IBADA YA UTAKASO

 

Ibada ya utakaso ni ibada muhimu sana kwa mtu kufanya especially baada ya msimu mbaya au muendelezo wa misimu mibaya mfululizo,  NA KAMA IBADA ZOTE ZINAZOENDA NA MAJIRA LAZIMA ZIFANYIKE NDANI YA MAJIRA INAYO-ISHIA   YAANI KABLA YA KUANZA MAJIRA MPYA.

SASA IBADA YA UTAKASO INATAKAGA SADAKA  YA KWENDA  KUMGUSA MUNGU NA WANADAMU WENZIO WAFUNGUE MOYO WAKUOMBEE KWA MUNGU, KUNA VITU KWENYE MAISHA NI VIGUMU KUVUONDOA, UKILEGEZA HAVIONDOKI, SASA INAKULAZIMU KUTUMIA MIFUMO ILIYOPO KUVING’OA.

WAPENDWA NAAMAN ALIKUWA NA UKOMA AKAFANYA IBADA YA UTAKASO KUPITIA NABII ELISHA AKATAKASIKA NA UKOMA UKAONDOKA NA UKOMA ENZI HIZO KUONDOKA HAIKUWA RAHISI, AKATOA SADAKA MTUMISHI WAKE AKALETA TAMAA UKOMA UKAMVAA YEYE.

KUNA MAENEO KWENYE MAISHA YAKO YANAKUWA YANA UKOMA SUGU, MTU TANGU UFIKE UMRI WA KUOLEWA HUOLEWAGI TU, MWAKA HADI MWAKA YAANI TANGU UMALIZE CHUO HUPATAGI KAZI TU, MPAKA UNAKARIBIA KUFIKIA RETIREMENT AGE, TANGU UAJIRIWE KAMA OFFICER HUPANDAGI, WANA PANDA WENZIO TU KILA MWAKA, HUONI UKOMA WA CAREER , YAANIHUNA TOFAUTI NA UKOMA WA NAMAAN MTU WA SHAMU ?.

CHUKUWA DUA INAYO MGUSA MUNGU MFANO KAMA YA YATIMA INAMGUSA MUNGU MOJA KWA MOJA, MIMI MWENYEWE NATAKA KUJITAKASA KWELI-KWELI, MIMI WA KUPEWA NOTICE MBILI (2) KWELI JAMANI?, JAPO NIMEZIONDOA KINAMNA LAKINI NATAKA NI DEAL NA MZIZI WA TATIZO,  NATAKA NIJITAKASE KWELI KWELI, NILISHA JITAKASAGA  MWAKA 2019 NILIPATAGA MIKOSI DOUBLE DOBLE, IBADA IKAPITA MAMBO YAKAJIPA SASA NAONA DALILI SIO NZURI.

MWAKA 2019 NILIWAHI KUFUKUZWA KAMA MBWA KWENYE NYUMBA NILIYO PANGA KAMA OFISI, ILIBIDI NIJITAKASE KWA KWELI NA HIVI SASA NI MIAKA MITANO(5), SIJASUMBULIWA KABISA MPAKA MWAKA HUU, SIJAPANDISHIWA KODI HATA  MARA MOJA NA NINEPANGA KAMA SEHEMU SITA (6) HIVI, UTAKASO ULINYOOKA ULE NILITAKASIKA KWELI KWELI.

HAPA NAANGALIA KAMA VIPI MKESHA WA CHRISTMASS TURUKE NA UTAKASO, MAANA LAZIMA UFANYIKE KABLA YA MWAKA MPYA, ILI HUU MWAKA UNA UMALIZA NA MAGUNDU YAKE YOTE.

BAADHI MMETOA SADAKA YENU KWA WATOTO SO MUITUMIE PIA KUJITAKASA WEWE NA MAGUNDU YOTE HUFIKII HATA ROBO YA MSIBA WA WALE WATOTO, IMAGINE HUNA BABA WALA MAMA WALA KAKA WALA  NDUGU.

LOVENESS KAENDA HUKO KAKUTA BALAA ZITO, HAWANA CHUPI, HAWANA HATA YEBO-YEBO, HATA SIDIRIA VIBINTI HAVINA,  PAD NI ANASA WANATUMIA VITAMBAA IN 2024 FOR CHRIST SAKE. MIMI NIMEMWAMBIA LOVE TO STICK TO THE ORIGINAL PLAN YA NGUO, MUITIKIO SIO MKUBWA LAKINI WEWE USIANGALIE WENGINE KWENYE MAMBO YA KUJITAKASA,  JIANGALIE WEWE KAMA WEWE, USIJIENDEKEZE HAKUNA IBADA YA UTAKASO MKAVU, PASUKA UMALIZANE NA MAGUNDU YAKO, HATA UKIENDA KWA MGANGA KUONDOA NUKSI LAZIMA UFUNGUE MKOBA WA MGANGA KWA MAOKOTO.

