Mpendwa race sio Marathon! By the term Raceshort distance, high speed, quick results, sweet victory yaani katika lugha ya kiswahili tunamaanisha umbali mfupi, kasi zaidi, matokeo ya haraka na ushindi kwa hali ya juu. Aidha Mpendwa Ukiamua kuchukua Marathon approach kwenye maritual journey yako ni sawa tu! Cha muhimu ni kufika lakini hautafaa sana na moduli yetu.
Race isn’t cheap, isn’t easy either! Kwani unachallenge odds nyingo kwa wakati mmoja, You need to be strong, determined, focused, calculated and highly ambitious! Do you have what it takes?.
Kwa upande wangu naona wengi mnasifa hizo lakini mnacheza na timu mbaya yaani ulivyo mkamilifu kwenye kuwakatisha watu tamaa ya ndoa kwa kuwaambia ndoa sio deal! Ni kama umezaliwa kufanya hivyo yaani unakila kitu ni kwamba uko katika timu mbaya.
Is it a Godly Move to Race?
Like I told you God is Neutral! Hivyo wewe tu ukitaka njia defu au fupi yeye yupo flexible na pia shortcut sio dhambi jimalize tu mwenyewe as long as the means justifies the end. Mpendwa kuna maandiko watu walisubiria na kuna maandiko watu waliomba SPEED yaani waliomba mambo yaende kwa haraka na yote ni maandiko matakatifu aidha yote yako at your disposal.
Racing is only for the strong it aint for the weak so it’s very okay to take your time.
Should You Race?
Yes , Why not? Ume-race mambo mangapi maovu na machafu and you are perfectly fine! May be wounded a little moyoni lakini you survived! How can you not handle a little challenge? After all it’s a biblical challenge, You have played softball in your life! A little upgrade won’t kill you. After all remember the speedy and sweet victory at the end of this. Finally you get to show the successful smile to all Baals in your life!, Mpendwa Mabaali yote yaliyokuonea unamalizana nayo mazima.
Do you have what it takes ?
Of course you definitely do! Matter of fact I’m rooting for you, nakuamini sana hivyo kama mimi nakuamini inakuwaje wewe hujiamini? You are stronger than you think! Ingia kwenye race ujishangaze.
Can you do it?
Yes you can!, Absolutely! , you have my total confidence! You got this and You will win against all odds this time, I promise! Just believe in yourself TRUST THE INNER YOU.
Are you a Racer?
Hell no! until now you are a waiter! All you do is wait for things to be handed to you.To be honest you are a total LOSER! That’s why you keep loosing, kuna vitu ambavyo unajiendekeza kuwa kuvuka ni ngumu,Wewe ni loser na wanaume wanajua kuwa wewe ni loser hivyo automatically life sets you up for one demise after another!. Therefore, the only way to win is RE INVITING YOURSELF to this whole new you who is not a loser like you are now!. People don’t Wifey you up because you are not a Wife! , Not a bad person but definitely not a Wife! na ili kushinda ni kujiweka tayari na katika viwango amabayo watu wakikuona hawamuoni Loser wanayemuona sasa bali Mke.
What am I racing Against?
-
OLD LOSER YOU
Mpendwa kitu cha kwanza itakulazimu kujitambua na kujua thamani yako. Kuacha kuendelea kujifunza uongo wote kuwa huna thamani, Aidha wanaume wanakuvunja vunja ili waweze kukutumia ila Gundi ipo tutaunga hivyo vipande vipande vyako na wakirudi hawana bahati!!!, You will race against your old bad habits mpaka uwe NEW YOU yaani utashindana dhidi ya zile tabia mbaya zako au ule uzamani wako mpaka uwe mpya.
-
SOCIETY
Society break and dismantle you to fifth kama haija ku-humble down!! It will part you!! We are all victims of our society! , Huenda jamii ilikufanya au kukulazimisha kuzaa bila ndoa, Mpendwa you wil race to travail above society and it’s bullshit.
-
THE KINGDOM OF DARKNESS
Mpendwa shetani atakujaribu kwelkweli, lakini usimpe nafasi hata mara moja.
Will God Show Up and Shout Out for You?
Yoshua 1: 5
Hakuna mtu atakayekushinda siku zote za maisha yako.Na nitakuwa pamoja nawe kama nilivyokuwa pamoja na Musa, Daima nitakuwa nawe wala sitakuacha kamwe.
