Wengi mtasema ushaanza, Umeona tarehe za mwisho wa mwezi unaanza manipulation, Gharama lazima tena za pesa, YOU WISH! Gharama za pesa ndio rahisi sana kulipa maana hata kama millioni kama umeweka kupata hiyo million you can always get another million, Mtanielewa mwishoni kwa pesa sio gharama za kupaparika.
Mathayo 2:14-16
14 Kwa hiyo akaamka, akamchukua mtoto na mama yake usiku,wakaelekea Misri. 15 na wakakaa huko mpaka Herode alipofariki. Na hivyo likatimia neno alilosema Bwana kupitia Nabii: ‘Nilimwita mwanangu kutoka Misri.’
16 Herode alipogundua kwamba wale wataalamu wa nyota wame-mdanganya, alikasirika sana, akawatuma watu kuwaua watoto wote wa kiume wenye umri wa miaka miwili kwenda chini katika mji wa Betlehemu na sehemu zote za jirani, kufuatana na ule muda ambao wale wataalamu walikuwa wame-mhakikishia.
Kama wewe ungekuwa mmoja wa wale walio poteza watoto wao kwa ajili ya huyu mtoto YESU, aliye windwa na Herode Mfalme how would you feel towards Jesus? Hii ndiyo moja ya sababu Wayahudi wana-mchukia Yesu kindaki-ndaki, GHARAMA YA KUZALIWA KWAKE ZILIKUWA KUBWA SANA SANA KWA WATU WALIO-ULIWA WATOTO WAO WACHANGA WASIO NA HATIA!, THEY ASKED GOD FOR MESSIAH NA HIO NDIO ILIKUWA MOJA YA GHARAMA YA MASSIAH, MPO?
Mpendwa njoo kwa Mama yake Mariah, NIMESEMA SOMA KITABU CHOTE CHA INJILI KAMA UNANGOJA NIKUPE KIPANDE ENDELEA KUSUBIRI EMBE CHINI YA MNZAI.
The minute Bikira Maria ana ambiwa amebarikiwa, Kwisha kazi! Inaanza mikosi mfululu upande wake! She was young, georgous waiting to marry her boo Joe!, Baada ya Ujumbe wa Malaika! Wengi mngetarajia sababu she was going for Gods mission things will be GRAND and EXTRAVAGANT, Siku anazaa, Mfalme wa Mbinguni sio mfalme wa wasiwasi, Going on a mission for God sio safari ya wasiwasi, Lakini nini kinamtokea huyu Binti mdogo Maria ?, Kwanza anadhalilika kuonekana na mimba kabla ya ndoa, Akiulizwa mimba ya nani? ya Roho Mtakatifu, Watu wanaona dish lime yumba, Hapo hapo Bae Joe nae anataka kumkimbia kimya kimya, Yaani mambo yanakuwa meusi-meusi, Mtoto mwenyewe anazaliwa kwenye Banda la Ngombe like seriously? Kitoto cha Mbinguni?, Kwa sasa kitoto cha Mbinguni kitategemewa kuzaliwa Safeee premium private ward, Zizi la ngombe mazee Chezea Gods mission wewe.
MARIA ALILIPA GHARAMA KUBWA SANA KUWALETEA MASSIAH, KUBWA KULIKO SHEKELI ENZI HIZO AU MILLION 2 YA SASA, Amekipata kwa shida na tangu kinatakiwa watu wana winda kitoto chake Wakiue tuu, Mpaka waka kiwamba msalabani.
MUNGU ANAWEZA KUWA NA NIA NJEMA YA KUKUINUA NA KUKUPA VIKUBWA, LAKINI KABLA HAVIJAWA HALISI SHETANILAZIMA ATAINUA GHARAMA ZA KUFA MTU, USIPO KUWA MAKINIUTA SUSA ULE UNABII. MPENDWA SHETANI LAZIMA AWAPIME IMANI YENU KWANZA KAMA INAJAA KlBABA AU DEBE AU PIPA?
