KUMTUMIKIA MUNGU KUKIWA LIFE STYLE YAKO HUWEZI SUMBUKA

Watu wengi wanamtumikia Mungu kama kazi, jukumu, au task nyingine nzito tu kwenye ratiba zao za maisha. Hii ndiyo sababu wengi hudumu kwenye ibada kwa muda mfupi—wanachoka, wanavunjika moyo, au wanaacha kabisa.

Lakini kama kweli kumtumikia Mungu ni sehemu ya lifestyle yako, hautasumbuka kamwe. Kama vile ambavyo kuoga na kula ni sehemu ya maisha yako ya kila siku, vivyo hivyo kumtumikia Mungu lazima kuwe kawaida yako. Ukishafika kwenye kiwango hicho, ibada inakuwa siyo changamoto—bali raha!

 

SPIRITUAL DISCIPLINE NA BIASHARA YANGU

Mwaka wa tano sasa, nina affirmations za biashara ambazo nazitamka kila asubuhi. Najiuliza:
“Mimi ni nani kwa Yesu?”
“Natawala nini?”
“Kwa andiko gani natabiri mafanikio yangu ya leo?”

Nikisahau kufanya haya, daftari la mauzo linanikumbusha haraka: “Ulifanya nini asubuhi? Si ulijifanya busy?”
Basi nalo linaandika: “Kula chuma, hikooo!”

 

MBINGU NI WASHIRIKA WA BIASHARA YANGU

Nina mikutano na Mungu na Roho Mtakatifu 24/7 kuhusu kila kitu kinachoihusu biashara yangu. Mbingu siyo tu mshauri—ni mshirika wa karibu. Sifanyi mikutano ya dharura tu na Mungu juu ya biashara; nimevuka level hiyo!

Na yes, huwa nakesha nikitafuta majibu. Mara nyingi kinachosumbua asubuhi, jioni nina jibu tayari. Ni neema!

 

NAFASI NA CHEO KAZINI? ANZA NA MBINGU KWANZA

Unataka cheo kazini lakini ni mtoroo wa ibada?
Mbingu zikuamini vipi wakati hata ushirika wa kawaida huna nao?
Kama wiki nzima hupigi hata story na mbingu, unataka zipate wapi ujasiri wa kukupendekeza? Uhusiano wako na mbingu ni vuguvugu, lakini unategemea zikutetee kwenye nafasi kubwa? Haiendi hivooo!

Cheo ni matokeo ya kushikilia nafasi yako rohoni kwanza. Ukikalia hiyo nafasi rohoni, mbingu zitakupa “files” za watu unaowaongoza. Ukishindwa bado, wewe ni mzembe tu!

 

ROHO MTAKATIFU: SIRI YA MAFANIKIO YANGU

Mimi siwezi kutoa rushwa ili nipate taarifa. Nina Roho Mtakatifu.
Kuna wakati mtu alikuwa anauza bidhaa kutoka China. Watu walikazana kupata chanzo chake—wakashindwa!
Wakaja kwangu, nikamwuliza Roho Mtakatifu.
Jibu? “Ngoma iko Uturuki.”
Wakabisha, wakagoma. Nikaenda Uturuki nikakuta bidhaa hiyo kwa mikono yangu.
Mpaka leo, wanadhani mfanyakazi wao aliwauzia siri. Hapana! Siri ni Roho Mtakatifu!

 

UJASIRI WA KIROHO HAUJI BURE

Watu wanashangaa kwa nini mbingu zipo kimya. Nakwambia:
Haziwezi kuongea na wewe kama hutaki hata kuwa karibu nazo.
Mnataka “adooo adooo” tu—kwenda mbele za Mungu na kutoka na majibu kama ATM. Hapana!
Uhusiano wa kweli na Mungu hujengwa, hauchukuliwi kwa mkato.

YOHANA 4:21-24 – IBADA YA KWELI

“…Wabudu wa kweli watamwabudu Baba katika roho na kweli, maana hao ndio Baba anaowatafuta…”
(Joh. 4:23)

Kabla hujamwabudu Mungu, lazima kwanza umjue, umwamini na umkubali. Ndipo ibada yako inakuwa ya kweli.
Watu wanamkubali Mungu kwa kinda kinda tu—wakati hali inayotakiwa ni ile ya moyo ulioridhia kabisa.

Ukishamkubali, kufanya unachotakiwa kufanya kwake haionekani tena kama kazi, bali furaha.

 

USITAFUTE VITU, TAFUTA UHUSIANO NA MUNGU

Wengi wanamwendea Mungu kutafuta ndoa, kazi, biashara, au uponyaji.
Lakini ukweli ni kwamba, ukipata uhusiano wa kweli na Mungu, utapata vyote na zaidi ya hivyo!

Ni mara chache sana mtu anakuja kwangu akiwa na kiu ya kweli ya kumjua Mungu wangu—wanaokuja wanataka peanuts, si mtu aliye nyuma ya peanuts.
Kama huwezi kutamani kile Elisha alichotamani kutoka kwa Elia, hujatambua kilicho muhimu bado!

 

DELIVERANCE SI SHORTCUT

Watu wengi wanaomba waondolewe vizuizi, lakini ukweli ni huu: Vizuiwi vinatoka kwa kujifunza, kukua, na kuchukua hatua.
Mimi nitakufundisha tu—“I will only teach you the ropes.”

 

ENZI ZA KIU YA NENO ZIMERUDI?

Zamani mtu akibatizwa kwa Roho Mtakatifu, alikuwa na nguvu za ajabu—hatua yake ya kiroho ilikuwa dhahiri!
Siku hizi mtu yuko radhi atoe bahasha ili tu uulize kwa niaba yake kwa Roho Mtakatifu. Like seriously?!

 

SIRI YA KUDUMU: JENGA UHUSIANO NA MUNGU KATIKA KAZI YAKO

Una kazi nzuri? Hongera.
Lakini kama hutaweka Mungu ndani ya kazi yako, kazi hiyo itakukalia kama mzigo.
Uwepo kazini kama zombie, huombi, hulipi zaka, husemi lolote kiroho—halafu unataka breakthrough?

 

KUHUSU NDOA…

Mtu ameachwa, sasa anataka Mungu amletee ndoa mpya.
Lakini hajajifunza chochote. Nikamwambia, “Usipojifunza, utafika vyuo 12!”

Wanaume si mchezo! Hakikisha kwanza Mungu yuko ndani ya maisha yako.
Ukifanya hivyo, Mungu mwenyewe atakutafutia mume anayebeba utukufu wa mbinguni.
Game over!

 

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Scroll to Top