Business Favour

Mpendwa ukifanya maombi ukabahatisha matokeo mara moja hiyo ni breakthrough (mpenyo) kwenye  eneo hilo na ukifanikiwa kurudia matokeo yaleyale zaidi ya mara tano (5) hiyo ni favor!

Kwa mfano Mpendwa ukiomba yakuwa Mungu naomba niuze sana leo na ikawa ukauza sana na baada ya hapo ukame ukaendelea hiyo ni BREAKTHROUGH na kama ikitokea umemuomba Mungu siku isiishe sijauza na ukauza mwezi mzima bila kujiuliza hiyo ni FAVOUR.

Neno la Mtumishi

Wapendwa chagueni ni  wafundishe ku un-lock business favor ( ni process ngumu sana lakini ni njia ya muda mrefu na ikianza hiishi kamwe) au Business breakthrough ( Hii ni njia yenye matokeo ya haraka na muhimu kama unataka kuepukana na madeni ya haraka haraka), Mwanzo niliwafundisha Prosperity na imesimama muda mrefu na baadhi yetu wakasema sasa sisi amabao hatukusoma na tuliojiajiri utatusahau hadi lini? Msijali wakati umefika. Tutaanza na kimoja kasha tutaenda Upnyaji/  Heaing alafu tutarudi katika mahusiano.

Business Favor

Isaya 48:17

BWANA, Mkombozi wako, mtakatifu wa Israeli asema hivi; Mimi ni BWANA Mungu wako, nikufundishaye ili upate faida, nikuongozaye kwa nia ikupasayo kufata.

Sasa jambo hili sio la mara moja au mbili nila maisha yako yote ikijumuisha kaa unafanya biashara peke yako au na Mungu .Mpendwa usipende kufanya vitu bila kumshirikisha Mungu na pindi mabo yanapoenda kinyume au katika hali isiyo sawa unaanza kumkumbuka Mungu yaani unakumbuka shuka wakati kumekucha hakika utavuna mabua katika shamba la miwa.Umeajiliwa na kufanya kazi zaid ya miaka kumi (10) lakini hujawahi kutoa zaka hata shilingi kumi, na siku ukifukuzwa kazi ndiyo unaanza kufunga???, Mpendwa  nipende kukuambia pamoja na kufunga kwako na kuanza kujitolesha sadaka Barua utaipata na katika tarehe ile ile utaacha kazi.

ISHI NA MUNGU KWENYE MAMBO YAKO YOTE KILA SIKU ILI VIKIHARIBIKA UNAKUWA PAMOJA NAYE NA VIKITAKIWA VIENDE VINAENDA NA MUNGU, NA KATIKA MUNGU HAKUNA LINALOSHINDIKANA.

Uchumi/ Riziki ni kati ya vitu amabavyo Mungu anagawa mwenyewe! Kwa kanuni zake na kupata lazima utimize kanuni zake. Ndiyo maana kuanzia Makuhani, Musa, Waamuzi,Manabii, Yesu na Mitume hakuna aliyewahi kumfungulia mtu uchumi! Sio kwamba uchumi haukuwepo kulikuwa na SHEKELI ZA SILVER  na DHAHABU na watu walikuwa waroho wa shekel kuliko hata sasa mfano katika biblia tunauona kwa Yuda Eskarioti na Zakayo Mtoza Ushuru.

Wapendwa lakini hakuna hata sehemu moja mmoja wao anasimama na maombi specific ya kufungulia uchumi, hakuna kwa katika suala la uchumi Mungu alishaweka kanuni zake tangu agano la akale na utaona waliotimiza kanuni zake walibarikiwa sana nah ii uwe Mchungaji, Mwana maombi usipotimiza kanuni zake utaisoma namba kwani hakuna maombi ya kusimamia ni kuzijua kanuni na kuzitekeleza pekee, na kama hutaki biashara yako hiwezi kwenda kokote utaishia ufungs hsdi upate vidonda vya tumbo, lakini matokeo madogo kama sisimizi.

Wapendwa tuzifahamu kanuni za kukuza uchumi:

  1. Uchumi unakuzwa na Matoleo

Wapendwa utajiri wowote upo duniani tayari hakuna hata senti moja itashushwa kutoka mbinguni,tofauti na uponyaji lazima utoke mbinguni uwe delivered na malaika., Mpendwa maombi ya Upanyaji ndiyo maombi mazito kuliko maombi yoyote yale kwani lazima kuwe na muunganiko wa moja kwa moja (direct connection) na mbingu.

Lakini uchumi uko tayari kwa watu hivyo ni suala tu la kumanuva na kumgusa Mungu awaguse wale mataifa wakuletee hizo shekeli, Na njia pekee ya kumgusa Mungu ni kwakuwapa wengine wanaohitaji zaidi yako yaani ni lazima wewe uwavushe wengine ndio na wewe Mungu akuvushe, It’s a two way process!

TOA UPOKEE! Na ukitoa sana utapokea sana, ni wewe tu kujipimia, Mfano katika maisha yetu ya kawaida nchini Tanzania Tajiri Bakhresa anatoa na kusaidia sana , hivyo anapokea sana pia na utajiri wake unaongezeka kila kukicha.