Mpendwa kwenda na Mungu maana yake ni kwenda kinyume na nafsi yako ovu, kinyume na jami na kwenda kinyume na shetani mpaka hapo uko upande mmoja na Mungu, na hakika atajithibitisha kwako kwa sababu umemchagua yeyey dhidi ya udhalimu
Bridal Race :Month of Detoxification
Over the years watu wanakwambia vitu vingi na vingi kati ya hivyo vimekudisapoint na kukuvunja moyo na vingine vinaishi katika kichwa chako, na muda mwingi vina influence na kuchangia asilimia themanini (80%) ya maamuzi yako, kwa mfano unaweza kukuta mwanaume humpendi lakini ukikumbuka watu wanakwambia umri umeenda utazeeka mwenyewe basi unaanza kukubali wanaume ovyo ovyo. Mpendwa life is nothing but a game of perception! Kushinda you have to have a perception of a winner yaani Maisha ni mchezo ya dhana,fikra na mtazamo na ili uweze kushinda lazima uwe na dhana,fikra au mtazamo wa ushindi.
Huenda walikwambia kuwa wewe ni mbaya! Kwani Watu wangapi ni wabaya zaidi yako na wana ndoa nzuri tu! , Huenda walikwambia kuwa wewe ni Bonge kwani Vibonge wangapi wana ndoa?, Huenda walikwambia wewe hujasoma? Kwani wangapi hawajasoma na wana watu wao?, Huenda wamekwambia wewe umezaa kabla ya ndoa? Kwani wangapi wameolewa na watoto zaidi ya watatu (3) hata sio huyo mmoja wa kwako?, hivyo chochote unachojihukumu nacho ni ujinga kwa sababu wapo watu wanahivyo vitu tena hata zaidi na wana ndoa zao zimestawi vizuri tu.
Mpendwa shida ya kujihukumu unakuwa unajishuku muda wote yaani unakuwa na mashaka na unaacha kuwa reasonable! Jambo amabalo linakupelekea wewe mwenyewe kubomoa mahusiano mazuri uliyonayo kwa in-security zako na muda unavyozidi kusonga mbele unachosha! Kiasi ambacho hata mwanaume kama alikuwa na nia na wewe anashindwa kwa sababu ya Too much insecurity! na Too Much Drama!.
Kama una motto unaanza kujihisi tu mwanaumwe huenda hampendi motto huyu kwa sababu sio mtoto wake yaani Mwanaume hajafanya chochote lakini wewe ushaweka vikwazo kuwa ili uamini mwanaume anakupenda lazima ampende na motto wako ni ujinga ( Nonsense!!). Biologicaly hata wanyama wanapenda wanapenda vyao tu! Hauwezi kukuta kuku anapenda kifaranga cha mwenzie. Hivyo mpendwa ukimpenda wewe na ndugu zako inatosha. Mpendwa kosa moja la kuzaa kabla ya ndoa lisikupofushe kiasi cha wewe kufanya makosa mengine ya kumlazimisha mwanaume wako kuwa baba wa motto wa mwenzie, Mpendwa katika mfano hai , Sisi kwetu Mtu akizaa kabla ya ndoa na kuolewa na mtu mwingine, kipindi anaenda kwa Mumewe haruhisi kwenda na mtoto huyo na jina la mtoto anampatia la ukoo wetu, Huo ndio ukweli kwani huyo mtoto ni wetu wala sio wa huyo Mume.
Mpendwa baadhi yetu tunajiona kutokuwa salama kwa sababu ya maumbile yetu au muonekano. Ila inabidi tujiulize kwani Mwanaume alivyo tuona hakuona hao wengine wenye makalio makubwa? Kwanini alikufata wewe?, Lakini kwa sababau uko katika insecurity ukiona mwanaume anaonge na mwanamke au mdada mwenye makalio makubwa unakuza kosa! You get mody! Unaanza attitude!, Na kwa sasabu yeye hajaona wala kuwaza kile ulichokiona wewe anakuona ni mwanamke kisirani tu na kadri muda unavyozidi kwenda tabia zako hizo zinapita lile jema ulilokuwa nalo , hadi mwanaume anashindwa na kuamua kukuacha. Hivyo Mpendwa unatakiwa kupona hizo insecurity zako , You are perfectly fine! Totally and Completely!
