Career Hell

 

Mhubiri 9:10

Lolote mkono wako utakalolipata kulifanya, ulifanye kwa nguvu zako; kwa kuwa hakuna kazi, wala shauri, wala maarifa, wala hekima, huko kuzimu uendako wewe.

Powerfull verse! Na ina interpretation nyingi sanaaa! Mara nyingi hii verse ni controversial! So hata wewe unaweza kuwa na tafsiri yako sio lazima ukibalinae na yangu.

 

According to my understanding, Kuzimu inayosemwa hapa inaweza kuwa kuzimu ya motoni lakini not necessarily limited kwenye hio ya motoni mpaka ufe. Unaweza kujipeleka kuzim ya hapa hapa duniani ambako unajikuta uko in bondage of situations and circumstances ambazo zinakutesaaa na kukudidimiza na kukufosi uishi bila furaha wala sense of fulfillment.

 

Career hell mara nyingi ni matokeo ya uzembe na kutokujal, lack of responsibility and accountability kwenye nafasi Mungu alizotuweka. Mwisho wake ndo kujikuta huna kazi, wala ushauri hausaidiii tena,wala hakuna maarifa yanayofaaa, wala hekima ukishafika hio state ya

Unfortunately wengi mpo hapa kwenye situation ya Career hell!

Mungu amekufanyia nafasi nzuri, baada ya kukaa kwenye hio nafasi ukamuacha Mungu, kufanya ibada, kulipa zaka na sadaka kazi ya Mungu iendelee,sio shida zako kabisaaa. Katika miaka uliofanya kazi hakuna hata walau miezi 3 atleast umeenda kwa kumfurahisha Mungu.

 

Okay basi Mungu umemuweka pending hata vya kaisari kama hard-work  ,commitment, dedication  huku mpa Kaisari wala nini. Hio nafasi umeigeuza Chakalako la uvivu, Wizi,kusengenya wasio na kazi, majivuno kwa ulio soma nao na family members, ufujaji na vibomu wenyewe mnasema marupurupu  hujampa Kaisari chochote. A kajibambe hukooo! Alaaaa!

 

Congratulations  maana umefika stage Mbingu zimekufungia madirisha na Mi ango yotee.  Hazikutambuiii. Na Dunia inakuzomeaaaa. Kidogo kwa ibada zako za zamani Mungu Ana kurehemu hapa na pale hutofukuzwaa kazi ila utatumikia nafasi za chini mpaka kuongozwa na watoto rikala wanao utawaita BOSS! CA REER HELL!

 

Tatizo kubwa mtu umesha haribu misingi ya Career yako kitambo alafu unataka ufanye chupli chupli ya kupaka nyumba rangi, bila kurekebisha misingi huwezi pata matokeo. Ndo maana ghafla unaanza kutekeza masadaka na ibada za kutosha juu ya misingi mibovu. Kupata matokeo ni ngumu.  Umewafanyia watu ubaya miaka na miaka Damu

zao na familia zao zinakulilia. Kwa kumtoa mtu kazini umeharibu hatma za watoto wake, ana kulaani kila ukiamka na kila akilala.Umejizima data unataka uendelee ulipo. Thubutu!

 

Zaburi 11:3

Kama misingi ikiharibika, Mwenye haki atafanya nini?

 

Jinsi kazi zilizo misingi ishaharibika mda, boss akimuonea mtu ukakaaa kimya ndo Umefanya featuring kwenye kudhulumu haki ya mtu. Sawa ulibakia kazini ila hutafurahia hio kazi. Mwenye haki angefanya nini kwa ukimya wako? Misingi mingine umeharibu mwenyewe kwa raha zako wala boss hausiki Kama kuwa mchoyo boss hapo anaingiaje   ?

 

Umepanda ubatili miaka na miaka, kushinda njaa dakika za majeruhi haiwezi kuzuia mavuno manono ya shehena ya ubatili which is due kwenye hatma yako.

