MISINGI IKIHARIBIWA MWENYE HAKI ATAFANYA NINI? – SUNDAY WORD

Zab 11:3

Kama misingi ikiharibika, Mwenye haki atafanya nini?

THE DEVIL IS ALL FOR AN EARLY WIN!

Anapenda kuchukua ushindi na point zake tatu mapema sanaa. Anajua akisha uharibu msingi wako hakuna utakacho jenga! Automatically utaingia kwenye self-destructory mode, ambapo it will no longer be him doing the destruction but you!
Atakuwa anakupa tu kamba unajinyonga mwenyewe.

Na bila misingi kurekebishwa na kuwekwa sawa, nothing will ever be built from you. Nothing at all.

Ndo Maana Shetani Anapiga Sana Ndoa na Familia!

Watoto wakue bila baba na mama pamoja — wawe vulnerable and prone to destruction!
Nobody to install order and discipline in them. Wanakuzwa na dunia.

Ndo tumefikia “Usioe au kuolewa na mtu alielelewa na single mum” na even if you decide to be fair utajionea!

Sio wote, na it’s not a general thing, lakini unakuta wengi wa hawa watu hawajui wala hawajalelewa kuelewa the family sacrifice.
Kuelewa taking blows for your family. Kujua boundaries za what is right and what is wrong. Seeing the bigger picture ambayo ni the family.

Hawaja enjoy show ya mzee anachambwa wima wima na jioni anarudi zake maskini. Anavamiwa hadharani, anatukanwa kama mtoto mdogo, na jioni anarudi. Anarudi anakuta mshakula na kuosha vyombo. Anachemsha zake chai na mkate.
Na siku zinaenda! Na mkewe hamuachi.

Sometimes mzee anawalea miaka 10 hamna kelele! Wa 11 anapoteza kazi — basi mkewe anageuka anaconda!
Wanawake sisi kujiliza “Baba yenu hana msaada wowote, nitaondoka niwaache na baba zenu mle maweee!”
Mimi ndo kila kitu, baba yenu mnamuona hapo afu mnaniletea ujinga!
Anaongea hivyo wakati nyumba mnayo kaa ni ya mzee — kaolewa na begi lake tu.

Na mzee ananyamaza! Hajjitetee! Ha-set record straight! Nothing!
Just the silence! And no matter what, he always comes back home.
Like a real man he should. Kobe hatakiwi kushindwa na jumba lake.

Kuna siku mambo yanachachuka mnasema “Ya leo kaliii! Baba harudi nawaambia! Kwa show ile na smack down ile, sidhani kama atarudi! Hata kama mimi sirudi.”
Sasa ataenda wapi maskini? Au kwao kwa bibi?

Jioni anajikusanya zake saa 6, angoje pharaoh awe amelala, ana vizia arudi. Moto unawaka upyaaaa!
Sisi watoto kama vipanya kimyaaa!
Kuna siku kipanya kimoja kikakata kifungue mdomo dhidi ya Pharaoh — biii mkubwa!
Mzee akamtikisia kichwa “Don’t.”
Kobe sishindwi na mkonga wangu.

Afuu wamama sisi tuna control narrative! Tuna control story! No room for truth.
Na wanaume lile koromelo kweli lina kazi yake! Hawa semiii kituuu!
Tena ukisema umtete, anakugeuka na kuwa upande wa mkewe. 😅

When It’s Your Turn…

When it’s your turn to roast your husband, unajikuta kumbe mama yako hakufanya kituu kabisaaa.
And the resentment you felt towards her shames you.
Unawaza alikua na super power! This shit is deadly!

Unawaza miaka 30/40 ya ndoa amekaa vipi jamani, wakati mi 5 is like eternity!
Maneno aliyo yatupa mama yako hamna kituu ukilinganisha na sumu unazotema wewe, and you are not even 40 yrs yet!
Damn!
And it hits you hard — you will surely end up worse than your own mother you resented.

Na kaka zako grew up better men! They always go back to their wives and be men they should be!
Una wakumbusha baba yao si alikua anarudi kila siku kukipata?
It’s their turn to man up and keep their family together.
What doesn’t kill them should make them stronger.
Kobe hatakiwi kushindwa na jumba lake.

Wakimwambia mzee, “We are thinking about divorce,”
Ana wauliza: Mna jizima data? Je, mama yenu — is she a perfect wife in the history of perfect wives?
How many times she disrespected me mkiwa wadogo mpaka sahivi?
How much evil have I endured to be your father and keep this family together?
How much happiness have I sacrificed to be the father you see me today?