Mwanzo 1: 26
Kisha Mungu akasema,”Tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu”
Mpendwa Mungu amekuumba kwa sura na mfano wake, How can you be not perfectly fine?. Shida yetu weng tunaamini watu kuliko maandiko, na lazima watu wakutikise na kukughadhibisha ili kukuweka katika viwango ambavyo utakuwa dhaifu ili wakutumie vizuri na njia pekee ya kuepukana na haya ni kubadili mtazamo wako na kuuona ukuu wa Mungu kwenye maisha yako kwa kuanza kuona yo deserve good things and good things can happen and should happen to you.
Mpendwa unastahili wanaume wazuri kwani huna kasoro yoyote na hakuna kinachokuzuia wewe kubadilika , hakipo zaidi ni wewe kufanya uamuzi mmoja na kuusimamia.
Mpendwa kupona na kuweza kujitoa utumwani Babeli inachukua muda. Siyo kitu unachoweza kukifanya ndani ya siku moja (1), ni suala linalotokea polepole ,kidogo kidogo na baada ya muda unajikuta umekuwa mtu mwingine lakini pia kujirudi katika hali hii inachukua muda.
Mpendwa haitakuwa rahisi kushindana (doing the race) lakini you will have to try harder, Overtime utakuwa umeshinda in-security zako.Mpendwa nitakuwa nikiwaletea shuhuda nyingi sana kutoka pande zote za dunia hii ili kuwadhihirishia kwamba inawezekana ,unaweza kuinuka na kutoka katika gereza lako.
Mpendwa nitakuwa nikiwapa weekly convictions za kudeclare juu yako, maisha yako na hatima yako kila siku asubuhi na jioni.Mpendwa hizi convictions zitakusaidia kubadilisha ushuhuda mbaya ulio moyoni mwako, mashaka mashaka na wasiwasi.
Mpendwa mwezi huu kazi ni moja tu ,kudetoxify mindset zetu na kujitoa utumwani Babeli kifikra na kiakili.
Maritual Breakthrough Devotions
Mpendwa kabla ya kuanza program hii nipende kukupa angalizo kama ifuatavyo;
Iandae akili yako na kufanya uamuzi wa dhati kama unafanya program hii yaani unafanya mashindano (Are you racing?) or hufanyi , kama bado unahisi kwa kiasi Fulani bado upoupo kwenye zinaa kwanza hakika utavuna ubatili.
Aidha kama unaona umemaliza yaani ni suala la muda urudi kwa Baba kama kuzini umezini sasa na umefanya mambo yanayomuudhi Mungu ya kila aina,kila size na unaona hakuna jipya na hivi sasa unaona ukatayari kurudi kikamilifu, hakika hivi sasa ni muda sahihi (Perfect Timing) , ni wakati ulioamriwa,fanya mashindano (Do the Race).
Mpendwa kuchanganya mambo kutakuweka katika nafasi mbaya mno kwani Mungu na Shetani wote watakuwa hawakuelewi na wote watakupiga kwa wakati mmoja. Mwisho wa siku huyo Bwana unayezini nae atakuacha na Mungu atakufungia milango na madirisha, Hivyo Moendwa nakusihi uchague upande yaani PICK YOUR SIDE.
Declaration and Commitment
Mwanzo 24: 15
Kabla hajamaliza kuomba, mara Rebeka, Binti Bethueli, Mwana wa Milka, kewe Nahori, Ndugu yake Abrahamu akafika amebeba mtungi wake begani.
Declaration
My marriage shall happen SPEEDLY in jesus name. Kama Mungu alivyomjibu mtumishi wa Ibrahimu muda uleule alipotokea Rebeka, eo hii atanijibu na mimi ili mwenzangu aweze kutokea kutoka popote pale alipo.
Mwanzo 32: 26
Akasema ,Niache niende maana kunapambazuka. Akasema sikuachi usiponibariki.
Ee Bwana ,Sawasawa na Mtumishi wako Jakon alipong’ang’ania Baraka kutoka kwa Yule malaika mapaka ukambariki na mimi leo hii nag’ang’ania Baraka zako na maritual breakthrough siachilii wala siyumbi, mpaka unibariki leo, sio kesho wala wakati mwingine.
1 Mambo ya Nyakati 4: 10
Huyo Yabesi akamlingana Mungu wa Israeli, akisema Lau kwamba ungenibariki kwelikweli, na kuipanua mipaka yangu, na mkono wako ukawa pamoja nami, nawe ungenilinda nisipatwe na maovu wala madhara! Naye Mungu akamjalia hayo aliyoyaomba.
Mungu Baba kama ulivyosikia maombi ya mtumishi wako Yabesi, na kumjaila aliyoyaomba hapo hapo na kwa wakayi huo huo leo hii nisikie na mimi, nibariki nikutane na mwenzangu mwenye nia njema na wewe, tukafunge ndoa takatifu na kuanzisha familia naomba hayo kwa jina la Yesu.
