MUNGU ANATAKA UITAWALE DUNIA NA VILIVYOMO – SUNDAY WORD

Wengi wenu mnalia kwamba “dini haifanyi kazi!” Lakini ukweli ni mmoja: mmeiegemesha vibaya, mmeingia kwa ubabaifu, mnataka ku-operate kiubabaifu na bado Mungu ajitokeze kuwasaidia.
How?
Hata spell za giza, ukitingishika tu hupati kitu — sasa kwa Mungu unategemea nini?

MTU MBABAIFU HAPATI CHOCHOTE — MBINGUNI WALA GIZANI.

Hakuna dini nyepesi, nyooka, yenye usawa kama Ukristo.
Hakuna Mungu aliye straight, mnyoofu, mwenye haki kama Mungu wetu.
Na dini hii imekaa kwenye usalama wa kweli, mpaka imezidi!

Mungu wetu pekee ndiye anayejali hata nafsi ya mtu mmoja — hata kama huyo mtu ni:

  • mbabaifu promax

  • maskini wa kutupwa

  • mlemavu

  • ameparara

  • hana kitu

  • hajitambui

Still, kwa Mungu ana haki sawa na mfalme.
Damu yako ina thamani sawa na damu ya mfalme.

MWANZO WA MAMBO YOTE: DOMINION

Mwanzo 1:26

“Tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; atawale … dunia yote…”

Hapa ndipo hadithi yote inaanzia.
Hapa ndipo assignment ya mwanadamu ilitangazwa.
DOMINION.

Mungu aliweka kwenye record — Mwanzo kabisa — kwamba ulikusudiwa kuitawala dunia na vyote vilivyomo.

Not vibes.
Not hype.
Scripture.
Imeandikwa.
Bank on it.

Neno muhimu: ATAWALEEEEE!

Mungu hana kona kona.
Hana ujanja.
Hakudanganyi.
Alisema — akarekodi — alisimama imara:
“UMEUUMBWA KWA MFANO WANGU NA SURAYANGU.”

Lakini shida inaanza pale unapofanya kosa kubwa kuliko yote:
Kuacha kuamini Mungu alivyosema kuhusu wewe — na kuanza kuamini baba la uongo.

SHETANI: BABA LA UONGO, MUONGO WA KWANZA, NA MUUNDWAJI WA PROPAGANDA

John 8:44

“Haana hata chembe ya ukweli… anaponena uongo, husema la kwa lake; kwa maana ni muongo, na baba wa huo.”

Hiyo title haijaja kwa bahati mbaya.
Haijapigwa kura.
Haikutungiwa.
Ameistahili.
Ameifanya iwe yake.

Na bado, unamwamini zaidi kuliko Mungu aliyeapa mara nyingi kuhusu ukweli wa neno lake.

Na matokeo yake:

  • Unaanza kuamini wewe ni maskini milele

  • Unaanza kuona huna la kufanya

  • Unajiuliza “Kwa nini Mungu alinilea kwenye hii familia?”

  • “Kwanini hakuna anayenipenda?”

  • “Nimekosea nini?”

Yote hayo ni lies za PhD level.
Uongo wa postgraduate.
Uongo wa peer-reviewed papers.
Muongo aliye postgraduate accredited.

Na wewe unakula bila hata ku-chew!

USIJIKUBALI UONGO WA SHETANI — JIKUBALI UKWELI WA MUNGU

Kuna watu wamekuletea “speeches” za kipuuzi:

  • “Jikubali tu — hujaolewa.”

  • “Jikubali tu — huna kazi.”

  • “Jikubali tu — disability ni ability.”

  • “Jikubali tu — hakuna ways.”

Others even elevate crap into holy crap kwa kuliweka kwenye midomo ya watumishi.

But the Scripture is clear:

John 8:32

“Utaijua kweli, nayo kweli itakuweka huru.”

SIO KUJIKUBALI UONGO.
SIO KUTIA SAINI UTUMWA.
SIO KUUZIA SHETANI UHURU WAKO.

USHUHUDA: HOW I FOUGHT THE DEVIL WITH SCRIPTURE — NOT SELF-ACCEPTANCE

Nilipitia moto.
Moto halisi.
Ajali mbaya.
Medical records mbaya.
Watumishi wakinikazia: “Jikubali. X-ray zinaonyesha…”

X-ray my foot.

Nilikuwa tayari kufa nateseka lakini sio kukubali uongo kwamba nitaishi maisha ya upungufu, mateso, na kushindwa.

Niliamua moja tu:

Luke 1:37

“Hakuna lisilowezekana kwa Mungu.”

Na hapo ndipo nguvu ikanirudia.
Pole pole.
Siku.
Wiki.
Miezi.
Miaka.
10 years of fighting, denying the lie, and believing God’s Word.

Na nikapona — mpaka leo wengine hawaamini.
Makovu yamebaki, lakini mwili ni wa afya, nguvu, speed, na stamina.

WATU WAKIKUPIGA FIRING — USIJIKUBALI UONGO

People will fire you.
People will lie about you.
People will call you incompetent.

Ni uongo.
Ni voiceover ya baba la uongo.

Kama kweli hukuwa na kitu — kwa nini aweke kampeni nzito kiasi hicho kukumaliza?

DON’T UNDERESTIMATE THE DEVIL — BUT DON’T OVERPOWER GOD’S WORD

Shida ya wengi sio kwamba shetani ni mkubwa.
Ni kwamba:

  • yuko too loud

  • too intentional

  • too convincing

  • too conspiratorial

  • na watu wengi wanaamini kilio chake kuliko neno la Mungu.

MUNGU ALIKUPA DOMINION — KWANZA, KATI, NA MWISHO

Genesis 1:26Assignment

Genesis 1:28Blessing ya dominion

Genesis 27:40Ukishaamka, unalivunja kongwa shingoni

Esau alipigwa changa la macho.
Baraka zake zikachukuliwa.
But Scripture says:

“Utakapoponyoka, utavunja kongwa lake shingoni mwako.

Hiyo ndiyo nafasi ya comeback.
Hiyo ndiyo dominance inayorejea.
Hiyo ndiyo double portion after deception.

CONCLUSION: HUU NDO UKWELI — ANYTHING ELSE NI UONGO WA SHETANI

Mungu alisema:

  • Umeumbwa kwa mfano wake

  • Umepewa utawala

  • Umepewa dominion

  • Umepewa baraka ya kushinda

  • Umepewa uwezo wa kuvunja kongwa

Uongo wote mwingine:
ni propaganda ya baba wa uongo, muundaji wa misinformation, muanzilishi wa fake news.

STAND ON THE WORD.
DOMINATE.
BREAK THE YOKE.
LIVE IN DOMINION.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Scroll to Top