SUNDAY WORD – LUKA 9:37–62

LUKA 9:37–62

TOFAUTI YAKO NA YULE MZAZI MWENYE MTOTO ALIYE NA PEPO LA KIFAFA NI TATU TU!

 

Tatizo lako linaweza kuwa dogo kuliko la yule mzazi wa mtoto mwenye kifafa, lakini mateso na muda uliotumia kuvuka ni mrefu kupita maelezo.

1️⃣ BADO HUJAAMUA KUVUKA

Bado hujachoka. Bado hujafanya maamuzi ya kuvuka. Bado uko kwenye kifungo cha shida zako! Bado una stamina ya kustahimiliaaa na kuishi na hali zako. You can take NO for an answer! You can take anything for an answer. Vovote itakavyoenda, “sawa tuuuu.”

Kifafa hakikuwa kinapona. Ilitarajiwa mtu aishi nacho maisha yote. Hata sasa ni hivyo hivyo! Lakini yule mzazi wa mtoto alifika mahali akawa naiveee! Akawa desperate! Akazima data na kuamua kabisa kuwa akipambana, mtoto ataponaregardless ya tiba, sayansi, maneno ya watu, au ukweli wa dunia ulikuwa unasemaje.

Alichukua uamuzi binafsi kuwa “nikienda kwa Yesu mtoto atapona!” Hakuruhusu mtu yeyote kumvunjia moyo. Alisimama na Yesu. Alipofika kwa Yesu, hakucheza — wanafunzi walikuwa wameomba sana, bila mafanikio! Lakini yule mzazi alishikilia maamuzi yake kuwa leo mtoto lazima apone! Akamvaa Yesu mzima mzima — na mtoto akapona!

Je, wewe umefanya maamuzi ya kuolewa? Umeamua kweli kwenda kazini? Au bado uko kwenye ubabaifu hadi uangamie?

2️⃣ USIWE MWEPESI KUKATA TAMAA

Yule baba alianza kudili na wanafunzi wa Yesu lakini kazi iliwazidi uwezo. Hakukata tamaa — alisogea hadi kwa Yesu mwenyewe.

Ubabaifu wa wanafunzi haukumpunguzia imani hata tone! Hakurudi nyuma kwenye imani ya kuwa mtoto wake atapona. Wewe je? Mtumishi akishindwa tu jaribio la kwanza, unakata tamaa! Unasema, “Nilijua tu!” Hujakamilisha hata jaribio, unakata tamaa mapema mno!

Mwingine kabla hujasema kitu anasema kabisa: “Tatizo langu halina dawa, watumishi wote wameshindwa!” Hiyo ni total nonsense!

Mtumishi kushindwa haimaanishi kila kitu kimefeli! Labda wewe mwenyewe hujawa serious, au hujaweka misimamo. Labda hata mtumishi anakamilisha ubabaifu wako! Kanisani kuna siasa chafu sana!

Tunajikuta wote wababaifu — mtumishi na muumini. Pipa na mfuniko! Muhazini na mnadi swala! 😤

Kama yule baba ange-focus kwenye ubabaifu wa wanafunzi, angebeba mgonjwa wake kurudi nyumbani kuishi kwa matumaini. Lakini alijua nini alitaka. Akasema: “Msinivurugeni! Namtafuta Boss wenu! Kushindwa kwenu sio kesi ya jinai!” Akapanda juu, akazibe, akaamua kum-face Mwalimu mwenyewe!

STORY YA KWELI 💥

Nilienda kwa mtumishi akanambia kabisa: “Hilo swala siliwezi na silifanyiiii!” Nikamwambia, “Na mimi sijaona mwingine zaidi yako — utalifanyaaaa! Na litaendaaa!” Akanitazama: “Umetumwa?” Nikachomoa kibundaaa, nikaweka mezani: “Issue ni nini? Pesa? Hiyo hapo! Imani? Nimekuja nayo! Maandiko najua unayo! Tumalize hii issue chap chap basi!”

Akanijibu: “Siwezi!” Nikaja juu: “Kwanini hutaki?? Kama pesa siyo issue?!”