 

Sijataka kuwafundisha Career Growth wakati misingiyenyewe ya career zenu imajaaa ubatili mtupu. Ndo ingekuwa kupaka rangijumba bovu, mda wowote linaporomoka. Mngefanya hii program bado mkakipata kinacho waji a vile vile Kama ambavo jioni hii mnajitahidi kuukimbiza mwenge kwa maombi ya crush program na mwenge umegoma. MISINGI MIBOVU.

 

Luka 6:46-48

46 “Kwa nini mnaniita,’Bwana,Bwana’ nanyi hamfanyi ninay owaambia?

47 Nitawaambieni alivyo mtu anayesikia na kufanya ninay osema.48 Yeye ni kama mtu aliyejenga nyumba akachimba chini na kujenga msingi kwenye mwamba.Mafuriko yalipotokea,yakaikumba ile nyumba wala haikutikisika,kwani ilikuwa na msingi imara.

 

TUREKEBISHE MISINGI YA CAREER ZETU! Ill TUPATE MATOKEO YATA KAYO STAND THE TEST OF TIME LAZIMA TUANZIE KUREKEBISHA MISINGI YA NAFASI MUNGU ALIZOTUW EKA.

 

Kuan baadhi yenu  ITS TOO  LATE! WASHAONDOLEWA KWENYE HIZO NAFASI,WENGINE NYARAKA ZISHAANDIKWA  KWA HABARI YA KUTO RENEW CONTRACTS, WENGINE TER MINATION, WENGI TAYARI MKO BLACK LISTED HAMTOPANDA CHEO JAPO MNA KAUMUHI MU  HAMTOFUKUZWA.

 

Lakini wengine mna bahati bado hamna run out of Gods mercy. Kweli mmezingua big time! Lakini Mungu bado ana imani na nyie kwamba mtabadilika na kumrejea. Basi hii post iko JUST IN TIME.

 

Nafasi yoyote uliyokalia ni kwa rehema za Mungu.

Wangapi wames oma na hawana nafasi yoyote. Tena umesoma nao kabisaaa na walikuzidi akili. Ni rehema za Mungu umekalia hiko kiti. Je unakumbuka Hilo na kutimiza kusudi la Mungu kukuweka hapo au ndo upo kivyako vyako.

 

Misingi inatekebishwa kwanza kwa SELF REFLECTION! Wewe mwenyewe ujitafakari na kujitam bua kwamba umemkosea Mungu sana sanaa. Sio mimi Mtumishi nikwambie. Laaaa! Wewe Kama wewe jitathmi ni umemkosea Mungu kwa MDA gani, MAGNITUDE ya makosa yako hapo ofisini, DAMA GE ulioisababishia kampuni na watu wengine. Feel the remorse na weka nia ya kubadilika.

 

Luka 15:17

Alipozi ngatia moyoni mwake, alisema, Ni watumishiwangapi wa baba yangu wanaokula chakula na kusaza, na mimi hapa ninakufa kwa njaa. Sistahili kuitwa mwana wako tena;nifanye kama mmoja wa watumishi wako.

 

Exactly the Prodigal Son!     Ukijua makosa yako, na kurejea kama mkosefu ataanza kukusikia tena. Sasa usisubiri mpaka ufike hatua ya kula maganda ya nguruwe. Mwenyewe kuongeza kweli kusudi la Mungu kuniweka hapa sijatimizalolote. Ndo maana nimenasa hapa. Nikicheza mambo yatakuwa mabaya zaidi.

FANYA TOBA YA DHATI

Fanya toba ya dhatiii kwa upungufu wako wote kwenye hio nafasi. Wiki nzima. Sio toba ya juu juu tu! I guarantee you Ukifanya toba ya dhati sio ya procedure, ukaja kufanya CAR EER GROWTH hata kama mambo uliofanya ni mekundu kama Damu kibali chako kitatoka.

 

2 Mambo ya Nyakati 7:14

Ikiwa watu wangu, walioitwa kwajina langu, watajinyenyekesha , na kuomba, na kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya; basi, nitasikia toka mbinguni, na kuwasamehe dhambi yao, na kuiponya nchi yao.

MUNGU BADO ANA UWEZO WA KUIPONYA CAREER YA KO LEO HII.

 

 

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Scroll to Top
× IT Help Desk