Extreme Career Program – Devil Let Me Go To Work

7 days fasting deliverance program (9 Feb – 15 Feb)

Ideal for who?

  1. Hujawahi pata kazi yoyote ya maana maishani mwako.
  2. Unateseka na kunyanyasika kazi zote unazopata, hujawahi kupata kazi na kuwa na amani kazini na furaha.
  3. Unachofanya hakilingani na qualification zako, ni vile huna jinsi tu mkono uende kinywani.
  4. Familia yenu wote au almost mna patterns za kuwa na nobodies going nowhere career wise.

What is the program about?

Tutazingatia sana mambo ma 4 makuu.

  1. Kurekebisha misingi ilioharibika na ikakuharibia career path yako.

So kuvunja uta-vunja sanaa, uta-renounce, uta-kana. You will work so hard my love! Hakuna maombi ya kusema aminaaa. Hakunaaa! Wewe unahisi vinavyokuzuia kwenda kazini vidogo sasa? Lazima tujipange.

  1. Kufungua vifungo vinavyokufunga wewe na familia yako mpaka mnaishia hivyo.

Wewe ambaye unajidekeza na kujiona hujui ndio utajua Jumatatu jinsi ya kwenda front na kumsemesha shetani aliye nyuma ya your failed career life atoke. Mimi nakuninstruct tu. Mimi maagano ya kwenu ya mfe bila kazi za maana yanahusu nini? Nasema yavunjike kama nani? Yakinuliza huna ukoo wenu au shobo tu? Najibu nini?

Wewe uliye fungwa ndio utaenda kwa Pharao na kumwambia “Pharao let me go.” Balaa litaanza akisema “I won’t.” Ndio tutajua hiyo Jumatatu. Jinsi Pharao atakavyo kuja ndivyo tutakavyo mpokea. Be strong. Jitie moyo. Unataka kwenda kazini hutaki?

  1. Restoration.

Mungu akufidie muda uliopotea ukiwa mateka na umri uliokutupa mkono. Sababu kufunguliwa tu haitoshi. Muda usha kuhukumu.

You are almost 40 yrs uanze officer kweli? Si by 60 utakuwa manager au utakuwa una-stafu.

Restoration ni muhimu. Mungu akufidie fidie hasara ulioipata kwa kukaa magereza ya giza.

  1. Divine speed.

Kama nilivyokwambia muda usha hukumu na haupo mkononi mwako. Wenzio tuna nyumba 3, 3 kwa career hizi hizi tulizosoma wote chuo. Wewe uanze kazi leo utatufikia kweli si utakata tamaa.

Lakini divine speed ni tool ya Mungu kukupa mileage za fastaaa na matokeo ya haraka kukufidia tena muda uliopotea kwenye gereza la nguvu za giza.

Kwa hiyo wewe njoo na amani zote. Kwamba sio tu kutufikia unaweza kutuzidi mbali kabisa.

Prophet Elijah aliachwa na Mfalme Ahab masaa 6. Mind you Ahab alikuwa king using chariot of fastest horses in the whole kingdom. Na ongeza hayo masaa 6 ya kutangulia Jezreel. Lakini Elijah aliyekuwa kwa mguu mkono wa Mungu ulikuwa nae akafika wa kwanza Jezreel kabla ya Mfalme Ahab na msafara wake kudadaadekii.

Njia za Mungu hazichunguziki.

Why should you bank on this program? Umefanya program nyingi hazijakupa matokeo?

Hosea 12:13–14.

And by a prophet the Lord brought Israel out of Egypt, and by a prophet was he preserved.

Sababu zinaweza kuwa nyingi ikiwemo nabii wa kukamilisha exodus yako kutoka kukosa ajira ulikuwa hujapata.

Sawa umemlilia Mungu miaka na miaka hata wa Israel walimlilia Mungu muda mrefu. Siku ya siku akamtuma Musa akafanye jambo lake.

Exodus 3:7.

And the Lord said, “I have surely seen the affliction of My people who are in Egypt, and have heard their cry by reason of their taskmasters, for I know their sorrows.”

Kuwa kama wana wa Israel msaada wa Mungu kufika wakaudaka juu juu. Nenda kwa Pharao bwana wewe Musa. Hawakutaka hata kujua Musa katokea wapi au kivipi. La msingi mshipa wa kwenda kwa Pharao anao. Exodus iendelee mengine baadaye.

Shukuru Mungu Musa nimejileta ghafla sana. Nilikuwa nimejificha wapi kivipi niachie Mwenyewe. We focus na Pharao akuachie.

Swala lako ni chronic? Do I have the qualifications and up to the task?

