UTUKUFU ULIOPOTEA KWENYE UCHUMI NA MAISHA YAKO.

Ayubu 19:9

Amenivua heshima yangu, na kuniondolea taji kichwani pangu.

 

Watu wengi once upon a time waliyapatia maisha na wakashika nafasi na pesa.Walikuwa na utukufu wao sio wa kitoto! ALAFU UKAPOTEA! WOTEEEE! KAMA MOSHI WA UBANI!

 

Wapendwa hamna watu wanao nikausha damu kama hawa!, Wapo on a dangerous mission to return to the top! and on top is where they cannot return! Unless wajitambue kwanini waliporomoka!

 

UTAWASIKIA WENGINGE WAKISEMA PASTOR KWA GHARAMA YOYOTE NIREJESHEEE UTUKUFU WANGU!, THUBUTUUU!  MNATAKAGA WENYEWE KUTAPELIWA!

 

Utukufu hau-ondolewi ghafla tu bila sababu!, Na as Long as sababu zilizo sababisha utukufu wako kuondolewa zipo valid na Hujazitambua wala kuzifanyia kazi utukufu utausikia kwa wenzio.

 

KWANINI UTUKUFU WAKO ULIONDOKA?

  1. Ku-Operate eneo ambalo huna Neema ya Mungu ya  Kutosha na Kuacha eneo ulilobarikiwa.

Mpendwa unakuta mtu umebarikiwa kuimba, na ni katika hilo eneo Mungu amekupa kibali cha juu sana!, Unaacha kuimba na kuanza kuhubiri!, Utaporomoka!, Watu hawatakuelewa!, Kanisa halitajaa! Utaipata fresh!. Na hakika Tatizo sio wewe ni hiyo Field uliyoshobokea! Huna kibali nayo!.

 

Umebarikiwa kwenye   eneola upishi! Ukipika watu wanaji amba! Umepata mafanikio eneo hi o,ukiona watu wa nguo za uturuki wana vimba unaachana na jiko na unga wa ngano unafungua biashara Ya fashiooon!! Wewe mwenyewe umekuja na Lorry mjinina fashion wapina wapi? Unauza jiko Lako na kwenda Uturuki na hio safari ndo Ya kuelekea mwisho wa utukufu wako!

 

Wewe una kazi nzuri sanaa!,  Umebarikiwa! Lakini kwa vile umeona watu wanauza-uza vichupi ili wabaki mjini, na wewe una-washwa kuuza!, Ofisini umepewa utukufu kama wote lakini na biasharaunataka ufanye!, Ukiwaza wewe una mtaji na unaweza ku-Access mtaji mkubwa ZAIDI kuliko sisi pesa iko nje nje! lakini huwazi Je, neema za MUNGU eneo la biashara unazo? Unaishia kuchoma pesa! Wenzio tunapata sababu Mungu anajua asipo rehemu tumekufa na njaaa!, Ofisini hatuna utukufu wowote!, Wewe utaweka pesa na pesa na utabakia na madeni lakini hio biashara ndo itakuwa anguko lako na Shimo lako la uharibifu!.

 

  1. Kumuacha Mungu baada ya Kufanikiwa. 

Wewe kabla hujafanikiwa  ulikuwa unasali na kufunga na kutoa sadaka!, Ukipata ka-utukufu kadogo tu kosaaa! MUNGU BYE BYE! Ukiwa huna kazi program back to back!, Ukipata kazi huwezi fanya program unahitaji nguvu kufanya kazi!Utasataafu nafasi ulio Ajiriwa! na Biashara ikiwa mbaya huna fungula 10,huna limbuko mimi ndo mtumishiwako! Ukitoboa hujaokoka!

 

Kwanza una kanisa lako tangu mdogo!, Mambo ya online utapeli mtupu! Ni swala la mda tu utarudi ulipotoka!, Mpendwa Kama umetumia Formula flani za Kiroho kupata matokeo flani jua siku ukiacha kuzitumia na matokeo unayoyapata yata yeyuka kama yalivyokuja ghafla, Kadri unavyopata muweke Mungu Karibu.

 

  1. Kuridhika na Kiburi

Unapata mafanikio kidogo tu kiburiiii kama chote!, Kama interview za TRA! Wengi walioenda written waliniambia! , Kupata oral tu! Wakanikata! Sawa!, Sisi ndo Wandewa hapa mjini! Corporate Games zote Code tunazo!, Waliorudi tukayajenga wamekula mema ya nchi! Hata aliye-kwama bado tupo pamoja na mzingatia.

