Madeni ni moja ya changamoto kubwa katika maisha yetu ya kifedha. Mara nyingi, tunajikuta tukibeba mzigo wa madeni ambayo inaweza kuathiri sana maisha yetu. Lakini je, Biblia ina mafundisho gani kuhusu jinsi ya kuepuka madeni na kusimamia fedha zetu kwa hekima? .Mpendwa ili kuweza kuepukana na madeni inatubidi tujifunze namna ya kuruhusu Breakthrough (Kuvushwa ), Tutaangalia mifano kadhaa kutoka kwenye Biblia ambayo inaweza kutuongoza katika kufanya maamuzi bora ya kifedha :
Part 1 : Madeni
Mfano wa Elisha akimsaidia mwanamke aliyekuwa na shida ya madeni
2 Wafalme 4 : 1 – 7
Basi Mwanamke mmoja miongoni mwa wake za wanafunzi wa manabii akamwendea Elisha, akamwambia, ” Mtumishi wako, Mume wangu amefariki, na kama ujuavyo alikuwa mcha Mungu, lakini aliyemwia ( kumdai ) fedha amekuja kuwa twaa wanangu wawili wawe watumwa wake “. Elisha akamuuliza , ” Sasa nikusaidieje ? Nambie kile ulichonacho nyumbani” .Mama huyo mjane akamjibu, ” Mimi mtumishi wako sina kitu chochote ila chupa ndogo ya mafuta” . Elisha akamwambia, ” Nenda kwa jirani zako uazime vyombo vitupu vingi kadri utakavyopata “. Kisah uende, wewe pamoja na wanao, mjifunge ndani ya nyumba, na muanze kujaza mafuta hivyo vyombo. Kila chombo mnachojaza kiwekeni kando. ” Mwanamke akaenda na kujifungia ndani ya nyumba na wanawe na kuanza kumimina mafuta ndani ya vyombo. Vilipojaa vyote, akamwambia mwanaye mmojawapo, “Niletee chombo kingine.” Mwanaye akamjibu, “vyote vimejaa!”
Hapo mafuta yakakoma kutiririka. Akarudi kwa mtu wa Mungu na kumweleza habari hizo. Na mtu wa Mungu akamwambia, “Nenda ukauze hayo mafuta na kulipa madeni yako, ndipo wewe na wanao mtaishi kwa kutumia hayo yatakayobaki”.
Mahubiri
Mpendwa rudia rudia hili neno hadi likusemeshe. Kwa kawaida madeni na maombi hayana uhusiano kabisa.Tazama Mume wa Yule mama alikuwa Mcha Mungu na alitumika madhabauni kwa Elisha. Maana alikuwa mwanafunzi wa Elisha. Biblia inasema alikuwa MCHA MUNGU. Mkewe ana ujasiri wa kumkumbusha Elisha kuwa akumbuke Mumewe alikuwa mwanafunzi wake hivyo haikuwa sababu ya matendo maovu hadi kuwa na madeni yote yale.Hivyo Mpendwa pamoja na yule mume wa mwanamke pamoja na kuwa mtumishi muaminifu mno, Lakini alikufa na madeni. Hili ni funzo kuwa kusaliii sana na ibada za kutosha hazina uhusiano na madeni kwani Watumishi pia nao wana madeni.
Mpendwa Pamoja na Mwanaume yule kuwa mwanafunzi wa Nabii, ilifika hatua mdeni wake kama walivyo wadeni wengine katika maisha yetu ya kawaida wanavyo tishia kuja ofisini kwako ,hata kukufanya vitu vibaya. Yule Mdeni aliweka wazi kuwa kama imeshindikana nipeni watoto wakatumikie deni la Baba yao, yaani mwanafunzi wa Nabii ambaye hayupo tena duniani. Hakujali Unabiii , wala Utumishi wake hata uyatima wa wanawe aliona deni tu.
Mwanamke wa Mwanafunzi yule akaibuka kwa Elisha na Elisha hakushtuka wala kusikitika bali aliuliza NIKUSAIDIEJE? Mpendwa Wengi hapa ndio TATIZO LILIPO! Mnapoenda mbele za Mungu mnafanya kulalamika, kulaumu, kulia na kusononeka Lakini mnasahau kumwambia Mungu awasaidie vipi kulipa hayo madeni.
SPOILLER ALLERT! ; HAMTAAMKA ASUBUHI UKAKUTA MADENI YAMELIPWA! AU WATU ( DESTINY HELPERS) KWA NJIA YA AJABU WAMEJITOKEZA NA KULIPA MADENI.