Mpendwa ila tusisahau kuwa sio lazima kila sadaka Mungu aikubali! Hadithi inaanza mwanzo kabisa wa Biblia Mungu anakataa sadaka ya Mtu !, Tunaona Kaini anatoa sadaka lakini Mungu anaikataa kwani haikumpendeza na kumuadhibu juu! Kwa nini? Katika lugha rahisiKaini alitaka kumlaghai Mungu ( Kumlow-ball Mungu), Mpendwa Mungu anajua hadi senti yak mwisho alafu unampa vipi makapi? Ataikataa sadaka yako.

Na ndio sisi hao hupenda kusema tunatoa sana lakini kimya!!, hii ni kwa sababu unatoa MAKAPI! Moshi wa sadaka yako haufiki popote, haujavuka hata paa la Kanisa , Mfano katika Biblia Moshi wa Sadaka ya  Abeli ulifika Mbinguni,Mpaka Kaini akashangaa. Hivyo mpendwa nipende kukusihi kuwa ukwa serious na zingatizi kwenye matoleo yako , Mungu atakuwa serious na atazingatia majibu yako.

Mpendwa unawezakumdanganya mtumishi lakin hauwezi kumdanganya Mungu kwani mpaka ile pesa unayotoa na kumpa King’asti wako ili akupooze roho anajua ni kiasi gani, hata zile pesa unazomwagilia moyo anajua nazo ni kiasi gani hivyo ukienda mbele zake ni MAKAPI anaona hauko serious na hiyo biashara au promotion. Hivyo akija Yule alaye anakutafuna mpaka mizizi, na wewe utaishia kulalamika natoa ila sipokei.swali ni UNATOA NINI? Hapo Benki una million 17 (17 m) unatoa zaka 20,000 alafu unataka biashara ikue, itapambana na Alae! Na ataitafuna biashara yako haswa na Mbunguni wataendelea kusifu na kuabudu kama kawaida.

Malaki 3: 10 – 12

Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa nia hiyo, asema BWANA wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni na kuwamwagieni Baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha au laah. Nami kwa ajili yenu nitamkemea yeye alaye, wala hata-haribu mazao ya ardhi yenu; wala mzabibu wenu hautapukutisha matunda yake kabila wakati wake katika mashamba, asema BWANA wa majeshi. Na mataifa yote watawaiteni khei; maana mtakuwa nchi ya kupendeza sana.

Nami kwa ajili yenu nitamkemea alaye!! Huyu alaye sio mwema kabisa kazi yake ni kuharibu, kupukutisha vitu kabla ya wakati wake na kuhakikisha havikui wala haviendi popote yaani anahakikisha unabakia hapo ulipo, ni mbaya sana huyu alaye na Mungu anamkemea pale unapotoa ZAKA na SADAKA.

NB; Fuatilia Somo la Sadaka inayoleta Matokeo kwanza.

Aina za Matoleo yatakayo kuza Biashara yako.

Mpendwa matoleo yapo mengi sana! Lakini nitakufundisha machache kama framework au skeletoni kwa wanaoanza kujifunza (begginers), Ukifanikiwa katika haya utakuwa unaongez akadri utakavyo jaliwa! Lakini kumbuka framework hii ni muongzo wa kuanzia hivyo jitutumue uweze kufanikisha, ndiyo ngazi ya chini au ngazi wa wanafunzi.

  1. Zaka

Tumeona katika Malaki 3: 10 – 12 kazi ya zaka ni Mungu kukubaliki mpaka kusiwe na sehemu ya kuweka Baraka zako, ameahidi kukufungulia madirisha ya Mbinguni, na kumtuliza ALAYE! Mpaka biashara yako itasifiwa kuwa niya kupendeza,Neno linasema haya yote yatatoea kukiwa na ZAKA KAMILI lakini kibinadamu tunaweza kuanza na committiment ya kiasi Fulani kwanza mfano tunaweza kuanza na laki tano kamili (500,000) kama imekushinda unaweza kuanza na laki moja kamili (100,000) kila mwezi yaani kiasi kitakacho kuweka huru na utaweza kuwa commited nacho, usiruke mwezi, usitoe kwa kuchelewa, jipe hata muda wa miezi sita 6 ya kutoa kiasi hicho kwa uaminifu , hakika utamshangaa Mungu. Yale mawazo ya kuwa zaka nato a wapi sio muhimu cha muhimu ni kutoa, peleka kokote ila toa. Iwe unap Sali au kwa jane yatima, au kwa wanao kufundisha neo , kokote kule Mungu ni yuleyule.Lakini cha muhimu ni kila mwezi kitoke kiasi ulichopanga na kwa wakati.

  1. Malimbuko

Kutoka 34: 26

“Mazao ya kwanza ya ardhi yako utayaleta nyumbani kwangu mimi Mwenyezi Mungu, Mungu wako.”

Mithali 3: 9 – 10

Mheshimu BWANA kwa mali yako, na kwa malimbuko ya mazao yako yote, Ndipo ghala zako zitakapojazwa kwa wingi, na vyombo vyako vitafurikwa na divai mpya.

Ezekieli 44: 30

Na kitu cha kwanza cha malimbuko yote ya vitu vyote, na kila toleo la kila kitu cha matleo yenu, litakuwa la makuhani. Tena mtampa kuhani sehemu ya kwanza ya unga mbichi, ili kuleta Baraka juu ya nyumba yako.

Yeremia 2: 3 SRUVDC

Israeli walikuwa utakatifu kwa BWANA; Malimbuko ya u zao wake; Wote watakao mla watakuwa na hatia; uovu ujawajia; asema BWANA.

