Omega

Maombi ya Omega ni maombi ya kuzima moto na maombi ya saa ya hatari, Ni maombi mafupi lakini yanahitaji kujitoa na uzingatiaji wa hali ya juu sana.Mpendwa katika mfungo huu tutakesha siku saba (7).

Mathayo 11 :12

Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatikana kwa nguvu, nao wenye nguvu huuteka.

Ufahamu Moyo uliovunjika na kupondeka.

Zaburi 51: 17

Dhabihu ya Mungu ni roho iliyovunjks; Moyo uliovunjika na kupondeka,Ee Mungu hataudharau.

Mpendwa Moyo uliovunjika na kupondeka ni moyo usio na PLAN B, C- Z! ni moyo unaomtegemea Mungu tu, Mfano halisi ni ule Moyo unaosema nisipo olewa nitajizalia mwanangu tu basi! PLAN B yake ni kama ya namna hii, yaani wakati unakesha ukiomba Mume kwa Mungu kumbe tiyari una PLAN B yako rohoni mwako,Mfano mwingine ni ule wa Nisipoajiriwa nitadanga tu, sasa nitaishije? PLAN B ikiwa ni kudanga, Mpendwa katika nyakti kama hizi PLAN B yako ndiyo inayo yafunga maombi yako yote ya kazi na hakika shetani awezi kukuacha.

Moyo uliovunjika ni ule unaosema Mungu ukniacha nimekwisha mimi.Uhuni siuwezi,Yamkini nimefanya lakini fedheha yake imenila hakika Mungu ni wewe tu wa kuniokoa, sina msaada wowote zaidi yako Mungu kwenye hili, ukiniacha nimedhalilika.

Confess your victory (Kiri ushindi wako dhidi ya changamoto zako)

Kutegemeana na changamoto yako kiri ushindi dhidi ya changamoto zako. Kama ni ugonjwa kiri uponyaji kwa kusema nimeponywa kwa jina la Yesu , Kama ni kazi kiri kuajiliwa kwa kusemasitaingia mwaka 2024 bila kazi katika jina la Yesu na kama ni  ndoa kiri kuolewa kwa kusema nitaolewa na kuwa na familia yangu katika jina la Yesu na sitaingia mwaka 2024 bila mtu sahihi katika jina la Yesu.Mpendwa chochote unachoona kimekushinda na kushindikana kiri ushindi dhidi ya kitu hicho(Mpendwa unaweza kuona ni rahisi lakini ukifnaya kidogo tu utaona nafsi yako inavyokuzomea lakini usikate tamaa songa mbele mpaka nusu saa itimie.

Omba rehema

Lord have mercy on me,forgive me for my sins,Wash me and cleanse me of may sins and any inequities in jesus name

Bwana nirehemu,nisamehe dhambi zangu na unioshe na uovu wangu kwa jina la Yesu.

Let your mercy speak for me,let your favour speak to me in Jesus name.

Rehema zako zinene juu yangu, kibali chako kinene juu yangu kwa jina la Yesu.

Mpendwa maanisha hii sala kwa moyo wako wote, itafakari na kumaanisha kwa nusu saa.

Day 1 : Omega Program

Let there be Light in your Life to Overcome Darkness

Maisha yako hayaendi unavyotegemea sababu giza limezidi mwanga,Giza ni Totoro na giza huwa linapanikisha na kukatisha tamaa.Linaleta depression na jaka la Moyo.Unaona tu matatizo yako na huoni mwanga wowote,una vuka vipi hapo. Mpendwa leo tunaomba Baba yako aiye juu akuangazie katikati ya hilo giza kubwa kwa mwanga wake wa milele ili uone njia ya kutoka hapo.

Mwanzo 1 : 3 – 5

Mungu akasema, “Mwanga uwe”.Mwanga ukawa.Mungu akaona mwanga kuwa ni mwema.Kisha Mungu akatenganisha Mwanga na Giza, Mwanga akauita “Mchana” na giza akaliita “Usiku”.

Yohana 1: 5

Nuru hung’aa gizani nalo giza halikushinda.

Endelea kuomba na kumsihi Mungu kuwe na Nuru katika hilo eneo la maisha yako kama ni mahusiano,kazi,afya etc.

