Wapendwa uovu upo ndani ya kila mtu hata wale watumishi wa juu unao-waamini sana sanaa. Tunacho-tofautiana ni jinsi ya kukabiliana nao,The fact mtu hafanyi uovu dhidi ya wenzie haimaanishi uovu haupo ndani yake wapendwa UPO TELE kuliko hata wako, SEMA ANA-UMUDU NA ANAWEZA KU U-BALANCE NA KU U-CONTROL.
Kuna watu hampati kazi nzuri sababu SIKU MKIPATA, MTAFUNGUA JEHANAMU JUU YA WENZENU, Ofcourse some of them will deserve it from me and you preception maana muda wote wana kuchokonoa lazima ulipe kisasi lakini mbele za Mungu he expects better of you to forgive everything and everyone.
WAPENDWA NIAMINI MIMI WEWE UKIFANIKIWA KUPEWA NAFASI YA WATESI WAKO UTAFANYA MABAYA ZAIDI NA ZAIDI, KULIKO UNAOWACHUKIA NA KUWABEBA MOYONI SASA HIVI, MWISHO LAZIMA UNAKUWA HIVYO, LAZIMA WEWE UWE MBAYA ZAIDI NA UFIKE MBALI KWA UOVU KUZIDI WATESI WAKO; UNAWEZA UKAWA HUJUI BADO LAKINI UOVU ULIO NDANI YAKO NI WA KUTISHA KULIKO UNAO ULALAMIKIA KUTENDEWA YAANI ILI ROHO YAKO YA KUGOMA KUSAMEHE NI VUGU-VUGU LA HUO UOVU UNAANZA KUCHEMKA NA KUTOKOTA NDANI YAKO.
Watu wengi walilalamika kuteswa na Mama mkwe zao lakini hao-hao watu wamedumu kwenye ndoa miaka 30 kuendelea, lakini wao sasahivi ndio Mama wakwe yaani mapema sana miaka 10 mingi washa sambaratisha ndoa za watoto wao kitambo, SASA YEYE NA MAMA MKWE NANI MBAYA ZAIDI?
Kuna watu wamechelewa kuolewa lakini Siku ya kuolewa ambao hawatakuwa wameolewa hawana bahati! ATA WANYANYASA KULIKO ALIVYONYANYASIKA YEYE SABABU ANA MAJERAHA NA YANA KIU YA DAMU!
Wapendwa kuna watu hawakui kiuchumi sababu hapo hawana kitu lakini bado wana wanyanyasa na kuwachukia wasio na kitu sasa wakipata kitu balaa litakuwa zaidi.
MPENDWA UNAWEZA KUWA UME-OKOKA NA UNASALI SANAA LAKINI UOVU UMEJAA NDANI YAKO KEDE-KEDE NA UNA MZUIA MUNGU KUKUFANIKISHA SIO KWASABABU SASA IBADA ZAKO NI BATILI AU NI MUOVU LAKINI SABABU YA UOVU ULIO NDANI YAKO NI MKUBWA NA SIKU UKIPATA CHANCE TUMEISHA.
Wapendwa Mungu anajua Siku ukipata kazi ndio mwisho wa ibada, Anajua Siku ukivaa shela ndio mwisho wa wewe kwenda mbele zake, Sasa hizi heka-heka zako za maombi ya rasha rasha hazi mzugi, KABILIANA NA UOVU ULIO NDANI YAKO NA HAKIKISHA UNAFANIKIWA KUWA SAMEHE WALIO-KUKOSEA!
I HAVE BEEN THERE, I HAVE SEEN IT GO DOWN, I HAVE DONE THAT AND I AM LIVING WITH COSEQUENCES NDIYO MAANA NAKWAMBIA IT IS NOT WORTH IT, ACHANA NA KIU YA VISASI, RUN THE OPPOSITE DIRECTION OF REVENGE!; UOVU ULIO NDANI YAKO NI MKUBWA KULIKO HUO ULIO-TENDEWA.
