na Roho zote chafu zitoke kwa jina la Yesu.Nguvuiliyopo kwenye damu ya Yesu ikomeshe sasa utumwa wako katika hizi roho kwa jina la Yesu. Roho zinazokuzuia usikutane na Mume wako zishindwe kwa damu ya Yesu na zikuachie huru sasa. Asante Yesu kwa kuwa sasa yametimia.

2. Any Impure Spirits ( Roho zote chafu ) nje ya mwili wako zinazozuia ndoa yako zishindwe kwa jina la Yesu.

Roho zozote zinazuia (Block) ndoa yako kufikia hatima yake zishindwe sasa kwa jina la Yesu. Roho za familia, Ukoo, Kurithi na Nguvu zozote za giza zinazozuia ndoa yako zishindwe kwa jina la Yesu. Damu ya Yesu ikutakase sasa na kunena uhuru wako.

Roho yoyote inayokukosesha amani na kukunyima subirs kwa habari ya ndoa, iondoke kwa jina la Yesu, Roho yoyote ya kughadhibika(Kupanic) na kulazimisha ndoa ziondoke sasa wa jina la Yesu. Roho ya kutokuwa na amani ( Spirit of Restlessness isinipileke kwa mume asiye mapenzi yako Baba kwa jina la Yesu.

Roho zozote zinazonioteza njia na kunipeleka kwa watu wasio sahihi au njia isiyo sahihi  katika kukutana na Mwenza wangu nakataa kwa mamlaka  ya nguvu iliyoko katika damu ya Yesu.

3.Roho zozote zinazo mpoteza Mumeo mtarajiwa zitoke sasa kwa jina la Yesu.

Roho zozote zinazo mchelewesha na kumkwamisha mumeo mtarajiwa popote alipo zishindwe sasa kwa jina la Yesu.Roho zozote zinazo mzima mwenza wako kuja kwako na kuunganisha hatima zenu ziteketee kwa moto wa Roho Mtakatifu sasa.Damu ya Yesu inene habari ya uhuru wake sasa kwa habari ya kuja kwako kukamilisha hatima ya ndoa katika jina la Yesu lenye nguvu.

4.Sehemu yoyote ya maisha yangu amabayo haieleweki inyooshe sasa.

Baba mimi ni hekalu lako, nyoosha maeneo yote ambayo nakosea na hayapo katika namna unayohitaji. Yanyooshe sasa Baba.Babab nyoosha mambo yote ambayo hayaja kaa sawa na yanachelewesha hatima zetu kati yangu na Mume mtarajiwa yaweze kukamilika katika jina la Yesu.

5.Sitakuwa Mtumwa wa masharti ya Roho chafu (impure spirits) katika jina la Yesu.

Baba ndoa yangu haitakuwa na masharti kwa jina la Yesu.By the power in the blood of Jesus I revoke all conditions that delay my Marriage.Nabatilisha masharti yote ya nguvu za giza kwa habari ya ndoa yangu.Kwa damu ya Yesu nakataa masharti ya ukoo kuolewa nikiwa mzee, kuchelewa kuzaa, kuto-olewa, kuolewa na maskini na masharti yote yasiyo na tija nayakataa kwa jina la Yesu.Nitaolewa chini ya agano la Damu ya Yesu.Ndoa yangu haitapigwa muhuri wowote wa nguvu za giza katika jina la Yesu.

6.Dhambi zozote za Baba zetu zinazosimama kinyume changu na kinyume cha mwenza wangu zisamehewe kwa Damu ya Yesu.

Baba naomba unisamehe dhambi za baba na babu zetu zinazosimamam kinyume na sisi.Neno lako linasema hatoshitakiwa kwa dhambi za  Baba yake wala Mzazi kwa dhami za Wana wake.Baba yetu uketiye mahali pa juu tusamehe kwa dhambi hizi na uturejeshee furaha yetu.Baba ninashukuru kwa kuniunganisha na Mwenza wangu. Father I thank you in the Mighty name of Jesus.

