KUMTEGEMEA MUNGU MPAKA MWISHO UPATE MAJIBU YAKO (SUNDAY WORD)

Wapendwa kuanza kumtegemea Mungu sio kazi, tunaanza vizuri kama watu vile ila ssue nikuendelea kukomaa kumtegemea Mungu mpaka mwisho!, Program tunaanza hata watu mia tano (500), Yaani kama hii ya October tunaenda kumaliza tukiwa arobaini na tano (45), Ndiyo maana kanisani tupo maelfu ila  wenye matokeo thabiti ya imani hawafiki Mia moja ( 100) kwani 95% ni mashabiki tu.

 

Isaiah 40:30

30 Even the youths shall faint and be weary, and the young men shall utterly fall.

 

Kuchoka au kuchoshwa na mambo sio kujiendekeza ni nature ya ubinadamu wetu. Nabii lsaya aliona hiyo na aka-nena kwamba kuna muda hata VIJANA wanazimia.

 

Wapendwa anatumia classification ya Vijana kama kundi la watu ambao they have everything to win, wapo on their prime-time.Umri wanao mkononi, uzuri wanao mwilini, afya wanayo kibindoni, nguvu wanazo mwilini, chochote kinacho hitajika kwenye ushindi wowote wanacho.

 

Lakini Nabii Isaya anatoa hoja nzito sana, kwamba “HATA VIJANA WANAZIMIA NA KUCHOKA!” na wasiposaidiwa “WANAWEZA KUFELI KABISA”

 

lsaya 40:30-31

Hata vijana watazimia na kuchoka, na vijana wanaume wataanguka.

 

English Version imeweka vizuri sana, “Young men shall UTTERLY fall”  Zingatia kivumishi UTTERLY! Unaweza kujiuliza Fall how ?

 

Wapendwa inaweza kuqa Fall in career!, Fall in economy, Fall in relationship, Fall in life

NA KUNA KIJANA ANA-FELI MAISHA.

 

Na ndiyo kinacho-tokea sasa hivi, Vijana wadogo ndiyo wanafeli Maisha kuliko sisi age go, Wakati zamani Ujana ulikuwa utajiri, Sasahivi ujana mzigo. Maisha ya Sasa yanavyoenda Kijana na Mzee wote mnaisoma namba tu, Wembe ule ule!

 

Wapendwa Wengi mna-anza vizuri sana kwenye maisha, unapata kazi, unapata ndoa yako, unapata kabishara kako, mna anza vizuri kabisa lakini at some point mambo yanabadilika, Unaacha kukua kama ukibahatika una-plate au hapo hapo officer mpaka unastaafu au unaporomoka kabisa na kushuka kuwa kitu cha ajabu na kupokea kabisa.

 

Unaanza mwaka na msimamo mwaka huu namtegemea Mungu kwa issue ya Mume, Unaacha na zina na kujiapiza kabisa, Kufikia hii November usha baruzaaa na wanaume 6 hapo 1night stand hazija hesabiwa; I’m not judging kama Nabii lsaya alichosema “EVEN YOUNG MEN SHALL UTTERLY FAIL” Sasa Young woman si ndio wewe sasa umekamilisha i.e UTTERLY FAIL iliyo-andikwa my wangu!

 

Maandiko yanasema Mapenzi ya Mungu ni mtu ajue siku hadi siku na ainuliwe utukufu mpaka utukufu! Sio panda leo, kesho shuka, panda shuka.

 

Proverbs 4:18

18 But the path of the just is as the shining light, that shineth more and more unto the perfect day.

 

Ecclesiastes 7:8

8 Better is the end of a thing than the beginning thereof.

 

Mungu kama Mungu anapenda ukianza career ya 800,000/= TZS umalize na 8,000,000 /= TZS , Ukianza mwaka na uchumba umalize na ndoa, Utukufu wako wa mwisho uwe mkubwa kuliko wa mwanzo.