Sala

Bwana Yesu wewe ni nuru ing’aayo gizani, ng’aa katka mahusiano yangu,uchumi wangu na maisha yangu.Neno lako linasema GIZA HALIKUSHINDA KAMWE Bwana Yesu giza lisishinde tena mwaka huu.Kama Mungu aishivyo na wewe Mwana wa Mungu giza la mahusiano yangu lisishinde kamwe. Ng’arisha Nuru yako kwenye mahusiano yangu usiku huu na tokomeza giza lote

Day 2: Omega Program

Mathayo 17: 20

Yesu akawajibu, ” Kwa sababu ya imani yenu haba.\, Nawaambieni kweli, kama tu mkiwa na imani iwe ndogo kama mbegu ya haradali, mtaweza kuuambia mlima huu toka hapa uende pale nao utakwenda.Hakuna chochote amabacho hakingewezekana kwenu.

Mpendwa Yesu anasema HAKUNA CHOCHOTE AMBACHO HAKINGE WEZEKANA KWENU, HATA HIO NDOA,FAMILIA, KAZI NA MARADHI HAKUNA AMBACHO KISINGEWEZEKANA.

Mpendwa muda huu sio wa kurusha lawama, ni muda wakujiandaa na kujitune kuwa ,kweli hata imani  ndogo kama chembe ya haradali ni ya kunishinda kweli?, Hapana! Ninayo imani hiyo na Lazima niwe nayo.

Mathayo 19: 26

Yesu akawatazama akasema ” Kwa binadamu jambo hili haliwezekani, lakini kwa Mungu mambo yote huwezekana.”

Mpendwa peeka sasa hilo suala lako lililoshindikana mbele ya Mungu, usizungumze kwa uchungu sana kwani hii si vita.Zungumza taratibu tu na kwa unyenyekevu na Mungu kwamba neno lake linasema mambo yote yanawezekana.Mpendwa unasimama na anadiko hilo kwa kuamini na dhati kabisa maadam andiko hili limesha andikwa na wewe umefunuliwa kupitia andiko hilo basi usiku huu hilo suala lako linaenda kuwezekana. Mpendwa KWA MUNGU MAMBO YOTE YANAWEZEKANA likiwemo hilo suala lako la mahusiano, kazi au uzao.

Zaburi 121 : 1 – 8

1 Nitaipandia macho yangu milimani, Kutoka wapi msaada wangu utatoka? 2 Msaada wangu utatoka kwa Bwana, Aliyezifanya mbingu na nchi. 3 Hatakupa mguu wako usitikisike, Wewe azaye wewe hatakuhifadhi. 4 Tazama, hamhizi, wala hatalala, Yeye aliyekulinda Israeli. 5 Bwana ndiye alichochea, Mlinzi wako ndiye kivuli chako mkono wako wa kuume. 6 Jua halitakupiga mchana, Wala mwezi wakati wa usiku. 7 Bwana atakulinda na mabaya yote, Atakulinda roho yako. 8 Bwana atakulinda utokako na uingiako, Tangu sasa na hata milele.

Mpendwa msihi Mungu akuletee msaada wake kwenye changamoto yako sawasawa na andiko hio.

Yeremia 29: 11

Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi asema BWANA, ni mawazo ya amani wala si mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za baadaye.

Ee Bwana nimejua mawazo uniwaziayo kuwa ni ya amani wala sio mabaya bali ni ya kunipa tumaini siku zangu zote za baadaye.Nakuhisi Bwana fungua mlango wa rehema wa kibali wa upendo kwenye hili suala la Mahusiano,kazi, uzao na afya kwa jina la Yesu.

Day 3: Omega Program

Restoration.

Isaya 61: 17

Badala ya aibu yenu mtapata maradufu, na badala ya fedheha wataifurahia sehemu yao; basi katika nchi yao watamiliki maradufu; furaha yao itakuwa ya milele.

Yeremiah 17: 14

Uniponye, Ee Mwenyezi Mugu, nami nitapona uniokoe, nami nitaokoka maana wewe ndiwe sifa yangu.

Mpendwa tumia muda wa kutosha kumsihi Mungu akuponye majeraha yako na kukuokoa na changamoto zako.Ee Mwenyezi Mungu niponye na upweke nami nitapona.Niokoe na upweke huu(zama in details) nami nitaokoka.Niponye na majeraha yaliyotokana na mahusiano yasiyo sahihi, niokoe na mikono ya wanaume wasiyo sahihi nami nipate mtu sahihi, tumia muda wa kutosha kumsihi Mungu.

Day 4: Omega Program

Ayubu 42:10

Kisha Bwana akamrejeshea Ayubu mali yake, hapo alipowaombea rafiki zake; Bwana naye akampa mara mbili kuliko hayo aliyokuwa nayo kwanza.

Ayubu aliwaombea marafiki zake kwa Mungu lakini Mungu akambariki mara mbili ya mwanzo.Mpendwa kuna watu wa karibu unapita nao katika changamoto yaani wana changamoto kama ulivyo wewe au hata zaidi lakini kutokana na hali yako mwenyewe unaona yanini kujibebesha changamoto za watu ilihali mambo yako mwenyewe bado meusi (mabaya).