MY MARRIAGE SHALL HAPPEN SPEEDLY IN JESUS NAME! 2023 IS MY YEAR!
Are you read for your miracle?
Wengi mnajiuliza hivi kweli Mungu anataka niolewe? Ni kweli anataka na iko wazi katika maandiko yake matakatifu. Mpendwa hiki ndicho unatakiwa ukijue,ukiamini na kukishikiria na Mpendwa wengi sio kwamba huko nyuma hamkujibiwa, huenda mlijibiwa lakini mkayumba kiimani na miujiza ikapotea.
Mathayo 14: 30
Lakini alipouona ule upepo, aliogopa akaanza kuzama; akalia kwa sauti, “ Bwana, niokoe!”
Petro alimuomba Yesu muujiza wa kuelea kwenye maji na alipewakabisa lakini alivyoanza kuogop akadoubt muujiza kuyeyuka na ikatokea, Hivyo mpendwa jiandae Mungu akikupa SPEEDY MARRIAGE usiruhusu watu wakaanza kukuyumbisha kuwa ni mapema sana, hamjajuana vizuri sana, pata muda umchunguze yaani uache kumwamini Mungu uliyemuomba uanze kuamini akili zako na watesi wako hakika Muujiza utayeyuka mapema.
Acha Mawazo Potofu yanayofunga hatima yako leo hii
Mwanzo 2 : 18
Bwana akasema, si vema huyo mtu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye
Mpendwa haya ni maandiko ya kitabu cha kwanza kabisa kwenye biblia katika aya ya pili (2) na Mungu ndiye aliyetamka maeno haya kwa kinywa chake! Hilo wazo la kwamba Mungu ndiye amekusubirisha, Mungu ndiye anataka kujitukuza kwa upweke wako na machozi yako kwa zaidi ya miaka 10 ni batili kwani Mungu alishasema toka zamani si mwenzio ukawa peke yake lazima apate msaidizi ambaye ni wewe. Je ni andiko gani hapo ambalo Mungu amesema nitakutesa na upweke ili nijitukuze kupita wewe?
Isaya 34:16
Tafuteni katika kitabu cha BWANA mkasome; “ Apana katika hao wote aliyekosa kuwapo, hapana hata mmoja atakayemkosa mwenzake; kwa maana kinywa change kimeamuru na roho yake imewakusanya.
Mpendwa ile mitazamo ya Ooh Wanaume ni wachache, ni wakutafuta sana na kung’ang’ania au Mimi nimezeeka siwezi tena kupata Mume, Mimi ni mbaya ndio maana sitongozwi , Mimi sina Makalio, ni mfupi , wa kijijini au nimezaa nyumbani nimeshajiharibia, au sijasoma wanaume wanataka wasomi, ni mitazamo batili na haifai. Andiko liko wazi kabisa TAFUTENI KWENYE KITABU CHA BWANA MKASOME, HAPANA HATA MMOJA ATAKAYEKOSA MWENZIE KWANI KINYWA CHAKE KIMEAMURU! , Mpendwa hili sio OMBI ni AMRI, Hivyo kwa vyovyote vile ulivyo mtu wako yupo ni vile hamjakutana tu, hivyo nenda sasa mbele za Mungu ukijiamini na ukijua Mutu wako yupo muombe aweze kukukutanisha naye na hakika mtakutana.
2 Wakorintho 6: 2
Kwa maana asema, wakati uliokubalika nalikusikia, Siku ya wokovu nalikusaidia: tazama wakati uliokubalika ndiyo sasa; tazama siku ya wokovu ndiyo sasa.
Mpendwa ule mtazamo wa wakati wa Mungu bado ni Wakti gani?, Hii nichangamoto ya kusoma biblia vipande vipande! Wakati ulioamriwa waliosema wakina Isaya ulishafika siku nyngi sana! Yesu mwenyewe alithibitisha wakati ndiyo huu, yeye alishakuja kumaliza matatizo yote yakiwemo matatizo yako, Hivyo unavyobakia wewe mwenyewe na nabii Isaya anakushangaa kwani umejichanganya sana kwani Agano jipya ulioni?
