YOUR MIND IS THE GATEWAY TO SPIRITS (HOLY AND UN-HOLY)

Wapendwa kiukweli nimekuwa busy sanaa na mambo ya kaisari, Lakini on the bright side wale waliofanya October to remember BACK to BACK, Wamepata muda wa kupooza fuvu kidogo, December narudi na Program OMEGA ANOINTING, Yaani ni Mambo ya kuzima moto, Mwaka unaisha vipi malengo bado basi tutafosi  hata goli la mkono.

NINACHOKITAKA NI KUWAJENGA UFAHAMU LEO NI JUU YA AKILI YAKO KUWA LANGO LAKO LA USHINDI AU KUSHINDWA KUTEGEMEANA UNA FANYA PARTNERSHIP NA NANI?, WAPENDWA TUNARUDI PALE PALE DINI BILA CLEAR UNDERSTANDING OF THE WORD NI KAMARI KAMA KAMARI ZINGINE TU!

TOFAUTI KINA BABA LEVO WANA BET NA MZUNGU WEWE UNA BET NA MBINGU, MAANA UNAFANYA MAMBO USIYO YAJUA KWA SABABU UNAZO ZIJUA.

The only way you can access things of the spirit ni kupitia akili yako tu.Huwezi kwenda physically ulimwengu wa Roho, Michezo ya ulimwengu wa Roho ni michezo ya akili na fikira.

SASA KUPATA SPEED NA PACE KWENYE MAMBO YA KIROHO HAKIKISHA UNANOA AKILI YAKO KWELI-KWELI, SIRI KUBWA YA KUPATA MILLAGE KWENYE ULIMWENGU WA ROHO NI KUHAMISHA NENO LA MUNGU KUTOKA KWENYE BIBLE KWENDA KICHWANI MWAKO KUPITIA UELEWA ( CLEAR UNDERSTANDING) MUNGU ALIKUWA ANAKUPA MESSAGE GANI?

KUSOMA NENO NI STAGE YA KWANZA, KUWA TRANSFORMED NA NENO NDIYO HASAA LENGO LA MBINGU KUTOA MAANDIKO KUWAHUSU, HAWAKUSHI NDWA KUJIFUNGIA MBINGUNI NA KUENDELEA  KURELAX

WAMETOA SCROLLS ILI UPATE MESSAGE, HIYO MESSAGE IKUFANYIE TRANSFORMATION, UKIFANIKIWA KUWA TRANSFORMED NDO MBINGU SASA ZITAKULETEA EMPOWERMENT, UKISHINDWA KU-TRANSFORM KUPITIA NENO LA MUNGU KWISHA HABARI YAKO!, WAPENDWA KUNA LEVEL LAZIMA UFIKE NDIYO UWEZE KUDEAL NA MBINGU KWA VIWANGO VYA MBINGU

Mfano Mimi kwa level yangu niliyo fika kimchongo mchongo na mapambano mengi sana, Mbingu haziitaji kuniletea maono kama movie au mpaka niote ndoto hio-hio mara 20 ndo nipate ujumbe, Ilawazo tu kama  na download, Kwishaaa kazi, Kitu tu kinaingia kwenye mawazo yangu ndiyo hivyo hivyo kitakuwa navyowaza.

Nyumbani nawaambia hiki kitu kitaenda hivi, Wanabisha, Ni sualala muda tu, Wanabaki wanajiuliza umejuajeeee?, Nimechungulia future on serious note level niliyo fika holyspirit haniambii process , Ana nichapa tu na END RESULTS, IMEISHA HIYO.

Na mimi watu wana ni consult sana, Mwanaume niliye nae anataka SEX, Namwambia usimpe kwani najua atakuacha, Hata wewe nafsi yako inaweweseka, Umelala na wanaume 25 roho haijakusuta wa 26 Roho inakataa mpaka unakuja kuniuliza mimi kweli ? WE HUOGOPI ?, Hao 25 Ulimuuliza nani? kabla hujaruka nao live ? ILA HUYU MPAKA NAFSI YAKO IMEGOMA, UNATAFUTA USHAURI WIZARA YA MAMBO YA NJE ?

Mtu Anakuuliza NITAOLEWA ? Unamuona ukiendelea na IBADA definitely YES, Anaacha ibada na kurudia zinaa, Alafu mwisho wa siku anasema unabii wa uongo, Ulipewa huo unabii ukiwa dogy-style au ukiwa unasifu na kuabudu?