Marko 5:6-13

“6 Alipomwona Yesu kutoka mbali, alikimbia, akaanguka mbele yake, 7 akalia kwa sauti kuu, na kusema, Unataka nini kwangu, Yesu, Mwana wa Mungu aliye juu? Nakutolea kiapo kwa Mungu, usinitese. 8 Maana alikuwa amemwambia, Toka kwa mtu, roho mchafu. 9 Yesu akamwuliza, Jina lako nani? Akajibu, Jina langu ni Jeshi, kwa maana tuko wengi. 10 Akamwomba sana asiwatume nje ya nchi ile. 11 Basi, kulikuwa na kundi kubwa la nguruwe karibu naye, wakilisha. 12 Hao pepo wakamwomba, wakisema, Tupe ruhusa tukuingie nguruwe. 13 Akawaruhusu mara. Wale pepo wakatoka, wakaingia katika nguruwe; na lile kundi likapiga mbio, likaingia kwenye ziwa, walikuwa wapatao elfu mbili, wakafa majini.”

Baba kila roho chafu ndani ya maisha yangu naijibu kwa uwepo wako katika maisha yangu kwa jina la Yesu.Jeshi la roho chafu lilitetemeka kwa uwepo wa Yesu eneo lile.Roho zote chafu kwenye maisha yangu toka sasa kwa mwanga wa YesuNafunika mazingira yangu kwa moto wa Roho Mtakatifu.Roho zote za kufisha toka sasa kwenye maisha yangu kwa jina la Yesu.Baba nalitoa jeshi lote la roho chhafu nje ya maisha yangu kwa jina la Yesu.

Yohana 10:10

Mwizi huja tu kuiba, kuua na kuharibu;Mimi nilikuja ili wawe na uzima, tena wawe nao tele.

Baba ufunuo wako kwa habari ya ndoa yangu hauta-ibiwa,kuharibiwa wala kuuliwa kwa jina la Yesu.Nitaupokea ufunuo wako kama ulivo na kuu-ishi kwa furaha zote katika jina la Yesu.NITAUPOKEA UFUNUO WAKO NA KUU-ISHI KIKAMILIFU NA UTATIMIA KWANGU KAMA ULIVYOKUSUDIWA KWA JINA LA YESU. Katika jina la Yesu nimeomba Amen.

Day 2: Prayers to Be  Found By Your Husband.

Esta 2:17

Mfalme akampenda Esta kuliko Wanawake wote, naye akapata neema na kibali machoni pake kuliko mabikira wote; Basi akamtia taji la kifalme kichwani pake, akamfanya awe malkia badala ya Vashti.

1.Baba naomba kibali machoni pa Mume Mtarajiwa.

Baba naomba Mume wangu avutiwe na mimi na asichanganywe na wanaweake wengine.He wil not be delayed nor denied access to met me.Hata baada ya Ndoa aendelee kuvutiwa na mimi na nipate kibali cha kukubalika kwake kimwili,kiakili na kiroho kwa jina la Yesu.Mume wangu anipende kuliko wananwake wote aliowahi kukutana nao na nipate kibali cha kuwa mkewe katika jina la Yesu.

2.Mume mtarajiwa aone thamani yangu kama Mke na Partner sahihi kwake.

Baba nitakapo kutana na Mume wangu mtarajiwa anione katika nafasi ya mke na sio wananwake wa kuchezea. Anione wa thamani na manufaa kwake, mwenye kufaa kuwa partner  na Mke wake.Aione thamani yangu yeye na sio mimi kumbembeleza katika jina la Yesu. Na anichukue kama kitu cha thamani katika yetu yote katika jina la Yesu.Kama Mfalme alivyo-ona thamani  ya Esta na kumvika taji la Malkia, Mume wangu aone thamani yangu pia katika jina la Yesu.

3. Nakataa kuwa Vashti katika Uchumba na Ndoa Yangu.

Nakataa roho ya kukutana na Mume mtarajiwa na kuondolewa nafasi ya kuwa Mkewe wakati wa Uchumba kwa jina la Yesu.Uchumba wangu hautaishia njiani na nafasi yangu ya kuwa Mke haitabatilishwa katika jina la Yesu.Kikombe cha Vashti kupata na kukosa njiani hakita kuwa fungu langu kwa jina la Yesu.Utakachonipa kitakamilika Baba kwa jina la Yesu.

