AUGUST DELIVERANCE – DAY 1 – 7

DAY 1

Scripture Reading: Obadiah 1:17
“But on Mount Zion will be deliverance; it will be holy, and Jacob will possess his inheritance.”

KUNA UKOMBOZI KAMILI

Kwa kila mwana wa Mungu, kuna ukombozi kamili. Yesu Kristo amelipa gharama za ukombozi wetu. Kwa hiyo tuweke mahitaji yetu kwenye altare ya maombi. Tupambanie kupokea urithi wetu halali na ushindi wetu.

PRAYER POINTS

  1. Oh Lord, I receive deliverance today from every evil pattern from my father’s house in JESUS Name.

  2. The God that delivered David from the lion, bear, and Goliath shall deliver me from every giant of my life in JESUS Name.

  3. Oh Lord, judge every strong man and woman in my life and deliver me totally from their hands in JESUS Name.

  4. Oh Lord, deliver me from all oppressions of the marine world in my place of work/business, the house I live, and my family in JESUS Name.

  5. Oh Father, you are the All-Powerful GOD, show yourself strong and deliver me from those who are too strong for me in JESUS Name.

  6. Oh Lord, deliver me from all forms of spiritual attack from marine and witchcraft spirits in JESUS Name.

  7. Oh Lord, deliver me from any spiritual weapon fashioned against me and my household in JESUS Name.

  8. Oh Lord, I disconnect myself from every spiritual husband and spiritual wife in JESUS Name.

  9. Oh Lord, by your mercy deliver me from all evil friends in JESUS Name.

  10. Oh Lord, plead my cause with them that strive with me and fight against those who fight against me in JESUS Name.

  11. Oh Lord, deliver me from this evil addiction (Mention the addiction) that is trying to ruin me in JESUS Name.

  12. Oh Lord, deliver me from the guilt of bloodshed in JESUS Name.

  13. Oh Lord, deliver me from the hands of wicked and unreasonable men in JESUS Name.

  14. Oh Father, let the wickedness of the wicked fall upon them, save my soul from the snare of the wicked in JESUS Name.

  15. Oh Lord, deliver my soul from every evil beast that seeks to devour me in JESUS Name.

  16. I receive deliverance today from the evils of the wicked world in JESUS Name.

  17. Oh Lord, deliver me from the spirit of Lust in JESUS Name.

  18. Oh Lord, by your Holy Spirit in me continue to guide me; may I not miss it in life in JESUS Name.

  19. Oh Lord, by your mighty power, deliver me from all my troubles in JESUS Name.

  20. I prophesy today that I and the children the Lord has given unto me are immune from the wickedness and perversions of this world in JESUS Name.

  21. Oh Lord, because your thought towards me is good, cause my life to flourish continually in JESUS Name.

  22. I declare that by the blood of Jesus Christ I am free from every form of bondage in JESUS Name.

  23. Oh Lord, deliver me from all things that are pulling me backwards in life and destiny in JESUS Name.

  24. I lose myself from every satanic force that is holding me down in JESUS Name.

  25. Oh Lord, deliver me from the spirit of lies and vulgar words in JESUS Name.

  26. Oh Lord, deliver me from all battles prepared against me in JESUS Name.

  27. Oh Lord, send me help my Father, for vain is the help of man in JESUS Name.

DAY 2

Scripture Reading: Zaburi 91:1-16

Anayekaa chini ya ulinzi wa Mungu Mkuu, anayeishi chini ya kivuli cha Mungu Mwenye Nguvu, ataweza kumwambia Mwenyezi-Mungu: “Wewe ni kimbilio langu na ngome yangu; Mungu wangu, ninayekutegemea!”

NENO LA MUNGU

Hakika Mungu atakuokoa katika mtego; atakukinga na maradhi mabaya.
Atakufunika kwa mabawa yake, utapata usalama kwake; mkono wake utakulinda na kukukinga.

Huna haja ya kuogopa vitisho vya usiku,
wala shambulio la ghafla mchana;
huna haja ya kuogopa baa lizukalo usiku,
wala maafa yanayotokea mchana.

Hata watu elfu wakianguka karibu nawe,
naam, elfu kumi kuliani mwako,
lakini wewe baa halitakukaribia.

Kwa macho yako mwenyewe utaangalia,
na kuona jinsi watu waovu wanavyoadhibiwa.
Wewe umemfanya Mwenyezi-Mungu kuwa kimbilio lako;
naam, Mungu aliye juu kuwa kinga yako.

Kwa hiyo, hutapatwa na maafa yoyote;
nyumba yako haitakaribiwa na baa lolote.
Maana Mungu atawaamuru malaika zake,
wakulinde popote uendapo.
Watakuchukua mikononi mwao,
usije ukajikwaa kwenye jiwe.

