Laana ni tamko au neno la kutolewa kwa nguvu au mamlaka fulani, na mara nyingi linahusishwa na kutokubaliana au ghadhabu ya kiungu. Katika Biblia, kuna mifano kadhaa ya laana ambazo zimeelezewa kama hukumu au adhabu kutoka kwa Mungu au watu wengine.
Mithali 26 : 2
Kama shomoro katika kutangatanga kwake, Na kama mbayuwayu katika kuruka kwake; kadhalika laana isiyo na sababu haimpati mtu.
LAANA ISIYO NA SABABU HAIMPATI MTU.
Mpendwa zipo aina mbili za laana ambazo ni Laana ya kulaaniwa na watu na Laana ya kujilaani mwenyewe, na Laana zote hizi zinaweza kuleta athari katika maisha yetu.
Ukisoma Ayubu 2 : 19, 19 : 17 ; Mke wa Ayubu anamshawishi Ayubu amlaani Mungu ili aweze kufa na na kuepukana na magumu anayopitia nyakati hiyo. Aidha Ukisoma 2 Samweli 16 : 5 – 8 , 1 Wafalme 2 : 32 – 46 utaona Shimei ana MLAANI na kumtemea mate Daudi kwa kupora ufalme wa Saul. Joan anataka kumuua Shimei pale lakini Daudi anamzuia kwasababu anakubali kwamba anastahili hiyo laana kwani ni kweli alitenda kosa hilo.Lakini anakaa nalo rohoni na kumuhusia Joab asiruhusu Shimei akashuka kuzimu kuzimu na mvi zake zote yaani akamilishe jambo lao.
KUVUNJA LAANA
Wagalatia 3 : 13 – 14
Kristo alitukomboa kutoka katika laana ya sheria kwa kujitwalia laana hiyo kwa ajili yetu; Maana maandiko yanasema: “Yeyote aliyetundikwa msalabani amelaaniwa”.
Mathayo 16:19
Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni; na lolote utakalolifunga duniani, litakuwa limefungwa mbinguni.
Warumi 8 : 1 – 2
Sasa basi, hakuna hukum ya adhabu juu yao walio katika kristo Yesu. kwa sababu sheria ya Roho wa Uzima ule ulio katika Kristo Yesu umeniacha huru, mbali na sheria ya dhambi na mauti.
Ufunuo 12 : 11
Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana-Kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao; ambao hawakupenda maisha yao hata kufa.
SALA YA KUVUNJA LAANA
Mpendwa tutasimama na Wagalatia 3 : 13 kwa kila mmoja wetu kusema nakiri kuondolewa laana zotena kristo kwa kifo chake msalabani maana maana imeandikwa amelaaniwa yeyote aliyetundikwa kwenye mti, na Kristo pale msalabani alibeba laana zote ili niwe huru.
Katika jina la Yesu nasimika msalaba wake, damu yake, kifo chake, sadaka yake, ufufuo wake, maisha yake, mamlaka yake na utawala wake, naita hukumu kwenye kiti cha enzi cha Bwana wetu yesu kristo dhidi ya laana, uchawi na nguvu za giza.
Nainua laana ya Kristo msalabani dhidi ya laana zote zilizoinuliwa juu yangu kwa kuandikwa, kutamkwa au kurithiwa kwenye ukoo.
Laana ya kutokuolewa, kukosa kazi, kukataliwa na laana zote zilizo achiliwa juu yangu nainua Damu ya Yesu Kristo iliyomwagika msalabani dhidi ya sadaka zao za matambiko na vifungo vyote vilivyowekwa juu yangu kwa jina la Yesu.
SEHEMU YA PILI : SALA YA KUVUNJA LAANA
Namuinua Ysu Kristo mwana wa Mungu aliyrhai na aliyetolewa sadaka kwa ajili yangu dhidi ya Sadaka zao za Madhabahu na Madeni yote dhidi yangu.
Nainua kujitoa kwa Yesu msaabani dhidi ya chochote walichokitoa kunifunga na kunimaliza.Kwa Damu ya Yesu navunja laana zote juu yangu za kutamkwa kwa maneno, kuandikwa au kurithiwa.
Kwa jina la Yesu natangaza kuisha kwa uhalali wowote wa adui kunishika na kunitesa, shetani hana mamlaka na mimi tena kupitia madhabahu zake, sadaka wala nguvu zozote za giza.
Kupitia Damu ya Yesu niko huru. Asante Yesu niko huru sasa.
Naomba kuachiliwa kwa baraka ambazo Baba yangu wa Mbinguni ameziachilia kwangu kwa jina la Yesu kupitia waefeso 1 : 3 ! Naomba kupokea baraka hizo kwa jina la Yesu.