KUMUULIZA MUNGU JUU YA KITU AMBACHO HAKITOKEI HATA UFANYAJE AU KWANINI KIMETOKEA KILIVYO TOKEA 🔥

IS IT EVEN BIBLICAL KUULIZA ULIZA KWANINI?

YES! 💥
Jeremiah 33:3

“Call to Me and I will answer you and tell you great and unsearchable things you do not know.”

Ni 100% Biblical kuuliza! Lakini sasa — being Biblical doesn’t mean you just do it anyhow! 😤
Issue si kuuliza — ni UNAULIZA VIPI?
Hapo ndipo jibu linaweza kuja au lisije kamwe! Unaweza kuuliza jambo sahihi kabisa, lakini namna ulivyouliza ikakuzuia kupata majibu.

⚠️ WENGI MNAULIZA, LAKINI HAMJIBIWI!

Kwa nini? Kwa sababu hamfati utaratibu wa kimaandiko wa kumuuliza Mungu. Mnauliza kwa hasira, kwa roho ya kulalamika, au kwa “roho ya kudabukwa”! 😅
Unapomuuliza Mungu, unahitaji mtiririko, nidhamu, na unyenyekevu — siyo kelele na drama.

🙏 KAMA HUNA MAJIBU – ULIZA!

Wakati wa deliverance niliona kabisa – watu wengine walikosa majibu kwa sababu hawajawahi kumuuliza Mungu!
Wamekuwa wakiomba, wamefunga, wamezunguka, lakini hawajawahi kaa chini na kusema, “Bwana, kwa nini hili halitokei?”
Bila kuuliza, majibu yatatoka wapi? Situngi – Mungu yupo, uliza!

Lakini kumbuka — ukimuuliza Mungu, usimpangie lini atajibu.
Jeremia hakusema “Call to Me and I’ll answer you tomorrow at 8:00 a.m.” 😆
He said I will answer you! PERIOD.
Lakini hakutaja when — kwa sababu “when” ni yake Mungu, sio yako.

RULE #1: USIMPANGIE MUNGU MUDA

Ukimuuliza Mungu kitu, usimwambie ajibu kesho au ndani ya siku 7.
Atafanya siku itakayompendeza Yeye.
Wewe kazi yako ni kuendelea kuuliza, kugonga, na kutafuta bila kuchoka.
Bwana Yesu mwenyewe alisisitiza:
Luke 11:9-10

“Ask, and it will be given to you; seek, and you will find; knock, and it will be opened to you.”

Sasa wewe unamuuliza Mungu, lakini unaweka deadline — “Bwana hii wiki hii ya mwisho” 😤.
Sasa unaomba au unamlazimisha?
Wengi si kwamba Mungu kawa kimya — mwenyewe umejifungia mlango kwa kukasirika mapema.

RULE #2: JIONGEZE!

Kuna majibu hayaji bure.
Unataka kujua mambo yaliyo sirini? Lipa gharama! 🙌
Kuna majibu ambayo yatakuja tu ukijiongeza – kwa sadaka, kwa utii, kwa kujinyima, kwa ubinadamu wako kuvunjika.

Musa alijiongeza. Aliacha ikulu, akaenda jangwani.
Yule mwanamke alimpaka Yesu mafuta kwa machozi – alijiongeza, ndiyo maana Yesu mwenyewe alimtetea!
Jephthah alijiongeza, akatoa nadhiri — ghali sana — lakini Mungu akamjibu.

Wewe unataka majibu ya mbinguni lakini hutaki hata kufunga, kutoa, au kukaa uweponi wa Mungu!
Utajikuta unafanya “mifungo ya show” – hakuna mabadiliko, hakuna matokeo.

RULE #3: TULIZA MSHONO, SUBIRI JIBU

Baada ya kuuliza — kaa uweponi wa Mungu!
Usirushe swali na kusepa kwenye Netflix, Instagram, au umbea wa WhatsApp! 🙄
Majibu hayaji barabarani — yanakuja katika utulivu wa uwepo wake.

Mungu akijibu, atazungumza ndani ya utulivu, siyo kwenye kelele zako.