 

Haggai 2:9-12

9 The glory of this latter house shall be greater than of the former, saith the Lord of hosts: and in this place willI give peace, saith the Lord of hosts.

 

NINI CHANZO CHA KUISHIA NJIANI, KUGANDA, ANGUKO MPAKA MTU HAFIKIE HATMA ALIYO KUSUDIWA?

 

Vyanzo nivingi ikiwemo ubinadamu wetu kama alivyosema nabiii Isaya tumeumbiwa kuchoka na kuzimia. Chanzo kingine nikumuacha Mungu pale tunapo-ona mafaniko kidogo tuuu!, Mpendwa ILI UFIKE MBALI LAZIMA UPOKEEE MSAADA WA MUNGU MARA KWA MARA KWENYE SAFARI YAKO.

 

Acts 26:22-23

22 Having therefore obtained help of God, I continue unto this day, witnessing both to small and great, saying none other things than those which the prophets and Moses did say should come:

 

MTUME PAUL ANAKIRI KWAMBA ILIMBIDI APOKEE MSAADA KUTOKA MBINGUNI KUWEZA KUFANYA ALICHOPANGA KUKIFANYA!; Kuna mda una kila kitu cha kufanikiwa kwenye mishe-mishe zako LAKINI HUFANIKIWI UNA VYETI NA GPA KALI LAKINI KAZI HUPATI!, NI MZURl PISI YA KWENDA LAKINI UNATONGOZWA NA MASELA TU, UNA AKILI ZA BIASHARA BALAA, UKISHAURI WATU WAMETOKA KIMAISHAA ILA WEWE MTAJI HUPATI NG’OO  NDIYO UTAMKUMBUKA NABII  ISAIAH! “EVEN YOUNG MEN SHALL FAIL UTTERLY” KUDADADEKI.

 

Mpendwa ukisoma Yohana 21; Utaona Petro ambae ni mvuvi proffesional, mwenye experience ya kutosha sekta ya uvuvi, akiwa na zana zote za kazi yake uvivu, Mashua na Nyavu, Anatinga baharini katika muda muafaka ambao samaki wanapatikana kwa wingi muda wa usiku.

 

PETER HAD EVERYTHING HE NEEDED TO CATCH FISH, VARIABLE ZOTE ZILIKUWA MAHALi PAKE SIKU HIO, LAKINI HAPATI CHOCHOTEE, HATA VIDAGAAA BASI VYA KULUMANGIA ANATOKA DRY DRY, NYAVU NYEUPE KABISA, ANAPAMBANA USIKU KUCHA  YAANI BILA BILA, HAAMBULII KITU, BAHARI INA MTOA DRY DRY, ILE KWENDRA, LEO HUPATI KITU! HATA NGADU HUPATI! KAFIE MBELE.

 

ASUBUHI WANARUDI UFUKWENI MTU ANAWAAMBIA KATUPENI NYAVU UPANDE WA KULIA ACHENI UBABAI, NA ASUBUHI SAMAKI WANA KIMBIA KINA KIREFU KUKIMBIA MWANGA! LAKINI NDIYO WANAPATA WENGI MPAKA ALMANUSRA WACHANE NYAVU MPAKA KUOMBA ASSIST; ACHANA NA KUPOKEA MSAADA KUTOKA MBINGUNI, HATA KAMA ODDS ZOTE HAZIPO UPANDE WAKO LAKINI MATOKEO YATA BUST TU, HUO NDO MSAADA SASA KUTOKA KWA MUNGU! HAUNA UBABAIFU! UMENYOOKA KAMA RULER .