Kumbukumbu la Torati 18:4

Malimbuko ya nafaka yako, na divai yako, na mafuta yako na manyoya ya kwanza ya kondoo wako umpe.

Walawi 2: 12

Unaweza kumletea Mwenyezi Mungu mazao yako ya kwanza kama sadaka.Lakini hayo ayatatolewa madhabauni kama harufu ya kumpendeza.

Mpendwa kwa muda wako soma Kutoka 22:29, Kumbukumbu la Torati 29: 2 na Warumi 11: 16 kwani maandiko ya malimbuko ni mengi sana na Malimbuko maana yake ni uzo la kwanza inaweza kuwa ukianza mwezi, au wiki au siku. Ni wewe kujipimia na kuchota Baraka kadri ya hitaji lako.

  1. Mavuno

Kutoka 23 : 15 – 16

Mtu yeyote asije mbele yangu mikono mitupu tena, Sikukuu ya mavuno, hayo malimbuko ya kazi zako za kupanda mashambani tena, sikukuu za kukusanya mwisho wa mwaka,hapo ukapo kusanya uliyoyataabikia shambani.

Kumbukumbu la Torati 24:19

Uvunapo mavuno yako katika shamba lako, ukasahau mganda shambani, usirudi kuuchukua; na uwe wa mgeni, au yatima, au mjane; ili BWANA  Mungu wako akubariki katika katika kazi zote za mikono yako.

Walawi 19 : 9 – 10 BHN

Utakapovuna mavuno ya nchi yako, usivune kabisa hadi mpakani mwa shamba wala usirudi nyuma kaukusanya mabaki.Msirudie kukusanya kila kitu katika shamba la mizabibu, wala usiokote zabibu zilizoanguka chini; utawaachia maskini na wageni, Mimi ndimi Mwenyezi Mungu, Mungu wenu.”

Mpendwa kikubwa maandiko yanasisitiza kila ukifanya biashara ukapata basi kidogo waachie maskini na wasiojiweza au wagawie hapo kwenye ulichovuna. Wengi wetu hujisaha, huwa tukipata faida basi tunatumia yote kujispoil na kutapanya, Hii sio sawa,inabidi kuwabariki na wengine. Tena hapa Mungu hajapanga kiasi, wewe hata ukitoa kwa ushahidi ila toa. Mfano katika maisha ya kawaida uwapo Ofisini hata kama wewe ni Boss sio lazima safari zote za nje unaenda mwenyewe waachie wale Juniour wako hata zile mbaya mbaya ili nao wapate Per DM ni haki yao lakini wakumbuke Mungu ndiye anapendezwa na hilo.

Mpendwa hakikisha kila unapovuna mtolee Mungu vya kwake, lakini na wenzio kidogo nao waonje jasho lako kidogo. Sio mavuno yote unajichana wewe na familia yako tu haipendezi.Unavyokuwa mwepesi kuwabariki wengine na Mungu anakuwa mwepesi kuwafanya wengine wakubariki zaidi. Haya matoleo ya mavuno ni mepesi sana unatoa wakati wa neema zako zikiwa zimejaa, unshindwaje??

  1. Kupanda Mbegu

Mpendwa  mada hii nili-iongelea sana huko nyuma tafadhari  pitia mafundisho ya nyuma kama hatukuwa pamoja au pitia hapa (link)

  1. Sadaka za Maagano

This is my favourite. Mpendwa ni sadaka zisizokuwa na kanuni wala muongozo ni wewe tu unakubaliana na  Mungu yaani makubaliano binafsi kwa terms binafsi.

Mpendwa zinaweza kuwa za mara moja au endelevu. Mfano unaweza kutoa million moja kwa kuweka agano la Mungu kuwa akufanyie njia madeni yako yaishe, ni one time deal utashangaa wadeni wanakupa options labda nikufanyie kitu hiki nakusamehe. Aidha upande wa endelevu ni kama unajiunganisha na madhabahu za huduma, unaingia agano la Kingdom Finaceler! Kuwa kila mwezi nata milioni moja kwa huduma hii na Mungu hii aniwezeshe nisishuke milioni 15 (15 M) katika mauzo yangu. Hakika htoshuka kiwango hicho hata inyeshe mvua au jua. Secured by heavens. Mpaka siku ukivunja agano ndio mbingu hazitatimiza. Watu wengi ndio wanaponea hapa kwa kusponsor huduma. Mpendwa ukipewa list ya sponsors (wadhamini) wa huduma nyingi utachoka, huwa wanajua siri hii na wanaitumia kikamilifu, Mpendwa una mtolea Mungu ili akufanikishie wew mambo yako kwa makubaliano maalumu.

Mpendwa kama nilivyosema hapo mwanzo katika sadaka hii ni wewe unaweka agano na Mungu na inaweza kuwa maagano mengi kwa Mfano kama Mimi Mchungaji wenu nina agano na Mungu la kifanya huduma hii, ya kwamba sitalazimika kukopa wala kuomba kuendesha huduma na niliachilia sadaka, Mpendwa unaweza kusema sasa huduma ya Mungu mwenyewe sasa sadaka ya nini?, Mpendwa haiku hivyo! Mimi namshukuru Mungu sijawahi kumtafuta mtu yeyote aniboost.God takes care everytime. Mpendwa Pia kwa upande wako unaweza ingia agano la kuwa kila mwezi biashara isiingie kwenye madeni. As long as unatoa mlichokubaliana hakika katika biashara yako  madenii hayatakuwa fungu lako. Mimi nina agano na Mungu Biasshara zangu ziwe zinakua kila mwaka yaani Growth Convenant! Sitabaki sehemu moja, na kila mwaka I’m scalling Mind you natoa pesa na sio muda January to December!, reasonable amount kwenye scale yangu ni above 10 million kila mwaka! RESULTS ARE NOT CHEAP.