Kiukweli sina qualification yoyote. Nipo kimchongo mchongo tu. Sina bachelor ya divinity. Sina hata certificate ya divinity. Sijasomea uchungaji wowote popote. Usiwe mwepesi kukata tamaa.

Which is excellent for you uache kufocus kuniangalia mimi umuangalia Yesu aliye nyuma yangu. Focus na who matters.

Yesu hakuwa mjinga kuchagua mitume watu wa kuokoteza wasio na qualification za maana na mwizi Yuda Iskariote yule, Petro mvuvi, wengine wakulima, tafrani. Hata mimi nimepita pita skuli japo mambo yangu sio mazuri.

Ukiningalia mimi au mtumishi yoyote kwa vifungo vyako tumesha feli. Siviwezi wala mtumishi wako haviwezi. Ataweza vipi roho zina karne karne duniani? Si uongo wa reja reja.

Lakini Yesu Kristo Mwokozi aliyekaa kuume kwa Baba ndio kazi zake hizi. Alizijia duniani na hata Jumatatu ikibidi aje tena kwa ajili yako kwa kazi hizo sio shida zake. Just believe.

Yohana 10:10.

Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu. Mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele.

Yesu anataka uwe na uzima na uwe nao tele hilo eneo la ajira.

Yohana 19:30.

So when Jesus had received the sour wine, He said, “It is finished.” And bowing His head, He gave up His spirit.

Kazi ya ukombozi Yesu alisha ikamilisha. Hakunaaa kilichobakia. Alimaliza kila kitu.

Kama Yesu alimaliza kila kitu miaka 2000 iliyopita mbona bado wewe umefungwa?

Yohana 8:32.

Tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru.

Kweli gani unayoijua hapo ulipo? Lazima uwe kifungoni.

Mshukuru Mungu pamoja na ubabaifu wangu wote na michongo yangu yote kweli ya ukombozi alioikamilisha Bwana Yesu miaka 2000 iliyopita naijua. Naijua kindakindaki. Na Jumatatu nitakupa hiyo kweli bure. Ushindwe wewe tu.

We njoo na akili zako timamu tu. Ukijua kweli hiyo Jumatatu itakuweka huru.

Ukombozi wetu toka nguvu za giza usha kamilika miaka 2000 iliyopita. Kinachotufelisha ni kwamba hii kweli hatuijui. Ndipo shetani anapotushikia.

Wewe umepelekwa mahakamani sheria hujui inasema vipi, haki zako huzijui, hujafungwa tu? Kifungo cha maisha kitakuhusu.

Jumatatu nimejipanga kwa case yako. Maandiko yamejitosheleza ni kureference tu. Lazima utoke gerezani. Bwana Yesu kazi alisha ikamilisha na chawa nipo vere vere kushadadia uhuru wako. Na maandiko ninayo. Nimejipanga.

Mahakama ya ulimwengu wa roho itakuwa ndogo Jumatatu.

“Oooh tunamdai bibi yake alikuwa ngariba huyu kauwa vigori wengi sana.” Nakuja na wigi la kondoo lile jeupe la ma-judge. Ni kweli bibi yake alikuwa ngariba na uhalali upo kweli, lakini maandiko yanasemaje?

Ezekiel 18:20.

The soul that sinneth, it shall die. The son shall not bear the iniquity of the father, neither shall the father bear the iniquity of the son.

Muachieni aende kazini kabla sijavua hili wigi la kondoo.

Isaya 43:26.

Unikumbushe, na tuhojiane. Eleza mambo yako, upate kupewa haki yako.

Upele umepata mkunaji. Shaka ondoa. Tajiri wa maandiko nipo upande wako. Huwezi kushindwa safari hii.

Njoo na akili zako timamu tumalize kazi hii.

Nawaomba hii program ifanyike na watu wa hapa hapa sababu it’s an extreme program.

Sio nyepesi kwa mgeni. Day 1 tutamwacha mataa ya Ubungo, afu om zitakuwa nyingi maskini. Maana anatamani ila ndio mpagani pro max.

Extreme program inataka walau uwe unajua jua hata kama sio sana. Umekaa hapa kidogo na una idea hata kwa mbali utajikongoja.

So don’t invite new people. I know wamekuchosha na unataka wapate kazi. Lakini hii ni complex program napita short cuts. Watabaluzza baluzza tu.

Ila nyie wa humu nawategemea muache ubabaifu na mstand up for yourself for once kumwambia devil let me go to work.

You can do this. Jesus is behind you. Nawategemea.

Marko 9:23–25.

Jesus said to him, “If you can believe, all things are possible to him who believes.” Immediately the father of the child cried out and said with tears, “Lord, I believe; help my unbelief.”

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Scroll to Top