Day 1: Alpha Prayers
“Tazameni, Mimi ninafanya kitu kipya.Kinafanyika sasahivi, nanyi mtaweza kukiona. Nitafanya njia nyikani, na kububujisha mito jangwani. “ [Isaya 43:19]
Mpendwa Muombe Mungu afanye kitu kipya kwenye mahusiano yako, uchumi wako, afya yako na chochote ambacho unahitaji. Siku nzima Muombe Mungu afanye jambo jipya.
Kitu gani hujakiona kikifanyika miaka ya nyuma maishani mwako na unataka Mungu akifanye mwaka huu?.Zungumza na Mungu kupitia mstari huu wa Isaya.
Day 2: Alpha Prayers
Madhabahu yapo ya pande mbili (2) amabayo ni Madhabahu ya Mungu na Madhabahu ya Nguvu za giza.Mpendwa madhabahu ni mfumo wa kuweka na kusimamia maagano na Madhabahu ndio hutoa nguvu ya maagano kutekelezwa.
Madhabahu inaweza kuwa sehemu ya agano a kale.Jacob kuna eneo alilotengeneza madhabahu kwa mawe na kuyapa majina na Isaka pia.Madhabahu inaweza kuwa Taasisi kama Mfalme Suleiman alivyojenga hekalu na kulifanya Madhabahu kwa agano la kwamba kila atakaye hitaji kuelekea katika hekalu na ajibiwe kwa agano lililowekwa. Madhabahu pia inaweza kuwa mtu.Yesu alikuja ili kukamilisha agano la ukombozi wa dhambi.
Jinsi ya Kuinua Madhabahu ya Bwana kwenye maisha yako na kuisimamia ( Kumantain)
Unaweza kuinua madhabahu lakini usipomtumikia Mungu kwenye hiyo Madhabahu, Madhabahu inapoteza nguvu.Ili Madhabahu iendelee kuwa na Nguvu lazima itumike.
Sitazingatia sana kwenye kutengeneza madhabahu za maeneo. Maandiko yapo ya kutosha.Unaweza kutengeneza sehemu nyumbani kwako ukawa unaitumia kwa ibada, Bali nitazingatia na kutia msisitizo katika kufundisha namna ya kutengeneza mfumo wa madhabahu kwenye maisha yako ambao utatembea nao popote na kupata matokeo.Samweli alikuwa madhabahu inayotembea kwani hakuwa amebanwa na mipaka ya eneo na Manabii wengi walikuwa madhabahu zinazotembea.
Mfumo wa madhabahu za maeneo uliishia katika vitabu vya mwanzoni, ndio maana madhabahu nyingi za maeneo ziko katika kitabu cha Mwanzo, japo mpaka katika kitabu cha Waamuzi zili-inuliwa kwa uchache.
Elia ndiye mtu alyeinua madhabahu ya Mungu amabayo Mungu alishuka mwenyewe mbele ya umati na kujithibitisha kwa watu wote. Mpendwa najua unatamani, unaomba na unasujudu Mungu ashuke kwenye changamoto yako na kujithibitisha mbele ya watesi wako wote, na kuweza kum-maliza huyo Baali mkubwa anaye kutesa, Nikusihi Mungu ni mwaminifu sana.
Elia pia alikuwa ametoka kukata tamaa na kukumbilia msituni na kujilaza ili Mungu amchukue afe, kwani alichoka na kukata tamaa kabisa katika wakati ambao Jezebel alikuwa anamuwinda amuue na Jezebel alikuwa amewaua manabii wengi wengi sana kiasi cha kumtisha sana Elia (Man of Unshakable Faith), Jezebel alikuwa kama Shetani na Elia kwa busara yake akaona kuliko auliwe na mwanamke yule ni kheri afe mwenyewe msituni.