Samweli 1: 1

Ni habari ya Hanna anafanya agano na Mungu. Akimpa mtoto atampa Mungu huyo amtumikie madhabauni.

Mpendwa wengi mnafeli hapa kwa kuweka nadhiri, Nature ya agano la Hanna ililazimu nadhiri sio agano lako la biashara.Mpendwa Hanna asingeweza kutoa mtoto bila kumpata kwanza, lakini wewe mpendwa tayari unayo biashara una mtaji lakini utaka kutoa maeneno matupu, hapo hamna agano dada, kuna story tu. Ndiyo maana katiak aina  ya maombi yasiyojibiwa niya nadhiri, Mpendwa tulia utafakari hakika hakuna agano bila sadaka katika hadithi hiyo uko peke yako japo hadithi hiyo umepiga na mbingu, wanakusikiiza kasha wanaendelea kusifu na kuabudu maana haupo serious.

  1. Sadaka Nyinginezo

Mpendwa sio lazima kila sadaka unayoiachia basi ina sababu au lazima ikufanyie kitu, Hapana! Sadaka nyingine unatoa basi tu na nyingine unaachilia kwa sababu nyingine zisizo za kibiashara.

Mfano mpendwa kuna sadaka za shukrani, kuna muda unaweza kumshukuru Mungu ukatoa nje ya ratiba, Sadaka za ibada unatoa tu, siyo kwamba sababu unatoa hizo 5 za nyuma basi hizi za ibada hutoi. Sadaka ya kujenga ufalme wa Mungu una support watumishi na huduma kwa niaba ya amabao hawajajaliwa na nafasi hiyo.Tofauti na agano hili huna makubalianao na Mungu. Akikupa sawa na asipokua ni sawa tu ni kiu yako tu kuona huduma inasonga mbele tu.

Mpendwa sadaka za aina hii niza kusupport injili iende mbele tu, wewe kunufaika ni part of the equation, Na  mra nyingi zinakuwa za kawaida sio za kuuma, Sasa wengi mnatoa hizi alafu mnataka matokeo ya zile 5 za nyuma, Mpendwa haiku hivyo na haiwezekani.

KAMA UNATAKA KU-UNLOCK UCHUMI WAKO TOA HIZO 5 ZA KWANZA KIKAMILIFU NA HIYO YA SITE (6) IWE KAMA BONUS TU!.

  1. Biashara inataka ratiba na consistency ya Maombi.

Mpendwa fahamu kuwa maombi ya kukurupuka ayawezi kukupa matokeo unayoyataka, Kwa sababu siku au kipindi mambo yatakapo kuwia magumu utasali mara tano au zaidi, lakini siku mambo yakiwa mazuri utasali mara moja (1) au hutosali kabisa maana lilija zitakuwa nyingi.

Mpendwa tengeneza ratiba yako ya maombi yako tena ikiwezekana ufanye ndani ya biashara yako, Kuuleta uwepo uwepo wa Mungu, Mpendwa sasa usiwe mnafiki kuweka ratiba usiyoweza kuifata.Wengi huanza nan a maombi ya kukabidhi siku na kusimamia mstari mmoja kasha kufunga na baadaye shukrani. Wengine wakifungua basi imetoka mpaka kesho kabla hawajafungua wanashukuru kwa ajili ya jana na kufungua siku hiyo kwa neon la Mungu. Wengine wanafungua Wiki na Maombi na Kufunga tarehe 31 kwa maombi. Mpendwa kikubwa weka ratiba utakayoweza kuisimamia na kuitimiza, na uhakikishe inatimia.

Mpendwa vitu hivi siyo rahiai nawaambia from experience hasa mambo yakiwa mazuri.Ratiba inasema tarehe moja ukaendeshe maombi dukani Oda zinakuwa back to back, utasikia tarehe 8 tyari imefika, au unafungua oda ya mteja unakuta siku imeisha.

Mpendwa ratiba inaweza kukubana hivyo inakuhitaji uwe consistent! Kama upo level za juu ratiba za siku ndizo nzuri kabisa. Lakini kama neema imekolea una biashara nyingi sana hata once per week pia siyo mbaya ili upitie zote.Ikishindikana kabisa mpendwa fanya hata once per month! Kitu cha msingi ni kuwe na siku za maombi zinazofahamika na kuheshimiwa kama ulivyo muda mwingine wa ibada, Na ifanyike hata iweje, No execuses.

Ibada maana yake ni kumuita Mungu kwenye biashara yako, Mnaweza kumuita mtumishi au hata wenyewe tu mkamaliza kila kitu, Biblia si mnayo! Key point ni kumshukuru Mungu na kuendelea kunmsihi awabariki kweny biashara yenu.