Utakanyaga simba na nyoka,
utawaponda wana simba na majoka.

AHAIDI ZA MUNGU

Mungu asema:

“Nitamwokoa yule anipendaye; nitamlinda anayenitambua!
Akiniita, mimi nitamwitikia;
akiwa taabuni nitakuwa naye;
nitamwokoa na kumpa heshima.
Nitamridhisha kwa maisha marefu,
nitamjalia wokovu wangu.”

DAY 2 CONTINUA …..

Ukiridhika na hali yako unaweza kuona Shetani sio mbaya sanaaaa!
Taka ushindi hata mdogo… ndo utamjua vizuri.

Kama umesharidhika na kazi yako ya sook, huna makuuu, unachopewa unapokea—unaweza kuona the devil is not real!
Walokole ni just dramatic people who overdo everything!
Catholic is the religion to go! Masaa yako 2 Jumapili is all it takes.

JICHETUEEEE!

Jichetueee… utake hata mshahara wa 2 million tu to better yourself!
Ndo all hell will set loose!

Boss wako yule yule atakununia na anaweza hata kukuchapa makofiii!
Kila interview ukipigwa not selected for oral ndo utajua Shaïtwan Rajeem kweli kweli!

Kakuwekea mguu wa shingo, na 40yrs zako Gen Z wanakudhalilisha kwenye interview—hataríiii!
Unatamani hata malaika washuke!

It takes grace to finally accept you are good for nothing after all.

Utaanza kuona Catholics are not praying! Pentecostal are a joke!
Utatamani ukae maombini na uweponi 24/7!

Wewe tenaaaa! Unaona dini sahivii hawaombi kabisaaa… nyakati za mwisho hiziii.

UKIKAAA UNAFANYA UMALAYA…

Ukikaa unafanya umalaya huwezi kuona ubaya wa Shetanííí!

Ubaya gani wakati mabwana unapataa na wanakuhonga pesa nzuri…
You live the baby girl lifestyle!
All you have to do is open your kitumbuaaaa… baaaasssss!

SASA WEWE MAMA MUUZA…

Jaribu ku-retire na kuolewa… ndo utamjua kama Shaïtwan ni Rajeem!

Oraa! Jaribu hata kuolewa na the most poorest, uneducated, total trash man per your standard…
Uone kama Shaïtwan ataruhusu hata hio offside!

Heheheheheheee! Thubutuuuuu!

Yani kwa wanaume ulio-omokaaa nao na waka kuhongaaa…
Ukiwalinganisha na mwanaume unae foul-isha kuolewa nae… ni uchafuuu kwa waleee…

Lakini na veve atakataa katuuu katuuu kukuoa!
Na itakuumaaaa sanaaaa sanaaa… sababu he is nothing and absolutely trash kwako na portfolio yako…
Lakini he also looked down on you big time!

Minal Shaïtwan Rajeem!
Ndo utamjua Shetani sasa vizuríííí!

NDO UTAELEWA…

Ndo utaelewa kwanini walokole wakipambana na Shetani wanatoka mpaka jasho mwili mzimaaaa!
Wameonja kipigo chake kitakatifuuuu.

Ukiona huna upinzani wa Shetani… jua hufanyi kitu chochote cha manufaaa kwako.
Tayari upo anapokutakaaaaa.

Jichetue!
Kutaka vikubwáaaa… ndo utamjuáaaa!

THINK ABOUT IT…

If you are not applying for jobs… you won’t get rejected!
If you are not investing in your business… you can’t go bankrupt!

Kama hutafuti ndoa na heshima… hakutakuwa na mwanaume mbaya kwako!

Maana unavotaka na wao wanataka hivo hivo…
Uwape utamuuu na wao wakupe pesa.

Ukiona vipizaa watoto wako ambao hawata wakubali na kuishi nao…
Sana wakikufirikía… watakupa jina lao tu lisilo na urithi, lisilo na chochote.

Huwezi kuwa na vita kwenye mahusiano yako… vita ganíííí?

DAY 3

Scripture Reading: Warumi 8:1-11

1. Kwa hiyo basi, sasa hakuna tena hukumu kwa wale walio ndani ya Kristo Yesu. 2 Kwa maana sheria ya Roho wa uzima katika Kristo Yesu imeniweka huru kutokana na sheria ya dhambi na mauti.

3 Mungu amefanya lile ambalo sheria ilishindwa kufanya kwa sababu ya udhaifu wa mwili wetu wa asili. Mungu aliihukumu dhambi kwa kumtuma Mwana wake wa pekee katika hali ya mwili kama sisi, ili awe sadaka kwa ajili ya dhambi.

