Exodus

Day 1: Grace of God/ Neema ya Mungu

Yohana 15:8

8 Mnapozaa matunda kwa wingi Baba yangu anatukuzwa, na hivyo mnadhihirisha kuwa ninyi ni wanafunzi wangu.

Mpendwa Yesu anataka tufanikiwe kuliko sisi tunavyotaka kufanikiwa.Unaweza usione hivyo ila iko hivyo na ameweka katika maandiko kabisa.Yesu anataka uolewe kuliko wewe unavyotka uolewa, Ili wasio okoka waitamani ndoa yako na wamatamani Mungu aliyekupa ndoa.Yesu anataka uwe Boss wa Ofisi, ufike katika viwango vya juu ili uweze kuakisi ukuu wa Yesu na Mbingu.Watu wakiona matunda uliyozaa wasema kama ndio hivi wanibatize na mimi, sihitaji kufikiria.Nafikiria nini sasa?.

Yohana 10: 10

Mwizi huja tu kuiba, kuuwa na kuharibu; mimi nilikuja ili wawe na uzima, tena wawe nao tele.

Yesu anataka tuwe na uzima tee.Sasa kukiwa na na mambo yanakusumbua uzima hauwezi kuwepo, Muda wote unamashaka nitaolewa kweli?, Nitapata kazi kweli?, Huu sio uzima tele hata Rafiki yetu Yesu hafurahii hali yako hata kidogo.

Sasa kama ni hivyo mbona bado ambo magumu na hayaendi?.Maandiko yanaenda hivi na Mambo yanaenda kule.Tupo tu kwenye imani hii kwa vile tunaogopa kuwa mambo hayaendi, Na Muda mwingine mpaka unajiuliza hivi kweli walioandika maandiko haya waikuwa serious kweli? au yamkini yana watu na watu. Mpendwa tatizo ni kuwa hujifunzi neno la Mungu kwa undani, unaegesha egesha vitu juu juu na kujaribu kupenya kwa uchache.Hivyo shetani akikutikisha kwa uchache ulioegesha hakika unatikisika, Yaani akichaleenge hako kauelewa kako huwezi kufikia malengo.

Biblia inasema watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa.Vile hujui unajaribu kujitoa kujiokoa mwenyewe,unahisi ukiweka bidii saba mambo ayko yatakuwa mazuri mpendwa unatoa mimba, unafanya mapenzi kinyume na maumbile lakini ndoa hupati, unalala na Boss lakini kazi hupati.

Waefeso 2: 8 – 9

Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa nia ya imani; amabayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu; wala si kwa matendo na mtu awaye yote asije akajisifu.

NEEMA YA MUNGU NDIYO JIBU! VYOTE UNAVYOTAKA NA UNAVYOVITAMANI NA VIMESHINDIKANA PASSWORD YAKE NI NEEMA YA MUNGU.

Je, neema ya Mungu ni nini? unaweza kuwa unajiuliza hili swai.Yapo maandiko mengi yameeleza hili, ila mimi nitajaribu ku summarize maandiko mengi na kukupa definition fupi.

Grace of God ia s Disposition of understanding of limitless provision and possibilities that are contained in God but only accessed by the body of christ.

Neema ya Mungu ni uelewa juu ya uwezo wa Mungu usio na kikomo wa kufanya vitu amabao unawez kupatikana kupitia Yesu Kristo.

Limitless Possibilities au uwezekano usio na kikomo na kwamba kila kitu kinawezekana kwa Mungu.Mpendwa kwa maana kila kitu kinawezekana kwa Mungu kupitia his grace / Neema yake.Limitless Posibilities yaani hata kurudiana na EX wako. Mpendwa kwa uwezo wako vitu vingi haviwezekani na havitakaa viwezekane sadabu ndiyo ilivyo. Ila kwa neema ya Mungu vilivyoshindikana vinawezekana, sasa kwa nini uendelee kuteseka na Shetani na jitihada mfu ambazo zitakuumiza zaisi.

2 Timotheo 2: 1

Basi wewe mwanangu, uwe hodari katika neema iliyo katika Kristo Yesu.

Je ulikuwa unajua kuwa  kwa Kristo kuna neema? Leo umejua kwamba kuna neema ndani ya Kristo inayowez kukufanyia mambo yako yoter yaliyoshindikana kuwezekana. Mpendwa maandiko yanakwambia kwamba uwe hodari katika neema iliyo katika Kristo Yesu.Na Mpendwa tunajua kuwa Yesu sio mchoyo, kama ndani yake kuna neema anayosema Timotheo basi changamoto zetu zimeisha.

1 Petrio 5: 10

Lakini mkisha teseka muda mfupi,Mungu aliye asili ya neema zote na ambaye anawaiteni kuushiriki utukufu wake wa milele katika kuungana  na Kristo, Yeye mwenyewe atawakamilishieni na kuwapa uthabiti, nguvu na misini imara.