Je ni lazima uwepo kwenye hiyo ibada/ maombi? Mpendwa ni vizuri kuwepo lakini siyo lazima uwepo , ila ni lazima ifanyike katika muda na mahali pale kama mlivyo panga, na siku kama unadharura wewe kama Boss ibada lazima iendelee. Mpendwa tekeleza hili utakuja kunishukuru, utaanza hadi kuuona uwepo wa Mungu kwenye biashara yako.Nakwambia usipokuwa mvivu na kuhakikisha watumishi wako wanakamilisha ratiba mtaona favor inaanza kuwafata na mnaanza kuinuliwa.

Mpendwa mwanzo unaweza usione mabadiliko lakini zingatia maombi kwenye ratiba ile-ile, Hivi karibuni utashangaa mna ziada katika biashara hiyo hiyo iliyokuwa imejaa madeni.

Hata kazini ratiba yako wewe ya ku-commit career yako kwa Mungu ifanye even once per week au Month. Ambapo unafanya maombi ya kazi tu, unamshukuru Mungu  kwa kuwa hapo, unamwambia Mungu matamanio yako na kuachilia sadaka. Utaona vitu unavyo commit kwa Mungu vinaanza kusogea.

Mpendwa kusali bila ratiba ni hatari sana maana shetani anakuwa anakuinulia vitu vingi kukuchanganya na kukutoa kwenye mood, sasa hapo unajikuta umeanguka kwenye miiba na mambo ya dunia yanakusonga songa lakini ukiwa na ratiba ukawashirikisha watu wengi kama Pastor na Wafanyakazi wako itakubana na  kukulazimu kuitekeleza hiyo ratiba, mpaka itakuwa sehemu ya biashara yako.

Mpendwa na mkifata ratiba Mungu anakuwa sehemu ya biashara hiyo, na Roho Matakatifu anakuwa sehemu yenu na anawapa mawazo ,plans,insider informations kwa sababu mmejiunganisha na Mbingu kwenye biashara zenu kwa ratiba maalumu.Ibada yenu niya uhakika, kwamba kuwa kipindi Fulani mnafanya ibada na mmefanikiwa ku maintain hilo kwa muda mrefu, hata wanaotumia nguvu za giza wataanza kuwaepuka, maana watagundua kuna uwepo wa Mungu katika eneo hilo kasha wataacha kukuchezea kabisa.

Hata ofisini utaona watu wanakukata jicho la wasiwasi, na kiti chako cha ofisini hawatathubutu kukikalia, sasahivi ukiinuka tu wamejibwaga.

Mpendwa kikubwa ujitie mapana kuweka ratiba kali kuwa Nafungua na kufunga maombi, Ni kweli inatakiwa kuwa hivyo lakini utaweza?

Usiwe mnafiki kwa Mungu anza mara mbili (2) kwa mwezi, ukikua kiimani utaanza mara moja kwa wiki, kisha mara mbili (2) kwa wiki, kisha mara moja mpaka mbili kwa siku.Ukifanikiwa katika hili utanipa matokeo mpendwa.

Wakristo wengi wana biashara lakini kufanya ibada kwenye Biashara hizo ni labda biashara iwe ngumu sana.Atafanya hapo na ikifunguka kidogo ndiyo unakuwamwisho wa ibada.sasa kupata consistency ya matokeo hayo ni ngumu , matokeo yatakuwa ya kukata kata kama ibada ilivyo navyo ya kukata kata.

  1. Imani ya Vitendo Kuback-up Maombi

Mpendwa unaweza kuwa mtu wa maombi saa, laikini kimazoea tu hivyo katika hali hii unahitaji vitendo ili kuback-up imani yako japo kidogo.Mpendwa kama nilivyokueleza hap mwanzo utajiri wote tayari upo dukani hakuna hata senti moja itakayotoka mbinguni kuja kwako. Sasa kama huna vitendo hiyo ni changamoto.

Baada ya maombi mazito unafanya nini baada ya hapo, Wengi hupenda kwenda kuombewa na kweli mnapewa unabii mkubwa na decree nzito, Then baada ya hapo unakaa ukisubiri?, Unasubiri nini wakati tyai umeshaambiwa hakuna hata senti itakayotoka mbinguni?

Mpendwa baada ya upako ina maana umepewa nguvu ya kufanya yale uliyoshindwa kuyafanya., Mpendwa amini katika huo upako! Test mitambo! Kama ulikuwa huuzi, baada ya hapo nunua mzigo na uuweke dukani, Mwambie Mungu kuwa kama wanafunzi nitatupa nyavu kwa sababu Mtumishi kasema.

Sasa unafanya maombi mazito unategemea yafufue jitihada ulizozifanya bila maombi na zikafeli.Umeomba kazi imeshindikana sababu uliapply bila kumshirikisha Mungu umeona hutwi umeanza kuhahah na maombi.Ni vema umejua kosa lako sasa jirekebishe. Anza maombi kwanza kisha omba kazi, hakika utauona ukuu wa Mungu.

Na kama uko kazini umefanya matoleo ya kwanza anza kuomba kazi kubwa zaidi ya hiyo unayoifanya. Just apply kila siku kwenye big positions and in big companies.Sasa bila kuaplly hizo kampuni haziwezi kuota kuwa wewe una ndoto ya kufanya kazi hapo.Maombi yawe backed up na vitendo kukamilisha maombi hayo.