4 Kwa kufanya hivyo, Mungu ametutimizia matakwa ya haki ya sheria kwa kuwa sasa maisha yetu yanaongozwa na Roho na wala hatuishi tena kwa kufuata matakwa ya mwili.

5 Kwa maana wale waishio kwa kuongozwa na asili yao ya dhambi, hukaza mawazo yao kwenye mambo ya mwili; bali wale waishio kwa kuongozwa na Roho hukaza mawazo yao katika mambo ya Roho.

6 Matokeo ya mawazo yaliyotawaliwa na tamaa za mwili ni kifo; lakini mawazo yaliyotawaliwa na Roho huleta uzima na amani.

7 Watu wenye mawazo yaliyotawaliwa na mambo ya mwili ni adui wa Mungu. Watu kama hao hawakubali kutii sheria ya Mungu, na kwa kweli hawawezi.

8 Watu wanaotawaliwa na mwili, hawawezi kumpendeza Mungu.

9 Lakini ninyi hamuishi kwa kufuata matakwa ya mwili, bali mnaongozwa na Roho; ikiwa kweli Roho wa Mungu anaishi ndani yenu. Mtu ye yote ambaye hana Roho wa Kristo, yeye si wa Kristo.

10 Lakini kama Kristo anaishi ndani yenu, ingawa miili yenu imekufa kwa sababu ya dhambi, roho zenu zinaishi kwa sababu mmekwisha kuhesabiwa haki.

11 Na ikiwa Roho wa Mungu ambaye alimfufua Yesu kutoka kwa wafu anaishi ndani yenu, Mungu aliyemfufua Kristo Yesu kutoka kwa wafu ataipatia uzima miili yenu ambayo hufa, kwa njia ya huyo Roho wake ambaye anaishi ndani yenu.

PRAYER POINTS (Kutoka DAY 1)

  1. Oh Lord, I receive deliverance today from every evil pattern from my father’s house in JESUS Name.

  2. The God that delivered David from the lion, bear and Goliath shall deliver me from every giant of my life in JESUS Name.

  3. Oh Lord, judge every strong man and woman in my life and deliver me totally from their hands in JESUS Name.

  4. Oh Lord, deliver me from all oppressions of the marine world in my place of work/business, the house I live and my family in JESUS Name.

  5. Oh Father, you are the All-Powerful GOD, show yourself strong and deliver me from those who are too strong for me in JESUS Name.

  6. Oh Lord, deliver me from all forms of spiritual attack from marine and witchcraft spirits in JESUS Name.

  7. Oh Lord, deliver me from any spiritual weapon fashioned against me and my household in JESUS Name.

  8. Oh Lord, I disconnect myself from every spiritual husband and spiritual wife in JESUS Name.

  9. Oh Lord, by your mercy deliver me from all evil friends in JESUS Name.

  10. Oh Lord, plead my cause with them that strive with me and fight against those who fight against me in JESUS Name.

  11. Oh Lord, deliver me from this evil addiction (Mention the addiction) that is trying to ruin me in JESUS Name.

  12. Oh Lord, deliver me from the guilt of bloodshed in JESUS Name.

  13. Oh Lord, deliver me from the hands of wicked and unreasonable men in JESUS Name.

  14. Oh Father, let the wickedness of the wicked fall upon them, save my soul from the snare of the wicked in JESUS Name.

  15. Oh Lord, deliver my soul from every evil beast that seeks to devour me in JESUS Name.

  16. I receive deliverance today from the evils of the wicked world in JESUS Name.

  17. Oh Lord, deliver me from the spirit of Lust in JESUS Name.

  18. Oh Lord, by your Holy Spirit in me continue to guide me, may I not miss it in life in JESUS Name.

  19. Oh Lord, by your mighty power, deliver me from all my troubles in JESUS Name.

  20. I prophesy today that I and the children the Lord has given unto me are immune from the wickedness and perversions of this world in JESUS Name.

  21. Oh Lord, because your thought towards me is good, cause my life to flourish continually in JESUS Name.

  22. I declare that by the blood of Jesus Christ I am free from every form of bondage in JESUS Name.

  23. Oh Lord, deliver me from all things that are pulling me backwards in life and destiny in JESUS Name.

  24. I lose myself from every satanic force that is holding me down in JESUS Name.

  25. Oh Lord, deliver me from the spirit of lies and vulgar words in JESUS Name.

  26. Oh Lord, deliver me from all battles prepared against me in JESUS Name.

  27. Oh Lord, send me help my Father, for vain is the help of man in JESUS Name.

DAY 4

Scripture Reading: Waefeso 6:10-18

10 Hatimaye, muwe imara katika Bwana na katika nguvu zake kuu.
11 Vaeni silaha zote za Mungu ili mpate kusimama na kupingana na hila zote za shetani.