Leo tutasimama na hili neno.siku nzima.Masaa 12 utakuwa unaomba Mungu akupe neea / grace for (Hiko unachotaka kama ni ndoa, kazi, mtoto, cheo, mahusiano n.k yaani chochote unachotaka). Msihi Mungu kwamba umetambuwa kuwa wewe kuvuka hapa sio kwa nguvu zako ila kwa neema zake tu.Msihi Mungu aachilie tu hiyo neema leo ukavuke hapo.

1 Wakorintho 15 : 10

10 Lakini kwa neema ya Mungu nimekuwa hivi nilivyo, na neema yake kwangu imekuwa bure, Badala yake,nilifanya kazi kuliko mitume wote ingawaje haikuwa mimi bali ni neema ya Mungu iliyokuwa pamoja nami.

Msihi Mungu kwa neema yake haitakuwa bure, Neema atakayokupa ya kuolewa , kupata kazi,Uzao , cheo na madaraka haitakuwa bure badala yake neea yake itakapo kupeleka itakuwa sahihi kwako na pamoja na kukupa neema wewe pia utajitoa kwa kiwango kikunwa.

UNLOCK THE DOORS OF GRACE.

Neno la Mtumishi

Mpendwa Mfungo huu ni moja kati ya mfungo  mzuri, kama Adacadabra! ni fumba na kufumbua shida zako zimetoweka na kwa ufupi tunamuomba Mungu afanye yeyey maana upande wetu imeshindikana na hapa anayesimia kazi hii ni Mungu Pekee kwani kwa upande wetu tumeshindwa kabisa, Sisi tunashinda njaa kuonesha tunangoja huruma yake kwani hatuna la kufanya na kwasabu tunaomba Mungu atuvushe vile vipengele tulivyonasa tunachohitaji ni kuomba na kazi ya kufanikisha unamwachia Mungu, sasa kama kuomba na kuita Mbingu unaona tabu basi Mpendwa itabidi ubaki.

Day 2 : Exodus/ Kutoka

The End of Delaying Spirit ( Roho ya Mambo Yako Kuchelewa)

Mpendwa huenda umefanya maombi  yako yote unayoyajua au hata kuyasikia, umeto asadaka, umepanda mbegu, umeota hadi ndoto kuwa mambo yako yataisha,umepewa mpaka neno lako la unabii kuwa jambo lako litaisha, Ymkini Mungu mwenyewe amekupa ishara kuwa Mumeo ni yule au kazi yako iko seemu fulani na Wengine Mungu amewapa ahadi kabisa kwa maono kuwa jambo lao watalifanikisha Lakini Unfortunately in the world of fresh, ulimwengu wa mwili haijawezekana yaani ni BILABILA.Siku tu ndizo zinaenda lakini jambo halijitikisi, kama ni single uko single hadi very single, kama una bwana anakupiga matukio ni anakupiga tu matukio kama huna Mungu, Kama ni kazi ni unawatch movies tu. Mpendwa hiyo ni SPIRIT OF DELAY inakurudisha nyuma na kukuchelewesha na roho hii ni mbaya sana.

Mathayo 25 : 1 – 3 (Hakikisha Unasoma)

Biblia inasema kulikuwa na Bikira 10 wameitayarisha kumlaki Bwana Harusi. LAKINI BWANA HARUSI ALICHELEWA! hadi wote wakalala na alipofika wale Bikira watano (5) Taa zao zinaisha mafuta na harusi wakaikosa.

Wapendwa leo tuna kazi ya kumsihi Mungu, Bwana Harusi wako ASICHELEWE.Bwana Harusi angefika kwa wakati wale Bikira Wote 10 wangepata Mume. Zahama ya wale Bikira watano (5) waliozimikiwa taa isikukute sababu Bwana Harusi wako HATOCHELEWA wa jina la Yesu, kazi yako HAITACHELEWA katika jina la Yesu na  chochote unachokusudia kupata hakitachelewa kwa jina la YESU.

Mwanzo 26: 12

Mwaka huu Isaka alipanda Mbegu katika nchi ile, akavuna mara mia zaidi, maana Mwenyezi Mungu alimbariki.

Genesis 26: 12

Then Isaac sowed in that land, and reaped in the same year a hundredfold; and LORD blessed him.

Ukisoma maandiko yanasema Isaka alipanda mwaka ule ns mwaka uleule akavuna mara mia moja (100), Soma kwenye English Version utafaidi zaidi.Mwaka uleule Mungu alimbariki Isaka akavuna alichokipanda mara 100.

Ee Mungu toka February wanao wanapanda makusudi mioyo yao na wakapokee mwaka huu. Any spirit of delay (roho ya kuchelewesha) pambana nayo Mungu, kaipiger mpaka isujudu kama Dagoni lilivyosujudu.Mungu wa Isaka mwaka huu na sisi tukavuna mara mia 100 ya jitihada zetu.

Danieli 9:19

Ee mwenyezi Mungu, utusikie; utusamehe Ee Mwenyezi Mungu, Ee Mwenyezi Mungu kwa hisani yako utusikie na kuchukua hatua, wala usikawie, Ee Mungu wangu kwa ajili ya mji huu na watu hawa wanaoitwa kwa jina lako.