Mungu anamtuma Malaika Msituni amwambie Elia kuwa Bwana Mungu yupo nawe na kipindi hiki ukienda atakuja huko huko.Tazama Elia alibaki mwenyewe akiwa solo yaani jeshi la mtu mmoja na anaambiwa aende vitani na Mungu atamkuta huko na Manabii wa Baali wako mia nne (400) na kwasababu Elia alikuwa mwenyewe hii inamaana Jezebel alikuwa ameua manabii wote wa Mungu na kuwamaliza akimbakiza Elia pekee.
Mpendwa kati ya changamoto yako na ile ya Elia nani anatakiwa kukata tamaa? Elia alikuwa anapambana na kifo kiilicho wazi yaani bila Mungu kuingilia kati ndio ungekuwa mwisho wa Nabii Elia, Lakini bado Elia anaenda kwa ujasiri. Lakini wewe mpendwa unakata tamaa,unainamisha moyo ,unajaa uchungu sio sahihi na pepo huyo mchafu atoke! Inuka Sasa Jenga Mandhabahu.
Elia alivyoamua kwenda hakuwa na kurudi nyuma. Alikuwa haweki jiwe moja na kubomoa, aliweza kukumbuka Manabii wote walio uawa na Jezebel bila hatia na kuomboleza tu (alikuwa ha anguki hata mara moja).Haonekani akiwaambia Manabii wa Baal anzeni nyie wala kuwaza kutumia njia za uongo ili kufanya Baali asile sadaka ile na kuchukua ushindi. Mpendwa hii ina maana ukiamua kubakia na kupambana na chanamoto tulia hadi woga wako ukumeze, Ukiamua kujenga madhabahu hakika usirudi nyuma! Usitazame changamoto yako wala kuwaza njia zamkato kwani sio muda wake muda huo tazama tu ukubwa wa Mungu.
1 Wafalme 18 : 20 -40
Neno la 1 Wafalme 18:20-40 linazungumzia kisa maarufu cha mtume Eliya na manabii wa Baali juu ya kuthibitisha ni mungu yupi wa kuabudu, Mungu wa Israeli au Baali. Hapa ni tafsiri ya Kiswahili cha Biblia ya Neno:
20 Basi Ahabu akatuma watu kwa Israeli wote, akawakusanya manabii wote pamoja juu ya mlima Karmeli. 21 Eliya akakaribia watu, akasema, “Hata lini mtakuwa na shaka kati ya watu wawili? Ikiwa Bwana ndiye Mungu, mfuateni yeye; lakini ikiwa Baali ndiye Mungu, mfuateni yeye.”
Lakini watu hawakusema neno.
22 Ndipo Eliya akawaambia, “Mimi ndiye nabii wa Bwana pekee aliyebaki, lakini manabii wa Baali ni mia nne na hamsini. 23 Tuleteeni, sasa, mafahali wawili; na waache wao wachague mfa hali mmoja kwa ajili yao, wamkate vipande-vipande na kuuweka juu ya kuni, lakini wasiwake moto. Mimi nami nitamletea mfa hali mwingine na kuutayarisha juu ya kuni, lakini sitawasha moto. 24 Kisha mnaoweza, mwite jina la mungu wenu, nami nitaomba jina la Bwana. Mungu atakayeitikia kwa moto, huyo ndiye Mungu.”
Nao watu wote wakamjibu, wakisema, “Neno hili ni jema.”
25 Eliya akawaambia manabii wa Baali, “Chagueni mmoja wa mafahali hawa, mkamtayarishie kwanza, kwa kuwa ninyi ni wengi. Kisha mwite jina la mungu wenu, lakini msiwake moto.”
26 Basi wakatwaa mfa hali mmoja wa hao waliokuwa wamewapa, wakamtayarishia, nao wakalia jina la Baali kutoka asubuhi mpaka mchana, wakisema, “Ee Baali, tuitikie!”
Lakini hapakuwa na sauti wala mtu aliyetia sikio; nao walipotembea hapa na pale karibu na madhabahu waliyokuwa wameifanyia dhabihu.
27 Ikawa mwendo wa adhuhuri, Eliya akawacheka, akisema, “Pigeni kelele kwa sauti kubwa; maana yeye ni mungu, huenda amekuwa akifikiri, au ana shughuli, au yupo safarini; labda amelala, naye atakeshwa usingizi.”