12 Kwa maana hatupambani na binadamu, bali tunapambana na tawala na mamlaka na nguvu za ulimwengu huu wa giza na majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.

13 Kwa hiyo, vaeni silaha zote za Mungu ili mpate kusimama imara siku ya uovu itakapokuja; na mkishafanya yote, mtakuwa bado mmesimama.

Kwa hiyo simameni imara mkisha jifunga na kweli kama mkanda kiunoni na haki kama kinga ya kifuani; na kuvaa Injili ya amani kama viatu miguuni, ili muweze kusimama barabara.

Zaidi ya haya yote, jivikeni imani kama ngao ambayo itawawezesha kuzuia mishale yenye miale ya moto kutoka kwa yule mwovu.

Vaeni wokovu kama kofia ya vita kichwani na chukueni upanga wa Roho ambao ni neno la Mungu.

Ombeni wakati wote katika Roho, katika sala zote na maombi. Kwa hiyo muwe macho na siku zote endeleeni kuwaombea watu wote wa Mungu.

MAELEZO YA VITA VYA KIROHO

For we wrestle not against flesh and blood, but against principalities, against powers, against the rulers of the darkness of this world, against spiritual wickedness in high places.

THE THING ABOUT PRINCIPALITIES:
Umeziona na utaacha ziko vile vile. Umezaliwa umekuta watu hawaolewi, utakufa utaacha hawaolewi vile vile. It is a principle.

POWERS:
Wana nguvu za kufanya wanachotaka muda wanaotaka. Bila Higher Power ya Mungu, unabaki mateka wao.

RULERS OF DARKNESS:
Hawa wanamiliki nguvu za giza, wanahakikisha katiba ya giza inatekelezwa.

SPIRITUAL WICKEDNESS IN HIGH PLACES:
Hawa wako nyuma ya wachawi, maagano ya giza, na nguvu zote za kipepo.

TOFAUTISHA DELIVERANCE YA SHOW NA YA KWELI

Show deliverance ni ile ya mikutano, drama, na makelele. The real deal ni vita ya kiroho ya kweli – kupigana na nguvu za giza moja kwa moja.

Kama hujasoma Injili, hujui silaha za kiroho, huna imani, wala wokovu, hutashinda.

SILAHA ZA KIROHO

  • Mkanda wa Ukweli: Jua ukweli wa Mungu. Bila neno, huna mkanda.

  • Kinga ya Haki: Uishi maisha matakatifu; bila haki, huna ulinzi kifuani.

  • Viatu vya Injili: Uisome Injili; bila Injili, huwezi kusimama imara.

  • Ngao ya Imani: Kuzuia mishale ya adui kwa imani isiyoyumba.

  • Kofia ya Wokovu: Utambulisho wako upatikane katika Kristo.

  • Upanga wa Roho: Neno la Mungu ndilo silaha ya kushambulia adui.

MAOMBI

Ombeni wakati wote katika Roho, katika sala zote na maombi. Endeleeni kuwaombea watakatifu wote, mkisimama imara kwa silaha za Mungu, bila kuogopa vita vya kiroho.

DAY 5

Warumi 6:14-16

14 Kwa maana dhambi haitakuwa na mamlaka juu yenu kwa sababu hamtawaliwi na sheria bali mnatawaliwa na neema.

Watumwa Wa Haki

15 Tufanyeje basi? Tuendelee kutenda dhambi kwa kuwa hatutawaliwi na sheria bali tuko chini ya neema? La, sivyo!

16 Hamfahamu kuwa kama mkijitoa kumtumikia mtu na kumtii kama watumwa basi mnakuwa watumwa wa huyo mnayemtii? Mnaweza kuwa watumwa wa dhambi ambayo matokeo yake ni mauti au mnaweza kuwa watumwa wa utii ambao huleta haki.

MAELEKEZO

TUMIA PRAYER POINTS ZA JANA

USIKU NAWEZA FANYA VOICE KUILEZEA ZAIDI

DAY 6

1 Wakorintho 15:55-58

“Kifo, ushindi wako uko wapi? Uwezo wako wa kuumiza uko wapi?”
Kifo hupata sumu yake katika dhambi, nayo dhambi hupata nguvu yake katika sheria.
Lakini tumshukuru Mungu anayetupatia ushindi kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo.