Mwanzo 29: 17 – 30

“17 Lakini Lea alikuwa na macho mepesi. Raheli alikuwa mrembo wa sura na umbo. 18 Yakobo alimpenda Raheli, basi akasema, ‘Nitakutumikia miaka saba kwa Raheli mkubwa wako.’ 19 Labda Bwana atakubali neno langu,’ Yakobo akawaza, kwa hiyo akakubali. 20 Basi Yakobo akamhudumia Raheli miaka saba; lakini miaka hiyo ilimwonekana kama siku chache kwa sababu alimpenda sana.

21 Kisha Yakobo akamwambia Labani, ‘Nipe mke wangu, kwa maana muda wangu wa kumhudumia umekwisha, nipe mke wangu ili nifunge ndoa naye.’ 22 Basi Labani akakusanya watu wote wa mahali pale wakafanya karamu. 23 Usiku wa huo Labani akamleta Lea kwa Yakobo, naye akamchukua na kufanya naye ndoa. 24 Labani akampa Lea mwanawe Bikira Lea apewe mjakazi Zilpa amlizae Yakobo. 25 Siku ya pili asubuhi, Yakobo alipokuwa ameamka, alimwona Lea. Basi Yakobo akamwambia Labani, ‘Mbona umenitenda hivi? Je, sikukutumikia miaka saba kwa Raheli? Kwa nini umenidanganya?’ 26 Labani akamwambia, ‘Katika nchi yetu si desturi kumtoa mdogo kabla ya mkubwa. 27 Kamilisha juma hili la sherehe kwa binti huyu, kisha tutakupa na huyu nyingine kwa ajili ya kazi ulizonifanyia, na utumikie nami kwa miaka mingine saba.’ 28 Yakobo akafanya hivyo. Akamaliza juma la sherehe kwa Lea, kisha Labani akampa binti wake Raheli awe mke wake. 29 Labani akampa Raheli mwanawe Bilha mjakazi wake aolewe naye. 30 Yakobo akalala na Raheli pia, akampenda Raheli kuliko Lea. Akamtumikia Labani miaka saba mingine.”

Hii ni sehemu ya Biblia inayoelezea jinsi Yakobo alivyomtumikia Labani miaka saba kwa ajili ya kupata mke wake Raheli, lakini Labani alimdanganya na kumletea Lea badala yake. Yakobo alikubali kuendelea kufanya kazi kwa Labani kwa miaka mingine saba ili apate pia Raheli kama mkewe.

4.Mila na Desturi za Kwetu hazitanichelewesha kwenda kwa Mume Wangu.

Roho zozote za kifamilia kiukoo zinazozuia na kuchelewesha Ndoa yako kama Labani alivyotumia Mila na Desturi kama njia ya kuchelewesha ndoa ya Raheli (Rachel) hazitafanikiwa kwa jina la Yesu.Nakataa kusubiria ndoa yangu miaka saba (7) zaidi kama Raheli ili miiko ya kimila itimie. Naondoa kila aina ya mamlaka waliyo nayo kulazimisha miiko na mila zao juuu yangu kwa jina la Yesu.Baba ucheleweshwaji wa aina yoyote unaosababishwa na mila na desturi zetu ushindwe kwa jina la Yesu.Kuchelewa kwa Ndoa yangu sio fungu langu kwa jina la Yesu.

5.Baba nakataa udanganyifu wa majira na mkorogo juu ya hatima yangu.

Baba nakataa roho ya udanganyifu kama aliofanyiwa Yakobo na kupewa Lea badala ya Raheli juu ya Mume wangu Mtarajiwa katika jina la Yesu.Majira na hali hazitomlazimisha Mume wangu kumuoa Lea badala yangu kwa jina la Yesu.Nakataa ucheleweshwaji na usubiridhwaji usio na msingi katika jina la Yesu.Nakataa  ghiliba yoyote na Udanganyifu kwenye mahusiano yetu kwa jina la Yesu. Nitaolewa kwa wakati kwa jina a Yesu.