Mungu wa Daniel uliyemuokoa na roho ya kucheleweshwa majibu yake baada ya Malaika mwenye majibu yake kuzuiliwa kwa siku 21 na Prince of Persia, mpaka ukamtuma Malaika wako Michaeli akapambane nao mpaka majibu yakaruhusiwa kufika kwa Danieli. (Danieli 10:10-19)

Mungu unajua majibu yetu yamezuiliwa wapi. Iwe kwenye falme za Uajemi au Mizimu au waganga au NGUVU zozote za giza na wanasababisha ucheleweshaji wa majibu hayo, leo hii baba katikati ya huu mfungo kama alivofunga mtumishi wako Danieli tunaomba msaada wako na Malaika wako wa vita Michaeli baba, akapambane na wanao shuka hayo majibu na kuyaachia yatufikie kwa wakati. Siku hii ya leo Mungu deal na Waajemi wetu wotw wazuia majibu. Piga mmoja mmoja mpaka wakayatapike majibu hayo. Mungu sisi sio wakamilifu hata kwa mbali ila Mungu tumeweka jitihada na tumain thabiti juu yako na Mbingu. Mungu tunaomba hii favor kwa jina la yesu

Zaburi 13:1-4

Mpaka lini ee mwenyezi Mungu , utanisahau? Je, utanisahau mpaka milele? Mbaka lini utanificha uso wako? Nitakuwa na wasiwasi rohoni hadi lini, na sikitiko moyoni siku hata siku? Hadi lini adui zangu watafurahia taabu zangu? Uniangalie Na kunijibu, ee mwenyezi Mungu, Mungu wangu.

Mungu unajua kuugua kwangu na kutangatanga kwangu.Uniangalie na kunijibu ee mwenyezi Mungu.Mungu wangu.

Mathayo 9:9

Yesu aliondoka apo, na alipokuwa anakwenda zake, alimwona mtu mmoja aitwaye Mathayo, ameketi katika ofisi ya ushuru , Basi, Yesu akamwambia, “Nifuate”. Naye Mathayo akainuka , akamfuata.

Bwana Yesu niko huku natangatanga na dunia nikingoja wito wako wa kukufuata.Nikufuate wapi bwana Yesu. Nimekaa uku gizani nakungoja siku zote hizi. Nikumbuke bwana Yesu kama ulivomkumbuka Mathayo mtoza ushuru.

Isaya 55:6-7

Mtafuteni BWANA, maadamu anapatikana , Mwiteni ,maadamu yuko karibu. 

Ee Mungu patikana kwetu wanao, tuitikie wanao na utukomboe na hili loho la ucheleweshaji. Tukaribie Bwana na kutuokoa.

2 Wakorintho 2:6

Kwa maana Mungu anasema, “Wakati ufaao nilikusikiliza, na siku ya wokovu nilikusaidia. Tazameni, huu ndio wakati ufaao; leo ndio siku ya wokovu”

Ama kwa hakika wakati ufaao ndo huu na leo ndo siku ya wokovu wetu. Leo ndo mwisho wa mambo yetu kuchelewa kwa namna yoyote ile sawa sawa na neno hili katika jina la yesu.

I decree and declare your freedom from delaying spirits , Tangaza wokovu wako toka kwenye roho za kucheleweshwa. Kwa mamlaka ya jina la Yesu tangaza uhuru wako sasa, shuhudia kuvuka kwako na kuwa huru sasa.

1 Wafalme 18:46

Mkono wa Bwana ulikuwa juu ya Elia; akajikaza viuno, akapiga mbio akatangulia Ahabu mpaka kuingia Yezreeli.

Mkono wa bwana ulivo na Elia na ukampa Devine speed mpaka akawahi kufika Yezreeli kabla ya Ahabu alietangulia na gari la Farasi waendao kasi, leo hii ukawe juu yako na kukupa Grace/Neema for Devine speed kwenye ndoa yako iliyo chelewa, kwenye kazi iliyochelewa, kwenye cheo kilichochelewa, kwenye mtoto aliechelewa.Chochote cha kwako kilicho chelewa maishani mwako mkono wa Mungu wa Elia unaenda kuwa Pamoja na wee na kukupa DEVINE SPEED. Kwenye hilo eneo ukavuke kwa kasi mpaka washangae, walioona umechelewa wakabaki wanashangaa umevukaje kwa kasi ivo.

Siku nzima ya kesho ni kufanya tu affirmations juu ya mkono wa Mungu kuwa juu yako na kupokea Devine speed kwenye eneo hilo kwama na kuchelewa muda mrefu.Ni mwendo wa mkono wa Mungu juu yangu, napokea Devine speed kuvuka katika hii changamoto ya kutokuolewa. Ndoa yangui itawahi kama Elia alivowahi Yezreeli. Bwana harusi wangu hatochelewa kwa jina la yesu, Atawahi na ndoa yangu itakuwa kwa wakati. Lile fungu la mabikra waliokosa Harusi halitakuwa fungu langu kwa jina La yesu. Napokea devine speed ya kuvuka apa kwa mkono wa Mungu na nimevuka kwa jina la yesu.(Nafahamu mara nyingi uwezavyo)

Mkono wa bwana huu juu yangu napokea Devine speed ya kupata kazi , zile interview zote nilizofanya  na majibu yakazuiliwa na kucheleweshwa mkono wa bwana ukawe juu ya zile kazi na wakanikumbuke na Devine speed kafanye nwaniletee. Kwa jina la Yesu.