Basi, ndugu zangu wapenzi, simameni imara na thabiti.
Endeleeni daima kuwa na bidii katika kazi ya Bwana, mkijua kwamba kazi mnayofanya katika utumishi wa Bwana haitapotea bure.

TUMIA PRAYER POINTS ZA JANA

MAELEZO YA KIFO

Kifo kinachozungumziwa hapa sio lazima kifo cha uhai! Watu wanahisi kufa uhai ndo mwanzo wa balaa!
Lakini ukweli ni kwamba kufa kwa uhai ni hitimisho la balaa lililoanza zamani – kufa kwa tumaini lako, kufa kwa ndoto na maono yako, kufa kwa furaha yako, kufa kwa faraja yako… na mwisho wa yote, roho yako inashindwa kung’ang’ania, uhai wako ndo unafika ukomo.

Kwa maisha yetu sisi watu wa Karikoo – ikitokea umekufa halafu kama Lazaro mtumishi anaita: “Fulaniii toka njeee!” unaweza hata kusema: “Sitokiiii, acha shobo na mimi!”

UKITAFAKARI

NMB wanamiliki kiboga chako!
Figo zako ni mali halali ya CRDB Bank!
Bado VIKOBA!
Bado SACCOS!
Bado loan sharks wa riba kausha damu!
Bado ndugu wa karibu na watu binafsi!

Utoke uende wapi sasa? Umesahau nini?
Sana sana ukitoka ni kwenda kurudishia jiwe la kaburi na kuwaambia: “Acheni shobooo na kifo changu, tafuteni sehemu nyingine ya kutafutia kiki. Na sitaongea mara 2.”
Unarudi ndani ya kaburi na kurudisha jiwe! Kudadaadeki!

HALI HALISI

Kwa sasa Wakristo wengi hatunaaa jeuri ya kusema “Death, where is your sting?”
Inasikitisha sana! Mahusiano yamekufaaa, yameozaaa, yana toa funza kabisaaaa!

Aliyeua mahusiano yako anakutambia kabisa:
“Huolewiii ngooo! Ndo nisha semaaa! I dare you! Olewaaa! Nimekaa pale! Ukiolewa nitwe mbwaaa tena koko!”
Mwenyewe unasikiliza na unaliaaaa na kukata tamaa afu basiii!

UCHUMI NA AFYA

Huwezi sema “Death, where is your sting?” wakati uchumi wako uko mahututi!
Kuishi kwako ni kwa kuunga ungAAA.
Unajipa moyo eti “Hata Yesu alikuwa maskini” – wapiii???

Yesu alivaa vazi lenye thamani ya ujira wa miaka 3 wa askari wa Kiyahudi wenye vyeo! Yesu alikuwa na mhasibu – Yuda Iskarioti!

Afya ikiwa mgogoro una lichungulia kaburi kila siku!
Unaanzaje kusema “Death, where is your sting?” wakati moyoni una waza kisije kufanya kweli ikawa ndo basiii tena!

MSINGI WA SHIDA

Kifo hupata sumu yake katika dhambi, nayo dhambi hupata nguvu yake katika sheria.
Tunarudi pale paleeeeee!
Tabu ipo paleeeeeee!
Huwezi kukishinda kifo bila kuishinda dhambi!

Warumi 6:23
Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti.

Unataka kushinda kifo cha mahusiano yako?
Funga ofisi ya PAPA hilo!
Kila ukifungua, mshahara wake ni mauti mapya ya mahusiano yako.

MAISHA NA KAZI

The more unamuibia Mungu zaka na unamuibia boss wako, ndo hutapata amani kazini!
Wewe ni bright person – Straight A’s, excellent certificates – lakini kazini wamekugeuza tambala la deki!

Kupata kitu lazima uwe chawa na ulambe watu miguu for a living!
Ukisikia mauti ya career ndo haya sasa! Career ni dead kama Lazaro dead!

Ukiwa mwizi, mla rushwa, tapeli… the more wages of sins unaongeza kwenye destiny yako!

NJIA YA USHINDI

Lakini tumshukuru Mungu anayetupatia ushindi kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo.
Basi, ndugu zangu wapenzi, simameni imara na thabiti.

Njia ya Bwana wetu Yesu Kristo ni ipi???

Yohana 14:6
Yesu akamjibu: “Mimi ndimi njia, kweli na uzima. Mtu haji kwa Baba ila kwa kupitia kwangu.”

Njia ya Yesu Kristo ni Injili zote nne na kweli zote alizofundisha.
Utaijuaje? Acha ubabaifu!
Soma Injili, wewe mwana mpotevu!
Kuna kweli kama zote!
Hata ukikota 2 au 3 tu, zitakusogeza.