AKILI YAKO ILIVYOKUWA KWA MUNGU ILIFUNGUA ACESS YA TRANSFORMATION KUPITIA HOLY SPIRIT, AKILI YAKO ILIVYO SHAKE WELL BEFORE USE IKAFUNGUA MILANGO KWA ROHO CHAFU ZIKAWEKA MAPANDO YAKAUA UNABII WA MUNGU ULIOKUWA ON PROGRESS NA KUMANIFEST MAANGUKO MAKUBWA.

 

MTU AU KITU KIKISHA KU-DEFEAT KIAKILI KIMESHA KU-DEFEAT KIMAISHA, KWISHA KAZI, HATA SISI WAKOMAVUUU WA IMANI MAJARIBU YANA TU-BEEP ILA WE KNOW WHAT WE KNOW!, VITA YA VISU UNAENDA NA SILAHA ZA KI-NUCLEAR UNAWAPA SHOW-SHOW! HAWARUDII TENA KWA SABABU IMANI SIJA-IEGESHA EGESHA, NENO NALO LIJUA HATA HILO DOGO NALOJUA KWA MAPANA 60,  SIO WA KUCHEZEWA SEKTA HIYOO.

SIKUAMKA ASUBUHI NAJUA NENO, UNASOMA KWA KURUDIA RUDIA MPAKA UPATE MESSAGE MAANA MWANZO NI MAANDIKO TU, EVENTUALLY UNAPATA MESSAGE TOKA TAARIFA ZA KALE UNAZOSOMA, HIYO MESSAGE INATAKIWA KUKUJENGA KIROHO

Isaiah 61:7-9

7 Instead of your shame you shall have double honor, And instead of confusion they shall rejoice in their portion. Therefore in their land they shall possess double; Everlasting joy shall be theirs.

UKIANZA KUSOMA HILI NENO UTAONA MUNGU AMEONGEA MAMBO YA MSINGI MNOOO KUPITIA NABII ISAYA, KWANZA INATAKIWA UJUE ALIONGEA HILI NENO KUHUSU NANI?,DEFINITELY WATU WAKE! JE WEWE KWA MIENENDO YAKO NI MTU WA MUNGU KWELI?, KAMA SIO DON’T BOTHER, IT WILL NEVER COME TO PASS, MUNGU NI MUNGU WA WATU WAKE WANAO MTUMIKIA, KUBET NA KUCHEZA KAMARI NDIYO UNA DHAMBI ZAKO KAMA ZOTE NA JANABA JUU UNAUNGANA NA HIOI ANDIKO.

 

AKILI NI KUJICHANA LIVE KWAMBA MIMI SIO MTU WA MUNGU, KANISANI  NINA MIAKA  SIJAENDA, NENO SISIKILIZI, IBADA SIFANYI, ZAKA SILIPI NA SADAKA SITOAGI, HAPA KWA STATE NILIOPO MBINGU ZITANITOA DRY DRY! NA MIMI HIZO DOUBLE PORTION NDO NAZITAKAAA MPAKA NAZITAKA TENA! SIWEZI KUZIKOSA!; INVOKE MINISTRY YA TOBA NA KURUDI KUNDINI ILI U -QUALIFY

Inawezekana pia ni mtu ibada tu na kwa Mungu upo-upo ila kivile, Lakini Mbingu haziwezi kukukata jumlajumla! Zaka yako ina ‘onekana kila mwezi!, Mahudhurio ya ibada upo upo, visadaka upo upo, kusoma neno una beep beep! LAKINI PAMOJA NA KUWEPO KWENYE MFUMO WA MBINGU BADO UNACHEZA KAMARI NA MBINGU! HUZIAMINI SANAAA KUKUTENDEA!,WEWE TATIZO LAKO NI UNAFUNGUA NA KUFUNGA AKILI ZAKO KAMA KINYONGA.

UNACHOTAKIWA NI KUFUNGUA AKILI ZAKO ILI  UPOKEE MESSAGE YA MUNGU TOKA NENO LAKE NA HIO MESSGAE UINGANGANIE MPAKA IKUFANYI E TRANSFORMATION, HATA KAMA MAZINGIRA YANA NENA TOFAUTI NA YANA KUZOMEA WEWE ZINGATIA CREDIBILITY MBILI (2) YAANI !YA MESSAGE NA MTOA MESSAGE!