Mpendwa biashara inataka sana imani ya vitendo, Roho mtakatifu anaweza kukusemesha kabisa fanya kitu Fulani kwa wakati huo kikaonekana hakina maana. Kutokana na ubabaifu wako ukapuuza.Baadaye kikawa deal na hukufanya, umekosa. Mfano Roho Mtakatifu anaweza kukwambia pika kilo nane (8 kg) wakati unapika kilo mbili (2kg) kila siku, unaweza ukapuuza na kikatokea kitu cha ajabu , watu wamejaa na chakula hauna.

Mimi Roho mtakatifu ananisemesha kila siku kwa habari ya bidhaa mpya, amabazo kuna wakati ananiambia naona hii kweli jamani mbona ni majaribu. Nika waambia partners wangu wakabeza na kununa na wananipiga mikwara kuwa ikishindikana shares zako ndio zitarecover hio hasara. Natii hivyo hivyo na not once ameni disappoint lakini sasahivi wanaamini natumia prophecy kuchungulia trends., sababu ya records safi ya kupropose kitu kabla ya wote na kikakubali.

Mpendwa kumsikia Roho mtakatifu ni jambo moja na kutii where you put your money or faith ni jambo jingine.

Winning in business unamuhitaji Roho mtakatifu sana na cha kushangaza waombaji ndiyo wanamsikia sana na ndio ambao hawatekelezi maelekezo yake. Roho mtakatifu anasema wekeza kiasi cha milioni kumi (10M), Wakati umetoka kwenye upako that figure inakaa kichwani, Lakini shetani anakuja anakwambia umesahau eeh? Wewe si una dead stock ya milioni kumi na saba (17 M) alafu unaenda kuweka tena milioni kumi (10M) haya! Mimi nipo. Kwa namana Fulani unaona anapoint ya msingi na kitnedo cha kumsikiliza tu UMELIWA.

Mpendwa changamoto tuliyo nayo makanisa mengi imani ya watu wetu wengi ni ya ngazi ya kuomba tu sio kuzidi hapo.Mtu anaomba alafu basi.Bila action yoyote wala kutekeleza walichokiomba nan i mtihani kupata matokeo katika hali hiyo na jambo la kushangaza ni kuwa wale watu wasio OMBA katika utendaji hawana mpinzani na wanapata matokeo makubwa sana, kuna mtu nikiagiza mimi ni lazima aagize mara mbili , anaamini tu kwa kuwa bidhaa ile mimi nimeikubali  yeye pia  akiagiza atauza na hakika anauza vya kutosha.

Wapendwa wengi mnaomba Prosperity alafu kazi ahamuombi,kisa uliomba huko nyuma.Umeomba Prosperity! Matokeo yake upako unabaki hewani, kuweni serious. Pindi unapomaliza Maombi anza kuomba kazi kubwa kubwa, Mungu wako sio wa kinyonge.

Unaomba na kukesha alafu duakni huweki mzigo! Sasa hayo mauzo makubwa utayapata wapi? Utauza hewa? Una kampuni una maliza program alafu unashindwa kumanage staff waweze kutafuta odda. Sawa kabla ya maombi odda zilikuwa tabu kweli lakini ndiyo maana umeomba? Watume tana washushe nyavu. Mpendwa Grace inakupa uwezo wa kufanya ulichoshindwa kufanya kabla ya Moambi ku-unlock hio Grace, kufanya kuko palepale isipokuwa kipindi hiki unafanya under Grace.Sasa usipofanya huto-unlock chcochcote. Mambo yatatulia yakingoja wewe ufanye kwanza ndipo yalipuke.

Mpendwa ibada haiku exempt from taking actions kama marketing strategies, day to day tasks za kukuza biashara yako. Ibada inaweka upako hizi actions zinakuwa na impact kubwa sana. TAKE BLD ACTIONS Back up hizo prayer na Bold actions. Mpendwa mimi watumishi wangu wanajua kabisa  baada ya kufanya ibada kubwa cha moto kinakuja, hakuna mabacho sitafanya, wanajiandaa mapema ni actions back to back.

Mpendwa always trust God with the next move! TRUST GOD! Amini maneno ya pastr kwamba sasa upo huru na umefunguliwa. Sema sasa sabab nipo huru kwa siku nafanya applicastions 20! Kwa siku natembelea wateja 20! BE BOLD IN ACTIONS!.

Yakobo 2: 26

Maana kama vile mwili pasipo roho umekufa,vivyo hivypo imani pasipo matendo imekufa.

  1. The Plan

Mpendwa na katika maombi you need a plan. Mungu anajua fika ni kwa namna gani utafika ngazi ya kuwa mkurugenzi au supplier mkubwa lakini wewe hujui,na kama hujui mpendwa miaka itasonga na hutofika popote kwa ni hata maandiko tu yapo kinyume na wewe. Hivyo mpendwa wale wa I am a child of God destined for greatness! My dear! Unless ni huduma au evangelism, Biblia inaweka wazi kabisa.

Proverbs 16:3

Commit your work to the Lord, and your plans will be established.

Proverbs 16:9

The heart o f man plans his way, but the Lord establishes his steps.

Luka 14:28

Kwa maana , ni nani  miongoni mwenu amabaye akitaka kujenga mnara hata keti kwanza akadirie gharama zake ili ajue kama ana kiasi cha kutosha cha kumalizia?

Mpendwa sasa wewe unafanya mabo yako kiholela-holeayasipo enda unaanza kuona Mungu hakupendi.Mungu hakupendi kivipi wakati umekurupuka?, Pia kwa sababu huendi popote ni huna plan au mpango wa kazi wa kwenda popote na hiyo biashara mnacheza na shetani.