Mwanzo 24:15-18

“15 Ikawa, hata kabla hajamaliza kusema moyoni mwake, tazama, Rebeka alikuwa akija, na mtungi begani; naye akashuka chanzoni kunyonyesha, wala hakuwa amemjua mwanamume.

16 Mtu huyo akamwendea, akamwambia, ‘Nipe, tafadhali, kunywa kidogo maji kutoka kwenye mtungi wako.’

17 Naye akasema, ‘Ninywe, bwana wangu.’ Akaifungua haraka mtungi wake, akampeni maji,

18 Akakimaliza kumpa kunywa, akasema, ‘Nitakunywesha na ngamia wako, pia, hata watakapomaliza kunywa.'”

Hii ni sehemu ya Biblia inayoelezea jinsi mtumishi wa Ibrahimu alivyoenda kutafuta mke kwa ajili ya mwana wa Ibrahimu, Isaka. Mtumishi huyo alikutana na Rebeka karibu na kisima na alipomwomba maji, Rebeka alimpa maji na pia alikubali kumnywesha ngamia wa mtumishi huyo. Hii ilikuwa ishara ya Mungu kuwa Rebeka ndiye mke sahihi kwa Isaka.

6.Kabla hatujamaliza Mambi haya mruhusu Mume wangu ajitokeze ,anione na kuniapproach.

Baba naomba nionekane na kutambulika kama Mke kwa Mume Mtarajiwa katika urahisi kwa jina la Yesu.Atambue kuwa mimi ni Mke na asisite na kutaka kuonja onja kwa Jina la Yesu.Baba nifahamishe mtungi ninaotakiwa kubeba ili Mume wangu atakaponiona anitambue kama mke wake kwa urahisi.Ikiwa hu mtungi ni sehemu au mtu au kitu nifahamishe Baba ili atakapo niona niwe katika hali au njia sahihi na atambue dhahiri kuwa mimi ndio Mke wake kwa jina la Yesu.Baba nifanyie wepesi  wa kukukutana na kutambulika kama Mke kwa jina la Yesu.

Mwanzo 30:22-24

Kisha Mungu akamkumbuka Raheli,akalikubali ombi lake na kumjalia kupata watoto.Raheli akapata Mimba,akajifungua mtoto wa kiume, akasema, “Mungu ameniondolea aibu angu” kwa hiyo akakmwita mtoto huyo Yosefu akisema,”Mwenyezi Mungu na aniongezee mtoto mwingine wa kiume”.

7.Baba nikumbuke mwanao kwa habari ya ndoa na kuifuta aibu yangu.

Baba nikumbuke mwanao katika jina la Yesu.Baba nikumbuke kwa habari ya ndoa.Nikumbuke Baba usiku hiuu , Nikumbuke mimi mwanao katika habari ya Ndoa kama ulivyomkumbuka Raheli na kujalia watoto hivyo kumuondoea aibu yake,niondolee na mimi aibu yangu pia kwa jina la Yesu.Baba nikumbuke mwanao,kumbuka sala zangu,sadaka zangu ,utii an unyenyekevu wangu na unikumbuke kwa habari ya Ndoa kwa jina la Yesu.Baba napiga magoti mbele ya kiti chako cha rehema usiku huu na kukusihi unikumbuke mwanao katika habari ya Ndoa kama ulivyomkumbuka Raheli na kumuondolea aibu katika jina la Yesu.FATHER REMEMBER ME IN JESUS NAME.

Yohana 4:17-18

Huyo Mwanamke akamwambia, “Mimi sina Mume.” Ysu akamwambia,”Umesema kweli, kwamba huna Mume.Maana umekuwa na waume watano,na huyo unayeishi naye sasa si mume wako.Hapo umesema kweli”

8.Yoyote Asiye Mume Wangu Mtarajiwa kwenye maisha yangu ya mahusiano ifike  tamati.