TUKIRUDI KWENYE NENO LETU LA NABII ISAYA!, MSEMAJINI NANI ? MUNGU!,MUNGU NDIYO ANAYESEMA  BADALA YA AIBU ATATOA DOUBLE PORTIONS, KAMA ANAYESEMA NI MUNGU MASHAKA YAKO YANATOKA WAPI?, KAMA NINGEKUWA MIMI NDO NASEMA UNGESEMA MMMMH! LAKINI MUNGU NDO AMETOA HIO SMS! KUSOMA HILO NENO NI KAMA UMEPOKEA E-MAIL TOKA MBINGUNIKWAMBA DOGO SIKIA! BADALA YA AIBU TUTA KUPA DOUBLE PORTION! UHAKIAA

 

KWA LEVEL YANGU MIMI NACHO HAKIKISHA TU NI JE IMEANDIKWA?, NIKIONA IMEANDI KWAAA! KWISHAA KAZI! HUNIAMBII KITU YAANI OVER MY DEAD BODY I WILL TAKE YOUR WORD OVER THE HEAVENS, MIMI NIKIJIHAKIKISHA IMEANDIKWA DOUBLE NI MWENDO WA KUPOKEA NOTHING LESS THAN DOUBLE!, HATA SINGLE PORTION SIPOKEI

Majaribu hayo Kivipi nipokeee! lmeandikwa DOUBLE then it should be double, Michezo ya Mbinu ni imenyooka, SALAMA YA SHETANI HILO NENO NISILIFUME NA NISILIJUE!

I DEMAND DOUBLE SABABU DOUBLE WAS PROMISED, NA ALIYE PROMISE NAMUAMINI MPAKA NAMUAMINI TENA HATA MUDA AMBAO SIHITAJI KUMUAMINI LAKINI KWA KUJIPENDEKEZA TU NAMUAMINI, YAANI NI CHAWA PROMAX WA MBINGUNI!

NA IMANI HII IT  WILL CUT BOTH WAYS SIO KWENYE DOUBLE PORTION TU, HATA KWENYE WIZI MIMI SISHIRIKI SIO KWAMBA SINA NJAA, NAJIPENDEKEZA KWA MUNGU KATIKA UCHAWA WANGU WA KILA SIKU! BORA MNIFUKUZE, MNITENGE LAKINI CHORI-CHORI ME NO WAY NO DAY, HATA PENALTY MTU KANILIPA IMEZIDI NAREJESHA, HATA KAMA MCHINA KANIPIGA KANIPA BIDHAA FAKE NATOA MSAADA WOTE SIWATAPELI WATEJA WANGU! HASARA ROHO YANGU TU!

SIO KWAMBA UKIOKOKA NYEGE NDIYO ZINA EXPIRE, NDIYO ZINAZIDI, LAKINI HUJIENDEKEZI HATA ITOKEEE MTU ANAKUTAKA NA WEWE UNAMTAKA YANI MMETAKANA ILE-ILE LAKINI I SAY NOO!

SIO KWAMBA UKIPIGA HIO SHOW MOJA TU BASI ACESS ZAKO ZOTE ZA MBINGU ZITAKUWA REVOKED! NOT NECESSARY! MBINGU ZINAWEZA KUKUKAUSHIA LAKINI SHETANI HAWEZI KUKU KAUSHIA, NDIYO UMEMFUNGULIA LANGO LA SEBULENI, ATAMTUMIA HUYO MZINZI MWENZIO KUKU DEFEAT! NDIYO KWANZA VITA IMEANZA RASMI NA MBINGU HAZIWEZII KUKUOKOA  MAANA VITA INAPIGWA UWANJA WA  NYUMBANI WA SHETANI N UMEJIPELEKEA MATEKA MWENYEWE BAADA YA KUMPIGA FIRE.

MIMI KUNA WATU NAWAJUA WANAFANYA UMALAYA TANGU 2010 WAMEJIUZA BONGO MPAKA DUBAI MPAKA MALASIA, MPAKA MACAU, MPAKA BANGKOK,  MPAKA PARIS INSHORT DUNIA WAMEIMALIZA KWA KUDANGA, SASA HIVI NA 40 ZAO WAMEONA WAZAE TU., MMOJA KAENDA CLINIC KAKUTWA NEGATIVE “. ANASEMA ITS OFFICIAL KASTAAFU NA KUNA WATOTO WADOGO TU WAMEKULIA KANISANI KUFANYA UMALAYA KIDOGO TU SHETANI KAWADAKA NA KAWANYENGA  KITU POSITIVE, WANAISHI KWA MATUMAINI NA KUTAFUNA  KARANGA.