Mpendwa always have a plan juu ya biashara yako.Iko wapi na unataka iende wapi na jinsi gani?.Mfano unauza online na unahitaji duka,litacost milioni 15 (15M) hivyo nitasevu kwa mwaka na miezi mitatu 3 , hapa Mungu atakufungulia mlango lakini ukienda na ule mtazamo wa baba nataka duka sijui nitapata vipi duka hili ilawewe ni Mungu kama wewe ni form 4 au chini Mungu anaweza kukurehemu kwani Mtu anajaliwa kwa kie anachifahamu, sasa unakuta graduate mzima tena wa Commerce anaomba hivyo, ni matumizi mabaya ya mkopo wa serikali, kwa sababu unajua vyema juu ya business plan na Mungu anajua uliandika moja chuoni , ni uvivu tu!.

MPendwa ukiwa na paln akini sio intensive ila detailed ukaikabidhi mbele za Mungu hutokosa majibu kwani ata endorse hiyo plan, na hata ukikosa hiyo million 15 ndani ya mwaka mmoja . Unaweza kuwa na plan zaidi ya moja.

Mpendw ahata ofsini you should have aplan to be the Director of Somehting. Sio Officer ujana wako wote. Unatakiwa uongoze hata wakati wa ujana wako. Establish a valuable plan and commit it to the Lord. I want to be the Manager by 30. Senior Manager by 35, Director by 40. Anza kudadavua talk is cheap weka uzani kwenye huo mpango wako, may be kuna  accolades zitatakiwa. Get them! Like CPA, CSP, ACCA, CISA! Get Certificates.

Mpendwa Mungu ni Mungu wa haki. Sio rahisi amuache mwenye vyeti akupromote wewe. That is day dreaming. Uvivu hutaki kujiendeleza na unataka muujiza. Yesu mwana wa Mungu hakuwa mvivu hata kidogo sasa wewe Mungu ata uendorse uvivu wako kivipi? Acha execuses tafuta vyeti.

Mpendwa ukiwa na vyeti vyote muhimu bila hata kuomba sana Mungu atakufanyia nafasi iliyo njema.Pastor sina vyeti ila kuna nafasi niombee kwa Mungu anitendee muujiza, Mpendwa kama ni Pastr njaa atakwambia let apes haraka , nafasi hii ni yako na ukisita atakwambia nimepata maonao kuwa nafasi hii ni yako, utapeleka sadaka italiwa na nafasi itatangazwa ikikosa mtu itatangazwa tena na ikishindikana wataenda recruitment agency!. Wapendwa Mungu ni Mungu wa haki hakikisha kuwa haki iko upande wako, sawa kuna Favor na Divine Grace lakini je are you that deep kwenye ibada? Una uhusiano huo na Mungu?

Hivyo mpendwa always have aplan usikae kizembe! Moja ya sababu kubwa maombi ya graduates wengi hawajibiwi ni void of plans.Mombi matupu.Mungu akupeleke chuo bado akutengenezee plan. Hata kama kazi huna, commit plan  yako ya kutafuta kazi na Mungu atakutengenezea njia kama nitaomba kazi huku na huku, nitaenda recruitment companies sio una nextflix and chill alafu usiku machozi Mungu nikumbuke katika kazi.

Hata kama biashara unayoipenda umechoka kuwa mahari hapo hapo, kaa chini waza labda nitafute sehemu nzuri, kodi million 24 (24M)nipate mkopo wa Millioni 30  (30M), huku na huku million 70 (70M) ikipatikana baba mimi vingine namaliza mwenyewe, Mungu nitapambana kufa na kupona kwenye duka hilo.Nifanikishie hapo tu, Figure yako ni million 70 (70M) na unakuwa nayo hata ukikurupushwa usingizini.

Mpendwa siku ya ijumaa Pastor anaweka mikono, ifikapo usiku unaanza katika maombi yako kuwa Baba nakuja kwako 70M baba heshima na utajiri wote ni wako, 70 M ni zako. Ukienda kuwekewa mikono may be na Bella au ni Pastor wako, moyoni unasema uako ulio ndani ya huyu pastor, Mungu uketiye mahali pa juu naanguka miguuni mwako juu ya ile Plan na hususani ile million 70 (70M), Wakati pastor wa watu anasema ni receive! Hajui sumaku yangu ina nasa 70 M ahkika mpendwa utaipata hiyo 70M kuliko ulivyotegemea kuwa serious.

Mpendwa changamoto kubwa uki commit plan yako kwa Mungu akaifanikishe lazima uikamilishe kama ilivyo laasivyo itakughalimu. Mpendwa mimi Back in the days katika maisha haya, nilicommit plan ya kupata gari. Kuna mchepuko wangu katika enzi za usichana wangu alikuwa na Allion! Enzi hizo nimetoka chuo damu bado ya moto kijana Yule wa hovyo akaniambi aknunua gari like million 16 ( 16M), Gari lilikuwa zuri sana, nakumbuka siku ya siku kwenye tembea tembea zetu akanishusha Kinondoni na wakati huo mtaani mzuri ni mimi tu.Marafiki na majirani wote Bwana wako ana gari? Kuna muda ananiazima binti mdogo gari.Mpendwa huko mbeleni siku ya siku nikaja kujua kuwa lile gari nila mdada wa 40s huko jimama lake ndo lina muazima muazima na kumlaghai alioe, wapendwa hii story tutaimalizia siku nyingine.