Mayahudi wanafanikiwa ku-go past vifo vya watoto wao,WanaKaza Roho na KUMPOKEA MASIAH hivyo hivyo kiroho ngumu, Wanachagua kiganga yajayo na kuachana na yaliyotokea, Na ina walipa, YESU anawapatia makubwa sana na kuwaweka huru na utawala wa giza mazima.
Mariah anasimama thabiti na Gods mission, Anavimilia yote, Not once she complains nor doubts God! She takes all the heat, Analipa Gharama zote ilimradi jambo la Mungu likamilike kikamilifu,Not once she complains nor changes her mind.
AND SOMETIMES IT MAY LOOK LIKE THE DEVIL IS WINNING AND GOD HAS LEFT YOU ALONE LAKINI IT IS NEVER THE CASE! NEVER!.
Mpendwa wakati YESU anateswa na kusulubiwa Msalabani, Mitume walifadhaika sana, Muda wote wakawa wanangoja PLOT TWIST, There was no PLOT TWIST! YESU ALI-UWAWA MBELE YA MACHO YAO IN COLD BLOOD.
Yuda baada ya kuumuza alikaza FUVU kwasababu alijua of all People,Yesu ndo kiboko yao, There is no way hatojiokoa, Kama wingu lilifunguka kuwahakikishia HUYU NI MWANANGU MPENDWA ndio wamsulubishe si radi za kufa mtu zitalogwa kila upande, alivyoona hamna cha radi wala nini na YESU officialy was declared dead, Akaona nimefanya mambo mabaya, Hela tena sio tamu, Akajinyonga.
Kina Petro wanapoteana kila mtu ana ugulia upande wake, Hawana hamu na Pilato, Kwa muda ule wote wanaona kazi walio-ifanya miaka 3 yote BURE, Na mbaya zaidi wote wamekimbia Mwalimu wao mchana kweupe.
So hata wewe sometimes unaona kumtumikia Mungu unajichosha, Ni nonsense,Hamna faidaaa yoyote, Aibu ziko pale pale, Ufukara uko pale-pale, Mateso yako pale pale, Upweke upo pale-pale, Na ukiwaza sanaa unaanza kuona Mungu hakupendi.
Sio tu inaonekana Bali ipo waziiiikabisaaa shetaniameshinda miaka na miaka na bado ana Shinda na anakutambiaaaa kweli kweli kwenye maisha yako,wakatihuo Mungu yupo kimyaaaaaaa na hana mda na wewe!
Hata mitume walijisikia hivi kwa zile Siku 3, Mungu haku watumia ujumbe wowote kwa Malaika wala nini, Walilipa gharama za usaliti wao, Kwanini wamkimbie mwalimu wao mchana kweupe?, Kweli Simmon wa Kirene ndio wa kumsaidia Yesu msalaba baada ya wao kula na kunywa vyake kwa miaka 3? , Siku 3 walikaaa wana jamba-jamba. Sijui walipata wapi ujasiri wa kwenda kuchungulia kaburini Siku ya 3 kama kafufuka kweli ?, Kama na waona walivyokuwa wanaenda roho mkononi endapo wangemkuta kaoza anatoa funza.
Hata wewe shetani akikutambia LIPA GHARAMA za mikwara yake, Jua Mungu yupo na atajithibitisha kwako tu, Ni swalala muda, Kamweee giza haliwezi kushinda mbele ya Nuru. Tatizo wengi shetani akiwapiga gharama kidogo mna muacha Mungu na kurudia njia zenu, NDI O MAANA HAMVUKI MMENASA!
Mtu umekuwa na Mwanaume kabla hajaoa, akaja kaoa mtu mwingine ukageuka mchepuko sasa, Bado upo, Unafanya maombi ya Mtu Sahihi, Shetani kukupiga gharama kidogo tu, Umejirudisha kwa Ex unaendelea kuwa SIDE OSTRITCH, Sababu unaikimbiza 40yrs ushavuka kwenye Chick na Hen. Mpendwa Watu wengiwalio-olewa ambao mimi nimewaongoza hawakuolewa na Watu walio kuwa nao wakati wanakuja 2022.