Day 3 : Exodus/Kutoka.

Open Doors of Favour

Zaburi 90:17

Na Fadhili za bwana, mungu wetu, ziwe juu yetu, na kazi ya mikono yetu uifanye thabiti, Naam, kazi ya mikono yetu uifanikishe.

 Psalm 90:17

Let the favor of the lord our God be upon us, and establish the work of our hands upon us; yes, establish the work of our hands!

 Bwana unifadhili mimi kwa maana nakukimbilia wee. Lord open dier of Mercy, Door of favor, Door of Breakthough anajua kwa nguvu zangu na jitihada zangu nimeshindwa.

Isaya 58:11

Mimi mwenyezi Mungu nitawaongozeni daima, nitatosheleza mahitaji yenu wakati wa shida.Nitawaimarisha mwilini, nanyi mtakuwa kama bustani iliyomwahiliwa maji, kama chemchemi yam aji ambayo maji yake hayakauki kamwe.

Baba tosheleza hitaji langu (taja hitaji lako) unaona jinsi nilivokauka. Baba ninyeshee maji maji ya furahaa. Futa uchungu wangu, futa kukataliwa kwangu, futa sononeko langu, futa vyote vinavonifanya kukosa rahaa. Ninyeshee maji yako ambayo kama chemchemii ya furaha isiyokauka niwe na furaha milele.

Mithali 18:22

Apatae mke apata kitu chema: Naye ajipatia kibali kwa Bwana.

 Proverbs 18:22

22 He who finds a wife finds what is good and receives favor from the Lord.

Siku nzima ni kufanya affirmation za kuita favor of the lord kuvuka hilo eneo. Fanya declarations. Shuhudia favor of the lord to fall upon you. Omba Mungu aachilie favor juu ya hilo jambo lako!,Fanya kwa moyo wote kwani Mungu akiamua kuku favor the rest is history.

Lord bless me with favor of marriage, apate mke amepata kitu chema.na kibali machoni pa Mungu.Mungu baba naomba kibali/favor ya kuwa mke.Mungu unajua nipo teari.Lord open door of favor for marriage, and door for breakthough katika hilii jambo.

Mithali 19:14

Nyumba na mali ni urithi apatao mtu kwa ambaye; Bali mke mwenye busara, mtu hupewa na BWANA

Mungu umesema mke/mme mwenye busara mtu hupewa tun a wewe Bwana. Bwana nikumbushe na mimi kwa kibali cha mume mwema. Mungu unajua aina ya wanaume wanaokutana nao. Mungu mimi nahitaji mtu tutaeishi kuzingatia sheria zako na njia zako. Ni epische na kikombe hiki cha wanaume wa mataifa wasiojua njia zako kama Ibrahimu alivopambana kumuepusha mwanae Isak ana wanawake wa mataifa . Mume mwema mtu hupewa na wee Mungu na mimi nakuja mbele zako kuomba wa kwangu.

Zaburi 5:12

Maana wewe mwenyezi Mungu wawabariki waadilifu; wawakinga kwa Fadhili zako kama kwa ngao.

Psalm 5:12

12 surely, LORD, you bless the righteous; you surround them with your favor as with a shield.

 Mungu naomba favor yako ikanivushe kwenye hii changamoto. Ni kibali na Fadhili zako tu Mungu.

Zaburi  106:4

Ee BWANA, unikumbuke mimi, kwa kibali ulicho nacho kwa watu wako. Unijie kwa wokovu wako.

 Psalm 106:4

4 Remember me , LORD, when you show favor to your people, come to my aid when you save them.

Baba yangu uliye mbinguni unikumbuke mimi moja wako. Nimekungoja mda mrefu. Unikumbuke ukiwa una wafavor watu wako. Uninitiated wakovu wako kwenye shida hii ( ITAJE)

Day 4 : Exodus/Kutoka

Oh Lord Show Me Mercy

Zaburi 51:1-2

Nihurumie, Ee Mungu, kadri ya Fadhili zako; ufutilie mbali makosa yangu, kadiri ya wingi wa rehema zako. Uniooneshe kabisa hatia yangu; unisafishe dhambi yangu.

Mungu najua nimekutana dhambi nyingi, na mimi si mkamilifu, uovu wangu u mbele yangu daima, yamkini changamoto yangu ni matokeo ya uovu wangu na mshahara wa dhambi zangu.Nakusihii ufutilie mbali makosa yangu,unioneshe kabisa hatia yangu na unisafishe dhambi zangu kadri ya wingi wa rehema yako isio pimika.

Zaburi 25:6

Ee BWANA, kumbuka rehema zako na Fadhili zako, maana zimekuwako tokea zamani.

Baba nirehemu mimi mwanao toka katika hii changamoto kwa maana nakukimbilia wewe baba.