 

Mambo uliyoshindwa kufanya na yakashindikana kabisa YATAWEZEKANA ASUBUHI KWEUPEEE KABISAAA! Wavivu wanajua huwezi shindwa KUVUA usiku ukakosa alafu asubuhi uchane Nyavu, Bahari hio hio ? Thubutu, Lakini Peter alipo-pokea msaada toka kwa Yesu alichana Nyavu asubuhi kweupeeee

 

Mpendwa Unaweza kuwa una vyeti vyako vizuri tu, lakini unafanya interview hupatiii kitu, Interview 10 zote hupiti, Mwanamke mzuri na kazi yako nzuri lakini hupati Mume, Wanakuja wanaotaka kumega kisela tu; SEEK HELP FROM GOD, SEEK HELP FROM HEAVENS.

 

 

Isaiah 40:31

31 But those who wait on the Lord, Shall renew their strength; They shall mount up with wings like eagles, They shall run and not be weary, They shall walk and not faint.

 

UKIJISUBIRIA MWENYEWE KIFATACHO NI KUZIMIA NA KUANGUKA TU KAMA NABII ISAYA ALIVYOSEMA; KUNA TOFAUTI YA KUMSUBIRIA MUNGU NA KUJISUBIRIA MWENYEWE; TOFAUTI NI KUBWA SANAAA!

 

WAPENDWA WENGI MNAJISUBIRIA WENYEWE AU MNASUBIRIA TU UPEPO MBAYA UJIPITIE WENYEWE NA SIO KUMSUBIRIA MUNGU ATENDE JUU YA HIO CHANGAMOTO; MTU HUJAOLEWA  MADAI YAKO UNASUBIRIA MUNGU AKUTENDEE  HILO ENEO LAKINI ON THE MEAN TIME UNAENDELEA NA ZINAA ZA HAPA NA PALE UNAFANYA TENDA NDOGO NDOGO KWENYE NDOA ZA WENZIO NA MAHUSIANO YA WENZIO, SISTER PLEASE.

 

MTU HUNA KAZI NA VYETI SHOGA ANGU UNAVYO, UMANDE HUKU UKIMBIA DADA,ULIPAMBANA LAKINI WAKATI UNAMNGOJA MUNGU KWA HIO KAZI UNA ISHI KWA KUTEGEMEA MA SPONSOR AM BAO NI WAUME ZA WATU, SISTER PLEASE; KUNA TOFAUTI KUBWA SANA YA KUMSUBIRIA MUNGU ENEO FLANI NA KUJISUBIRISHA UPEPO UPITE NA KAMA KARMA ITA KUHURUMIA!

 

JE UNA MSIBIRIAJE MUNGU  KIMAANDIKO?

 

1. UNA SOMA MAANDIKO; KUANGALIA NANI ALIPITIA CHANGAMOTO KAMA YANGU KWENYE MAANDIKO? NA ALIFANYA NINI KUVUKA ? UNASOMA MAANDIKO NA KUONGEZA UFAHAMU WA MAANDIKO NINI KIME ANDIKWA JUU YA HIO CHANGAMOTO YAKO ?

 

2.Engage in quality strategic prayers; Fanya maombi ya kila aina. Maombi ya shukrani, Maombi ya kukiri maandiko, Prayer in spirit, Prayer  in thanks giving, Maombi ya vita. Unavuruga vuruga, Wengimnaomba maombi aina moja, PRAYER WITH FASTIN, Sasa ndiyo inakuwa mwake-mwake! Sio prayers umevimbiwa, Una-wait kweli wewe?.

 

3.Engage in praise ministry; Tumia muda wa kutosha kumsifu na kumuabudu Mungu kwa utukufu wake bila kujali hio changamoto. Paulo na Sila walikuwa wakiomba na kusifuuu peke yako, ila milango ya gereza ilivyofunguka wafungwa wote wali-enjoy, Sasa wewe msifu Mungu hata kama huna company siku Akishuka na kukuvusha Wapambe watakuja tu.

 

4. Ministry of sacrifice; Sacrifice muda wako, Resources zako na Moyo wako kwa Mungu.  Jitoe kujenga Ufalme wa Mungu.

 

 

Psalm 50:5

5 Gather my saints together unto me; those that have made a covenant with me by sacrifice.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Scroll to Top
× IT Help Desk