Maombi ya Yesu ni maombi ambayo Bwana Yesu alimuomba Mungu Baba katika nyakati tofauti tofauti,Mpendwa maombi haya ni mepesi ila magumu kwani Yesu hakuwa mtu wa maneno mengi, alikuwa na maneno machache sana ila mazito sana. Maombi haya mpendwa yanahitaji maandalizi mazito kabla ya kuyafanya ,Mimi pia nitafanya maandalizi ya kutosha usiku huu na maombi haya yatachukua siku tano (5) za kufunga.
Day 1 : Maombi ya Yesu
Furaha ya Yesu
(Mat 11: 25 – 27; 13: 16 – 17)
21. Saa ilelile, Yesu akafurahi kwa uwezo wa Roho Mtakatifu kisha akasema, ” Nashukuru Ee Baba, Bwana wa Mbingu na Dunia, maana umewaficha wenye hekima na wenye elimu mamabo haya ukawafumbulia wadogo. Naam Baba ndivyo ilivyokupendeza.”
22 Kisha akasema,” Baba yangu amenikabidhi vitu vyote. Hakuna amjuaye Mwana ila Baba, wala amjuaye Baba ila Mwana, na yeyote amabaye Mwana atapenda kumfunulia.”
Day 2: Maombi ya Yesu
41 Kwa hiyo wakaliondoa lile jiwe.Yesu akaangalia mbinguni akasema, ” Baba ninashukuru kwa kunisika.42 Ninajua ya kuwa huwa unanisikiwa wakati wote,lakini nimesema hivi kwa faida ya hawa walio hapa,ili wapate kuamini kuwa umenituma.”43.Baada ya kusema haya akapaza sauti akaita, “Lazaro,toka nje!”.44Yule aliyekuwa amekufa akatoka, mikono yake na miguu yake ikiwa imeviringishwa vitambaa.Yesu akawaambia, ” Mfungueni awe huru!”
Day 3: Maombi ya Yesu
Marko 7: 31 – 37
(Yesu amponya mtu aliyekuwa Bubu na Kiziwi)
31Yesu akaondoka katika eneo la Tiro, akapita katikati ya Sidoni akaenda hadi Ziwa la Glilaya kwa kupitia eneo la Dekapoli.32.Hapo, watu walimletea kiziwi mmoja maaye a alikuwa hawezi kusema sawa sawa, wakamwomba amweke mikono ili aweze kupona.33 Yesu akampeleka yule Kiziwi kando mbali na watu akaingza vidole masikioni mwake kisha akatema mate na akaugusa ulimi wake.34 Ndipo Yesu akatazama mbinguni, akahema kwa uchungu, akamwambia “Efatha!” yaani “Funguka”35.Wakati huohuo masikio ya yule mtu yakafunguka na ulimi wake ukawa huru ukaanza kusema vizuri.
Day 4: Maombi ya Yesu
Yohana 12: 27 – 50
27.”Moyo wangu unafadhaika sana.Niombeje?”Baba nepushe na mambo yanayotokea?.La, Nilikuja ulimwenguni kwa sababu hii. 28. Baba, dhihirisha utukufu wa jina lako!” kisha ikasikika sauti kutoka mbinguni,”Nimedhihirisha utukufu wa jina langu,na nitafanya hivyo tna”.29 Umati wa watu waliposikia sauti hii, baadhi walizani ilikuwa ni sauti ya radi, na wengine wakasema,”Malaika alikuwa anaongea naye.”
Day 5: Maombi ya Yesu
34 Yesu akasema,”Baba, uwasamehe kwa maana hawajui walitendalo!” Wakagawana nguo zake kwa kupiga kura.
PRAYER POINT!
Bwana Yesu wasamehe wote walio niloga,walio nifunga na kuzuia hatima yangu, kupiga vita ya kuanguka kwangu na kugawana furaha yangu!, wasamehe wote waliozuia (ku-block) hizo prayer points kwani hawajui walitendalo.