Zaburi 40:11

Nawe, BWANA, usinizuilie rehema zako, Fadhili zako na kweli yako na zinihifadhi daima.

Baba usinizuilie rehema zako juu ya  ( TAJA HILO JAMBO) Fadhili zako na kweli yako vikanikague mimi Baba leo hii na kudhihirisha kama niko tayari na nimelipa gharama usinizuilie gharama zako juu ya hilo jambo, nak ama bado baba nioneshe bado wapi baba nitarekebisha.

Nehemia 9:31

Ila kwa rehema zako nyingi hukuwakomesha kabisa, wala kuwaacha; kwa maaana wee u Mungu mwenye neem ana rehema.

Baba yetu uketie mahala pa juu, kwa rehema zako usiniache tukomeee kabisa. Baba unaona tulivokosa raha,tulivonyong`onyea , tulivokosa amani na kutahayari juu ya huli jambo. Usiruhusu baba litukomeshe kabisaa. Usituache baba si kwa wema wetu bali kwa kuwa wewe ni Mungu mwenye Rehema na neema.

2 Samweli 24:14

Naye Daudi akamwambia Gadi, nimeingia katika mashaka sana; basi sasa na tuanguke katika mkono wa BWANA; kwa kuwa rehema zake ni nyingi; wala nisianguke katika mkono wa wanadamu.

Ee Mungu naomba niangukie mkononi kwako baba, maana kuna rehema nyingi, nisianguke mikononi kwa wanadamu baba. Wananisema vibaya baba, wanasema Mungu wangu yuko wapi baba? Mbona naaibika pekeangu, wanasema nina mikosi baba, wanasema nimelogwa baba, wanasema nina loho ya kukataliwa, wanasema vingi baba, Naomba unirehemu.

Yakobo 2:13

Maana hukumu haina huruma kwake yeye asiyeona huruma. Huruma hujitukuza juu ya hukumu.

 James 2:13

13 because judgment without mercy will be shown to anyone who has not been merciful.  Mercy triumphs over judgment.

Baba hukumu imekuwa kali Sanaa! Hukumu inanielemea baba. Hali yangu imekuwa ya ukiwa hadi watu wangu wa karibu wamenigeuka. Achilia rehema baba.Nakikaribia kiti chako cha rehema maana neno lako linasema rehema inashinda hukumu baba, napiga magoti chini ya kiti chako cha rehema. Nirehemu baba.

Waefeso 2:4

Lakini Mungu,  kwa kuwa ni mwingi wa rehema, kwa mapenzi yake makuu aliyotupenda.

 Neno lako baba linasema ten ana ten ana tena kwamba mungu wee ni mwingi wa rehema. Naomba unirehemu mimi mwanao kwakuwa si mkamilifu. Na shetani amepata uhalali wa kushikilia jambo langu la ( LITAJE) katikati ya mateso yangu Mungu kumbuka rehema zako na unirehemu.

Tito 3:5

Si kwa sababu ya matendo ya haki tuliyoyatenda sisi; bali kwa rehema yake, kwa kuosha kwa kuzaliwa kwa mara ya pili na kufanywa upya na Roho Mtakatifu.

Ee Mungu tukapokee majibu yetu ya tuliyoyangoja muda mrefu sio kwa sababu ni haki yetu au tunastahili ila kwa sababu ya huruma na rehema zako.

Waebrania 4:16

Basi na tukikaribie kiti cha neema kwa ujasiri, ili tupewe rehema, na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji.

Leo siku nzima kazi ni moja, karibia kiti cha rehem ana kuomba neema ya kukusaidia katika shida yako.

Day 5: Exodus/ Kutoka

Na uhakika nature ya haya maombi venye yanagusa your darkest demons, and untouched chambers of your heart wengi uchungu umewazidi na mmeacha.Kama tunaendelea na mfungo ni nusu ya tulioanza. When things get real wengi mnashindwa kukomaa na kulegea.Sasa the best parts ni hizi siku 3 zilizobakia jitahidi usikose mpendwa.

TAHADHARI !!

KAMA UME BREAK MAOMBI MANAKE HUJACOMMIT HIZI SIKU 4! USIRUKIE HII YA 5! ANZA TU UPYA! ,TABIA YA KUFANYA MAOMBI VIPANDE SIO KWENYE MAOMBI HAYA.TAFADHARI  MAOMBI YA LEO YANATEGEMEA PAST 4 DAYS! KAMA HUKUCOMMIT KUFUNGA PAST 4 DAYS USIRUKIE DAY 5

NI MAOMBI HATARII!! NDO MAANA MDA MWINGINE UNAAMBIWA BE CAREFUL WHAT YOU PRAY FOR ! NDO MAANA SIKU 4 NON STOP TUNAOMBA DIAMENTIONS 4 ZA NEEMA KWANZA KUJIWEKA TAYARI NA DAY 5.MPENDWA NI MAOMBI HATARI SANA! LAKINI SABABU TUNA BANK YA NEEMA TUNAWEZA KUENDELEA. KAMA HUJAOMBA NEEMA HIZO SIKU 4 SIT DAY 5 OUT! SIO MAOMBI YA KUTOKA UNAKOTOKA NA KUOMBA!