Haya, go be a father I raised you to be for your kids.
Mke ume mchagua mwenyewe! Kapambane na hali yako.
Ndo uanaume huooo!
Hata ukioa mwingine mtaishia hapa hapa!
Mimi nimenyanyasika na mke wangu maisha yangu yote.
Wadogo zangu wame divorce mara 2, wengine 3 wako wenyewe uzeeni!
There is no happy ending son — in the end, life does dirty us all.

Shetani Ana Haribu Misingi Yako

By making you soft, fragile, mad, and easily defeated.
He programs you for failure.

Unless you reprogram yourself, success for you isn’t an option.
Hata mtu atake vipi ufanikwe, utarudi pale pale.

Imagine mtu huna kazi, huna maisha, huna chochote, na kusoma injili hutakiii!
Yet unataka watu wafanye deliverance juu yako.
Watu hawatafanya!
Utahama makanisa kwa makanisa, huduma kwa huduma, ila mwisho wa siku utabaki na ujeuri wako na wao watabaki na karama yao.
Who loses most? You my love.

Wakati ungesoma Injili ikiwezekana na nyaraka za mitume kabisaaa — unamtia mtumishi moyo kwamba nia ya dhati unayo, na you are already halfway anyways!
Anapata nguvu za kumalizia the other half!

Misingi Imeharibika Tangu Vizazi na Vizazi!

Watu wengi misingi yetu imeharibika tangu vizazi na vizazi!
We grew up without discipline, morals, boundaries.
Our parents and grandparents failed us.
Na tusipo kuwa makini, we will fail our children.

Just because your mother alikuwa anamjibiza baba yako, basi na wewe unamjibiza mume wako bila kuwaza mara 2 — yule sio baba yako mzazi aliepitia jando akafunzwa kuishi na mwanamke jeuri na kiburi.

Mume ni chiwawa amelelewa na single mom whom he worships.
Akikusema tu kwa mama yake kwamba unamjibu, kunyaaa!
Tumbo la uzazi lina mchezaa alivyo kapatia shida katoto kake kalikomuharibia mpaka maisha.
Anapitisha verdict: Mpe talaka zake mwanangu, nakutafutia mke mwingine!
Bi Sandra ndo mwenyekiti wa single moms wasiotaka ubabaifu wa walizao! 😅

Hata Kazini…

Hata ukipelekwa kazini, tabia zako chafu zitakulast mwaka tu — kila mtu asha kujua sio management material.
Majibu ya kunyaa! Dharau! Nyodo! Kwishaaa kazi!

Hutaolewa huwezi kudumu kwenye miji ya watu.
Unaingia mji wa watu alafu unataka wewe ndo uwe contawa, u-control na ku-dictate mji wa wenyewe uende vipi.
Mtoto wao wenyewe!
Heheheheeee!
Mwaka mrefu wameshakupa cheti chako na wamesha muolea mtoto wao mke mwingine mapema sanaaa!

Personal Revelation…

Mimi binafsi I used to pride in being a baddie, unruly! Unbothered! Unhinged!
Lakini nikajiharibia maisha mwenyewe.
Then I learned discipline mtu mzima kabisaaa.
I learned morals. I learned to keep quiet need it be.
I unprogrammed myself from failure.

Sasa hivi mtumishi nawasaidia watu — na cha kwanza wakivuka ni kuni cut loose.
Yaani mtu akivuka tu, mtu wa kwanza kumfanya vibaya ni mimi mtumishi wake!
Kama Moses, mimi nabaki nje nakuangalia unavyoingia Canaan!

Ni swala la muda tu maana sawa, umevuka, but you are still inexperienced!
Utanikumbuka tu mtumishi wako!
Higher levels, bigger devils!

Unarudi na stories that touch the heart!
Nakulima block moja takatifu!
Narudi Misri, tunaanza upya safari ya Canaan na watu wengine!

Fanyia Kazi Misingi Yako

Kama kweli unataka kuvuka for real, fanyia kazi misingi yako na irekebishe.
Misingi mibovu ndo imekukuza wewe mbovuuu!
Ili wewe ubadilike uwe mpya, lazima mabadiliko yaanze kwenye misingi yako.

Hata ukipaka rangi nyumba ya zamani, ilihali misingi ni ile ile mibovu, itabomoka tuuuu.

Msijifanyie marekebisho juu juu na ku-ignore misingi.

Hata Ukiokoka…

Hata ukiokoka wakati maagano ya waganga uliyoingia ujanani yapo active,
laana za ukoo juu yako zipo vere vere,
maagano ya ukoo yapo pambee,
nira za shetani zipo shingoni mwako,
trauma and unforgiveness bado inakutafunaaa,
spirit spouses bado wamekuoa na pete zao zipo kidoleni —
wewe kuishi maisha ya ushindi ni uongo!

~ THE END ~

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Scroll to Top