28 Basi wakapiga kelele kwa sauti kubwa, wakajikata-kata kwa visu na mapanga, kama desturi yao, hata damu ikawashukia.
29 Ikaisha kuwa mwendo wa adhuhuri, wakawa na unabii mpaka saa ya kuchinjwa kwa sadaka; lakini hapakuwa na sauti wala mtu aliyetia sikio, wala hakuna aliyevitazama vitu vyao vya dhabihu.
30 Kisha Eliya akawaambia watu wote, “Karibuni kwangu.” Basi watu wote wakakaribia. Akajenga upya madhabahu ya Bwana iliyoanguka. 31 Eliya akachukua mawe kumi na mawili, sawa na idadi ya makabila ya wana wa Yakobo, ambayo neno la Bwana lilikuwa limewaambia, kusema, “Jina lako litakuwa Israeli.” 32 Akajenga madhabahu kwa hayo mawe katika jina la Bwana; akachimba mtaro mkuu karibu na madhabahu, uwe na uwezo wa kubeba se’ahi mbili za mbegu. 33 Akapanga kuni, akamkata mfa hali vipande-vipande, akauweka juu ya kuni. 34 Kisha akasema, “Jileteeni maji mengi, mkaumwage juu ya hiyo dhabihu na juu ya kuni.”
35 Kisha akasema, “Fanyeni hivyo tena,” wakafanya hivyo tena. “Fanyeni mara ya tatu,” akasema, wakafanya mara ya tatu. 36 Maji yakatiririka karibu na madhabahu, hata mto wa maji ukajaa.
37 Ikawa wakati wa kutoa dhabihu ya jioni, nabii Eliya akakaribia na kusema, “Ee Bwana, Mungu wa Ibrahimu, Isaka na Israeli, leo na ijulikane ya kuwa wewe ndiwe Mungu katika Israeli, na ya kuwa mimi ni mtumishi wako, nami nimelifanya neno hili kwa maagizo yako. 38 Ee Bwana, nijibu, nijibu, ili watu hawa wajue ya kuwa wewe, Bwana, ndiwe Mungu, nawe umewageuza mioyo yao.”
39 Ndipo moto wa Bwana ukashuka, ukateketeza dhabihu, kuni, mawe na udongo, ukalisafisha hilo bonde la maji.
40 Na watu wote wakawa wamejipindukia, wakasema, “Bwana, yeye ndiye Mungu! Bwana, yeye ndiye Mungu!”
Hatua za kufanya kuinua Madhabahu ya Bwana.
1.Rekebisha uhusiano wako uliovunjika ,au ulio-yumba, au kusuasua na Mungu.
1 Wafalme 18 : 30
Kisha Eliya akawaambia watu wote, Nikaribieni mimi. Watu wote wakamkaribia, akaitengeneza madhabahu ya bwana iliyo vunjika na Kabla ya yote haya Eliya anaona kabisa uhusiano wa Mungu na watu wali ulisha vunjwa! watu wapo kwa Baali kwani hadi madhabahu ya Mungu walisha ivunja , hivyo katika hali ya kawaida walikuwa akingoja Elia kudhalilika.
Mpendwa hata wewe unajua unavyo sujudu kwa shetani ili upate ndoa, unafanya kila kitu kuanzia kufata miiko hadi kuvunja amri za Mungu, kulala na wame za watu sio shida kwako, kupasha viporo na ma -ex ukidai mahawala hawaachani pia sio shida kwako. Mpendwa kama umewekeza kwa Baali yaani uko miguu yote miwili sikufichi umewekeza katika udhalimu na katika hali hiyo huwezi kuinua Madhabahu hivyo Tubu, Rekebisha Madhabahu uliyovunja na rudisha uhusiano wako na Mungu.
2.Tumia Maagano na Neno la Mungu.
1 Wafalme 18:31
Elia akatwaa mawe kumi na mawili (12), kama ilivyo hesabu ya makabila ya wana wa Yakobo, aliyejiliwa na neno la BWANA na kuambiwa jina lako litakuwa Israeli.