 Mpendwa Ukipitia changamoto nyingi na za muda mrefu inafika mahali unakata tamaaa kabisa kabisa, unakuwa upo mradi upo. Unakuwa unatumia Imani ya reserve.Sio kweli kwamba hilo jambo limeshindikana , sio kwamba Mungu hataki tu kukuokoa basi tu, sio kwamba hizo nguvu za giza zinakumiliki jumla jumla, Na sio kweli kweli kwamba Mungu haoni jitiada zako na hujamgusa kabisa.Mungu anaweza tena hajawai kushindwa na jambo, Na hilo jambo analisema over and over , Na Mungu tunaemtumikia sio wa kuishi kinyonge hivi.

Marko 9:23

Yesu akamwambia, ukiweza; yote yanawezekana kwake aaminiye

Marko 10:27

Yesu akawatazama, akawambia,”kwa binadamu haiwezekani, lakini kwa Mungu si hivyo, maana kwa Mungu mambo yote huwezekana”

Luka 18:27

Akasema, yasipowezekana kwa wanadamu yanawezekana kwa Mungu.

Yeremia 32:27

Tazama ,mimi ni BWANA, Mungu wa wote wenye mwili,je! Kuna neno gumu lolote nisilo liweza?

Yaani maandiko mengi yanasema, Mungu hajawahi shindwa jambo LOLOTE! Sasa hilo lako lisilosikia maandiko niaje? Sababu zipo nyingi ikiwemo dhambi , ibada hafifu, laana, vifungo, etc.Ndiyo maana tumeomba neema/grace kuweza kuvuka maana uhalali umeshindikana. Mungu mwenyewe tu akifurahi kwa neema zake huwavusha watu wake.

Mathayo 17:20

Yesu akawambia kwa sababu ya upungufu wa Imani yenu kwa maana, amin nawambia mkiwa na Imani kiasi cha punji ya haradali mtauambia mlima huu1 ondoka apa uende pale; na utaondoka; wala halitakuwako neno lisilowezekana kwenu.

Neno linajieleza kabisaaa Imani ndogo tu ya mbaaali unaweza unauambia mlima wako  wa upweke jobless , ndoa iliyovunjika, utasa, mlima wote unaokunyima rahaa ng’oka na ukajitose baharini ukakutwe.

Mathayo 21:21

Yesu akawajibu, kweli nawambieni kama mkiwa na Imani bila kuwa na mashaka, mnaweza sit u kufanya ivo bali hata mkitambia milima huu ng’oka na ukajitose baharini, ikafanyika hivyo.

Yesu analudia kusisitiza kwamba kuteseka na milima hio ni uzembe wako tu, ukiwa na Imani kidogo tu , BILA KUWA NA MASHAKA (hapa ndo kuta za jela zilipo). Mashaka dada ndo deal breaker. Unaweza kuwa na Imani na mashaka yakaharibu kila kitu.

Ayubu 5:8

Lakini mimi ningemtafuta Mungu,Ningemwekea Mungu dua yangu; yeye afanyaye mambo makuu. Yasiyotambulikana, mambo ya ajabu yasiyo na hesabu.

Umefanya vema hizi siku 4 umemtafuta Mungu na umepeleka shauri lako tayari , Dua yako imefika mezani pake.

Yohana 14:18

Sitawaacha ninyi yatima, naja kwenu.

Yesu alisema hatatuacha yatima, ila anakuja kwetu mambo yamekuwa magumu na machungu sana. Umepambana mbaka umefikia stage ngumu. Ni muda wa yesu kuja kwako.

2 Wafalme 6 : 1 – 6

1 siku moja, wanafunzi wa manabii wakamlalamikia Elisha wakisema, “Mahali apa tunapokaa ni padogo sana kwetu! 2 turuhusu twende Yordani tukate miti ili tujijengee mahali patakapotutosha” , “Elisha akawajibu” , “Nendeni”3Mmoja wao akamwomba akisema, “Tafadhari uwe nasi uende na watumishi wako” ,Naye akajibu “nitakwenda”  4 hivyo akaenda Pamoja nao, na walipofika mtoni Yordani wakaanza kukata miti , 5 mmoja wao alipokuwa anakata mti, shoka lake likachomoka na kuanguka majini, akalia akisema , “ sasa bwana wangu nitafanya nini? Shoka hili tulikuwa tumeliazima”6Elisha akauliza, “Liliangukia wapii?”mtu huyo akamwonyesha. Elisha akakata kijiti na kukitupa majini nah apo hapo shoka likaelea juu yam aji. 7Elisha akamwamulu alichukue naye akanyosha mkono akalichukua.

Mpendwa Elisha alikuwa ni mwanafunzi wa Elia na alikuwa ni  mwanafunzi mzuri.Alimjua mno na kufanikiwa kufanya miujiza mingi bila maombi ,Imani yake kwa Mungu ilikuwa kubwa mno,.Mnaona apo kwenye shoka. Anauliza wapi anatupa kijiti , Hapigi magoti walaa hainui mikono juu.