KUWA IMARA

Endeleeni daima kuwa na bidii katika kazi ya Bwana, mkijua kwamba kazi mnayofanya katika utumishi wa Bwana haitapotea bure.

Muda unaotumia kumjua Mungu na Mwanae Yesu hautapotea bure!
Utakua kiroho na utaweza kuuliza kifo:

“Where is thy sting?”

Kwa sababu kifo hakitakuwa na jeuri juu yako – sio cha mahusiano, sio cha uchumi, sio cha career, sio cha afya, sio hata cha furahaaa!

Kama mashariki ilivyo mbali na magharibi, ndivyo kifo cha aina yoyote kitakavyokuwa mbali na wewe.

DAY 7

HAKIKISHA YOU ENCOUNTER JESUS THE SON OF THE LIVING GOD

Hakikisheni kwenye maisha yenu ya Ukristo mna MU-EXPERIENCE Yesu Kristo, Mwokozi, Mwana wa Mungu aliye hai!

Yesu kama Yesu—ana dimensions nyingi sana! Ukisoma Injili utaona:

  • Kuna Yesu seremala,

  • Yesu aliyepiga watu wanaofanya biashara hekaluni,

  • Yesu mwalimu,

  • Yesu nabii anayesema yajayo,

  • Yesu mponyaji,

  • Yesu aliyefufuka toka wafu,

  • Yesu mtoa mapepo,

  • Yesu anayesamehe dhambi.

The more dimensions you know about the ministry of Jesus Christ, the better for you! The easier your deliverance will be.

Kama unamjua Yesu kwenye angle ya “mtu mwema,” hujakosea—kweli alikuwa mtu mwema. Lakini hii angle haiwezi kukusaidia chochote kwenye deliverance yako.

Likewise, kama unajua Yesu alikuwa seremala—sio uongo, lakini bado haina msaada wowote kwenye wokovu wako na kufunguliwa kwako.

Kama unajua Yesu alikuwa Myahudi na alizaliwa na Bikira Maria—sio uongo. Lakini yet again hii siyo key information muhimu kwa deliverance yako.

Wengi Mnamjua Yesu Vipande Vipande

Watu wengi mnamjua Bwana Yesu vipande vipande… na sometimes kipande unachojua siyo unachohitaji kwa ajili ya kufunguliwa.

Ili uwe Mkristo halali na kamili—you must know about Christ in depth! Mkristo manake you are for Jesus.

Lakini how can you be for Jesus endapo vitu unavyojua ni vile vile ambavyo hata Muslims na pagans wanajua?

Hoooowww???!!!

Suala kama Yesu ni Myahudi, alizaliwa na Bikira Maria, alifundisha, alikuwa mwema sana, aliponya watu, aliuwawa na Wayahudi—even pagans and Muslims know this information! Wanajua hili kweli.

Lakini je, hii kweli imewakomboa na kuwafungua? Hapana!
Sasa wewe itakukomboa vipi?

Ndio maana sio ajabu kukuta Mkristo ana mapepo kuliko hata wapagani na dini zingine—Mkristo jina tu!

Deliverance inahitaji kuwa well-equipped

Deliverance ministry siyo mchezo. Kufanikisha deliverance, lazima uwe well-equipped na dimensions zifuatazo za ministry ya Yesu Christ kikamilifu.

Ili ulishinde giza, lazima uwe na mwanga wa kutosha.
Giza la maisha yako haliondoki kwa ubabaifu—ni kuingiza mwanga na nuru ya Kristo ndani yako!

Kwa kufanya hivyo, giza lililofunika maisha yako litaondoka bila kuaga.

1. Ujue Yesu Ni Mungu

Hapa ndio tunachana na Waislamu, Wayahudi, na dini zingine zote. Lazima ujue for a fact bila kubumba-bumba.

John 1:1-3
1 In the beginning was the Word, and the Word was with God, and the Word was God.
2 He was with God in the beginning.
3 Through him all things were made; without him nothing was made that has been made.

Yohana 1:14
Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli.

Yohana 8:58
Yesu akawaambia, “Nawaambia wazi, kabla Ibrahimu hajazaliwa, Mimi nipo.”

Waebrania 1:3
Yeye ni mngao wa utukufu wa Mungu, na mfano kamili wa hali ya Mungu mwenyewe, akiutegemeza ulimwengu kwa neno lake lenye nguvu.

Wakolosai 2:9
Maana, ukamilifu wote wa kimungu umo ndani ya Kristo katika umbile lake la kibinadamu.

Tito 2:13
Tukilitazamia tumaini lenye baraka na kufunuliwa kwa utukufu wa Kristo Yesu, Mungu mkuu na Mwokozi wetu.