Daniel alifunga siku 21 – majibu yalichelewa kwa sababu ya mapambano ya kiroho, lakini hakuacha.
Wewe unataka uombe leo, kesho jibu, keshokutwa ushuhuda — siyo hivyo! 😅

RULE #4: USIMPANGIE MUNGU CHA KUSEMA

Ukishapanga unachotaka Mungu aseme, basi umemfunga mdomo.
Kama majibu yako ni lazima yaendane na matamanio yako, hutapokea chochote.
Ukimuuliza Mungu kuhusu mtu, biashara, au ndoa, lazima uwe tayari kusikia chochote – hata “NO!”
Ukiwa siyo tayari, Mungu atakaa kimya.
He doesn’t speak to stubborn hearts. ❤️‍🔥

RULE #5: UWE TAYARI KUMTII

Mungu si ATM ya majibu!
Wengi tunamtumikia Mungu ili tupate majibu, badala ya kumtumikia kwa upendo na uhusiano.
Ukionyesha kwamba majibu yatakuondoa katika uwepo wake, Mungu mwenyewe atayazuia kwa upendo — akuepushe usipotee.

Deuteronomy 31:8

“The Lord Himself goes before you; He will be with you; He will not leave you nor forsake you.”

Ukibaki uweponi, hata kabla ya majibu, utakuwa salama!

NJIA ZA KUMUULIZA MUNGU VITU (BIBLICALLY APPROVED)

 

1️⃣ “Tatu Kavu” – 72 Hours of Fasting (Esther Fast)

Funga siku 3, unakunywa maji tu.
Soma Kitabu cha Esther chote, tafakari, kaa uweponi.
Usitoke kwenye uwepo, usichafue na dhambi ndogondogo.
Usipojibiwa — rudia! Hata mara 20!
Usifanye kwa show — ni vita ya kiroho.

2️⃣ Siku 7 za Masaa 12

Kama mwili umeanza kugoma, hii ni bora zaidi.
Mfano ni Mfalme Daudi baada ya mtoto wake kuugua.
Funga saa 12 kila siku kwa siku 7.
Unakula chakula rahisi kama ugali na maharage au uji bila blueband.
Usijifanye “Ramadhan ya kikristo” kwa mazoea – kaa uweponi wa kweli!

3️⃣ 21 Days Daniel Fast

Ni mimea tu! Hakuna nyama, hakuna maziwa, hakuna utamu!
Ni “serious seeking mode.”
Usi-google tu kwa haraka — soma kitabu cha Daniel, fahamu spirit ya fasting hii.
Funga, omba, meditate.
Mungu atazungumza – kwa uhakika!

4️⃣ 40 Days Fast – The Level of Jesus, Moses & Elijah

Hii ni ngazi ya juu ya imani.
Ni mfungo wa maamuzi, nidhamu, na roho iliyokomaa.
Ukipiga hii — majibu lazima yaje.
Ni mfungo wa ukamilifu, wa wito, wa maamuzi makubwa.
Ukiwa bado hujawahi kufika 40, bado mtoto kimaspiritu! 😅
Hapa ndipo majibu ya hakika yanatoka.

🕊️ CONCLUSION

Kumuuliza Mungu si kosa — ni imani ya juu.
Lakini namna unavyouliza, moyo ulio nao, na uvumilivu wako ndivyo vinavyobeba majibu yako.
Usimdanganye Mungu, usimpangie muda, usimwambie nini aseme, na usiogope majibu yatakayokuja.
Endelea kuuliza, endelea kungoja, endelea kutii.
Mungu siyo binadamu — Yeye ni DEITY, a Supernatural Being!
Heshimu uwepo wake, tambua ukuu wake, na kaa kimya kusikia.

🔥 MAMBO YA MUNGU SIO MICHEZO. MUNGU SIYO WA KUPANDIWA KICHWANI.
UKILETA KIBURI, UTAKUWA JIVUUU KAMA WANA WA AARON. 🔥

“God is not mocked. What you sow, you shall reap.”
(Galatians 6:7)

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Scroll to Top