Baba nioneshe mwanaume yoyote ninaye ingia naye kwenye mahusiano na sio mume wangu kwa jina a Yesu.Baba niepushe na roho ya kuparamia wanaume wasio sahihi kama mwanamke huyu kwa jina la Yesu.Mungu nipe hekima ya kujua hata niliye naye kama sio mhusika na kuweza kufanya maamuzi sahihi katika jina la Yesu.Bwana ongeza utashi wangu katika maamuzi ya kuolewa na niepushe na roho ya kutanga tanga katika mahusiano kwa jina la Yesu.Fungu la mwanamke huyu halitakuwa alangu kwa jina la Yesu.Baba nifanyie wepesi wa kukutana na kumjua mtu sahihi kwa jina la Yesu.

Mathayo 13:14

Na Neno la Nabii Isaya linatimia kwao,likisema, Kusikia mtasikia, wala hamtaelewa; Kutazama mtatazama, wala hamtaona.

Baba ninaomba roho wako aniongoze kwenye programu hii nisikie ,nielewe na niweze kuvuka. Baba ninashukuru kwa kuwa najua wewe ni mwaminifu na imeshatendeka kwangu na umeachilia Roho wako wa ufunuo nipate kuyajua na kuyaelewa mafundisho yako na kuweza kuvuka in katika jina la Yesu.

Day 3: Prayers To Be Found By Your Husband.

Esta 2:14

Huenda jioni na asubuhi hurudi katika nyumba ya pili ya wanawake,mikononi mwa Shaashgazi, msimamizi wake mfalme, aliyewalinda masuria.Wala haingii tena kwa mfalme, isipokuwa awe amempendeza mfalme, naye akaitwa kwa jina.

1.Baba niepushe na mahusiano batili ambayo hayatafikia hatima ya Ndoa.

Baba niepushe na mahusiano yatakayonikosea heshima,uaminifu na kujaa chaos, udhalimu na yasiyo na sifa wala yenye kukurudishia utukufu kwa jina la Yesu.Nakataa mahusiano ya kufanywa mtumwa wa ngono na mpango  wa kando kwa jina la Yesu. Nisiolewe na mtu asiyejua thamani yangu kwa jina la Yesu.Nisi-ingie kwenye mahusiano yasiyokupendeza kwa jina la Yesu.Nipokee Mahusiano yatokayo kwako pekee Baba kwa jina la Yesu.

Mithali 18:22

Apataye Mke apata kitu chema, Naye ajipatia kibali cha bwana.

2.Kibali cha bwana cha kuwa Mke kiwe juu yangu.

Baba neno lako linasema apataye Mke amepata kibali machoni kwa bwana.Baba naomba kibali chako cha kuwa Mke kiwe juu yangu kwa jina la Yesu.Mume mtarajiwa apate kibali machoni pako cha kunifanya Mke wake katika jina la Yesu Kristo.Baba achilia kibali cha ndoa juu yangu.  Let it manifest now in the name of Jesus and so is done in Jesus name.

Mithali 19:14

Nyumba na mali ni urithi apatao mtu kwa Babaye; Bali Mke mwenye busara mtu hupewa na BWANA.

3.Baba nipeleke kwa Mume wangu maana Mke mwema mtu hupewa na Bwana.

Baba nakuja mbele yako kwa habari ya Nda yangu, Mke mwema mtu hupewa na Bwana.Baba unajua mimi ni Mke mwema mwenye uhitaji wa Mume.Baba unaona sirini na unauona Moyo wangu na utayari wangu wa Ndoa.Baba naomba unipeleke kwa Mume wangu uliyekusudia kumpa Mke mwenye busara katika jina lililo kuu na lenye mamlaka la Yesu. Mke mwema anatoka kwa Mungu.Baba nifanyie nafasi ya kuwa Mke mwema kwa maana niko tayari. Katika jina la Yesu naomba.