Hakujichukulia mawe ilimradi alikuwa anatumia maandiko ya Mungu. alikuwa akifahamu mbele ata-invoke maagano ya Jacob (Yakobo), ndio maana hata maandalizi yalilala na kufata maandiko.
1 Wafalme 18 : 38
Ikawa, wakati wa kutoa dhabihu ya jioni , Nabii Elia akakaribia na kuesma Ee Bwana, Mungu wa Ibrahimu, wa Isaka na wa Israeli na ijulikane leo kuwa wewe ndiwe Mungu wa Israeli na ya kuwa mimi ni mtumishi wako, na ya kuwa mimi nimefanya mambo yote haya kwa neno lako.
Mpendwa Nabii Elia anatumia maagano ambayo Mungu alikuwa nayo na Ibrahimu, Isaka na Yakobo hafanyi maombi bila misingi kwa sababu Mungu anasimamia Maagano yake. Ndio maana ili uweze kupata matokeo ujue Mungu aliahidi nini na mahali gani. Alafu umbane hapohapo hakika hawezi kugeuka. Tunaona elia aki-invoke maagano ya Ibrahimu , Isaka na Yakobo ( Kama huyafahamu pitia Biblia yako Mpendwa)
Mpendwa natoa maandiko mawili tu ya kusimamia kwenye mabo mawili muhimu ambayo ni Mahusiano na Kazi , hivyo kama changamoto zako hazipo apo basi tafuta andiko sahihi mpendwa.
-
Kazi
2 Wathesalonike 3: 10
Kwa kuwa hata wakati ule tulipokuwapo kwenu tliwaagiza neno hili, kwamba ikiwa mtu hataki kufanya kazi basi asile chakula.
Maombi : Baba nataka kufanya kazxi. Nipatie kazi niifanye kwa Moyo wangu wote (Jimalize).
-
Mahusiano
God sets the lonely in families, He leads out the prisoners with singing; but the rebellious live in a sunscorched land.(Psalm 68: 4- 6).
3. Sadaka
Ukisoma vizuri kuanzia Mwanzo madhabahu nyingi ziliwekewa SADAKA kukamilisha maagano. hili liko wazi kabisa.
Madhabahu kavu bado sijaiona. Hata Noah pamoja na kupambana na Mafuriko hakuwa na raha ya kufikia kiasi cha kuto toa sadaka hivyo tunaona akijenga Madhabahu na kutoa Sadaka.
1 Mambo ya Nyakati 21: 24
Lakini Mfalme Daudi alimwambia Ornani, ” La, Hasha; nitavinunua kwa thamani yake kamili; sitamchukulia Mwenyezi-Mungu kitu kilicho chako au kumtolea tambiko la kuteketezwa amabalo halijanigharimu kitu.
Daudi anakataa kumtolea Mungu SADAKA ya kitu ambacho hakija mgharimu chochote.
Sadaka zipo za aina tatu :
- Sadaka za vitu unavyotoa kwa watu wengine au watumishi: Wengi hapa mnajimaliza kweli kweli lakini hii haitengi aina mbili za chini.
- Sadaka ya Ibada na kumtumikia Mungu: Madhabahu ili iwe na nguvu ibada inabidi iwe ya kutosha kwelikweli.
- Sadaka ya sifa na moyo wa shukrani kwa Mungu: Paulo na Sila wakiwa gerezani wanaomba na KUsifu. Milango ya Gereza lao inafunguliwa kwa sifa na Moyo wa shukrani.
4. Baraka na Matamko ya Kinabii
Watu wengi mnajitahidi kuzunguka kumtafuta Mungu kwa watumishi mabalimbali ambacho ni kitu kizuri. Lakini changamoto inakuja Mama yako au Baba yako wa kiroho anakutamkia vitu vizuri vya kupendeza?, Unashindwa kupokea kwa imani?, Unaona unapaka mafuta kwa mgongo wa chupa! kutokuamini kwako kunakukosesha Mambo. Neno lako linamrudia Mtumishi bila kufanikisha kiichokusudiwa.