Mungu Ana Nafsi Tatu

Mungu Baba, Mungu Mwana, na Mungu Roho Mtakatifu.
Na zoezi la wokovu—alikabidhiwa Mungu Mwana kwanza, ambaye baada ya kazi yake, akamuachia Mungu Roho Mtakatifu.

This is ABCD of Christianity!

Hata Waroma wanajua hii. Waroma ndio wakali wa kubalua juu juu maandiko, lakini kwa hili—wapo serious sana. Wana hadi Siku ya Utatu Mtakatifu kuonesha how deep they are.

Kanisa na Utajiri

Juzi imetoka list ya 2025 ya makanisa tajiri zaidi duniani—na Kanisa Katoliki lipo kileleni number 1.

Lakini kwenye list ya watumishi matajiri zaidi duniani—Papa hayupo kwenye top 10!
Hiyo top 10 ina mapastor wa Kinigeria watano.

Papa hana hata private jet.
Anasafiri na Air Italia kila anapoenda.

Lakini hao watano wa Nigeria—hakuna hata mmoja ambaye kanisa lake lipo kwenye list ya makanisa tajiri zaidi duniani.

Back to Our Topic

Ukifanya deliverance—Injili ya Yohana ndio inatakiwa kuwa your go-to gospel!
Kwa sababu Mtume Yohana alienda in depth ku-establish kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu.

Na katika Injili yote ya Yohana—Yesu alifanya kazi zake in full capacity ya umungu.

Hii capacity ndio unayoihitaji wewe kupambana na miungu na nguvu za giza zilizokufunga.

Only if Jesus is God…

…ndio anaweza kuwa na wewe popote, 24/7.
Anaweza kuona kila unachofanya na kukusaidia kila unapo muhijati.

Anaweza kuwa ndani yako na kuwa Bwana wa maisha yako.

Ukijua hili—utavuka kama 50%.
Maana dhambi nyingi mnazotenda si kwa sababu ninyi ni wabaya—hapana.

Ni kwa sababu ya woga:

  • Nitawezaje?

  • Nitaishi vipi?

  • Sina kazi, nitakula nini?

  • Nitazeeka bila kuolewa?

Unajiona uko peke yako. Ndio unajikuta unafanya moves za kijinga.

Lakini ukijua Yesu ni Mungu, yupo hai, yupo na wewe, ana operate in full God capacity—you will fear no evil!

Utatamba kama Mfalme Daudi:
“Nijapopita katika bonde la uvuli wa mauti, sitaogopa mabaya.”

Bila kumjua Yesu ni Mungu…

…na kutanua uelewa wako kumchukulia Yesu kwenye capacity yake ya Mungu—na Mungu anayekupenda sana—utajitesa.

Safari yako ya wokovu itakuwa ngumu bila sababu.
Kuufanya mgumu moyo wako—ndio kutakakokutesa.

2. Ujue Yesu Amekuja Kutukomboa na Dhambi

Wakolosai 1:14
Ambaye ametukomboa kwa damu yake, tukapata msamaha wa dhambi.

Ukombozi wa dhambi upo ndani ya Yesu Kristo.
Kujaribu kushinda dhambi wewe mwenyewe—utwange maji kwenye kinu.

Dhambi zina madeni, zina madai ya halali, zina laana na minyororo.

Lakini ukiwa ndani ya Yesu—utafunguliwa na dhambi na mabalaa yake yote.

John 8:36
So if the Son sets you free, you will be free indeed.

NIMEPATA EMERGENCY… ANZENI NA HAYA, NITAKUJA KUKAMILISHA.

Invest in Yourself to Win and Overcome

Kuna ndugu yangu alifukuzwa na pastor, akaumia moyo sana. Aliponisimulia kwa uchungu, aliona kama mimi sijaathirika kabisa—na hili lilimwumiza zaidi, akataka kujua kwa nini niliunga mkono hatua ya pastor. Nikamwambia kwa uaminifu kabisa: “Kama angekupa nafasi, ningeshangaa sana!”

Kumkataa kwake ndiko kuliniongezea imani kwa pastor. Kwa sababu ndugu yangu ni mpagani aliyechangamka—anasema anaamini Mungu, lakini kanisani haendi. Mimi pia siendi kanisani mara kwa mara, hasa nikiwa nje ya nchi, kwa sababu ya changamoto za lugha na pia kupata kanisa sahihi. Lakini tofauti yangu na yeye ni kwamba mimi ni muumini wa kweli. Ninasikiliza mahubiri makubwa mara kwa mara, na ninajifunza sana kiroho hata nikiwa mbali na kanisa.