Nilikuwa nimetoka kwangu na mipango yangu — kwamba hii issue inamalizwa leo hapa kwako! Mtumishi akaomba kwa hasira sana! Mpaka machozi yakamtoka! Akanifukuza kabisaaaa! Kwa maoni yake, nilimbully. Kwa mtazamo wangu, nilimsaidia kuishi kwenye uwezo wake kamili!

Watumishi wengine hawawezi kukupeleka kazini lakini kila siku wanatoa ushuhuda kwamba watu wengine walienda! Sasa kumbe kazi wanaweza tu? Hivyo kanisani kuna siasa chafu mno!

3️⃣ AMINI KWENYE UWEZO WA MBINGU

Kutokuwa na imani kwa mbingu kunafanya mtu kuwa mtumwa wa dhambi! You just can’t trust the heavens!

Watu wanafunga, wana kesha, wanatoa sadaka — lakini hawaziamini mbingu hata kidogo juu ya hiyo shida yao! Mtu anafunga siku 30 lakini 80% anaamini hakuna kitakachobadilika. 20% tu ndiyo labda Mungu atamkumbuka!

Kwa moyo huo, Mungu atafanyaje makubwa? Kwa imani ipi?

Kama uko kwenye hali hii, kuliko kuji-overdose na maombi, nakuambia tafuta kwanza chimbuko la mashaka yako juu ya uwezo wa Mungu kwenye maisha yako!

Yule baba aliyekuwa na mtoto mwenye kifafa aliamini kuwa Mungu anaweza. Ndio maana alimchukua mtoto na kumpeleka kwa wanafunzi. Alijua watarejea nyumbani bila pepo. Na hakuwa tayari kuamini kingine! Hata hali ilipokuwa mbaya — wanafunzi walishindwa — bado he stood his ground! Alisema, “Leo hatutarudi nyumbani na pepo!” Leo ni mwisho wa mateso!

🔥 USIYAKOSE YAFUATAYO:

Wengi sio kwamba hawaombi! Mnaomba sana! Mpaka mnawazidi watumishi! Lakini kuamini mnachoomba na kusimama imara, haipo.

Unafunga siku 30 kuombea mahusiano, siku ya 31 mtu mmoja akikwambia “sidhani kama utaolewa…” Basi hapo hapo unavunjika! Unaliaaaa! Unamwona Mungu dhaifuuu mbele ya watesi wako!

Unakata tamaa, unarudi kwa ex wako — mume wa mtu — unazinilina naye ili kujipoza. Why? Emotions zako zimeoza kabisa.

Mimi mambo yakishindikana, namwambia Mungu: “Jitetee mwenyewe!” Nakaakaaa kimya, bila kuchukua hatua yoyote. Na Mungu ananipa encounter moja baada ya nyingine, kunithibitishia: “Bado mimi ni Mungu!”

🎯 CHALLENGE OF THE MONTH:

Amini Mungu yupo upande wako — na atakupa mume, kazi au kile unachokitaka bila kusita hata nusu sekunde! Usiyumbe kwa siku 30!

Kila unapoamka, confess kwa kinywa chako:

“Mungu anaenda kunipa kazi/mume/ninachokitaka. Na ninaliamini kwa 100%!”

Kisha nenda kwenye shughuli zako. Ukimaliza siku nzima bila kutikisika, usiku mshukuru Mungu! Sema:

“Asante Mungu kwa kunipa hicho kitu!”

Tiki kwenye calendar yako. Uone siku 31 za bila mashaka au ubabaifu imani yako inavyotoboa!

MPAKA HAPA NILIPO FIKA, NIMEKUWA MGUMU KUTOA UNABII KWA WATU. MAANA WANATAKA KUNIPANDA KICHWANI!

Kuna mtu alikuwa na mwanaume, akachukuliwa na mwanamke mwingine. Roho Mtakatifu akaniambia atarudi na watafunga ndoa. Nilimpa neno la faraja, nguvu na imani.

Hapo hapo nikajipata kwenye kesi! Sms kila siku: “Bado hajarudi… bado kimya…”

Nilibii bila siku 3 kupita, narushiwa follow up.
Lakini baadhi yao walisimama. Mmoja amerudi 2024, kaposa! Mwingine 2025, hadi mimi nilisahau!

Ukiwa umejipata — huduma

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Scroll to Top