Siku nyingine mtumishi hata kama huna inami naye sana akikupa neno lake kalisimamishe wenye madhabahu yako na msihi Mungu lisimrudie bila kutekeleza alicho liagiza.
Intergrity (Uadilifu) wa mtumishi haukuhusu sana.endapo kama ametumia kanuni na misingi kukubariki,baraka zinapita.
2 Wafalme 4: 16
Akasema, Panapo wakati huu mwakani, utamkumbatia Mwana. Akasema, La! Bwana wangu, Wewe mtu wa Mungu, usiniambie mimi mjakazi wako uongo.
Mpendwa hapa Elisha ana muahidi mwanamke Mshunani kwamba atapata Mtoto. Hamuamini Elisha sana lakini anataka mtoto hivyo ananpita na neno la Elisha wima wima.
2 Wafalme 4: 17
Yule Mwanamke akachukua Mimba, akazaa Mtoto Mume wakati huo huo mwakani, kama Elisha alivyo mwambia.
Neno tu la Elisha ndio lilifungua changamoto ya huyu mama.Elisha hakutumia andiko lolote zaidi ya neno lake tu la kitumishi.
Balaa linakuja mbele yule mtoto anapata kufariki. Mama yake anajua kabisa mpaka muda huo hakuna andiko la kumfufua mtu. Lakini anajua neno la Elisha halishindwi kitu.
2 Wafalme 4: 20- 21
Akamchukua, akampeleka kwa mama yake, naye akakaa magotini mwake hata adhuhuri, kisha akafa. Mamaye akapanda juu, akamlaza juu ya kitanda cha yule mtu wa Mungu, akamfungia mlango kisha akatoka.
2 Wafalme 4 : 27 – 28
Naye alipofika kwa yule mtu wa Mungu kilimani, alimshika miguu.Gehazi akakaribia amwondoe, lakini Mtu wa Mungu akamwambia mwache; Maana roho yake ndaniyake inauchungu na BWANA amenificha wala hakuniambia.
2 Wafalme 4: 28
Yule mwanamke akasema, Je! naliomba mwana kwa bwana wangu?, Mimi sikusema, usinidanganye?.
Mpendwa mwanzo kabisa anapomwambia atapata Mwana huyu mwanamke alimwambia USINIDANGANYE.kamkumbusha Elisha. Mtoto kufa si uongo huo.Alishika neno lilelile. Mpendwa hali hii ni kama umeshaambiwa UTAOLEWA unaanza kuyumba yumba!! Kuna watu niliwaaambia kama Mungu aishivyo 2022 wataenda kazini wakayumba.
2 Wafalme 4: 34 – 44
34. Ndipo akajilaza juu ya mtoto, mdomo wake juu ya mdomo wa mtoto, na macho yake juu ya macho ya mtoto na mikono yake juu ya mikono ya mtoto. Na alipokuwa amekaa hivyo, mwili wa mtoto ukaanza kupata joto. 35. Elisha akasimama na kutembea chumbani, kisha akarudi na kujilaza tena juu ya Mtoto. Mtoto akapiga chafya mara saba, halafu akafungua macho.36.Elisha akamwita Gehazi na kumwambia, “Mwite yule mama Mshunami.” Alipoitwa Elisha akamwambia,”Mchukue Mwanao”.
Day 3: Alpha Prayers
1.Genuine Repentance
Ukiona madhabahu za giza zinakuonea ujue lazima kuna kitu kinawapa au kiliwapa mamlaka ya kukunyanyasa. Na mara nyingi dhambi na udhaifu ndio hutoa uhalali kwa shetani na madhabahu zake. Ili kuuondoa uhalali huu lazima utubu ndani ya Moyo, Udhamilie kubadilika na kwenda kwa Mungu, ndio uombe rehema ya Mungu kuifungia hiyo madhabahu na uhalali wake wote juu yako.