Mwenyewe  kuna mambo yana nisumbua miaka na miaka lakini mwaka huu mwisho, NATAKA NIJITAKASE KWELI KWELI MPAKA NITAKASIKE, KAMA NAAMAN MTU WA SHAMU,  UKOMA STOP MWAKA HUU WA 2024, KUNA MAENEO SIWEZI KUENDELEA KUKOMAA WAKATI IBADA ZIPO.

NAVYO WAAMBIA NATAKA KUJITAKASA SIO KWENYE SADAKA  HII YA NGUO TU, CHAKULA CHA SIKUKUU LAZIMA NILISHE KITUO KIMOJA KIZIMA PEKE YANGU. WATOTO ASUBUHI WANAKUNYWA CHAI YA MAZIWA, TOAST, MAVAZI, WATAKULA MCHELE WA 3000 SIO CHENGA, KUKU ROBO, MBUZI  MBILI(2) ZITACHOMWA NA MCHOMAJI NAMPELEKA MIMI, CHEFF WA KUPIKA MIMI, VIAZI GUNIA ZIMA LIPIKWE LOTE, TAMBI NA MCHUZI, YAANI NYAMA AINA 4 , SODA,  CAKE YA SIKUKU YA MAANA, MWAKA HUU WANAPATA NA GIFT BAGS.

NISHAPASUKA, UTAKASO SIO JAMBO DOGO, NAVYOSEMA NATAKA KUJITAKASA NIMEJIPANGA KUTAKASIKA, MWAKANI KIKOMBE KIKIFURIKA MNAANZA KUONA MUNGU ANAPENDELEA WAKATI MUDA WA KUPASUKA HUKU MNAJIZIMA-DATA. NA MIMI SIO KWAMBA NINA PESA, NINA MADENI NAONA NAKIMBIZANA NA SERIKALI LAKINI UTAKASO KWANGU MUHIMU, HASARA ZA KUTO-JITAKASA NI KUBWA KULIKO HIZI GHARAMA ZA UTAKASO, NA UTAKASO WA UBABAIFU HAUNA MATOKEO.

UKIAMUA KUJITAKASA NI MWENDO WA NAAMAN MTU WA SHAMU TU, UNABEBA SHEHENA YA ZAWADI ONLY FOR PROPHET ELISHA TO REJECT IT, THE ORPHANS ARE NOT IN LUXURY CONDITIONS KAMA NABII ELISHA, SO WATAPOKEA! NA NITA TAKASIKA.

OFCOURSE NI GHARAMA HATA KULOGA NI GHARAMA ZAIDI, MAMBO YA KIROHO TANGU ENZI ZA IBRAHIM NI GHARAMA, WE MALAIKA KUJA KWAKO UCHINJE MBUZI MCHEZO, HATA AKIJA MAMA YAKO MZAZI HUCHINJI CHOCHOTE HALI ILIVYO NGUMU, NDIO MTU HUMJUI, NDIYO WATU HUWAJUI? UNALETA UBAHILI KUMBE MALAIKA HAO YAANI USHAPISHANA NA BARAKA MCHANA KWEUPE.

WAPENDWA KESHO NDO MWISHO, WATOTO WALE HAWANA BABA HAWANA MAMA NA WEWE NDIYO UNA MIKOSI KAMA YOTE, KWANINI ISIFANYIKE KOLABO KATI YENU?, WEWE PASUKA NGUO 1,2 AU 100  KUTOKANA NA UTAKASO UNAOHITAJI KUPOKEA.

HANA ALIENDA SHILLO KUJITAKASA NA UTASA, HAKUTAKA AKIENDA TENA SHILLOH MWAKANI MAJIRA MAPYA AENDE TASA VILEVILE, HIZI IBADA ZIPOGO NA MUNGU NI YULE YULE, WEWE TU KUWA SERIOUS KUJITAKASA NA MIKOSI YAKO!

WENZANGU MNAFANYAGA IBADA GANI MBONA MUNGU WENU MKUBWA SANA, NDIYO HIZI, KESHO MWISHO WA KUPOKEA HELA IKIFIKA KESHO JIONI NAFUNGA NAMKABIDHI LOVENESS FOUNDATIONS AANZE  KUKABIDHI, MPEMDWA UKITOA BAADA YA KESHO UTAKUWA UNAJIUNGA NA CHRISMASS  CELEBRATIONS KWENYE UTAKASO WANGU. NGUO NI MUHIMU KULIKO CHAKULA IF YOU ASK ME, CAUSE THEY RARELY RECEIVE NEW CLOTHES!

WAPENDWA MUNGU AWABARIKI SANA, ATIZAME IBADA YENU NA MOYO MNAO-MTOLEA NAO AWAPE HAJA ZA MOYO WENU.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Scroll to Top
× IT Help Desk