You need this kind of faith kuihamisha milima yako, sometimes unaukemea tu mlima , unaondoka! Kwa mamlaka ya jina la Yesu. Mashaka ndio yanakuponza. Kama umesoma physics unajua shoka kuelea ni impossible. Lakini limeelea.Sasa kuelea kwa shoka au wee kuolewa au kupata kazi kipi kigumu Zaidi? Don’t underestimate your God. Muda mwingine anaona unamchukulia pouwa sana. Kama hana maajabu. Wakati maajabu ndo sifa yake.

2 Wafalme 6:13-20

13Mfalme akamwambia , “Nendeni mkapeleleze mjue mahali alipo nami nitawatuma watu wamkamate” Basi wakamwalifu kwamba Elisha alikuwa huko Orthani. 14 kwahiyo mfalme akapeleka huko jeshi kubwa Pamoja na farasi na magari ya kukokotwa jeshi hilo likafika huko wakati wa usiku na kuuzingira mji.15Mtumishi wa Elisha alipoamka mapema kesho yake na kutoka nje akaona jeshi Pamoja na farasi na magari ya kukokotwa limezingira mji.Akarudi ndani aksema “ole wetu ee bwana wangu! Sasa tunafanya nini?”16 Elisha akajibu, “Usiogope sababu walio Pamoja nasi ni wengi kuliko walio Pamoja nao” 17 Kisha Elisha akaomba, “Ee mwenyezi Mungu, umfumbue macho ili apate kuona!” basi mwenyezi Mungu akamfumbua macho huyo kijana, akaona farasi na magari ya moto yakiwa kila mahali katika milima wote. Kumzunguka Elisha.18 Waalamu waliposhambulia, Elisha alimwomba Ee mwenyezi Mungu akisema, “Nakuomba uwafanye watu hawa wawe vipofu” mwenyezi Mungu akasikiliza ombi lake na kuwafanya vipofu. 19 Ndipo Elisha akawaendea na kuwambia , “mmepotea njia , Huu sio mji ambao mnautafuta ,nifuateni mimi nami nitawapeleka kwa yule mnaye mtafuta” Naye akawaongoza mbaka Somaria.20 Mara walipoingia mjini, Elisha akaomba, akisema, “Ee mwenyezi Mungu wafumbue macho ili waone”.

Mpendwa kuna muda Imani inakuwa ngumu sababu huoni kitu! Giza nene! Ni rahisi kukata tamaa manake unapambana vita kama kipofu. Yamkini kama mtumishi wa Elisha ukiona ukuu wa Mungu even once in a life time ingekuvusha pakubwaa sana. Itakuondolea mashaka mengi mengi kwenye Maisha yako. Na hata siku nyingine Nabiii au kuhani akisema Bwana anakuja unakuwa na uhakika kabisaa toka moyoni MUNGU YUPO.Imani thabiti kabisa kabisa inakuja pale mtu anapopata personal encounter with God or the heavens. Mpaka ukutane na tukio ambalo utashuhudia NGUVU ikishuka toka mbinguni nak u move things to your favor utavuka pakubwa Sanaa.Wapenwa Mmekuwa watii, hata mambo yaliyogoma hamkukata tamaa, even wakati mambo yalipokuwa shubiri kabisa you kept the hopes burning, Mungu ameona jitiada zenu, Na mimi nimeona jitiada zenu.

Kesho kwa wale mliofanikiwa kufunga zote 4 kwa kujitaidi. Nasimama na neno la Elisha na kumsihii Mungu awape ENCOUNTER/TUKIO muone nguvu yake na uwezo wake kwenye hizo changamoto zenu. Afanye jambo litakalo waondoa mashaka yenu yoote.Mashaka kwamba je anasikia?, je utapata kazi?, je utaolewa? ,je utazaa?, je yupo kwelii na ana nguvu za kukuokoa? Je utapata pumziko? ,je utapona?, je utaludi kwa mumeo.

Set the bar at highest level umewahi set! Ni Ebenezer tunamzungumzia apa.weka viwango vya juu kabisa aku surprise Zaidi wale wanitamkie ndoa! Sasa kesho weka uzazi, kama Mungu anakusikia na anakujali na huyo mwanaume ni sahihi kesho atamke ndoa, within 24 hours only! Kama ni kazi popote ulipofanya interview uitwe kazini within 24 hours. Kama ni mtoto na umeolewa kesho ubebe mimba!. Wewe sema ulichotaka Mungu afanye ujue kwamba YEYE NI MUNGU , YUPO, ANAKUPENDA SANA NA HAKUNA ASICHOWEZA akikufanyia hilo basi mashaka yako fullstop.Lazima ujicommit kwamba ukikuvusha  hapo hatorudi nyuma tena kujawa na mashaka mashaka.KAA TAYARI KWA TUKIO NDANI YA SAA 24!