Mpendwa leo ulitakiwa uwe umefanya Genuine Receptance! Zaburi ya 51 ni nzuri sana lakini pia kuna maandiko mengi kuhusu Toba,Fanya Sasa!.
Madhabahu ya Mungu kwenye Mahusiano yako.
Ee Bwana, Mungu wa Abrahamu,na wa Isaka na wa Israeli na ijulikane huu 2023 ya kuwa wewe ndiwe Mungu katika Israeli, na Mungu wangu ya kuwa mimi ni mtumishi wako, na yakuwa nimefanya mambo haya yote kwa neno lako.
Ukanikumbuke kwenye mahusiano yangu mwaka huu 2023 usiwe kama miaka mingne. Ukajitukuze mbele ya adui zangu na changamoto zangu na ijulikane kuwa wewe ndiye Mungu.
Ukanipandishe viwago, ukaniketishe katika nafasi ya Mke, ukanibariki mahusiano ya furaha, amani na upendo.Niolewe kwa ndoa inayotoka kwako na niondoke nyumabni kwetu kwa heshima na sio mwaka mwingine bali mwakaa huu 2023.
Baba naomba rehema dhidi ya madhabahu zote zinazozuia hatima yangu.Rehemu Baba uhalali wowote ulio katika madhabahu yoyote inayonisababishia kuchelewa, kuganda kwa mambo yangu, kukwama, kuchelewa na kuto songa mbele. Rehemu Baba ! Unirehemu sawa na fadhili zako na wingu la Rehema zako. Uyafute makosa yangu na kuniondolea uovu wangu.
Baba nimejua sababu kubwa ya ucheleweshwaji endelevu wa ndoa yangu, consistent failure, consistent stagnation, Lord have Mercy ! ni rehemu mtumishi wako, warehemu wazazi wangu,rehemu vizazi vyangu vya nyuma. Rehemu udhaifu wangu wote.
Katikati ya ghadhabu yako Baba kumbuka Rehema! Kumbuka Rehemaa! Mwaka huu Baba nikusuhudie.Ukajithibitishe kwangu na nikakushuhudie na sio katika mwaka mwingine ni mwaka huu 2023.
kuanzia leo baba nadhamiria kukutumikia wewe peke yako, sitatumikia tena wanaume wala fahari zao, wala miungu mingine, wala waganga,wala mizimu.Mimi na familia yangu tutakutumikia wewe Mungu wa kweli na utawala wa mbinguni. Najitenganisha na kujiondoa katika kutumikia miungu mingine, madhabahu za giza, nguvu za giza bali nitakutumikia Mungu wa Israeli peke yako, Mwanao Yesu Kristo na Utawala wenu wa Mbinguni. Natangaza utumishi wangu na utiifu wangu kwako Mungu pekee na sitakuwa mtumwa wa shetani wala fahari wake katika jina la Yesu.
Ufunuo 12 : 11
Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana-Kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao; amabao hawakupenda maisha yao ata kufa.
Kila madhabahu ya giza inayonikandamiza na kunizuia kufikia hatima yangu ya Ndoa!
Ninasihi kwa Damu ya Yesu dhidi yake!, Katika jina la Yesu kwa Damu ya agano la milele naamuru na kujitangaza kuwa niko huru kutokana na kukandamizwa na madhabahu na mapatano yote mabaya dhidi ya ndoa yangu.. Madhabahu zozote zinazozuia, kuchelewesha na kukwamisha ndoa yangu, Damu ya Yesu ikaondoe uhalali huo na kuniweka huru kwa jina la Yesu.
Ninaiponda madhabahu hiyo kwa damu ya Yesu,Ninajiweka huru kutokana na uendeshaji wa madhabahu hizi kwa jina la Yesu. Imetosha ! Natangaza Mwanzo mpya, Imetosha kuolewa tumezeeka, Imetosha kusubiria Ndoa miaka 10, kuteseka na Mahusiano na kufanywa mjinga. Ninaita utaratibu mpya katika uhusiano wangu ! Natangaza mwanzo mpya wa mahusiano yangu.
