Strong Man

Katika nyakati mbalimbali kwenye maisha yetu ya kila siku tumejikuta tukipata changamoto mbalimbali na tumekuwa tukiomba na kuombewa na hatupati suluhu , Watesi wetu (Strongman) wamekuwa wakitunyanyasa na kututesa. Mpendwa Biblia imwewza kutoa mafundisho na njia ya kuwashinda wenye nguvu (strongman) wanaotutesa na kufungia milango neema zetu ,tufatilie kwa pamoja:

Part 1 : Strong Man/ Wenye Nguvu

Marko 3 : 27

Hawezi mtu kuingia ndani ya nyumba ya mtu mwenye nguvu na kuviteka vitu vyake, asipomfunga kwanza yule mwenye nguvu;ndipo aiteke nyumba yake. 

Ukisoma Marko 3: 22 – 30 utaona kujaribiwa kwa nguvu za Yesu Kutoa Pepo, Wanadai anatoa Pepo kwa nguvu za Beelzebuel (Mwana Mfalme wa Pepo ) ambaye ndio shetani mwenyewe.

Mpendwa Yesu anaipinga hoja yao vikali kwa kutumia hoja ya Shetani anawezaje kumtoa Shetani mwenzake?.

Marko 3 : 23

Akawaita akawaambia kwa mifano, Awezaje Shetani kumtoa Shetani ?

Part 2 : Strong Man / Wenye Nguvu

Mpendwa kumshinda shetani inahitaji uishinde nguvu yake,umfunge ndio uweze kujikomboa kutoka katika kifungo chake.

Yesu alimaanisha kuwa yeye anaweza kumtoa Shetani kwa sababu ananguvu zaidi ya Shetani.

Ukirudi nyuma Marko 1 : 12 – 13 , Yesu anamshinda shetani kwa kishindo pale alipomjaribu baada ya mfungo wa siku arobaini (40) hadi shetani anaondoka zake, na aliendeleza ushindi wake wa kishindo dhidi ya shetani maranyingi sana.

Mpendwa kuna muda mambo yanakuwa hayaendi yamefungwa na washirika wadogo wadogo wa shetani kwama wachawi, majini, wanga na pepo  ambao ukikombolewa huwa wanakimbia.

Part 3 : Storng Man/ Wenye Nguvu

Mpendwa kuna muda maombi yanakuwa hayatikisi kitu. Unaombewa lakini hakuna mabadiliko; Mpendwa ifikapo nyakati hiyo fahamu unapambana na wenye nguvu.

Mpendwa itafika kipindi utalaumu watumishi na kuwaona hawana msaada lakini ni kwasababu nguvu zao ziko chini ukilinganisha na hila za shetani. Kifikapo kipindi hiki mpendwa unahitaji msaada kutoka kwa mwenye nguvu kumzidi huyo strongman/mwenye nguvu amabaye ni Yesu Kristo.

Yesu ndiye mwenye uwezo wa kukusaidia dhidi ya huyo strongman/ mwenye nguvu, ili uweze kuvamia nyumba yake na kukomboa mali zako alizo ziteka nyara.

Hivyo kama kuna changamoto umeomba sana na haina maendeleo yoyote. Fanya Sala hii ( katika Prayer Point ) ili uweze kuomba msaada wa Yesu ili uweze kumfunga huyo mwenye nguvu aliyezuia matokeo yako.

Prayer Point

Bwana Yesu, niokoe na mateka ya mwenye nguvu/ strong man kwenye eneo (TAJA ENEO ULILOKWAMA KWA MUDA MREFU).

Waefeso 6:12

Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu ya nyama bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.

Bwana Yesu nasimama  na mstari huu kuomba usaidizi wako katika kupambana na hizi taasisi za wenye nguvu zinazo nikandamiza kwa maana sio vita ya mwili bali ya roho na nimeshindwa kwa muda mrefu.Naomba uingilie kati kwa niaba yangu ee Bwana wa majeshi.

Part 4 : Strongman / Wenye Nguvu

Ufunuo 12 : 11

Nao wakamshinda kwa damu ya mwanakondoo, na kwa neno la ushuhuda wao; amabao hawakupenda maisha yao hata kufa.

Nainua Damu ya Yesu iliyomwagika Calvary dhidi ya kushikiliwa kwa namna yoyote katika eneo lolote dhidi ya Strongman / mwenye nguvu na washirika wake kwa jina la Yesu.Naandika ushuhuda mpya wa kushinda kwangu katika eneo hilo kwa jina la Yesu.

1 Yohana 3: 8

Yeye atendaye dhambi ni wa ibilisi, kwa sababu ibilisi amekuwa akitenda dhambi tangu mwanzo.Kwa kusudi hili Mwana wa Mungu alidhihirishwa, ili aangamize kazi ya ibilisi.

Mwana wa Mungu uliedhihirishwa ili uziangamize kazi za shetani naomba uangamize kabisa kazi hizo kwenye eneo ( taja) mfano, Mahusiano yangu ,uchumi wangu etc. na uniweke huru kabisa.Nakusihi sana mwana wa Mungu unikumbuke na kunifanyia msaada wako kwenye eneo hilo.

Part 5 : Strongman / Wenye Nguvu

Luka 10 : 28

Akawambia, Nilimwona Shetani, akianguka kutoka mbinguni kama umeme.

Ee Bwana Yesu nakusihi sana uniokoe na huu utumwa wa strongman/ wenye nguvu na kwa mara nyingine shetani aanguketoa kwenye eneo la mahusiano yangu / kazi yangu kama umeme na niwe huru tena.

Yohana 12 : 11

Sasa ni saa ya hukumu kwa ajili ya ulimwengu huu, sasa mkuu wa ulimwengu huu atatupwa nje.

Bwana Yesu hukumu eneo langu la kazi / mahusiano na ukamtupe nje mkuu wa ulimwengu na washirika wake na kuniweka huru.

Warumi 16: 20

Naye Mungu wa amani atamponda shetani chini ya miguu yenu upesi. Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo na iwe pamoja nanyi.

Neema yako Bwana Yesu iwe juu ya Mahusiano yangu/ Kazi / Uzazi ukampondeponde mwenye nguvu ns washirika wake walio katika hilo eneo.

Zaburi 18 : 17

Akaniokoa na adui yangu mwenye nguvu, Na wale walionichukia, Maana walikuwa na nguvu kuliko mimi.

Bwana Yesu ukaniokoe na mwenye nguvu aliezuia eneo langu la mahusiano/kazi/uzao/linalokusumbua muda mrefu na kuniweka huru.

 

 

 

2 thoughts on “Strong Man”

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Scroll to Top
× IT Help Desk