Day 6: Exodus/Kutoka

 Sifa Kwa Mungu

Zaburi 109:1

Ee Mungu wa sifa zangu, usinyamaze

Mpendwa Kusifu ni moja ya mbinu kubwa sana kivita ambayo tunaisahau au sijui kuichukulia poa.Wa israel walikuwa wakiona tu Mungu amewaacha basi wanaanza kusifu non stop. Na wakisifu tu MUngu ana move in their favor.

2 Mambo ya nyakati 20:22

Wakati walipoanza kuimba na kusifu , mwenyezi Mungu aliwavuruga akili wanajeshi wa Amani. Moabu na wa mlima sehemu waliyokuja kupigana na Yuda.Na wanajeshi hawo wakashindwa.

Mpendwa Ukiludia kusoma nyuma utaona kabla hawajaanza kusifu mambo yalikuwa baridi na tulivu kama kwenye Maisha yako. Sema wakajiongeza kusifu na kuimba na Mungu sasa ndo akashuka.

Joshua 6

Utakutana na Habari za yeriko na ukuta wake. Mji ulifungwa tight hakuna mtu kupita. Mji una kuta refuu balaa. Na una majeshi ya uhakika.

Yoshua 6:20

Basi watu wakapiga kelele, na makuhani wakazipiga tarumbeta; hata ikawa, hapo watu waliposikia mlio wa mabaragumu hawo watu wakapiga kelele kwa sauti kuu sana, na ule ukuta wa maji ukaanguka chini kabisa hata watu wakapanda juu, wakaingia katika mji, kila mtu akasonga mbele kukabili, wakautwaa huwo mji.

Matendo 16:25-40

Unakutana na paulo na Sila wakiwa gerezani kwa kazi ya Mungu. Yaani kazi ya MUngu ndo iliwapeleka gerezani picha linaanza sio hata tamaa zao, wala sio makosa yao maybe, kazi ya Mung undo inawafikisha gerezani na wanapozi.

Wanangoja usiku mnene ambako kumetulia ndo wanaanza kuimba na kusifu non stop.Ingekuwa wee kazi ya Mungu ikupeleke gerezani afu Mungu akukalie kimya ungekuwa ushadata na kujiapiza kuwa ni mwanzo na mwisho kuhubiri.

Matendo 16:25

Usiku wa manane Paulo na Sila walipokuwa wakiomba na kumwimbia Mungu nyimbo za sifa, wafungwa wengine wakiwa wanawasikiliza , Ghafla kulitokea tetemeko kubwa lililotikisa msingi wa gereza ,milango yote ya gereza ilifunguka , na minyororo waliyofungwa wafungwa wote ikadondoka.

Kesho we focus tu kumsifu Mungu  kwa nyimbo na mapambio. Unaweza pia kutumia zaburi za sifa au tenzi za rohoni. Hata nyimbo za gospel.Usiombe chochote, tafakari tu ukubwa wa Mungu na umpe sifa na utukufu. Siku nzima ya kesho mpaka saa 12 jioni.

Day 7: Exodus

Mungu aanze kukuonekania

Yoshua 1:5

Hapatakuwa mtu yeyote atsksyeweza kusimama mbele yako siku zote za Maisha yako ; kama nilivokuwa Pamoja na Musa, ndivyo nitakavyokuwa Pamoja na wewe; sitakupungukia wala sitakuacha.

Musa alikuwa ameshafariki na Joshua alikuwa anakazana kuvijaza viatu vya Musa. Kumbuka kote walikotoka ni Musa tu ndo walikuwa wanamsikiliza.Akiwa ameanza tu kuwaongoza viumbe wazito sharti la kwanza wanampa kwamba watamtii endapo tu Mungu atakuwa Pamoja nae kama ilivokuwa kwa Musa. In short no God no deal for Joshua. (Joshua 1;16).Mungu atakuwa alisikia sharti lao zito, akaona Joshua mambo yatakuwa mazito kwake. So Mungu anamuhakikishia Yoshua kuanzia siku hiyo atakuwa Pamoja na Yoshua kama alivokuwa na Moses naa ana muahidi hakuna mtu atasimama dhidi yake kamwe na akafanikiwa. Na Zaidi hatampungukia kamwe kwa chochote .Mpendwa matatizo yote uliyonayo ni kwa sababu Mungu hajakuonekania. Kila mtu na kila kitu kinasimama dhidi yako. Umepungukiwa mpaka basi, Hali yako si hali.

Hitimisho

Kuhitimisha huu mfungo kesho msihii MUngu kuanzia sasa awe Pamoja na wee kama alivokuwa na Joshua na Musa. Msihi Mungu watu au vitu vilivosimama dhidi yako visipate uhalali tena. Na asikupungukie kwa chochote.

SIKU NZIMA MSIHI MUNGU AKUONEKANIE KWENYE ENEO LAKO LA CHANGAMOTO.

Mpendwa tumekamilisha mfungo wa Exodus , wengi wamepata matokeo na hata kama bado usishushe imani endelea tu kumkumbusha Mungu kwamaba umefunga kwa maoyo sana siku hizi saba (7), muulize kikwazo ni kipi? na kama hakipo basi muombe Mungu akuonekanie.

 

 

2 thoughts on “Exodus”

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Scroll to Top