Yeye hajawahi kusoma hata Injili moja. Hajui hata Biblia ina vitabu vingapi! Kujiunga kwake na kanisa kulichochewa na kuona maisha ya waokovu yamebadilika, akasema: “Hapana, na mimi nataka.” Lakini je, mshirikiano gani unaweza kuwepo kati ya mpagani asiye na msingi wowote wa Neno na mchungaji wa Kipentekoste? Ni kama kupima tu imani ya pastor.

Tofauti za Madhehebu

Angalau angeanzia kanisa lake la Lutheran ili akumbuke misingi, kwa sababu amekuwa mbali na kanisa muda mrefu sana.

  • Wakatoliki wako kwa ajili ya enzi za Mitume na mapokeo ya kitume.

  • Lutherans na Anglicans ni kama watoto wa Wakatoliki waliokataa mamlaka ya Papa lakini bado wamebaki karibu katika mafundisho.

  • Pentekoste? Hawa ni religious fanatics wa Roho Mtakatifu! Wote wako kwa ajili ya Agano Jipya na huduma ya Roho Mtakatifu.

Sisi kama Walokole tunapenda kuona Biblia ikiishi sasa, si historia tu. Hata Agano la Kale tunalitumia ili kukamilisha Agano Jipya, si kwa sababu hatuliheshimu, bali kwa sababu tunataka kuishi katika yale Yesu aliyotuachia na hata zaidi.

Greater Works

Yesu alisema:

“Yeye aniaminiye, kazi zile nifanyazo mimi, ataifanya na yeye; tena atafanya kubwa kuliko hizi; kwa maana mimi naenda kwa Baba.”
—Yohana 14:12

Hili ndilo tunalotamani sisi Walokole—kuona yale makubwa kuliko hata Yesu aliyofanya. Lakini haya makubwa hayawezi kufanyika bila Roho Mtakatifu. Roho Mtakatifu hawezi kufanya kazi ndani yako bila Neno la Mungu. Ukisoma Injili zote nne, unajipa msingi imara. Bila hivyo, ni ndoto kusema unataka kupambana kiroho.

Usidandie kwa juu juu

Ukija kwa pastor wa Kipentekoste, ujue umeingia SGR express! Hapa hakuna mwendo wa kobe. Hapa kuna maombi, mapambano, na vita vya kiroho. Walokole tunapenda vita—hata vya jirani! Tunapenda kuona nguvu za Mungu zikidhihirika. Lakini vita vinahitaji maandalizi ya kiroho.

Kama hujasoma hata Injili moja, unataka kwenda vitani na nani? Na silaha ipi?

Hakuna aliyezaliwa na maarifa ya Biblia kichwani. Wote tulianza taratibu—kitabu kimoja baada ya kingine, Injili moja baada ya nyingine. Hakuna aliyekwepa. Lakini wengi mnaongea sana kuhusu mateso yenu, mapambano yenu, majaribu yenu—lakini hakuna hatua mnayochukua kiroho.

Jifunze maandiko

Kama unataka kujiunga na dhehebu fulani, jifunze falsafa na theolojia yao. Fuata taratibu zao. Hakuna atakayekufukuza ikiwa una msingi sahihi.

Hata katika makanisa ya nje, mara mbili tu nikiongea na wachungaji, wanagundua mara moja nina msingi mzuri wa Neno na maisha yangu ya wokovu. Wakinipima kwenye Injili, nipo tayari. Wakinipima kwenye Agano la Kale, nipo imara.

Lakini kama hujasoma hata Injili moja, tayari wewe ni wa daraja la pili kiimani. Si kwa sababu watu wanakukataa, bali kwa sababu ujinga wako wa maandiko unakugharimu sana.

Anza leo

Anza kusoma Biblia kila siku. Katika miezi sita, maisha yako ya kiroho yatabadilika kabisa. Soma sura tano za Agano la Kale na tano za Agano Jipya kila siku. Hii itakupa msingi mkubwa sana wa maandiko.

Maandiko ndiyo pasipoti yako ya kutoka gizani. Ukitoa sadaka, ibebe na andiko. Ukitoa zaka, tembea na Neno. Vinginevyo, inakuwa kama zawadi ya hiari tu, haina nguvu ya kiroho.

Epuka ubabaifu

Ubabaifu ndio unakufanya ushindwe. Kama tatizo ni maandiko, suluhisho ni moja: soma Neno.

Baada ya miezi miwili ya kusoma Biblia kwa mpango, hautakuwa na maombi ya kulalamika tena. Utakuwa tayari kumdhalilisha ibilisi kwa Neno la Mungu. Injili nne, manabii, nyaraka—ukijua haya, hakuna kitu kitakachokusumbua kiroho.

 

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Scroll to Top