Umiliki

Wapendwa ni ndoto ya kila mmoja wetu kumiliki vitu, thamani, ardhi au mali kubwa na jambo hili linafahamika hata  katika ulimwengu wa Kiroho, hata Shetani anafahamu kuhusu hili.Biblia ina mifano mingi na mafundisho kuhusu umiliki ,tujifunze sasa:

Mathayo 4: 8 -11

8. Kisha Shetani akamwongoza Yesu mpaka kwenye kilelel cha mlima ulio mrefu sana na kumwonesha falme zote za ulimwengu na vito vya kupendeza vilivyomo ndani.9. Shetani akamwambia Yesu, “Ukiinama na kuniabudu, nitakupa vitu hivi vyote.”

Wapendwa wengi wenye kutaka kumiliki mnasujudu na kumuabudu shetani ili mpate zaidi!! .Mtu anafikia kiasi cha kukubali kufanya tendo la ndoa nje ya maumbile, Kuzini na Mume wa mtu ili kupata vitu au mali, fancy apartment, Brazillian Hair  huku ni kumsujudia shetani hata ukifanya wizi ofisini mpendwa unamsujudia shetani. Inawezekana Mungu kakupangia kumiliki kitu au umemuomba na kashakupa lakini moyo wako hauna subira hivyo unaona bora umsujudie muovu ili upate kwa haraka.

Shetani ni muongo sana wapendwa hiyo ndio sifa yake.Akikupa kitu lazima uzidi kumtumikia ama sivyo atakudhalilisha na wengi  hili amlizingatii jambo ambalo mwisho wa siku mtu anafikia umri wa miaka thelathini (30s) tiyari ameshajinyonga.Shetani ashampatia vitu akatamba navyo kidogo, sasa imefika muda amempokonya kamuacha adhalilike.

Wapendwa hata kwenye maandiko  kuna muda Mungu aliahidi kuwapa vitu watu tena kwa kiapo lakini vilikawia mpaka wanakuja kudai. Mtu anaapiwa kitu ana miaka 40 anakuja kudai na miaka 80, Lakini Mungu alivyo mwaminifu anamuweka hai mpaka neno lake litimie.

Mungu hutupa neno lake mara nyingi kwa ndoto, manabii na watumishi etc. lakini changamoto yetu wanadamu tukiona linakawia tunapenda kwenda upande wa pili na kuishia kusujudu, Tujifunze kitu kutoka kwa CALEB!:

Yoshua 14 : 6- 15

  1. “Wana wa Yuda walimkaribia Yoshua huko Gilgali, na Kalebu, mwana wa Yefune, huyo Mkenizi, akamwambia: ‘Wewe wajua neno la Bwana alilomwambia Musa, huyo mtu wa Mungu, katika habari zangu na katika habari zako tulipokuwa huko Kadesh-Barnea.
  2. Nilikuwa na miaka arobaini na tano wakati huo, nikiwa na umri wa miaka 85 sasa.
  3. Lakini niko na nguvu kama nilivyokuwa wakati nilipotumwa, naam, nina nguvu kwa ajili ya vita na kwa ajili ya kazi nyingineyo.
  4. Basi sasa, nipe eneo hili la mlima ambalo Bwana aliniahidia siku ile; maana wewe mwenyewe uliisikia siku ile kuhusu haya mahali pale, kwamba walikuwako Warefai huko, na miji mizito yenye maboma; Bwana yu pamoja nawe, nawe utawafukuza hao watu wa nchi hizi, kama Bwana alivyosema.
  5. Basi sasa, Bwana ameyaishi maneno hayo yale yaliyonena siku ile, naye ameyatimiza kwa kuwa mimi ni nina miaka 85 sasa.
  6. Na tazama, mimi ni leo hivi kama nilivyokuwa siku ile Musa aliponipeleka; kama nguvu zangu zilivyokuwa siku ile kwa ajili ya vita, vivyo hivyo zilivyo siku hii, kwa kuamua vita, na kwa kutoa hukumu.
  7. Basi, nipelekele kwa hao Warefai wale, kama Bwana alivyonena. Nipelekele huko ili niwafukuze;
  8. Yoshua akambariki, akampa Hebroni kuwa milki.
  9. Hebroni ndiye urithi wa Kalebu mwana wa Yefune Mkenizi hata leo, kwa sababu alifuata kwa moyo wake Bwana, Mungu wa Israeli.
  10. Hebroni mwanzo wake ulikuwa mwaka wa arobaini na tano; naye akawa na kutembea na Wana wa Israeli kutoka Kadesh-Barnea hata siku hii, katika mahali pale, hali ya kuwa mpaka wakati ule wa Musa yule mtumishi wa Bwana, nchi ya Kanaani ilikuwa na utulivu wa vita.”

Hii ni sehemu ya Biblia inayoeleza jinsi Kalebu alivyopewa urithi wa ardhi ya Hebroni kama vile Bwana alivyomwahidi kupitia Musa, na jinsi Kalebu aliendelea kuwa mwaminifu kwa Mungu hadi katika umri wake wa miaka 85.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Scroll to Top
× IT Help Desk