Mpendwa usiku wa leo anza kwa kuwaombea wengine na Mungu awakumbuke pia.Ayubu alipowaombea wengine ndipo alipopokea breakthrough yake,Mpendwa waombee wengine kwa moyo wa dhati  kabisa usiku huu.

Zaburi 71: 20 – 21

Wewe, uliyetuonyesha mateso mengi, mabaya, utatuhuisha tena. Utatupandisha juu tena tokea pande za chini ya nchi.Laiti ungeniongezea ukuu urejee tena na kunifariji moyo.

Psalms 71: 20-21

Though yoh have made see troubles, many and bitter, you will restore my life again; from the depth of the earth you will again bring me up. Yuo will increase my honor and comfort me once more.

Sala

Baba neno lako linasema ijapokuwa nimepitia mabaya, mateso na changamoto nyingi utayarejesha maisha yangu tena, utanipandisha kutoka pande za chini ya nchi.Usiku huu Baba nakusihi kwa moyo mmoja unipandishe tena sawasawa na neno lako.Nirudishie heshima na faraja zako kwa mara nyingine tena kwa Jina la Yesu.

Marko 11: 24

Kwa sababu hiyo nawaambia, Yeyote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba manayapokea, nayo yatakuwa yenu.

Mpendwa mstari huu ni mgumu sana lakni ni mwepesi sana kwani upo moja kwa moja (direct).Mpendwa matumizi ya neno YEYOTE yana maana kubwa amabayo ni kutokuwa na vipingamizi au vizingiti katika maombi lakini pia mstari huu unakuja kumalizia kwa kusema MUYAOMBAYO AMININI KWAMBA MNAYAPOKEA NAYO YATAKUWA YENU.Mpendwa hapa ugumu uko wapi? na wengi wetu hapa tutasema Ugumu upo kweyne kuamini utayapokea! na ni kweli hapa ndipo kazi lilipo.Kwanza Shetani hapa atakuvuruga sana hadi utaanza kukumka mambo yao ya mwaka 1960 ya kia ombi kutojibiwa.Mpendwa kuvuka kwako ni kuongeza imani na kumwamini Mungu hata kama mazingira sio rafiki,hapa ndio brekthrough. ilipo.Hata akikukumbusha vipi wewe unang’ang’ana na Mungu.

Day 5: Omega Program

Anza kutafakari na kuandika sehemu kitu kimoja kikubwa ambacho unataka kumuona Mungu December akikutimizia.Mpendwa chukua muda wako! Najua una list ya Page 7 lakini zingatia kwenye kitu kimoja unachokihitaji sana.Mpendwa nipende kukusihi kwamba ukimuona Mungu kwenye hiyo changamoto yako utapata nguvu upya na kuendelea na safari nyingine kwa nguvu zote.

Mpendwa kuwa specific sana ili linapotokea usianze kubabaika kwa kusema ni bahati tu, kuwa halisi. Mfano unataka Ndoa lakini ndoa ni mchakato kuipata siku hii hii itakuwa ni kuhitsji sana kuzidi kiwango, Mpendwa unapokuwa halisi ni rahisi kwako kupokea Mfano wewe huna mtu au mwenzi unaweza kuandika “Nikutane na Mtu sahihi December Hii” au Kama uko na mtu unaweza kusema “Mwezi huu aweze kuniuliza taratibu za ndoa zinakaaje”, Kama ni Kazi ” Nipigiwe simu nilipofanya Mahojiano  ya Kazi (Interview), Kama ni uchumi unaweza kuandika “Mwezi huu niuze Millioni Kumi (10M) hii ni kutegemeana na mtaji wako sasa sio una mtaji wa millioni mbili (2) unataka uuze Millioni 10.Mpendwa andikeni vitu kwani muda huu sio wakuzubaa wala kumuamsha aliye lala.

Sala ya Mtumishi Ibrahimu

Mwanzo 24:12-14

12 Naye akaomba,”Ee Mwenyezi Mungu,Mungu wa bwana wangu Abrahamu, nakuomba unijalie nifaulu leo na umfadhili Abrahamu Bwana wangu.13 Niko hapa kando ya Kisima ambapo binti za wenyeji wa mji huja kuteka maji.14 Basi, Msichana nitakayemwambia atue mtungi wake wa maji na anipatie ninywe, naye akanipa mimi pamoja na kuwanywesha ngamia wangu, na awe ndiye uliyemchagulia mtumishi wako Isaka.Jambo hilo litanionesha kwamba umemfadhili Bwana wangu.