Kikubwa nilijiapiza kuwa lazima ni nunue Allion, mpaka nikarudi madhabauni,Na kusearch kiundani spiritual economics. Nikalazimika kuanza Biashara yote hiyo ili Mungu anibariki ninunue Allion,  Wapendwa Mungu ni Muaminifu sana tu ikafika 16 M  Cash. Nikamwambia mtoto wa mjini mmoja sitaki ya hapa nataka from japan. Wakati huo nina mashoga zangu wa Magomeni, watto wa uswazi wenye vyumba vyetu vya urithi tuna 16 M benki utatuambia nini? nikasahau Mungu kabisa.

Mpendwa sikumbuki vizuri ikawaje niliropoka kwa mtoto mmoja wa mjini alikuwa ana connection za nje, akaniambia wewe unanunua gari la nini sasa? Mtoto mdogo gari lote hilo?, akasema hiyo hela hata kesho tunaondoka nchini humu, Twende tukatafute maisha, hapa Bongo hakuna maisha, Twende china tukatafute mizigo hela nyingi hiyo.Tukirudi tuna nunua prado.huyu alinivuruga kabisa, Tuliondoka na habari ya gari iliishia hapo.

Fast Forward biashara ilikua lakini mimi ndoto ya kumiliki gari ilikufa ni mpaka nilipoenda kulia kanisani.Kila nikipanga mpango wa gari hauendi popote.Mpaka leo hii nafundisha mada hii ndiyo nimekumbushwa na Roho Mtakatifu kwamba nilicommit plans za Gari alafu sikufanya kitu. Baada ya Maombi sana Mpendwa nilipewa rehema nikaweza kumiliki Gari. Mpendwa Moral ya hadithi hiyo ni kwamba ukipata 70M za kuadvance biashara usianze kuona mbona viwanja vya madale au sehemu za starhee nzuri, au GOba mbona kuna upepo mzuri sana siku hizi!! FOLLOW THE PLAN THROUGH! CHA MOTO MWENZIO NILIKIONA! PESA NINAZO HADI NAKOPESHA LAKINI KUMILIKI GARI NI MTIHANI!

Wapendwa nimeona mtu anaomba pesa ya kukuza biashara anapewa na Mungu anajizima data bbaada ya hapo! Aniulize mimi niliyechukua pesa ya gari! Utaomba na kuomba ,utalia na kulia juu ya kukua kwa biashara yako lakini hadi upate rehema umri umeenda.Hivyo mpendwa ukiwa serious Mungu atakuinua viwango na viwango na utukufu mpaka utukufu.Wapendwa sasahivi sirudii tena makosa yangu ya nyuma, Niki commit plan zangu na hakikisha sina ubabaifu, kama nilisema nitaongeza products hata uniambie kuna deal la chapu nasema shetani pita huko naijua hiyo! Na Mungu ananikuza.

Mpendwa niamini mimi unapewa 15 M leo imetimia kesho unaambiwa mpemba anauza IST milioni 5.5 anataka kurudi zake Chake Chake. Unaanza kwa kweli biashara inahitaji gari!, Mpendwa usifanye hivyo kwani sio plan ulizopeleka kwa Mungu na usipo aminika kwa Mungu katika viwango vidogo hauto aminika katika viwango vikubwa.

Mpendwa kama unataka Mungu akupe biashara kubwa Onesha Ukomavu, Onesha uaminifu na utayari wa kumiliki biashara kubwa.Be all about that level of success! Kama ni position onesha maturity ya kuweza kukaa kwenye nafasi hiyo hakika atakuketisha. Mpendwa Mungu ahwezi kumuweka mtu mzembe, asiye jail, mvivu na aliyechini ya kiwango kwenye nafasi asiyostahili.Utaendelea kusubirishwa Mwaka hadi Mwaka, sawa unaomba sana ila hauko tayari bado.Hata biashara kubwa hawezi kukupa kwani hautaweza kusimamia utaibiwa kila kitu na kubaki hapo hapo. Mpendwa usisahau Mungu anaweza kugomea plan vile vile kama plan yako niya ovyo haipokei wala haibariki lakini usivunjike Moyo rekebisha mpaka iwe aktika kiwango kinachohitajika na Mbingu.

Hitimisho

Wapendwa huu ndiyo mwisho wa mada yetu! Na Mungu akijalia tena kwa wakati mwingine nitawafundisha HOW UNLOCK CAREER GROWTH AND PROMOTIONS, Yaani nafanya yale yale ya ku-commit plans kwani hapo mwanzo nilijicommit mahusiano huku najicommit mambo ya kazi.

Wapendwa Career ndiyo uwanja wangu wa nyumbani sababu sikuwahi kuwa promoted! Na ninajua kwanini ila nitakwambia kwa mapana kwa nini hupigi hatua upande wa kazi na ukijua utapiga hatua na utakuwa promoted mpaka utaona unakosa muda wa familia. Wapendwa nah ii ni dhahili katika maisha yetu ya kawaida unaweza kuwa na rafiki yako mliye maliza wote chuoni lakini yeye akawa promoted zaidi ya  mara kumi (10) na wewe uko palepale tena ukwa unamuita BOSS kutoka katika jina lake VIVIAN kwa uchungu sana.

 

 

 

2 thoughts on “Business Favour”

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Scroll to Top
× IT Help Desk