Mpendwa futa kabisa hayo mawazo yako ya wakati wa Mungu bado. Nimekuoa andiko la ushindi. Ijaze akili yako kwamba wakati ulioamriwa na kukubalika na Mungu ni sasa , hivyo muombe Mung uolewe. Hii ndiyo iwe conviction yako, kama vile kinywa cha mwanaye kipenzi aliyependezwa naye kilivyokiri kwa kusema WAKATI NI SASA! NA SASA YAKO NI 2023 HAKUNA WAKATI MWINGINE.
Yohana 4: 35
Hamsemi ninyi, Bado miezi mine ndipo yanakuja mavuno?, Tazma mimi nawaambieni, inueni macho yenu mtazame mashamba, yakuwa yamekwisha kuwa meupe, tayari kwa mavuno.
HALELUYA GOD IS SO GOOD!!.
Mpendwa hii yote inakuja kwa kujua Moyo wako unakiri nini?, Moyo wako uki-kiri wakati wako wa kuolewa bado hakika utazidi kukawia, uki-kiri wewe ni mzee itakuwa halisi kila kijana atakuona mzee kwake , ukikiri huwezi kupata mume kwa sababu Fulani hiyo sbabu itajitukuza.
Mpendwa mbingu zilishamaliza hizi debate kwa maamndiko yaliyonyooka moja kwa moja kama Yeasu anavyosema “Wakati uliokubalika ni sasa”, Sasa wewe unakazania nini kuwa kuwa wakati bado?.Mpendwa mbingu zimeshaweka msimamo wake kuwa wakati ni sasa.
Mpendwa nimeenda kwa kina ili kukuonesha vitu sambamba na maandiko matakatifu ili kukuonesha kwa uhalisia kuwa vitu vingi unavyodhani vinakuzuia usiolewe ni batili na ujinga kabisa na maandiko yanakanusha.
Luka 17: 21
Wala hawatasema, Tazama upo huku au kue kwa maana tazama ufalme wa Mungu umo ndani yenu.
Mpendwa huenda ndani yako kumejaa upinzani na kumalizika kabisa, unawezaje kufanya mabo yatokee nje? Kwa sababu unachokiri ndani yako ni kushindwa hivyo unajiua mwenyewe. HOW CAN YOU WIN ON THE OUTSIDE? BADILISHA UKIRI WAKO SASA.
Mithali 23: 7
Maana aonavyo nafsini mwake, ndivyo alivyo.
Mpendwa ukijiona umeshinda hii ngori na mwaka 2023 ni mwaka wako. I tell you hata shetani mwenyewe atashindwa kukuzuia, hata mizimu ya kwenu itashindwa. UKIJIONA UNAOLEWA 2023 IT WILL COME TO PASS.
Warumi 12:22
Wala msifuate kanuni za dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza na ukamilifu.
Now you know better! Acha kujitembeza kumbi za usiku ukidai unataka kutoka ili uweze kuonekana! Utang’atwa na mbu tu! Na wakati mwingine mtu atataka kulala nawe na kuondoka!. Mpendwa achana na njia za dunia hii kwani ni ngumu sana! Mungu wako ana nguvu sana! Acha mtazamo wa kuwa Rebeka likuwa anajitebeza usiku kama popo?, Kuwa mtulivu mtoto wa kike.
Mathayo 9: 29
Ndipo alipowagusa macho akasema, Kwa kadiri ya imani yenu na itendeke kwenu.
Mpendwa hili suala tumeshalimaliza na litatendeka kama unavyo amini na Mpendwa hakikisha unaaamini mambo ya msingi na yatakayokupa ushindi kama una amini mambo yasiyosahihi hakika utavuna mabaya.
2 Wakorintho 4: 18
Tusiviangalie vinavyoonekana, bali visivyoonekana. Kwa maana vinavyoonekana ni vya muda tu; bali visivyoonekana nivya milele.
Mpendwa usikae na kujiaminisha na mitazamo ya ovyo kama Valentine ya 6 niko single! Ni ujinga! Neon la Mungu linasema hakuna atakaye kosa mwenzie, Wewe angalia hapo mpendwa na waza mwenzio yuko wapi? Na nini kina mchelewesha?
Mathayo 21: 21 – 22
Yesu akawajibu, “Kweli nawaambieni kama mkiwa na imani bila ya kuwa na mashaka manaweza si kufanya tu hivyo bali hata mkuambia mlima huu “ Ng’oka ukajitose baharini, itafanyika hivyo, Na mkiwa na imani chochote mtakachoomba kwa sala, mtapata”
Asante sana mama nimesoma nimepata nguvu Naomba Mungu anisaidie
Amen, Mungu ni Mwaminifu sana.