📖 Zaburi 23:1
“The LORD is my shepherd; I shall not want.”
ISSUE SIO KUUJUA HUU MSTARI, ISSUE NI KUUAMINI, KUUSHIKA, NA KUVUKA NAO MAPITO!
Unaweza kuwa na maarifa ya Biblia yote—kutoka Mwanzo hadi Ufunuo—lakini moyoni mwako huamini wala kuishi hata andiko moja! Si kama uzinzi tu!
👉 Unajua Mungu amekukataza kutenda zinaa,
Lakini bado unazini kama kwamba hakuna kesho!
Swali ni: JE, UNA IMANI KIASI GANI KWA MUNGU?
Kwamba mradi tu BWANA ndiye Mchungaji wako, basi HUTAPUNGUKIWA NA KITU???
Mtu anamwomba Mungu kazi. Mungu anamjibu hadi anaenda interview.
Lakini badala ya kuendelea kumtegemea Mungu, anaanza kuwatafuta watu wamsaidie ‘kumchomeka’ huko kazini, akidhulumu haki za wengine!
Anaona watu ni bora kuliko Mungu ambaye alimpeleka kwenye interview hiyo!
Mwingine anaomba mume kwa bidii. Mtu wa kwanza anayekuja anamwambia “tufanye zinaa kwanza” na anakubali, ili tu aolewe!
Anapendelea kumfurahisha mzinzi, aolewe naye, badala ya kumfurahisha Mungu wake!
Halafu huyo jamaa asipomuoa kwa sababu amejirahisisha, anamwita cheap slut, not wife material—na unakuja tena kulaumu Mungu!
WENGI WETU TUNAROPOKA TU!
“BWANA NDIE MCHUNGAJI WANGU,” lakini hakuna tabia za kondoo!
Mara nyingi tunaonyesha tabia za mbwa mwitu, halafu tunataka Mungu aheshimu ahadi yake aliyoitoa kwa kondoo wake watii!
TUMEKUWA WOLVES, JAMANI! A PACK OF WOLVES!
Unaweza kusema:
“BWANA NDIE MCHUNGAJI WANGU SITAPUNGUKIWA NA KITU KATIKA CAREER YANGU!”
Lakini zaka za Mungu zote unazifyekaaa!
At least ulipa pungufu… lakini HAPANAAA!
Ukiamua kutenda dhambi, unaifanya kwa ukamilifu!
Halafu unajiuliza,
“Mbona sikipandi kwenye kazi yangu?”
“Kila siku napitwa kwenye promotions!”
Wengine wanasema:
“BWANA NDIE MCHUNGAJI WANGU SITAPUNGUKIWA NA MUME”
Lakini kila siku unamegwa kiselaaa!
Upwiruuu mtumishi unaimaliza akili!
Unadhani unapenda?
Unaendelea kujiuguza, kuumia, na kujichubua moyo!
📖 Yohana 10:27–30
“Kondoo wangu waisikia sauti yangu; nami nawajua, nao wanifuata. Nami nawapa uzima wa milele; wala hawatapotea kamwe; wala hakuna mtu atakayewapokonya katika mkono wangu. Baba yangu aliyenipa hao ni mkuu kuliko wote; wala hakuna mtu awezaye kuwapokonya katika mkono wa Baba yangu. Mimi na Baba tu umoja.”
Kuwa kondoo wa Mungu si maneno tu!
👉 Inahitaji kuisikia sauti ya Mungu!
👉 Inahitaji kutii amri zake!