It is a heartfelt Prayer! Inatakiwa kuomba kwa dhati ya kutosha na kweli,Mpendwa sasa omba sala hiyo kama ilivyo kisha uifanyie maboresho kuendana na uhitaji wako. I reflect ulichokiandika unatazamia breakthrough kutoka kwa Mungu.

Mfano wa sala katika suala la Ndoa.

Ee Mwenyezi Mungu, Mungu wa wazai wangu, nakuomba unijalie nifaulu leo na uwafadhili wazazi wangu.13 Niko hapa kitandani nakesha peke yangu kwa habari ya ndoa yangu tangu mwaka unanza hadi sasa unapoelekea kuisha.Basi kati ya changamoto zangu lukuki naomba unikumbuke kwenye jambo langu moja (Litaje) for imeediate breakthrough, Mfano Nikutane na Mtu sahihi kabla ya December kuisha. Jambo kama hili linaonesha kwamba umenifadhili mtumishi wako sawa sawa na neno lako Mwanzo 24: 12 – 24 ulipomfadhili mtumishi wako Abrahamu na mwanae Isaka kupitia mtumishi wao. Naomba haya yote katika jina la Yesu.

Day 6: Omega Program

Speed

Genesis 24:12

12 And he said, Ooh Lord God of my master Abraham, I pray thee, send me good speed this day and show kindness onto my master Abraham.

Mpendwa hii ni kutoka katika marejeo ya Biblia ya KJV! Ukisoma tafsiri za kiswahili neno speed limetolewa hivyo usistuke.

Sala

Ooh Lord! I decree and declare divine speed kwenye mahusiano yangu, kazi au chochote kile unachoombea. Divine Speed inasaidia kuvuka vikwazo vyote vya shetani na washirika wake kwa jina la Yesu, Chochote cha kwangu kilichocheleweshwa kinaenda kunifikia kwa devine speed kwa jina la Yesu.

Kuanzia sasa naenda kukamata speed kwa habari ya ndoa yangu, habari ya kazi yangu na uchumi wangu kwa jina la Yesu, Chochote kilichokuwa kinasua-sua na kunishinda sasa naenda kukabiliana nacho kwa moto wa devine speed! chochote kilichelewa maishani mwangu kitakuja kwa kasi Sitashuka tena bali nitapanda kwa speed, maisha yangu yatapanda mbele kwa jina la Yesu. Hakika huu ni mwaka wangu, mwezi wangu na wakati wangu kuyapokea majibu yangu kwa jina la Yesu.

Warumi 9: 16

Basi kama ni hivyo, si katika uwezo  wa yule atakaye, wala yue apigye mbio; bali wa yule arehemuye yaani Mungu.

Prayer

Ooh Lord I am trying but it is not enough, Lrt your mercy bring me speed,I am tired of catching  up! Lord give me speed of a reader and a pacesetter!,This Month, This Day grant me speed for excellence.

Esta 8: 8 – 10

“8. Basi andika amri nyingine kwa jina la mfalme kwa ajili ya wayahudi kama unavyoona vyema, kisha uifunge kwa kutia muhuri wa pete ya mfalme kwa kuwa hakuna andiko lililo andikwa kwa jina la mfalme na kutiwa muhuri wa pete ya mfalme linaloweza kutanguliwa.

9. Basi, waandishi wa mfalme wakaitwa palepale, siku ya kumi na tatu ya mwezi wa tau,ndiyo mwezi wa siwani; na kama vile Mordekai alivyo-amuru, Wyahudi wakaandikwa pamoja na wakuu wa Tarafa na wakuu wa mikoa ya Bara Hindi mpaka Kushi, Mikoa mia moja ishirini na saba, kila mkoa kwa mwandiko wake, na kila taifa kwa kwa lugha yake na wayahudi kwa mwandiko wao na lugha yao.

10.Mordekai alikuwa ameandika nyaraka hizo kwa jina la mfalme Ahasuero, akazipiga muhuri wa pete ya mfalme na waliozipeleka walikuwa ni matarishi waliopanda farasi wenye nguvu na waendao kasi

Prayer

Oh Lord  of Heaven upgrade me with speed! I decree that every devine help that divine speed brings me after now will be IRREVERSIBLE and IRECOVERABLE.The new level of joy that you promised me from the beggining of this year, seal it with the stamp of Heaven, That position of Authority with God and Man that Empowers a man to choose what he decrees-take me there speedly!. Lord before the end of this month, send your ministering angles to deliver my package of joy speedily.

Neno la Mtumishi:

Kwa waletuliokuwa pamoja nawapongeza sana.