2 Wafalme 7-14
Elisha na mfalme Ben-hadadi wa Aramu
7 Baadaye Elisha alikwenda Damasko Wakati huo mfalme Ben-hadadi alikuwa mgonjwa na alipoambiwa kwamba Elisha alikuwa Damasko alimwambia ofisa wake Hazaeli,”Mpelekee mtu wa Mungu zawadi umwambie atafute shauri kwa Mwenyezi-Mungu kama nitapona au laah.” 9 Hazaeli akapakia zawadi za kila aina ya mazao ya Damasko kiasi cha mizigo ya ngamia arubaini na kumpelekea Elisha. ( NYIE KUPELEKA CHOCHOTE KITU KWA WATUMISHI WENU AAAH, UOVU HUO UKO NDANI YENU.
Alipofika kwa Elisha alimwambia,”Mtumishi wako, Ben-hadadi, mfalme wa Aramu amenituma kwako; yeye anauliza,’Nitapona ugonjwa huu?’.10 Basi Elisha akamjibu,”Atapona; lakini Mwenyezi-Mungu amenionesha kwamba atakufa.” 11 Ndipo Elisha akamkazia macho akiwa na hofu hata Hazaeli akashikwa na wasiwasi. ( KUMBUKA ELISHA NI MTUMISHI GAIDI HABABAISHWI NA MTU WALA KITU NA ALIMJIBU NAAMAN MTU MZITO WA SHAMU DIRISHANI JUU YA UKOMA WAKE HAKUTAKA HATA KUONANA NAE LAKINI ANAONA UNABII JUU YA HUYU HAZAEL ANATETEMEKA UTUMBO NA KUANGUA KILO KIKUU MPAKA HAZEL ANASTUKA ATAKUWA KAONA NINI HUYU NABll JUU YAKE ?).
Ghafla, Elisha mtu wa Mungu, akaanza kulia. 12 Hazaeli akamwuliza,”Bwana wangu, mbona unalia?” Elisha akamjibu,”Kwa sababu ninajua maovu ambayo utawatendea watu wa Israeli. Utateketeza ngome zao kwa moto, na kuwaua vijana wao, utawapondaponda watoto wao na kuwararua wanawake waja wazito.” ( ELISHA NABII GAIDI NA MKALI-MKALI ALIWAITIA VIJANA BEAR/DUBU AKAWARARUA MPAKA WAKAFA KISA WALIMCHEKA ANALEGEA NA KULIA MACHOZI MAZITO KISA TU UNABII ANAO UONA JUU YA HAKA KA-MTU HAZAEL KALIKOTUMWA NA MFALME WAKE! MPAKA MUDA HUU HUYU HAZAEL HANA HISTORIA YA UOVU WOWOTE, NI MTU WA KUAMINIWA NA MFALME, UOVU WA KUTISHA UMO NDANI YAKE UMETULIA YAANI UMEPOA UNAMTETEMESHA ELISHA MPAKA KWENYE MIFUPA, HAZAEL ANASHANGAA NA KUONA MBONA MIMI MTU POA TU? MBONA NABII ANAKUWA DRAMATIC SASA ?).
13Hazaeli akauliza,”Lakini mimi mtumishi wako ni kitu kweli? Mimi niliye mbwa tu nitawezaje kutenda mambo hayo makubwa?” Elisha akamjibu,”Mwenyezi-Mungu amenionesha kwamba utakuwa mfalme wa Aramu.” HAZAEL ANASHANGAA UOVU GANI TENA JAMANI? MIMI KA MBWA TU?.
14 Ndipo Hazaeli alipotoka kwa Elisha, akarudi kwa bwana wake. Mfalme Ben-hadadi akamwuliza,”Elisha alikuambia nini?” Hazaeli akamjibu,”Aliniambia ya kwamba hakika utapona.” 15 Lakini kesho yake Hazaeli akachukua blanketi akalilowesha maji ,kisha akamfunika nalo usoni mpaka akafa.Hazaeli akatawala Aramu mahali pake.
UNABII WA ELISHA HAU KAWII, MAAANA ALIPORUDI TU KWA MFALME NA KUMDANGANYA ATAPONA, KESHO YAKE ANAMFYEKA KWA KUMZIBA HEWA NA HUO NDIO UNAKUWA MWANZO TU WA UOVU WAKE .