SHETANI HII  MI-CONCORD NI WATU WA NYUMBANI ANAJUA HAIENDI POPOTE, HANA HARAKA NAYO ATAINYENGA HATA KESHO KWANI HARAKA YA NINI, ILA WEWE ANAJUA ASIPO KUMALIZA LEO ANAWEZA KUKUKOSA JUMLA JUMLA! NDIYO MAANA UKITELEZA TU ANAPITA NA WEWE WIMA-WIMA.

Tukirudi kwenye Neno la Nabii Isaya, LINA MESSGAE GANI? kupata the full message sometimes inabidi usome the whole chapter or paragraph, Sometimes One line inajitosheleza, NA MESSAGE INAWEZA ISIWE MOJA KWA WOTE, KILA MTU AKAPATA MESSAGE YAKE KUTOKANA NA ROHO WA MUNGU ATAKAVYO MFUNULIA, KWA NENO LA HILI,  MIMI MESSAGE NILIO IPATA NI MOJA!

MUNGU AMEFUNGUKA  WAZI-WAZI KWAMBA BADALA YA AIBU UNAWEZA KUPOKEA HESHIMA NA TENA UKAPOKEA DOUBLE PORTION, WEWE KAA UKIJUA HILO LINA WEZEKANA  MDUA WOWOTE  NA POPOTE.

SASA KWA MIMI HII MESSAGE INANISADIA NINI KWENYE TRANSFORMATION?;NDIYO NIMEJUA SASA KUANZIA SASA AIBU HAITAKUWA FUNGU LANGU KAMWE, NA MTU AKIAMUA KUNI AIBISHA NDIYO KAMPIGA CHURA TEKE KUNIONGEZA MWENDO! NDIYO KWANZA NITAPATA MARA  MBILI (2) KUDADADEKI, NATAMANI KWELI WAJIPENDEKEZE KUNI AIBISHA NIPATE DOUBLE HONOR PORTIONS!

MFANO JUZI NIMEPEWA NOTICE MBILI(2) KWENYE MAENEO MAWILI YA BIASHARA!, MOJA NIME CONSENT MAANA BIASHARA SIO NZURI SANA, NA MWENYE NYUMBA ALIFIWA NA MUME LAST YEAR SITAKI KU-MFRUSTRATE, HIYO INGINE ANAPANDISHA KOO, NIMECHEKEA SANA, SIONDOKII NA JEURI YA KUNITOA HATAKUWA NAYO NA KOO HATO ONGEZA, TANGU AGUSIE HILO JAMBO TUNAMPELEKA KIROHO TU, NIMEMFUNGA MPAKA MBINGU YA SABA (7) AACHE TAMAAA NA YEYE NA ILE NYUMBA TUMEKUTANA WOTE WAZITO.

Tushakubalina HATUONGEZI HATA KUMI (10) Tumtulizee, Kila mtu anamfunga kivyake, Tumemfunga hata kama nyumba yake asikanyage pale mpaka 2030, Hata kama sisi tukihama kifungo kitakuwa LIVEEE yaani mpaka hio 2030, Nyumba tulibomoa tukajenga wenyewe kisasa alafu analeta tamaa, Kaingia choo cha kike, Aliona ki-dunia anatumudu! Ngoja tuone kiroho!

SASA WEWE UNAJI-ITA MLOKOLE ALAFU WATU WANA KUTISHIA MAISHA HUTO OLEWA UTAZEEKEA NYIMBANI UMETULIA TU, WANAKUTISHIA MKATABA WA KAZI UKIISHA HAWAONGEZI UKA-DHALILIKE UPO TU YAANI MWANAUME ANA KUTISHIA NDOA NAIVUNJA HII UKADHALILIKE UKAWE MSUNGO UPO TU, WATU WANAKUTAMBUA HIO BIASHARA UTAFUNGA KWA MADENI UKADHALILIKE UNANG’AA SHARUBU TU, ALAFU UNAJIITA MLOKOE NA UMEMPOKEA YESU, AIBU  NAONA  MIMI.

Isaya 61:7

Badala ya aibu yenu mtapata maradufu ,na badala ya fedheha wataifurahia sehemu yao; basi katika nchi yao watamiliki maradufu; furaha yao itakuwa ya milele.

HILI NENO KAMA ULIKUWA HULIJUI NIMEKUPA LEO, POKEA MESSAGE HIO NA ISHI NAYO KWAMBA KUABIKAAA WEWE SIO FUNGU LAKO ABADAN ASILANI, WAKIKUBEEP WAPIGIE KWA HILI  ANDIKO.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Scroll to Top
× IT Help Desk