Ninaita utaratibu mpya wa mabo yangu, Mwaka huu 2023 hautakuwa kama miaka mingine, kutakuwa na mwanzo mpya, Mungu atafanya jambo jipya kwenye mahusiano yangu na litaonekana.
Hatima yangu na utukufu wa ndoa yangu na kuunganisha madhabahu ya kiti cha enzi cha Mungu chenye rehema na neema.Hatima yangu ya mahusiano, utukufu wa ndoa yangu na kuunganisha na madhabahu ya kiti cha enzi cha Mungu aliye juu Mbinguni.
Ifahamike katika ulimwengu wa roho kwamba kuanzia sasa mahusiano yangu na mimi tumetenganishwa na mfumo wa madhabahu ya ukoo, wala mfumo wa madhabahu zozote za giza, Mimi na mahusiano yangu tumeunganishwa na madhabahu ya kiti cha enzi cha Mungu aliye hai chenye rehema na neema. Mahusiano yangu na hatima ya ndoa yangu kuanzia sasa yanalindwa na mfalme wa wafalme, Mwana wa Mungu aliye hai, Agano jipya la damu ya ukombozi hivyo Nguvu za giza , za kibinadamu hazitakuwa na nguvu tena juu yake katika jna la Yesu.
I stand by the prophetic and apostolic relim by the mercy of God and power of the holy ghost, I decree and declare you free from oppression from evil altars! Yo are free in the name of Jesus.
Nakutangazia mwisho wa kipindi kirefu na endelevu cha kukosa bahati kwenye mahusiano, kuumizwa, kukata tamaa, kukataliwa, upweke na kukosa furaha katika jina la Yesu. Kama utawala wa Baali ulivyofika mwisho na kwako msimu huo umefika mwisho kwa jina la Yesu! nakutangazia mwanzo mpya ambao Mungu atafanya jambo jipya kwenye mahusiano yako na litaonekana kwa jina la Yesu.
Kwa jina lipitalo majina yote nasitisha, kuvunja na kubatilisha alama zozote za kuchelewesha kuolewa kwako, kutodumu kwenye mahusiano, kuachwa bila sababu mahusiano kutofika katika ngazi ya ndoa au kuishia njiani kwa jina la yesu na nguvu ya Mungu watu wote walio nyuma ya hili kuanzia sasa Moto wa roho mtakatifu uwatenganishe na wewe pamoja na mahusiano yako. Ktika jina la Yesu havitajirudia tena.
Katika Jina la Yesu naamuru hatima yako ya ndoa ifunguke na ukapate mwenzi ambaye mtaenda kufunga ndoa an kuwa na furaha pamoja, mkaanzishe familia pamoja. Mwaka huu 2023 usihishe bila Mungu unaye mtumikia kuku-kumbuka kwenye eneo la ndoa kama alivyomkumbuka Nuhu, kama alivyomkumbuka Raheli. May God remember you in your maritual affairs! May Lord remember you in 2023, akupe Mume, akupe nyumba yako na familia yako kwa jina la Yesu.
Mwaka 2023 ukawe mawaka wako wa breakthrough in Maritual Affairs. Ukafunge ndoa takatifu na Ukamuone Mungu kwa ukubwa kwenye mahusiano yako.
Naikabidhi January to December 2023 ukawe mwaka wako utakao muona Mungu kwenye mahusiano yako kama Elia alivyomuona mbele ya Manabii wa Balaai! akajithibitishe kwenye mahusiano yako kwa ukubwa!. Ukapate Breakthrough kutoka kwenye changamoto zako zote zinazo kukandamiza kwenye mahusiano yako katika jina la Yesu. Kama ilivyokuwa mwisho wa Baali na manabii wake ikawe mwisho wa kukosa furaha kwenye mahusiano yako kwa jina la Yesu, ukamuone Mungu kwa viwango vingine. Mpendwa kama Mungu aishivyo 2023 ukamshuhudie kwa habari ya ndoa takatifu!.