Mathayo 11: 12

Tangu siku za Yohana mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatikana kwa nguvu, nao wenye nguvu wanauteka.

Siku ya leo tunamaliza mkesha mmjoa mkubwa sana na nitawaombea waliokesha tu, na kama hukukesha na uko serious unaweza kukesha kwa kufuatisha mlolongo wa ratiba kama ulivyo polepole. Na nipende kuwataarifu wale wanaokesha nusu saa au muda kidogo tu katika mkesha huu utakosa suluhu yako kwani siri kubwa ya mkesha huu ni utii wa kiongozi wako, Mfano mkubwa naweza utoa katika biblia ” Naaman Mshamu aliambiwa na Nabii Elisha akajitose mto Yordani mara saba (7) na alipofanya tu ukoma ukaisha, laiti kama Naaman angejitosa mara sita au katika mto tofauti na Yordani hakika nakwambia asingepona kabisa.Hivyo nipende kukusihi mpendwa acha kufanya unachotaka, jishushe tii na kufata na unachoelekezwa na kiongozi wako hakika utapata suluhu ya changamoto yako.

Day 7 : Omega Program

Breakthrough

Kutoka 33:13

“Sasa basi nakusihi, kama kweli nimepata fadhili mbele yako,nioneshe sasa njia zako, ili nipate kukujua na kupata fadhili mbele zako.Naomba ukumbuke pia kwamba taifa hili ni watu wako”

Baba usiku huu nakopesha nioneshe nja zako sasa juu ya mahusiano yangu, kazi yangu, afya yangu na uchumi wangu nioneshe Bwana, Naomba kwa jina la Yesu.

Maombolez0 3: 37

Nani awezaye kuamuru kitu kifanyke Mwenyezi Mungu asipopanga iwe hivyo?.

Ni mpango wa Mungu ufanye mkesha huu ili akuvushe kwenye hiyo changamoto yako, Mpendwa wakati wako umefika sasa! inua imani yako na ukashuhudie ukuu wa Mungu wako usiku huu.

1 Samweli 3: 21

Naye BWANA akaonekana tena huko Shilo, kwa BWANA akajifunua kwa Samweli huko SHilo, kwa neno la BWANA, Nalo neno la Samweli likawajia waisraeli wote.

Sala

Bwana ukajifunue kwangu usiku huu wa mkesha unipatie encounter of a lifetime nione kweli Bwana Mungu wa Israeli amejifunua kwangu juu  ya changamoto yangu niliyokesha nayo siku 7.

Isaya 55: 8- 9

Mwenyezi Mungu asema hivi “8. Maana mawazo yangu si mawazo yenu, wala njia zenu si njia zangu, asema Bwana. 9. Maana kama vile mbingu zilivyo juu sana kuliko nchi, kadhalika njia zangu zi juu sana kuliko njia zenu, na mawazo yangu kuliko mawazo yenu.”

Isaya 55: 11

“Kama vile neno linalotoka kinywani mwa Bwana, haliendi huko bila kutimiza kusudi lake, wala halirudi huko bila kufanya yale aliyokusudia.”

Sala

Baba nakuja mbele zako kwa habari ya mahusiano yangu, kazi yangu, afya yangu, uchumi wangu n.k, nakiri kuwa mawazo yangu sio mawazo yako na njia zangu za kutatua changamoto zangu sio kama njia zako.Usiku wa leo na surrender suala hili la mahusiano,kazi, uchumu, afay n.k na kuruhusu mapenzi yako yatimizwe kwangu juu ya jambo hili. Usiku huu Baba achilia neno lako kwa habari ya mahusiano yangu,kazi,afya, uchumi n.k amabalo halitakurudia bila kuyatimiza mapenzi yako kwenye kile ulicholiagiza neno hilo, nslo lifanikiwe kwenye jambo ulilo lituma.Baba neno lako likanifungue katika eneo la (Taja jina la eneo unalotaka kufunguliwa)  na kunifanyia breakthrough kabla december haijafika katika jina la Yesu. Lord release your breakthrough kwenye mahusiano, kazi, uchumi na nk usiku huu kwa jina la Yesu.

Yakobo 1: 6-7,8

Lakini anapaswa kuomba kwa imani bila masha yoyote.Mtu aliye na mashaka ni kama mawimbi ya bahari amabavyo husukumwa na kutupwatupwa na upepo.Kwa hiyo mtu aliye na mashaka, mwenye nia mbili na asiye na msimamo katika mwenendo wake wote, asidhani kuwa atapata chochote kile kutoka kwa Bwana.

 

 

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Scroll to Top