Msihi Mungu : Jua Lisizame Changamoto Zako Hazijasujudu.

Katika Maisha yetu ya kila siku tunakutana na changamto nyingi na changamoto hizi huweza kujikita katika makundi mbalimbali ambayo huweza kuwa ya kimwili au kiroho na kama ilivyo kawaida yetu wanadamu huweza kutafuta njia mbalimbali kuweza kutatua changamoto zetu ili kuweza kujikwamua na dhiki au shida zinazotutatiza.Mpendwa  Kuna baadhi ya changamoto haziwezi kutatuliwa kwa njia ya kimwili mfano kwa kutumia fedha au mazoezi tunahitajika kufanya muungano ( connection ) na Mungu  ili kuweza kuzitatua ,Lakini  njia hii kuna muda hatupati matokeo kabisa kiasi cha kutukatisha tamaa. Nipende kukusihi mpendwa usikate tamaa, usimpe ushindi mwovu , wakati ni sasa piga goti ingia vitani kwa kumuomba na kumsihi Mungu Jua Lisizame changamoto zako Hazijasujudu.

Katika Bibia imeweza kutolewa mifano mbalimbali inayotuhimiza kumsihi Mungu kutatua changamoto zetu kwani yeye ni muweza wa yote. Tufatilie sasa.

1 Samweli 5 : 2 – 4 

 “Sawa, Wafilisti wakachukua sanduku la Mungu, wakaliingiza ndani ya nyumba ya Dagoni, wakaliweka karibu na Dagoni. Na asubuhi, walipoamka, tazama, Dagoni amelala kifudifudi chini mbele ya sanduku la Bwana. Wakautwaa Dagoni, wakamweka mahali pake tena. Lakini asubuhi, walipoamka, tazama, Dagoni amelala kifudifudi chini mbele ya sanduku la Bwana; na kichwa cha Dagoni, na mikono yake miwili ilikuwa imekatika juu ya kizingiti, iliyobakia hivi kwa Dagoni tu.”

Waamuzi 16:28

 “Ndipo Samsoni akamwita Bwana, akasema, Ee Bwana MUNGU, nakuomba, unikumbuke, nakuomba, unipa nguvu, nakuomba, unifiche mara hii tu, Ee Mungu, ili nipate kulipiza kisasi kwa ajili ya jicho langu moja kwa Wafilisti, kwa sababu ya macho yangu mawili.”

Tukiangalia hadithi za Dagoni na Samsoni, tunaweza kugundua ujumbe wa nguvu wa kuomba msaada na kumtegemea Mungu katika nyakati za changamoto. Katika hadithi ya Dagoni, sanamu ya Dagoni ililala kifudifudi mbele ya sanduku la Bwana, ikionyesha kutokuwa na nguvu mbele ya Mungu wa kweli. Katika Waamuzi 16, Samsoni, hata baada ya kupoteza nguvu zake, aliomba msaada wa Mungu kwa nguvu ya mwisho ili aweze kulipiza kisasi.

Tunapokutana na changamoto zisizoweza kushindwa, kama vile Dagoni alivyoshindwa mbele ya Mungu, na tunapohisi dhaifu kama Samsoni, tunaweza kumwomba Mungu kwa moyo wote kama Samsoni alivyofanya. Tukimwomba Mungu kwa imani, nguvu za kimungu zinaweza kutenda miujiza na kugeuza hali. Kama vile Dagoni alivyoshindwa na sanduku la Bwana, changamoto zetu hazina mamlaka mbele ya Mungu wa uwezo wote.

Hitimisho

Hivyo basi, msihi Mungu katika nyakati zako za shida na changamoto. Jua lisizame juu ya matumaini yako, kwani kwa imani, unaweza kuinuliwa kutoka chini na kuwa na ushindi kupitia nguvu za Mungu. Changamoto zako hazijasujudu mbele ya Mungu anayeweza kufanya mambo yasiyowezekana kuwa kweli.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Scroll to Top
× IT Help Desk