 

Pride ni kitu kibaya sana! Hata kama kitu ilikuwa ukipateee! Hutokipataaa! Na kitakuuma maisha yako yote!, Wafanya Biashara wengi wakipata Jina na ka-neema kidogo tu kosa! Mnaona mmefika na mmemaliza kila kitu! Mnaanza kudharau wateja, wafanyakazi, ndugu ,watumishi unavimba  kichwa!.

 

Mpendwa ni swala la muda tu! Kila kitu kita crush down!, Wateja watakukimbia, Wafanyakazi watakukimbia, mpaka mke au Mume atakukimbia. Shetani anakujaza uwadharau wateja alafu anawajaza wateja wakukimbie!

 

  1. Kupoteza Uelekeo na Kutaka Kufanya Kila Kitu.

Ukipata mafanikio kuna ku-data flani na kutaka ufanye wewe kila biashara! Matokeo yake zingine zinakufilisi HATA zile ulizopata nazo utukufu zina filisiwa na hizi zingine!, Mtu Huyo huyo uuze nguo,upambe harusi, uuze keki za sherehe! Wewe Huyo huyo dalali. Matokeo yake unapoteza focus kabisaaa!Kila sehemu una chovya chovya! Matokeo biashara zote zina kosa usimamizi! Zinakufa kifo cha mende!

 

Mimi mdogo wangu Ramsekiana niinspire sanaaa!, Natamani na mimi Umri huuu nifanye biashara za Ramseki!        Simakubwa hayaa jamani! Kila siku naingia Page yake! RAMSEKI na Mtoto mmoja wa mjini  wa kitambo KIMCHINA BUSINESS! Na wakubali sanaaa! Ila ndo imeishia hapo hapo kuwakubali!

 

Sasa unakuta mtu miaka 30 na unataka ukimbizane na kina Ramseki na Kimchina kwa mwiligani na akili gani? Unaweza kujitoa ufahamu wewe? Tarambe za tiktok utaziwezaaa? Kuunganisha metro China kwenda mashambani utaweza? AGE GO FAR MY DEAR! Jicho lenyewe lishaingia ukungu!, Utamalizia Akiba yako ya ujana usipate chochote!, Wale wapo 24/25 vichwa vya motooo!

 

Mtu unaanza huduma au kanisa likiwa kubwa unaacha madhabahu na kugeuka Manager au Administrator kufatilia sadaka kwa ukaribu!, Ukistuka waumini wamekata! maana neno limekata! Kifatacho cha kumanage hakuna!, Wapendwa Kuna mtu aliniuliza mbona hutoi misaada in person? Nilimjibu, Mimi ni mtu wa madhabahu na kueneza gospel na kuifundisha! Hapo ndo Focus yangu ilipo!, Ningekuwa mtu wa misaada ningefungua NGOs! Sababu misaada ni sehemu ya ibada nawapa wengine nafasi wenye filed  yao!

 

Kama hii charity ya December anafanya fulo flove foundation! Kuzunguka vituoni, kupata sizes na vipimo, kupata paper work na kufanikisha distribution nzima!, Sababu ni mtu Aliyesomea sociology she is the best!

 

Mwingine ni procurement anashinda kariakoo kunitafutia Ma-sale! Tupate bei nzuri!, Kazi inaenda huko nje,mimi Nina kazi Ya kuombea sadaka ,kuachilia neno na kuandaaa upande wa kiroho kwa walio toa! Ki a mtu na speciality yake! Na mambo so far yanaenda vizuri sanaaa!.

 

Mpendwa Ukiona utukufu wako umeporomoka Jiulize Kwanini? Alafu Fanyia Kazi! , Hili suala la Kujaribu Kurejea On-Top Bila Ku-solve issues zilizo kushusha hufanyi lolote!. Kwani Kama Sababu ni Pride bado itakushusha tena , Kama ni Kiranga cha Kufanya Kila Kitu bado kitakushusha tena. Mimi nilisha poromoka na nikiwa chini nikausoma mchezo! sijarudia makosa!, Tumia muda wako kuchambua nini kilikushusha na kwa nini? alafu kubaliana nacho!, Kama ulishafika juu kurudi juu tena ni jambo linalowezekana! Ukijua kilicho kuporomosha.

 

 

 

 

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Scroll to Top
× IT Help Desk