“If anyone would come after me, let him deny himself and take up his cross and follow me.”
— Matthew 16:24 | Mark 8:34 | Luke 9:23
Hii si maneno ya kupunguzwa au kusummarize, bali ni agizo lililo wazi na kali! Yesu anasema wazi: Unapotaka kumfuata lazima ukatae nafsi yako, uchukue msalaba wako, na umfuate. Hili halimaanishi ni mchezaji wa ligi ya chini au mtu mwenye tabia dhaifu. Kumfuata Yesu ni uamuzi wa mtu hodari, aliye tayari kuachilia maisha yake yote, kupoteza kile anachopenda, kuachana na mitazamo, maadili ya dunia, na kumfuata yeye na njia zake.
“If you would be perfect, go, sell what you possess and give to the poor, and you will have treasure in heaven; and come, follow me.”
— Matthew 19:21 | Mark 10:21 | Luke 18:22
Kumfuata Yesu si kwa wanyonge wala wenye mawazo rahisi. Kumfuata Yesu ni kujitoa, kuacha maisha yako ya zamani, hobby zako, matarajio, na hata mafanikio uliyojenga. Wengi wamechanganyikiwa, wanadhani Yesu atawafuata kwa ugeni au kwa maneno machache tu. Hapana! Mungu hafuati viungo vya mwili bali moyo na nafsi. Wengi wapo kwenye ‘kudanganywa’ kwamba Mungu atapotea kutoka ngazi zake na kuja kwako. Hili ni upuuzi wa wazi kabisa.
WHO FOLLOWS WHO?
Maandiko yamekua crystal clear: sisi watu ndiyo tunapaswa kumfuata Mungu, si Mungu kumfuata mtu! MUNGU HAKUWATAKI WANAFUATE WATU, LAKINI WANAFUATA SHIDA ZAO. Hii ni hatari sana. Unaweza kufuata shida zako popote zitakakuchukua—na zitakuangamiza hata makanisani na watumishi wake wote.
Nimekuta watu wengi hawamtafuti Mungu, bali wanatafuta suluhisho la matatizo yao. Hawawezi kuachana na matatizo na bado wanasema wanamfuata Mungu! Wanabadilisha makanisani kila mara kama nguo, wakidai wanatafuta neno la Mungu lakini ni majibu ya changamoto zao wanayotafuta. Hii ni dharau kwa wokovu.
KUTOA ZAKA NA KUMFUATA MTUMISHI?
Mtu mmoja nilizungumza naye, mpagani, alilalamika kwanini anatoza zaka lakini pastori hawezi kumsaidia kwenye tatizo lake. Hii ni akili ya kibinadamu kabisa! Kutoa zaka sio kumfanya pastori awe mmiliki wako, wala awe chombo cha kukudhibiti. Kutoa zaka ni kwa Mungu, sio kwa mtu!
Wengi mnaonekana kumfuata pastori badala ya Mungu. Hii ni biashara ya kipuuzi. Mtumishi ni mtu, na kama mtu ana makosa au hakuwa mzito kama unavyotegemea, si sahihi kumfuata kwa upuuzi. Hii ni sababu nyingine ya watu kuachana na imani halisi.
NIJIJUA NAFSI YANGU KWA MAKINI!
Kumfuata Yesu ni kuikataa nafsi yako. Huwezi kumfuata Yesu ukiifuata nafsi yako. Kila unapochagua kupenda nafsi yako zaidi ya Mungu, unamkana Yesu. Kila unapochagua kiburi, chuki, au tamaa badala ya kutii maandiko, unamkana Yesu.
ROMANS 10:9
“If you confess with your mouth the Lord Jesus and believe in your heart that God has raised Him from the dead, you will be saved.”
Lakini kusema maneno haya si mwisho wa safari. Kumfuata Yesu ni maamuzi ya kila siku, yenye nguvu, na usimamizi wa maisha yote yako. Haijalishi unavyosema, kama maisha yako hayaendani na maneno, bado haujawa mfuasi wa kweli.
NI UAMUZI LEO, HALIJAWEZEKANA KURUDI NYUMA
“I have decided to follow Jesus.” Hii si kauli ya mchezaji wa kumdharau Mungu au mtu wa kupotea roho. Ni uamuzi wa maisha, si chaguo la kuibadilisha mwendo wowote utakaoona unafaa.
Kama unadhani kuokoka ni mchezo, basi utapotea. Kama bado una woga, au hujui maana halisi ya kufuata Yesu, basi jipe muda usome maandiko na tafakari. Usitafute suluhisho za changamoto zako badala ya kutafuta Mungu.
NI UAMUZI MZITO NA MGUMU
Kumfuata Yesu ni kupita giza, mateso, kuteswa, na hata kupoteza mambo ya dunia—lakini mwisho wake ni uzima wa milele. Usijaribu kumfuata kwa upuuzi. Jikumbuke, mtu asiyebeba msalaba wake hawezi kuwa mwanafunzi wa Yesu (Luke 14:27).
HITIMISHO
Nimeamua kumfuata Yesu, si kwa machozi au kwa maneno tu, bali kwa moyo wangu wote, kwa dhamira isiyoyumba. Siku zote najikumbusha, uamuzi huu si wa kurudi nyuma. Hii ndiyo njia ya wokovu halisi na maisha ya milele.
Uamuzi ni wako leo. Utamfuata Yesu kweli kweli, au utaendelea kuifuata nafsi yako, matatizo yako, au hata watu?
Nimeamua, siwezi kurudi nyuma. I have decided to follow Jesus—na wewe je?