CAN ANYTHING GOOD COME FROM NAZARETH?

John 1:46

46 And Nathanael said unto him, “Can there any good thing come out of Nazareth?”

SOMETIMES UNA PITIA MAPITOOO MOB MPAKA UNAJIULIZA: “KUNA LOLOTE JEMA KWELI LINAWEZA KUTOKEA KWENYE HAYA MAPITO?”
Sometimes unaamini kabisaaa jema la kutokea ni hayo mapito kupita salama tu! Hamna jema zaidi ya hilo!

YAMKINI upo stage ya maisha ambayo unaona NYOTA NYOTA TU! Moja haikai wala 2 haisimami! Kila mtu kwenye maisha yako ni kama Nathanael—ana jiuliza:
“KUNA JEMA LOLOTE LINAWEZA KUTOKA KWAKO KWELI? KABISAA KABISAA LIKAONEKANA KWA MACHO? SIDHANI!”

YAMKINI umekaa muda mrefu sana bila kazi wala kipato.
YAMKINI umri umeenda bila mwenzi.
YAMKINI hujabahatika kupata uzao.
YAMKINI umeachika na watoto wako wa 4!
YAMKINI wewe ni mjane na kila mtu amekubadilikia.

Unapitia mapito, umeliaaa mpaka machozi huna tenaaa!
Moyo umeumaa mfululizo mpaka umekuwa sugu sasa. Mwanzo uliona isipotokea utakufa, lakini kwa ulipofikia una uhakika unaishi ili uteseke na hicho kitu—na siku kikitokea, kifo chako hakipo mbali; dunia ndo ina kuaga hivyo.

Umengoja mchana usiku, ikawa DECADE NZIMAAAA!
Hakuna kilichotokeaaa!
Watu wakoambiaa “FLANI!!!”
Wana STUKAAAAAAA!
“FLANI?? INAWEZEKANA KWELI KWAKE?”

NAOMBA NIKUTIE MOYO JIONI YA LEO!

Mungu haja kusahau!
Wala hawezi kukusahau!
Wala haitowahi kutokea yeye kukusahau.

Isaiah 49:14–16

14 But Zion said, “The Lord hath forsaken me, and my Lord hath forgotten me.”
15 “Can a woman forget her sucking child, that she should not have compassion on the son of her womb? Yea, they may forget, yet will I not forget thee.”
16 “Behold, I have graven thee upon the palms of my hands; thy walls are continually before me.”

Mungu anasema mzazi anaweza kusahau kichanga chake—ila sio Yeye kukusahau wewe, mja wake.

Kumbuka habari za Yusufu!

Kuanzia ndugu zake kutaka kumuua—ndugu zake wa damu kabisaaa. Baadaye kumuuza utumwani!
Imagine, baba yako tajiri, amepambana mpaka na malaika akashinda na jina wakampa, halafu wewe unauzwa utumwani kwa bei ya jioni! (Hapa umetia chumvi.)

Imagine anaenda utumwani kupiga mzigo, hana kinyongo—kazi anazifanya kwa moyo mmoja!
Mke wa Potifar anaelewa mzigo wa kiyahudi. Anamkomeshaaa bila kumkosea chochote zaidi ya kumnyima dudula yuyu tu. Anafungwa gerezani.

Imagine umeota ndugu zako wanakusujudia halafu wewe—umechill Ndichi! Kitu cha lockup!
Na wauwaji, waporaji, wabakaji na waovu wengine.
Na hakukaaa wiki! Alikaa miaka 2 gerezani.
Wiki tu bila mtandao mmedata—ndo miaka 2!

USIPOMKUFURU MUNGU NA KUAMUA LIWALO NA LIWE, LABDA SI WEWE.

Kisha likaja breakthrough!
Yeye kuwa msimamizi mkuu wa Misri!
Wengi stage hii hawafiki, maana pale pale kuuzwa utumwani, mnamaliza biashara na Mungu.

Kuna kipindi Mwamposa ilitokea ajali kwenye mkutano wake na watu walikufa.
Kwa sababu fulani serikali ikamuweka ndani for weeks—ina chunguza.
Imagine mtumishi wa Mungu umechill zako mahabusu? Hiyo 9,10 ni watu waliokuweka ndani kumuita kwenye mikutano yao bila haya wala kuona vibaya awaombee na kuwanga mkono! Na yeye hana kinyongo.

TB Joshua (RIP) pia aliwekwa ndani ilipotokea ajali kwenye hotel yake. Alikaa lockup muda mrefu sana.
Akasema: “Kama imani yangu haikufa kipindi hiki, basi haifi tenaaaa! Ata zikwa nayo.”

THINGS CAN TURN TO THE WORST—WORST THAN YOUR IMAGINATIONS.

2 Corinthians 4:8–18

We have troubles all around us, but we are not defeated.
We often don’t know what to do, but we don’t give up.
We are persecuted, but God does not leave us.
We are hurt sometimes, but we are not destroyed.

Hutakiwi kuyumbaaa kwenye imaniii kizembe.
Kama shida ushakulaaa, kilichobakia ni kujikaza na kukomaaa mpaka upate TUZO—sio uwe umekula shida za bure bure.

1 Corinthians 16:13

Be on your guard; stand firm in the faith; be courageous; be strong.

1 Corinthians 15:57

But thanks be to God, who gives us the victory through our Lord Jesus Christ.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Scroll to Top