Wengi baada ya maombi, yakaja mapigo mazito, Mtu ukonae miaka 4/5 anakwambia BASI, Sitaki tenaaa! Hapo umetoka kusali? Mna kumbuka nilisema bora ulipe gharama ya pesa, Sasa gharama za Ndoa unayotaka ndio heart break na Kama mnavyojua maumivu ya moyo hayapoi kwa ganzi, Si bora pesa na shetani hataki sh 10 yako anataka hiyo amani ya moyo wako, UKIJA KWANGU NAKWAMBIA NO BEGGING! LET HIM GO.
Wengi walivyo na kulipa gharama tangu 2022,THEY ON THEIR KNEES BEGGING FOR LOVE MAHUSIANO HAVANA TIJA WALA DIRECTION, NDiO WANAISHI HIVO KWA PENZI LA KUPIGIA MOGOTI!
Wengine wamechunwaaa wamebakia mifupaaa!
Wengine wame zeeka kwa manga ya so na disrespect !
Walio chagua kufa wame simama kuliko kuishi wamepiga magoti,waka Komaa na Mungu!WAKALI PA GHARAMA! Hutaki no sex kwendraaa ! Hutaki ndoajikatae teke teke! Nasimama na Mungu na simama kweli that’s on purrrr! BORA NIFE MPWEKE KULiKO KUFANYA BOOTY CALLS NA KUCHEZEWA KUSIKO NA MALENGO, KAMA MUOAJI HAMNA BASI MAHUSIANO HAKUNA BORA NITUMIE MUDA WANGU KUMUIMBIA MUNGU MAPAMBIO KULIKO SLEEPING WITH THE ENEMY!
MPENDWA GHARAMA WALI LIPA KWA MUDA, I WON’T LIE THERE WERE VERY DARK DAYS! GHARAMA ZILI LIPIKA, LAKINI PALIKUCHA, GOD CAME THROUGH, WAMEKUJA WANAUME HAWATAKI SEX DUNIA YA LEO!, WANA SALI DADA! NA WAMELI PA MAHARI NA KUOA KANISANI KABISA SHETANI WAMEMVUA NGUO STAND YA MKOA ASUBUHI KWEUPE, WALE WALIO KIMBIA GHARAMA NA KURUDISHA MAJESHI KWA BOOTY CALLS, KUPIGWA MITI KIJINGA JINGA NA KUENDELEZA UKUBWA JINGA WAPO EPISODE 360 YA UNMARRIED ANDSTILL FOOLISH AT HEART.
Mpendwa when the devil charges you pay the price and achieve your goals, Kukwepa gharama au kuahirisha kulipa gharama ni kujichelewesha kukamilisha matokeo yako, Lipa gharama once and for all! God will compensate you dearly!
Mambo ya kumkimbia Mungu pale shetani anapokuchapa na invoice matata ya ku prove your faith ndo yana wachelewesha, Na shetani akijua ndiyo udhaifu wako atakuwa ana kushinda kwa vigharama vidogo vidogo.
Kuna mtu ni boss analipwa 18m kwa mwezi anakwambia kila alipo muomba Mungu akue kazini alikuwa anafukuzwa kazi anateseka miaka 2, anaitumia kanisanikiroho safi, afu anapata ingine mshahara mara 3/4 wa ya kwanza, Yaani kabla haja Omba kupanda viwango ana mwambia kabisa mkewe ajiandae KISAIKOLOJIA miaka 2 ya njaa loading!,Na alifanya haya akiwa mdogo na majukumu sio mengi! Umri na majukum u ume Mkuta sahivi Ana 38 na ndo anachukua hio packeeee! Mkewe mwanzo waligombana sana alimuona ana tamaaa! Lakinisahivi anshukuru mumewe ha kumsikiliza, Sasa mtu 26yrs unakimbia gharama kweliii?