UNATAKIWA UWAZE USAIDIWAJE NA MBINGU? yaani unahitajika kuwa na MPANGO MKAKATI.
Hivyo, Wapendwa kwa kuhitimisha, Biblia ina mafundisho mengi kuhusu jinsi ya kuepuka madeni na kusimamia fedha zetu kwa hekima. Kwa kuzingatia mafundisho haya na kufuata kanuni za kifedha zinazopatikana katika Maandiko, tunaweza kujenga msingi imara wa maisha ya kifedha na kuepuka mzigo wa madeni.
Part 2 : Madeni
2 Wafalme 4 : 1 – 7
Basi Mwanamke mmoja miongoni mwa wake za wanafunzi wa manabii akamwendea Elisha, akamwambia, ” Mtumishi wako, Mume wangu amefariki, na kama ujuavyo alikuwa mcha Mungu, lakini aliyemwia ( kumdai ) fedha amekuja kuwa twaa wanangu wawili wawe watumwa wake “. Elisha akamuuliza , ” Sasa nikusaidieje ? Nambie kile ulichonacho nyumbani” .Mama huyo mjane akamjibu, ” Mimi mtumishi wako sina kitu chochote ila chupa ndogo ya mafuta” . Elisha akamwambia, ” Nenda kwa jirani zako uazime vyombo vitupu vingi kadri utakavyopata “. Kisah uende, wewe pamoja na wanao, mjifunge ndani ya nyumba, na muanze kujaza mafuta hivyo vyombo. Kila chombo mnachojaza kiwekeni kando. ” Mwanamke akaenda na kujifungia ndani ya nyumba na wanawe na kuanza kumimina mafuta ndani ya vyombo. Vilipojaa vyote, akamwambia mwanaye mmojawapo, “Niletee chombo kingine.” Mwanaye akamjibu, “vyote vimejaa!”
Hapo mafuta yakakoma kutiririka. Akarudi kwa mtu wa Mungu na kumweleza habari hizo. Na mtu wa Mungu akamwambia, “Nenda ukauze hayo mafuta na kulipa madeni yako, ndipo wewe na wanao mtaishi kwa kutumia hayo yatakayobaki”.
Mahubiri
Mpendwa Yule mwanamke analikuwa na bahati kwa sababu Nabii Elisha alikuwa na Mpango Mkakati ( Plan) na Ikumbukwe Elisha alikuwa nabii mkuu sana. Elisha aliuliza unanini Nyumbani ?, Hivyo nasi mpendwa hatunabudi kujiuliza tuna nini nyumbani mwetu kinachoweza kutumika kama usaidizi kwenye mipango mikakati ( Plan) ya utatuzi wa changamoto zetu?
Tukumbuke hadi hapa Elisha hajatazama juu Mbinguni wala kuomba hata alivyoambiwa na Yule Mke wa Mwanafunzi wake kuwa ana MAFUTA bado hakumuombea. Wengi wetu wapendwa tumekuwa tukiwaambia Watumishi watuombee madeni yetu yaishe na wanaotudai tupate kibali kwao watusamehe. Kwa andiko gani? hatuoni sehemu yoyote Nabiii Elisha anayakemea yale madeni???? Au ana simama katika unabii wake na kusema MADENI FUTIKA!, Hivyo basi tufahamu kuwa siyo sahihi kukesha tukiomba na kukemea madeni kufutika bali kuja na mpango sahihi wa kulipa madeni yetu na Mungu ni mwaminifu sana atatusaidia.
Mpendwa Elisha anampa yule mwanamke Mpango Mkakati ( Plan ) na kumwambia KAAZIME VYOMBO VYA KUTOSHA! na Tutambue katika maisha yetu ya sasa Nabii Elisha hayupo ila tuna Roho Mtakatifu pekee amabye tunatakiwa kukaa naye na kutengeneza Mpango Mkakati (Plan).
Baada ya Mwanamke kukamilisha mpango wa Elisha , Tunaona akimwambia jifungie na umimine ile chupa ya mafuta kwenye vyombo! Hapa tunaona Elisha akisimama katika nafasi yake ya Unabii na akiamuru ongezeko la mafuta mpaka yajaze vile Vyombo!. Mpendwa hii ni tofauti na wengi tunavyotaka kwani tunategemea muujiza wa kupata maombi na kukemea MADENI FUTIKA!.Mungu anamjibu kwa ongezeko la mafuta , na hivyohivyo hatasisi Mungu atatujibu kuendana na MIPANGO ( PLAN) tuliyokabidhi.