Mathayo 25:1-13 BHN

Wakati huo ufalme wa Mbinguni utafanana na Wasichana kumi waliochukua taa zao, wakaenda kumlaki bwana harusi. Watano miongoni mwao walikuwa wapumbavu na watano walikuwa walikuwa wenye busara.Wale wapumbavu walichukua taa zao, lakini hawakuchukua akiba ya mafuta.Lakini wale wenye busara walichukua mafuta katika chupa pamoja na taa zao.Kwa kuwa Bwana Harusi alikawia kuja, wale wasichana wote walisinzia, wakalala.Usiku wa manane kukawa na kelele:”Haya, Haya! Bwana Harusi anakuja, nendeni kumlaki”. Hapo wale wapumbavu wakawaambia wale wenye busara:”Tupeni mafuta yenu kidogo maana taa zetu zitazimika”.Lakini wenye busara wakawaambia,”Hayatatutosha sisi na nyinyi! Afadhali mwende dukani mkajinunulie wenyewe!” Bai wale wasichana wapumbavu walipokwenda kununua mafuta,Bwana Harusi akafika, na wale wasichana waliokuwa tayari wakaingia pamoja naye katika jumba la Harusi,kisha mlango ukafunga.Baadaye wale wasichana wengine wakaja,wakaita:”Bwana, Bwana tufungulie!” lakini yeye akawajibu, “Nawaambieni kweli, siwajui ninyi” Kisha Yesu akasema, “Kesheni basi, Kwani hamjui siku wala saa”.

4.Nakataa Roho ya ucheleweshwaji wa ndoa yangu! Bwana Harusi wangu hatakawia kwa jina la Yesu.

Kama Bwana Harusi asingechelewa kuja  wale Brides (Mabibi Harusi) wote kumi (10) wangeolewa kwa wakati.Naenda kinyume chochote kinacho mchelewesha Bwana Harusi wangu na kuchelewesha Ndoa yangu kwa jina la Yesu. Bwana Harusi wangu atakuja kwa wakati na hatochelewa katika jina la Yesu.Vikwazo vyote vinavyomkawisha Bwana Harusi huko aliko , Vikivizia nilale na kuishiwa mafuta vimchukue naomba vipotee sasa katika jina la Yesu.I declare and decree OPEN PATH by the power in the blood of Jesus kwa Bwana Harusi wangu kuja kwa wakati. Hakutakuwa na kuchelewa kwa habari ya Hatusi yangu kwa jina la Yesu.Nitaolewa kwa wakati ulio amriwa in Jesus name I pray.

Yeremia 33:11

Itasikika tena sauti ya furaha na sauti ya shangwe, sauti ya bwana Harusi na sauti ya Bibi Harusi, Sauti yao wasemao mshukuruni Bwana wa majeshi, maana BWANA ni mwema, rehema zake ni za milele; na sauti zao waletao sadaka za shukrani nyumbani kwa BWANA.Kwa kuwa nitawarudisha wafungwa wa nchi hii kama kwanza, asema BWANA.

5.Sauti ya Bwana na Bibi Harusi itasikika tena nyumbani kwetu kwa habari ya ndoa yangu.

Baba neno lako linasema sauti ya Bwana Haruai na Bibi Harusi zitasikika tena kwa jina la Yesu.Sauti za Bwana na Bibi Harusi zitasikika nyumbani kwetu na sio kwa wenzangu in the mighty name of Jesus na tutarejesha shukrani kwako Bwana.Baba umesema utawarudisha wafungwa wa nchi kama kwanza, Baba nimechoka kuwa mafungwa wa nchi hii, mfungwa wa upweke nirudishe kama kwanza; na sauti ya furaha isikike tena maishani mwangu kwa maana rehema zako ni za milele in the name of Jesus.

Baba tunashukuru kwa kukamilisha hizi siku tatu (3) za programu hii. Tunakushukuru kwa kuwa umetusikia na siku zote tunajua unatusikia. Tunashukuru kwa mafuno ya Roho Mtakatifu kupita in the right scriptures na kuweza kuzifanunu.Tunakushukuru kwa wale wote waliofanikiwa kufanya programu hii na wale watakao fanya baadae.Tunakushukuru kwa kuwa tuna amini umeshatenda na imekuwa kwa jina la Yesu, Tunaomba.

 

 

 

 

4 thoughts on “Prayers to be found by your Husband ( Maombi ya Kupatwa na Mumeo)”

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Scroll to Top
× IT Help Desk