Day 4 : Alpha Prayers
Zaburi 50 : 5
Nikusanyieni wacha Mungu wangu waliofanya agano nami kwa dhabihu.
Psalm 50 : 5
5. Gather my saints together unto me; those that have made a convenant with me by sacrifice.
Sadaka inakupa sauti mbele za Mungu. Mungu lazima atakusikiliza. Sasa chukua muda wako kuzungumza na Mungu juu ya hatima yako.Kama unatoaga sadaka lakini hupati majibu kabisa au unapata majibu madogo kaa uzungumze na Mungu wako. Toa hoja zako kicho UTOE SADAKA YAKO SASA.
1.Samweli 7 : 10
Hata Samweli alipokuwa akitoa hiyo sadaka ya kuteketezwa, Wafilisti wakakaribia ili kupigana na israeli; lakini Bwana akapiga ngurumo, mshindo mkubwa sana, juu ya Wafilisti siku ile akawafadhaisha; nao wakaangamizwa mbele ya Israeli.
Sasa basi Mpendwa msihi Mungu aitazame sadaka yako na awatazame wafilisti wako. Na kama imempendeza, kama imefika mbele za macho yake na kumgusa atembeze radi na mshindo mkubwa sana juu ya Wafilisti wako wote wanaokunyima raha. Wafilisti wa mahusiano yako, uchumi wako, uzao wako, ofisini kwako na Wafilisti wote wanaokukosesha furaha! Aitazame SADAKA yako na awapige radi moja ya kumaliza changamoto hio.
Zaburi 20 : 1 – 5
1 Bwana akujibu siku ya shida; Jina la Mungu wa Yakobo na akutie nguvu. 2 Na akutumie msaada toka patakatifu, Na toka Sayuni akusaidie. 3 Ayaone dhabihu zako, azipokee sadaka zako. 4 Akujalie kwa kufuatia moyo wako, Akayatimize mashauri yako yote. 5 Tutaushangilia wokovu wako na kusimama bendera zetu; Tena, katika Jina la Mungu wetu tutasimama. Bwana na atimize maombi yako yote.
Zaburi 126: 1 -6
Mwenyezi Mungu alipoturekebisha na kuturudisha Siyoni, tulikuwa kama watu wanao-ota ndoto! hapo tuliangua kicheko; tulishangilia kwa furaha. Nao watu wa mataifa mengine walisem; “Mwenyezi Mungu amewatendea mambo maubwa!” na kweli Mwenyezi Mungu alitutendea mambo makubwa na tulifurahi kwelikwel! Ee Mwenyezi Mungu ulekebishe tena hali yetu, kama mvua inavyotiririsha maji katika mabonde makavu. Wanaopanda kwa machozi, watavuna kwa Shangwe na wanaopanda mbegu kwa kilio watarudi kwa furaha wakichukua mavuno.
Zaburi 50:6
Na mbingu zitatangaza haki yake, kwa maana Mungu ndiye aliye hakimu.
Psalm 50 : 6
6 And the heavens shall declare his rightousness: for God is judge himself.Selah
Mpendwa zisihi Mbingu zitazame sadaka yako na kwa habari ya changamoto yako zizingatie haki yako na Mungu aliye hakimu ahukumu juu ya suala lako kwa maana umengoja muda mrefu!.
Day 5: Alpha Prayers
1 Wathesalonike 5: 16 – 18
16 Furahini wakati wote, 17 Ombeni pasipo kukoma, 18 Shukuruni katika kila hali; kwa maana haya ndiyo mapenzi ya Mungu kwa ajili yenu mkiwa ndani ya Kristo Yesu.
1 Nyakati 16:34
Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni mwema; upendo wake wadumu milele.
Mshukuru Mungu kwa wema wake wote aliofanya maishani mwako.Shukuru kwa ulivonavyo hata usivonavyo.Shukuru kwa vyenye dalili ya kwenda na hata visivyo na daili kabisa.
Mpendwa mshukuru Mungu sio kwa sababu umeona ila kwa kuwa Mungu anaaminika asilimia mia moja ( 100%).