Mpendwa sasa tuone sadaka inaingiaje katika muujiza huu ?, Sadaka ndiyo inazigusa Mbingu ziachilie Muujiza, na Wewe Sio Nabii kama Elisha hata Uagize Muujiza Upewe ! , Bali unastahili kwenda kwa unyenyekevu mbele ya Mbingu ukizitoa dhabihu zako takatifu! na Mungu anaguswa zaidi na sadaka na moyo wa matoleo.
Tukumbuke Sadaka sio kile ulichonacho kulipa deni. Tuangalie kwa umakini ! Yule mwanamke aliulizwa unanini yaani kiongezwe kama mbegu ya kulipa Deni, Mpendwa hii haikuwa Sadaka , hapa sadaka ilikuwa ni huduma ya marehemu mumewe aliyetumika katika madhabahu ya Elisha!.
Katika maisha yetu ya kawaida ni kama una madeni na huna kazi wala biashara hivyo unaulizwa una nini nyumbani kwako kinachoweza kuongezwa kulipa deni.
Part 3 : Madeni
2 Wafalme 4 : 1 – 7
Basi Mwanamke mmoja miongoni mwa wake za wanafunzi wa manabii akamwendea Elisha, akamwambia, ” Mtumishi wako, Mume wangu amefariki, na kama ujuavyo alikuwa mcha Mungu, lakini aliyemwia ( kumdai ) fedha amekuja kuwa twaa wanangu wawili wawe watumwa wake “. Elisha akamuuliza , ” Sasa nikusaidieje ? Nambie kile ulichonacho nyumbani” .Mama huyo mjane akamjibu, ” Mimi mtumishi wako sina kitu chochote ila chupa ndogo ya mafuta” . Elisha akamwambia, ” Nenda kwa jirani zako uazime vyombo vitupu vingi kadri utakavyopata “. Kisah uende, wewe pamoja na wanao, mjifunge ndani ya nyumba, na muanze kujaza mafuta hivyo vyombo. Kila chombo mnachojaza kiwekeni kando. ” Mwanamke akaenda na kujifungia ndani ya nyumba na wanawe na kuanza kumimina mafuta ndani ya vyombo. Vilipojaa vyote, akamwambia mwanaye mmojawapo, “Niletee chombo kingine.” Mwanaye akamjibu, “vyote vimejaa!”
Hapo mafuta yakakoma kutiririka. Akarudi kwa mtu wa Mungu na kumweleza habari hizo. Na mtu wa Mungu akamwambia, “Nenda ukauze hayo mafuta na kulipa madeni yako, ndipo wewe na wanao mtaishi kwa kutumia hayo yatakayobaki”.
Mahubiri
Mungu ni Mungu wa maandiko. Kama alisimama na Elisha na Yule mwanamke hawezi kushindwa kusimama na wewe.
Mpemdwa kama nilivosema andaaa madeni yako yote, zungumza na Mungu jinsi yanavyokutesa kama ambavyo yule mama alitaka kuchukuliwa wanae. Yamkini yamekuvua utu wako na yame kudharaulisha kiasi kikubwa nakusihi zungumza na Mungu yeye ni mwaminifu sana.
UNASAIDIWAJE?, Mpendwa mwambie Mungu akusaidie vipi, ili uweze kulipa madeni yako. Kama ni kupandishwa cheo mwambie, kama ni mauzo kuongezeka mwambie, kama ni kukutanishwa wa wasaidizi wa hatima ( Destiny Helpers ) mwambie.
TARAJIA KUPOKEA MAJIBU! Yule mwanamke angekuwa 50/50 hakika asinge azima vyombo kabisa au angeazima vichache. kuwa na imani katika sala hii. Wahakikishie wadeni wako kwamba utawalipa hivi karibuni. Mpendwa imani ni vitendo , huwezi kusema una imani ilihali huweki vitendo. Achilia sadaka yako kwa imani na uaminifu kabisaaa. Subiria muujiza wako.
Hata kama wewe una dai. Katika andiko hili tunaona mdai alilipwa deni lake lote. Hivyo nawe hunabudi kusimama na andiko hili.Umsihi Mungu na wewe utalipwa deni lako.
IMANI NDO KILA KITU ILI UWEZE KUPATA MUUJIZA KATIKA CHANGAMOTO YAKO.